Jamani nimeongea mpaka nimechoka. Huyu mwanamke anachunguza simu yangu kuliko maelezo. Kila nikibadili password anayo. Ananiangalia kwa makini anamemorize kisha anakuja kufungua simu kuchunguza. Yaani kwa kifupi nipo uchi.
Kama mnavyojua sasa hivi simu ndio kila kitu. Yaani ninachochat na marafiki zangu, account zangu za bank, ninayowasiliana na wazazi wangu, masuala ya kazini. Jamani yaani ni kila kitu. Niliweka app ya kumpiga picha akitoa password na imemkamata mara kibao.
Anachimba mpaka message za messenger, mpaka deleted messages anazifukua, mpaka zile locked messages za whatsapp anazo. Anachukua namba za watu anawapigia a. Tunachat masuala ya siri ya kifamilia kumbe yote anayajua ananichora tu.
Nimekuwa nikibadili password kila siku lakini wapi. Hii tabia kwa kweli inanikera sana na nashindwa la kufanya. Plz nishaurini.
Mkuu unachopitia ndio nachopitia kwa sasa.
Nilikua badili sana password lkn anazijua.
Nikahisi labda nahackiwa .
Mbinu yake ya kujua Password.
Nikiwa natumia simu, anaweza kua Yuko pemben, ANAJIFANYA ANACHAT, KUMBE AMEWEKA KAMERA YA SIMU YAKE.
Hizi simu za Iphone, Samsung, Google pixel, Zina ZOOOM SANA.
Kwahiyo wakati ambao Mimi naona ni Safe, yeye anazoom mpaka meseji, anajua passwords .
Nikilala au nikiwa Bafuni, Anachukua simu ana piga screenshots Kila kitu .
Tumegombana sana, lkn Mwisho nimegundua ANANIPENDA NA NI MWENYE WIVU SANA .
Kuna siku nikamwambia MKE wangu, wewe ni Pisi Kali sana, Nisamehee kwa kukuweka roho juu juu.
Ukweli ni kwamba, SISI WANAUME, TUNAPOCHEPUKAZ KUNA WAKATI TUNACHEPUKA NA KUJISAHAU KABISAAA KIASI KWAMBA, WAKE ZETU WANAKUA CURIOUS SANA KUTAKA KUJUA, KUNA NINI NYIMA YETU