Frank I Ritte
JF-Expert Member
- Apr 12, 2023
- 1,005
- 1,317
Ona ulivyo mtumwa hoja ni mkataba mbovu DPWorld na si mwarabu.Pole sana
Karibu Mwarabu
Ona ulivyo mtumwa hoja ni mkataba mbovu DPWorld na si mwarabu.Pole sana
Karibu Mwarabu
Usinilazimishe kuwa mzalendo, siutaki uzalendoMsiba huu yaani mtu hajui hata maana ya uzalendo!
Haya bibie nenda kawape siyo kondoo tu wape na vyote watakavyotaka.Kumbuka wewe ni kijakazi wao na kazi yako ni kutii kwa kila kitu watakacjokuomba maboss wako.Naenda kuwapokea mabosi wewe.
Lazima waje na mitandio na maabaya ya kijakazi wao.
Hivi nshawafunikia kondoo wawili ardhini, wakifika wanawafukuwa wenyewe.
Unaijuwa mandi wewe? Raha yake iliwe ya moto moto.
Cheza na kijakazi cha wenye Dirham zao wewe?
Basi andamanaOna ulivyo mtumwa hoja ni mkataba mbovu DPWorld na si mwarabu.
Hapana ukichoka kupaza sauti wewe,wengine bado wataendelea kupaza mpaka kieleweke.Pumzika tu na ugonge cheers ukimaliza mapumziko,karibu tena tuendelee kupaza sauti zetu.Inaweza kuwa fiction au non-fiction. Ukizingatia solid evidence hakuna, tukutane kwy roundtable kugonga cheers ku enjoy siku ya leo, ya nini kujichosha na siasa za kusadikika?!
Tutafute hela za kuhudumia familia zetu, kelele tumeshapaza, kama hawajasikia tufanyaje?!
Kwamba DPW akichukua ndiyo mizigo haitapita au itaathiri kazi zingine?
Kwa maelezo ni kuwa itasaidia kuongeza wafanyakazi hadi 71,000
Tatizo mtego alioutega bwana yule,hakujua kama siku moja angenasa mwenyewe,alivuruga utaratibu wa kuwapata wabunge,akawapata anaowataka yeye.Hili limenishangaza, kunishtua na kukatisha tamaa kabisa.
Nilikuwa na mazungumzo na wabunge wawili, mmoja ni mwanasheria, tena mzuri sana kwenye mambo ya corporate, akiwa amesoma miongoni mwa vyuo vikubwa na bora kabisa Duniani. Na mwingine alikuwa Naibu Waziri, kwa sasa yupo nje ya Baraza.
Hoja kubwa ilikuwa mjadala wa bandari, majibu yao, mmoja alisema hivi:
"hivi bwana ..........., unaamini, mimi na akili yangu, naweza kuunga mkono mkataba kama ule? Watu wanasema tu huko nje, hawajui kilichopo huku ndani. Ukiwa huku, unakuwa ni kama mtumwa. Tumeitwa kwenye kikao cha chama, tena tukaambiwa ni maelekezo. Bungeni pale kuna wachache, tena wale watu wao waliowekwa sawa, ndio waliokuwa wanaongea. Nakuhakikishia, wote ambao hatukuongea, kila mmoja alikuwa hataki, lakini kwa salama yako, unaamua kukaa kimya. Hawa watu wamejipanga hasa, na kila siku wanaoonekana ni kisiki mahali popote, wanaondolewa".
Mwingine aliyewahi kuwa naibu waziri, akasema:
"Wengine tumeondolewa, kwa sababu ya kuhisiwa tu kuwa tunaweza tusiunge mkono kila kitu. Tukawekwa pembeni. Na hapa, kwa hawa watu, si ajabu sisi wengine mwaka 2025, tukaondolewa kabisa hata kwenye ubunge. Na wakiwa wenyewe kabisa, itakuwa mbaya zaidi, maana hatutajua kabisa wanayopanga, hata wanayofanya. Kwa hiyo kwa namna fulani, ni afadhali hata ubakie kinafikinafiki, angalao tufahamu wanachofanya. Shida pia, ni wananchi wetu. Sisi tunapozitoa taarifa hizi, kuvujisha siri, tunatarajia wananchi waamke, lakini wananchi nao inakuwa kimya. Sasa ukiwa kimbelembele, upo pekee yako, nyuma yako hakuna watu, utafika wapi? Kwa kweli tumekwisha. Sasa hivi kila mahali wanapachikwa watu wao ili wapitishe haya. Na hao waarabu wanazidi kumiminika, wanapewa kila kitu, ukitazama mikataba yao, inatisha"
Walisema mengi, mpaka nashindwa kuelewa hii nchi kama hali ni hii, mwanga uko wapi?
Wananchi wanataka wabunge wafanye kitu kwa maslahi ya nchi na umma, wabunge nao wanatarajia wananchi ndio wafanye kitu kuiondoa nchi kwenye mkwamo, nao wananchi hawafanyi chochote. Na kama hali ni hiyo, sasa bunge ni la kazi gani?
Jamani, tupambane tupate katiba mpya lakini katiba yenyewe nayo tutaipataje wakati sisi sote ni waoga? Hata ikipatikana katiba mpya, wakiamua kutokuifuata, na watu tukawa waoga kuwawajibisha viongozi wanaoikiuka, itakuwa na msaada mkubwa? Uoga wetu, umekuwa mtaji mkubwa kwa watawala wenye dhamira mbaya ya kujineemesha wao na jamaa zao.
Katafuteni kazi nyingine bandarini hakuna deal za fasta tasta tena. Mama kanyaga twendeHili jambo ni la kufedhehesha mno ila wahusika wamelingangania tu.
NimekusomaHapana ukichoka kupaza sauti wewe,wengine bado wataendelea kupaza mpaka kieleweke.Pumzika tu na ugonge cheers ukimaliza mapumziko,karibu tena tuendelee kupaza sauti zetu.
Crap. We argue with sound minds.Hii habari yako Ni ya kutunga ,ya uongo na isiyo na ukweli wowote ule Zaid ya kutaka tu kuwadhalilisha waheshimiwa wabunge wetu.
Hakuna ushahidi wala hoja ya kuonyesha ukweli wa hoja yako,unasema waarabu wanaendelea kumiminika hapa nchini pasipo kuweka ushahidi wa namna ya wanavyoingia hapa nchini,hujaeleza wanaingia nchini kwa kufuata sheria au kwa kuvunja Sheria,hujaeleza Ni lini na kwa Tangazo lipi la serikali na la Tarehe ngapi na kupitia Nani lilipiga marufuku wageni wanaokuja kisheria nchini kuingia nchini.
Kwani Ni lini imekuwa jinai kwa mtu kuingia nchini kwa kuwa na vibali vyote na sababu ya kuja nchini? Watanzania wangapi wanasafiri kila Siku kwenda nje ya nchi? Wafanyabiashara wangapi wanaokwenda nje ya mipaka ya nchi? Je sisi watanzania hatutaki wafanyabiashara wa kigeni? Hatutaki wawekezaji wanaokuja kwa kufuata taratibu zote? Hatutaki wawekezaji? Hatutaki bidhàa zetu zipate soko nje ya nchi?
Mbona hujaeleza Kama hao wageni wanaoingia Kama wanavunja Sheria au wanazingatia Sheria? Nani kakwambia kuwa Tanzania haipokei watu wanaotaka kuja Tanzania? Hao wanaokuja ni magaidi? Wateka nyara? Ni majangili? Kama Ni watu wema na wanakuja kwa vihali rasimi kwanini unapata hofu na kusema wanamiminika? Na wanamiminikia wapi hapo ulipowakuta wamejikusanya na unashindwa hata kuwapiga picha au kutoa taarifa yenye ushahidi kuwa wamiminikaji wapo kinyume na sheria nchini
Mbona kipindi Cha corona ambapo baadhi ya nchi ziliposema raia wake wasije nchini kutokana na hofu ya Corona kwanini mlishangilia kwa kukenua meno yenu kuwa tunatengwa na Dunia na uchumi wetu utapolomoka? Kwanini leo wanapoingia kwa kufuata sheria unaanza Tena kulalama? Kwanini iwe nongwa? Kwanini iwe jinai mtu kuja kufanya biashara na Tanzania na kutoa fursa za ajira na kulipa Kodi?
Acheni unafiki wenu na kuandika vihabari vya kuokoteza na kuunga unga kwa maslahi yenu binafsi,Acheni chuki zenu binafsi,acheni kutumika kijinga ,acheni uchonganishi wenu wa kitoto na kijinga,acheni ushamba wenu, acheni kuishi nyuma ya wakati na acheni ukasuku.
Ungekua kweli umefanya kazi nje ya Africa kwa muda wote huo tena kwa position ya managerial usingepinga uwekezaji bandarini kwa sasa.Tatizo huna uelewa. Wenzako hatutafuti ajira mahali popote. Hatua hizo tulikwaishazipita.
Kama nimefanya kazi nje ya bara hili kwa miaka 21 tena kwenye managerial positions, nikaacha kwa kuamua. Nikajenga businesses zangu, nikaajiri watu 300, halafu kwa fikra zako, unadhani nafanya kazi bandarini!! Kweli mmeishiwa fikra. Kwa sababu mnayawaza yaliyo madogo tu.
Mimi kwa sasa nafikiria kulinda utu wangu, utu wa jamii yetu na proud ya nchi yangu. Na pia kufikiria vizazi vyetu vijavyo.
Kwa hiyo umeungana na waizi wa bandari yetu.Usinilazimishe kuwa mzalendo, siutaki uzalendo
Mimi sipingi hata kidogo masuala ya uwekezaji.Ungekua kweli umefanya kazi nje ya Africa kwa muda wote huo tena kwa position ya managerial usingepinga uwekezaji bandarini kwa sasa.
Hujaelewa kinachoendelea sasa.Katafuteni kazi nyingine bandarini hakuna deal za fasta tasta tena. Mama kanyaga twende
Ni ukweli usiopingika wapiga kelele na watetezi wa rasilimali za taifa hawana njaa kama nyie machawa msio na mbele wala nyuma zaidi ya kulipwa 2,0000 day.Wewe ni mjinga
Bandari haikuletei chakula mezani, wala kukulipia umeme au maji.
Fanya kazi
Au kaandamane
Maboresho ya bandari lazima yafanyike acheni uoga.Hujaelewa kinachoendelea sasa.
Itachukua muda kidogo.
Nguruwe hachoki kula, ukiliacha shamba watamaliza mihogo yote.Tafteni jambo jingine la bandari tushachoka.