Mkataba wa Bandari, Wabunge wasema waliburuzwa

Mkataba wa Bandari, Wabunge wasema waliburuzwa

Tafuta maisha kwa ajili ya familia yako, bandari haitakujengea nyumba
Unajua athari ya kiuchumi kwa nchi mpaka kwa mtu mmoja mmoja? Tatizo watu mnaishi kama ng'ombe. Hayo maisha unayoyasema utaishia kuyasikia tu.
 
Iwani walianza leo kuburuzwa?

Watupishe huko, wengine wajukuu zetu washapata wachumba wa Dubai.

Wamekumbuka shuka kumekucha?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] bibi nitafutie na mie mwanaume wa kiarabu basi.
 
Uoga wetu, umekuwa mtaji mkubwa kwa watawala wenye dhamira mbaya ya kujineemesha wao na jamaa zao.
Ulitaka tufanyaje tuingie barabarani na masime au tukapokonye silaha vituo vya polisi tulianzishe ?

404: Page Not Found
 
Mwananchi unataka afanyeje apigwe virungu na police ukiandamana?

Mbunge ana nafasi ya kuwasaidia wananchi akiwa pungeni.
1.Kama atafukuzwa uanachama kwa kusema ukweli ,akiahamia chama kingine wale wananchi watamchagua haraka sana.Tofauti na mwananchi akiandama au akiwa na Domo ataishia kupigwa marungu na police.

Labda sisi wananchi ni kuamka na kumkataa mbungu Fulani wa chama Fulani kupitia Sanduku la kura na kulinda kura

Nasikiaga pale Arusha GLema mwaka 2010 alipelekewa 900,000,000 alipotaka kuzichukua wananchi wakamwambia tunakuua wewe na mkeo na watoto wako.[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] duuuh hatariiiii.
 
Ikumbikwe watakuwa na exemption ktk ulipaji kodi..Nani ataweza kushindana na asielipa kodi?
Hakuna kitu kibaya km hiko asee hivi ni nani alishauri hii kitu iwe hivi hakuona mbele Gari inaenda kupinduka na kulala kifo Cha Mende ?

404: Page Not Found
 
Wewe ni mjinga

Bandari haikuletei chakula mezani, wala kukulipia umeme au maji.

Fanya kazi
Au kaandamane
Chupi uliyovaa alikuuzia yeye na ilipita hapo bandarini na hela uliyompa ndiyo ulipia umeme na maji, hapo utasemaje bandari hamlipii umeme au maji? Au haujui kazi ya bandari kwa taarifa yako bandari ndio hela yenyewe.
 
Hao wanaytaka wawatoe kafara kupitia kwa FFU wa Tanzania.

Hamjaona Kinondoni kisa cha Aquilina? Wamedanya vijana wakauwwa wao hajajitokeza, waejificha mitaro ya Jangwani.

Arusha kule huyu huyu Slaa aliiingia chini ya maspika alivyoona kimbembe cha FFUVijana mitaani wakalambwa virungu wakatupwa central hata dhamana hawakwenda kuwawekea.

Siku ya pili kamwagia bizari na tomsto sosi mashumbusi akavunga eti kapigwa kwemye maandamano. Halafu hajamlipa chke, mwanamke hajakubali, wakaenda Mwanza akamdai pesa zake, mzee kugoma akacheszezea vitasa vya mashumbusi akavunjwa mkono akajidai kateleza bafu hoteli, siku hizo Mwanza hoteli, Mwanza hoteli kuna bafu ya kuteleza pale? Fala sana huyo mzee. Huyo kwa pesa kamuuza mpaka mashumbusi.

Tuulizeni tuliokuwepo enzi hizo tuwarushie picha mjionee, zimo JF humu.
 
Kwamba uliyarikodi hayo mazungumzo uliyonukuu kwa "..." au unauwezo wa kukariri kwa kusikia mara moja tu?
Mkuu umewaza kama mimi.

Humu JF kuna watu wa ajabu sana! Mtu akishaweka alama za kufunga na kufungua semi (quoted and unquoted marks) ina maana anatoa maelezo ya msemaji kama yalivyo bila kuongeza wala kupunguza chochote.

Sasa mtoa mada anadai alikuwa kwenye mazungumzo na hao mabwana 2 aliowaainisha hapo juu, inakuaje aje anukuu kauli zao kama zilivyo kama hakuwarekodi au kuandika mahali? Kwasababu kwa akili ya kawaida huwezi kukariri maneno yao mutatis mutandis.

Nimeshangaa mno. Ila tusibishe sana, pengine aliwarekodi kwa simu au smart watch [emoji28].
 
Hili limenishangaza, kunishtua na kukatisha tamaa kabisa.

Nilikuwa na mazungumzo na wabunge wawili, mmoja ni mwanasheria, tena mzuri sana kwenye mambo ya corporate, akiwa amesoma miongoni mwa vyuo vikubwa na bora kabisa Duniani. Na mwingine alikuwa Naibu Waziri, kwa sasa yupo nje ya Baraza.

Hoja kubwa ilikuwa mjadala wa bandari, majibu yao, mmoja alisema hivi:

"hivi bwana ..........., unaamini, mimi na akili yangu, naweza kuunga mkono mkataba kama ule? Watu wanasema tu huko nje, hawajui kilichopo huku ndani. Ukiwa huku, unakuwa ni kama mtumwa. Tumeitwa kwenye kikao cha chama, tena tukaambiwa ni maelekezo. Bungeni pale kuna wachache, tena wale watu wao waliowekwa sawa, ndio waliokuwa wanaongea. Nakuhakikishia, wote ambao hatukuongea, kila mmoja alikuwa hataki, lakini kwa salama yako, unaamua kukaa kimya. Hawa watu wamejipanga hasa, na kila siku wanaoonekana ni kisiki mahali popote, wanaondolewa".

Mwingine aliyewahi kuwa naibu waziri, akasema:

"Wengine tumeondolewa, kwa sababu ya kuhisiwa tu kuwa tunaweza tusiunge mkono kila kitu. Tukawekwa pembeni. Na hapa, kwa hawa watu, si ajabu sisi wengine mwaka 2025, tukaondolewa kabisa hata kwenye ubunge. Na wakiwa wenyewe kabisa, itakuwa mbaya zaidi, maana hatutajua kabisa wanayopanga, hata wanayofanya. Kwa hiyo kwa namna fulani, ni afadhali hata ubakie kinafikinafiki, angalao tufahamu wanachofanya. Shida pia, ni wananchi wetu. Sisi tunapozitoa taarifa hizi, kuvujisha siri, tunatarajia wananchi waamke, lakini wananchi nao inakuwa kimya. Sasa ukiwa kimbelembele, upo pekee yako, nyuma yako hakuna watu, utafika wapi? Kwa kweli tumekwisha. Sasa hivi kila mahali wanapachikwa watu wao ili wapitishe haya. Na hao waarabu wanazidi kumiminika, wanapewa kila kitu, ukitazama mikataba yao, inatisha"

Walisema mengi, mpaka nashindwa kuelewa hii nchi kama hali ni hii, mwanga uko wapi?

Wananchi wanataka wabunge wafanye kitu kwa maslahi ya nchi na umma, wabunge nao wanatarajia wananchi ndio wafanye kitu kuiondoa nchi kwenye mkwamo, nao wananchi hawafanyi chochote. Na kama hali ni hiyo, sasa bunge ni la kazi gani?

Jamani, tupambane tupate katiba mpya lakini katiba yenyewe nayo tutaipataje wakati sisi sote ni waoga? Hata ikipatikana katiba mpya, wakiamua kutokuifuata, na watu tukawa waoga kuwawajibisha viongozi wanaoikiuka, itakuwa na msaada mkubwa? Uoga wetu, umekuwa mtaji mkubwa kwa watawala wenye dhamira mbaya ya kujineemesha wao na jamaa zao.
Hao Wabunge ulioongea nao ni wachumia tumbo tu! Iweje msomi uache akili yako ikamatwe na mtu mwingine? Kwa nini wasiungane kwa wingi wao na kukataa? Kwani walishikiwa bunduki? Mtu anadiliki kusema heri uwe mnafiki!!!? Mbunge anakuwa mnafiki kwa watu waliomtuma bungeni! Tufwile nyambala!!!
 
Back
Top Bottom