Mke wangu anachunguza mno simu yangu

Mke wangu anachunguza mno simu yangu

Anahangaika ni jinsi gani atakuacha. Anakutafutia sababu. Mtaachana huyo, ni suala la muda tu labda umng'ang'anie.
 
Huyu siyo kuwa anakufuatilia bali anataka kuverify upuuzi wake ili siku ukimkamata awe na sababu ya kukufanya ushindwe kumhukumu kwa kuwa utakuwa na kosa the same

Lkn nje ya hapo anahofia future yake kwako anaona ni vyemabkukuchimba kuwa na details zako ili ukizingua anakupasha

Anatumia projection kukupa shida yaani watu wakuogope wewe kwa sababu yake hivyo atakuwa kakuweka kwapani huna la kufurukuta

Mwanamke anapenda mwanamme unpredictable kabisa

Anza kuongea na watu physically punguza simu siku nyingine ujifanye umeisahau home apekue na asikute kitu

NB hawa viumbe huwa wanauwezo wa kunusa harufu mapema

Aidha mpige matukio kadhaa au mshikishe mimba mfululizo
 
Jamani nimeongea mpaka nimechoka. Huyu mwanamke anachunguza simu yangu kuliko maelezo. Kila nikibadili password anayo. Ananiangalia kwa makini anamemorize kisha anakuja kufungua simu kuchunguza. Yaani kwa kifupi nipo uchi.

Kama mnavyojua sasa hivi simu ndio kila kitu. Yaani ninachochat na marafiki zangu, account zangu za bank, ninayowasiliana na wazazi wangu, masuala ya kazini. Jamani yaani ni kila kitu. Niliweka app ya kumpiga picha akitoa password na imemkamata mara kibao.

Anachimba mpaka message za messenger, mpaka deleted messages anazifukua, mpaka zile locked messages za whatsapp anazo. Anachukua namba za watu anawapigia a. Tunachat masuala ya siri ya kifamilia kumbe yote anayajua ananichora tu.

Nimekuwa nikibadili password kila siku lakini wapi. Hii tabia kwa kweli inanikera sana na nashindwa la kufanya. Plz nishaurini.
Mkuu tumia hii mbinu. Tumia fingerprint kutoa lock kama simu yako haina tafuta simu yenye finger print. alafu badilisha password. Badda ya kubadili anza kutoa simu kwa finger print tu ili asijue passwor. Alafu ikifika usiku restart simu yako alafu iweke pembeni usiitumie kwa hapo hataweza kuitumia maana akishika itadai password baada ya kuwashwa na hapo hajui password wewe tu ndio unajua. kama utasahau kuizima simu hakikisha una set ile schedule power on/off ipishanishe dk 3 - 5 ili simu iwe inazima nakujiwasha yenyewe ukiwa umelala. na akishika tu anakutana na password ambazo hazijui. Wewe ukishika asubuhi unatoa password alafu unaendelea na fingerprint. Done
 
Usifanye hivyo mkuu! Ukamuumize mkeo kwa sababu ya wanawak

Mke ni rafiki yako, mwandani wako, msiri wako, familia yako, nk. Ndivyo hivyo hivyo inavyotakiwa kwa mwanamke dhidi ya mume wake. Mapasword ni ya nini kwenye simu? Huoni kwa kitendo cha nyinyi kuishi na hizo password za simu ni kiashiria kimojawapo cha kukosa kuaminiana baina yenu? Kwa nini msiwe na maisha ya uwazi! No passwords, no secrets.

Kwa mfano wewe na hiyo familia yako mnachat mambo gani ya siri ambayo mke wako hatakiwi kuyajua? Halafu kama ulikuwa hujui, ukishaoa familia yako ni mke na watoto. Hiyo familia nyingine, marafiki, michepuko, nk hutakiwi kuipa uspesho uliopitiliza. Ukifanya hivyo familia yako halisi itakosa utulivu.
Well said brother lakini tukubali kabisa kuwa si kila kitu tunashea na wake zetu. Wewe mkeo unamweleza kila kitu? Huna hata jambo moja ambalo hapaswi kujua?
 
Utamuua.....usifanye hivyo ! Huyo alipofikia hajiamini ....ukimpiga tukio atapata stroke huko.....itakuwa shida zaidi kwako.....nenda nae taratibu....kama unaweza mpige mimba awe busy au mtafutie shughuli awe busy but pia usimuache free sana maana akigundua kitu atakulipizia kisasi kwa kugawa nje....hatari sana akienda nje na stress .....ataanza kuhonga huko.....
Sure bro kama ni stroke anaweza kupata kwa kweli kwa sababu huyu mwanamke kama kunipenda nahisi ananipenda. Ila hii tabia ya kuchunguza simu, asee siipendi, ananikera mno.
 
Wanasrma "Ukiona mtu anakuchunguza sana ujue anakusaliti.

Inaonesha unamuonesha tabia za kisaliti saliti ambazo yeye anazijua Kwa sababu anazo sema wewe haumchunguzi.
 
Jamani nimeongea mpaka nimechoka. Huyu mwanamke anachunguza simu yangu kuliko maelezo. Kila nikibadili password anayo. Ananiangalia kwa makini anamemorize kisha anakuja kufungua simu kuchunguza. Yaani kwa kifupi nipo uchi.

Kama mnavyojua sasa hivi simu ndio kila kitu. Yaani ninachochat na marafiki zangu, account zangu za bank, ninayowasiliana na wazazi wangu, masuala ya kazini. Jamani yaani ni kila kitu. Niliweka app ya kumpiga picha akitoa password na imemkamata mara kibao.

Anachimba mpaka message za messenger, mpaka deleted messages anazifukua, mpaka zile locked messages za whatsapp anazo. Anachukua namba za watu anawapigia a. Tunachat masuala ya siri ya kifamilia kumbe yote anayajua ananichora tu.

Nimekuwa nikibadili password kila siku lakini wapi. Hii tabia kwa kweli inanikera sana na nashindwa la kufanya. Plz nishaurini.
We wa wapi?
Km una mambo yako na hutaki kupekuliwa au usumbufu wenzio huwa wanakua na cm ndogo inayoachwa ofisini au kwenye ye gari....😃😁

Halafu ya home huweki password unaiacha hapo ahangaike nayo ...
Km una mambo yako hakikisha unapoenda home mnaagana kabisa na watu wako na unafuta kila kitu mpk recycle bin then acha hapo
Akague mpk achoke
 
Back
Top Bottom