Mke aolewa na jirani baada ya mumewe Kupooza

MR LINKO

JF-Expert Member
Aug 20, 2016
3,034
3,480
Wakaazi wa kijiji kimoja nchini Zambia wameachwa na mshangao baada ya mwanamke kuolewa na jirani yake wa karibu wakati mume wake wa miaka mingi mumewe alipooza Rabison Mawere kutoka mtaa wa Mtendere mjini Lusaka alisema aligundulika kuwa na ugonjwa ambao ulimuandamana Oktoba 2021.

Akizungumza na ABN TV ya Zambia, Mawere alisema alishtuka na kuhuzunika baada ya hali yake kuwa mbaya na mpenzi wake wa siku nyingi kumtoroka na kuhamia kwa jirani. Kulingana naye, maisha yamekuwa magumu tangu alipougua, na kunazo siku ambazo analala bila kula chochote,

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 51 pia alilalamika kuhusu kuruhusiwa kutoka hospitalini licha ya kuwa bado ni mgonjwa.

Kulingana na rafiki yake, Mawere William ameteseka kwa muda mrefu na hatua ya mkewe kumtelekeza iliongeza chumvi kwenye jeraha hilo. Jamaa anawalilia Wasamaria Wema kujitokeza kumsaidia katika kulipa gharama ya hospitali, chakula, na malazi.
 
Hiki kiapo ni kigumu,"Tutakuwa pamoja kwenye milima na mabonde''! Huwa kinaishia pale pale Kanisa.
 
Back
Top Bottom