Mke wa Mrisho Gambo aondolewa uafisa elimu

Mke wa Mrisho Gambo aondolewa uafisa elimu

Kwa miongozo ya utumishi wa umma,Mtumishi wa umma kama mwalimu haifai kujiingiza kwenye siasa, kama huyo mke wa Gambo angetaka kugombea ubunge ama udiwani basi anapaswa kuandikia barua mkurugenzi apewe likizo bila malipo single kwenye siasa sio kukurupuka kupanda majukwaani namna ile.
Kwan amekwambia anataka kugombea?
 
Heshima sana wanajamvi,

Vita ya ubunge Arusha baina ya Gambo na Makonda vyazidi kupamba moto.

Mkutano wa Mbunge Gambo Soko Kuu Arusha ambao kwa kiasi kikubwa ulitumika kumnanga Makonda umeanza kuzaa matunda.

Mke wa Gambo Afisa elimu alipanda jukwaa na kumtetea mume wake Gambo.

Kitendo hicho kilimkasirisha Makonda ambaye ni Mkuu wa Mkoa Arusha alitumia mamlaka ya kumwondosha Mke wa Gambo katika nafasi ya Afisa Elimu.

Mke wa Gambo sasa ni Mwalimu wa kawaida na ameshapangiwa vipindi vya kufundisha na vifaa vyote muhimu ikiwemo chaki,fimbo & kifutio cha kufuta ubao.

Ngongo kwasasa Monduli.
Waliwapiga vita wapinzani, sasa vita imebaki baina yao wenyewe kwa wenyewe
 
Hilo katazo linahusu kujihusisha na siasa ,maana yake ni pana sio kugombea tuu,yeye kajihusisha na siasa tena waziwazi majukwaani, ulitegemea serikali imchukulie hatua gani
Yuko tu upande wa hasara...
Angemsifu mama!??

Walimu wanatumika na wanasiasa daily.. pamoja na wanafunzi wao.
 
Kwa hiyo alipopanda cheo aliambiwa atakaa hapo milele ??

afisa elim ni cheo Cha ujukuu wa kwanza kwamba ukikipata hakiondoki milele ???
 
Nitafurahi kama wakirogana au wakiuana kabisa itakua vizuri zaidi
 
Kwa miongozo ya utumishi wa umma,Mtumishi wa umma kama mwalimu haifai kujiingiza kwenye siasa, kama huyo mke wa Gambo angetaka kugombea ubunge ama udiwani basi anapaswa kuandikia barua mkurugenzi apewe likizo bila malipo single kwenye siasa sio kukurupuka kupanda majukwaani namna ile.
Hivi zile pesa walizochangishana walimu kwa ajili ya kumchukulia mama fomu ya kugombea zimerudishwa?
 
Yuko tu upande wa hasara...
Angemsifu mama!??

Walimu wanatumika na wanasiasa daily.. pamoja na wanafunzi wao.

Reference or citation mkuu .

Ni mwalim gan ulimwona mda wa kazi yupo jukwaani akimsifu mama wakat kaacha vipindi huko ?
Na jukwaa hilo lilikuwa ktk tukio gani ?

Usije ukatamka walim walozungumza siku ya mei mosi , au walim walozungumza kwenye shughuri yoyote ya kiserikali as walikuepo hapo kwasababu za kikazi na kwa utaratibu,

Matharan siku husika watoto wa halmashauri husika walisimamishiwa masomo ili walim washiriki tukio husika.

Sasa MKE wa huyo Jama alitumia masa Saba kwenye mkutano ambao haikua wa kiserikali, Bali ilikuwa ni wakifamilia. That's childish.
 
kwani huyo mama aliomba kazi ya ualimu au uafisa elimu mambo mengine ni ujinga ujinga tu huyo makonda ni mshamba kwahiyo anaona amemkomoa siyo!
Mkuu sio kumkomoa uyu mama amedandia mtumbwi wa vibwengo hii vita haimuhusu hata kidogo yeye afanye mambo yake sio kuingilia vagi lisilo muhusu watu wenye mamlaka sio wa kushindana nao wana uwezo wa kutumia mamlaka yao na kukuaribia ugali wako wacha ashike chaki akili imkae sawa
 
Inawezekana Afisa Elimu alifanya kosa. Ila kwa hali ya ugomvi ya mumewe na RC inawezekana ikaonekana ni kulipishana visasi.

Kwenye makaratasi inatakiwa mbunge awe na mamlaka kumzidi RC ila huko field mbunge ni mnyonge sana kwa RC
 
Utumishi wa uma ni bureaucracy, mtu mmoja hapaswi kutoa maaumizi jumuishi ya taasisi nzima!
 
Back
Top Bottom