Mkataba wa Bandari, Wabunge wasema waliburuzwa

Tafuta maisha kwa ajili ya familia yako, bandari haitakujengea nyumba
Kwani siku zote ni wewe ndiyo umekuwa ukimuelekeza jinsi ya kuyatafuta hayo maisha kwa ajili ya familia yake au mmekutana hapa JF tena kwa fake IDs? Tuvumiliane hata kama tuna mitazamo kinzani,wewe toa hoja achana na vimipasho visivyo na maana sana.
 
Hili limenishangaza, kunishtua na kukatisha tamaa kabisa.

Nilikuwa na mazungumzo na wabunge wawili, mmoja ni mwanasheria, tena mzuri sana kwenye mambo ya corporate, akiwa amesoma miongoni mwa vyuo vikubwa na bora kabisa Duniani. Na mwingine alikuwa Naibu Waziri, kwa sasa yupo nje ya Baraza.

Hoja kubwa ilikuwa mjadala wa bandari, majibu yao, mmoja alisema hivi:

"hivi bwana ..........., unaamini, mimi na akili yangu, naweza kuunga mkono mkataba kama ule? Watu wanasema tu huko nje, hawajui kilichopo huku ndani. Ukiwa huku, unakuwa ni kama mtumwa. Tumeitwa kwenye kikao cha chama, tena tukaambiwa ni maelekezo. Bungeni pale kuna wachache, tena wale watu wao waliowekwa sawa, ndio waliokuwa wanaongea. Nakuhakikishia, wote ambao hatukuongea, kila mmoja alikuwa hataki, lakini kwa salama yako, unaamua kukaa kimya. Hawa watu wamejipanga hasa, na kila siku wanaoonekana ni kisiki mahali popote, wanaondolewa".

Mwingine aliyewahi kuwa naibu waziri, akasema:

"Wengine tumeondolewa, kwa sababu ya kuhisiwa tu kuwa tunaweza tusiunge mkono kila kitu. Tukawekwa pembeni. Na hapa, kwa hawa watu, si ajabu sisi wengine mwaka 2025, tukaondolewa kabisa hata kwenye ubunge. Na wakiwa wenyewe kabisa, itakuwa mbaya zaidi, maana hatutajua kabisa wanayopanga, hata wanayofanya. Kwa hiyo kwa namna fulani, ni afadhali hata ubakie kinafikinafiki, angalao tufahamu wanachofanya. Shida pia, ni wananchi wetu. Sisi tunapozitoa taarifa hizi, kuvujisha siri, tunatarajia wananchi waamke, lakini wananchi nao inakuwa kimya. Sasa ukiwa kimbelembele, upo pekee yako, nyuma yako hakuna watu, utafika wapi? Kwa kweli tumekwisha. Sasa hivi kila mahali wanapachikwa watu wao ili wapitishe haya. Na hao waarabu wanazidi kumiminika, wanapewa kila kitu, ukitazama mikataba yao, inatisha"

Walisema mengi, mpaka nashindwa kuelewa hii nchi kama hali ni hii, mwanga uko wapi?

Wananchi wanataka wabunge wafanye kitu kwa maslahi ya nchi na umma, wabunge nao wanatarajia wananchi ndio wafanye kitu kuiondoa nchi kwenye mkwamo, nao wananchi hawafanyi chochote. Na kama hali ni hiyo, sasa bunge ni la kazi gani?

Jamani, tupambane tupate katiba mpya lakini katiba yenyewe nayo tutaipataje wakati sisi sote ni waoga? Hata ikipatikana katiba mpya, wakiamua kutokuifuata, na watu tukawa waoga kuwawajibisha viongozi wanaoikiuka, itakuwa na msaada mkubwa? Uoga wetu, umekuwa mtaji mkubwa kwa watawala wenye dhamira mbaya ya kujineemesha wao na jamaa zao.
Hao ni wapuuzi
 
We bandari imewahi kukuletea chakula mezani?

Labda haikuletei ww ila watu wana ajira direct au indirect hapo bandari, wanapitisha mizigo ya biashara zao , wengine wana biashara ambazo ji tegemezi kwa familia na ziko direct feed na bandari ,if they dont go to bandari hamna chakula nyumbani, So hoja yako haina credibility
Just because ww haikugusi haimaanish wengine haziwagusi
 
Huyu ni miongoni mwa uvccm tegemezi, si kwamba hajui akisemacho anajua vizuri tu ila kwa kuwa njaa inamsumbua hana namna nyingine zaidi ya kuabudu miungu watu ili mkono uende kinywani.
 
Labda haikuletei ww ila watu wana ajira direct au indirect hapo bandari, wanapitisha mizigo ya biashara zao , wengine wana biashara ambazo ji tegemezi kwa familia na ziko direct feed na bandari ,if they dont go to bandari hamna chakula nyumbani, So hoja yako haina credibility
Just because ww haikugusi haimaanish wengine haziwagusi
Kwamba DPW akichukua ndiyo mizigo haitapita au itaathiri kazi zingine?

Kwa maelezo ni kuwa itasaidia kuongeza wafanyakazi hadi 71,000
 
Wewe nawe unaona una uwezo wa kumfundisha mtu. Hivi wewe kwako nyumba unaona ni kitu kikubwa sana? Hayo maisha wenzako tulikwishapita zamani sana. Kwa sasa tunafikiria maisha ya watu wengine na vizazi vijavyo.
Kaandamane kuliko kupiga kelele kila siku
 
Hili limenishangaza, kunishtua na kukatisha tamaa kabisa.

Nilikuwa na mazungumzo na wabunge wawili, mmoja ni mwanasheria, tena mzuri sana kwenye mambo ya corporate, akiwa amesoma miongoni mwa vyuo vikubwa na bora kabisa Duniani. Na mwingine alikuwa Naibu Waziri, kwa sasa yupo nje ya Baraza.

Hoja kubwa ilikuwa mjadala wa bandari, majibu yao, mmoja alisema hivi:

"hivi bwana ..........., unaamini, mimi na akili yangu, naweza kuunga mkono mkataba kama ule? Watu wanasema tu huko nje, hawajui kilichopo huku ndani. Ukiwa huku, unakuwa ni kama mtumwa. Tumeitwa kwenye kikao cha chama, tena tukaambiwa ni maelekezo. Bungeni pale kuna wachache, tena wale watu wao waliowekwa sawa, ndio waliokuwa wanaongea. Nakuhakikishia, wote ambao hatukuongea, kila mmoja alikuwa hataki, lakini kwa salama yako, unaamua kukaa kimya. Hawa watu wamejipanga hasa, na kila siku wanaoonekana ni kisiki mahali popote, wanaondolewa".

Mwingine aliyewahi kuwa naibu waziri, akasema:

"Wengine tumeondolewa, kwa sababu ya kuhisiwa tu kuwa tunaweza tusiunge mkono kila kitu. Tukawekwa pembeni. Na hapa, kwa hawa watu, si ajabu sisi wengine mwaka 2025, tukaondolewa kabisa hata kwenye ubunge. Na wakiwa wenyewe kabisa, itakuwa mbaya zaidi, maana hatutajua kabisa wanayopanga, hata wanayofanya. Kwa hiyo kwa namna fulani, ni afadhali hata ubakie kinafikinafiki, angalao tufahamu wanachofanya. Shida pia, ni wananchi wetu. Sisi tunapozitoa taarifa hizi, kuvujisha siri, tunatarajia wananchi waamke, lakini wananchi nao inakuwa kimya. Sasa ukiwa kimbelembele, upo pekee yako, nyuma yako hakuna watu, utafika wapi? Kwa kweli tumekwisha. Sasa hivi kila mahali wanapachikwa watu wao ili wapitishe haya. Na hao waarabu wanazidi kumiminika, wanapewa kila kitu, ukitazama mikataba yao, inatisha"

Walisema mengi, mpaka nashindwa kuelewa hii nchi kama hali ni hii, mwanga uko wapi?

Wananchi wanataka wabunge wafanye kitu kwa maslahi ya nchi na umma, wabunge nao wanatarajia wananchi ndio wafanye kitu kuiondoa nchi kwenye mkwamo, nao wananchi hawafanyi chochote. Na kama hali ni hiyo, sasa bunge ni la kazi gani?

Jamani, tupambane tupate katiba mpya lakini katiba yenyewe nayo tutaipataje wakati sisi sote ni waoga? Hata ikipatikana katiba mpya, wakiamua kutokuifuata, na watu tukawa waoga kuwawajibisha viongozi wanaoikiuka, itakuwa na msaada mkubwa? Uoga wetu, umekuwa mtaji mkubwa kwa watawala wenye dhamira mbaya ya kujineemesha wao na jamaa zao.
Ni hatari sana aisee 🙄
 
Naona una mihemkoya DPW mpaka unakosea kuandika, rekebisha basi comment yako ili ueleweke.
Mihemko kawaida hiyo, nataka kuwahi eyapoti Emirates ya kutokea Dubai inaingia saa nane mchana.

Wageni wenye Dirham zao wasiwahiwe na wachaga huko.
 
Back
Top Bottom