Mkapa: Kuna mtu kanizomea? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa: Kuna mtu kanizomea?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Prodigal Son, Feb 17, 2010.

 1. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 971
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  RAIS mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, amesema, hakuna Mtanzania anayeweza kudiriki kumzomea kwa kuwa rekodi ya utendaji wake kitaifa na kimataifa inaendelea kumlinda.

  Mkapa amelakiwa kwa kishindo katika ziara ya siku moja wilayani Kilolo mkoani Iringa.

  “Mmeona mapokezi yangu, kuna mtu yeyote amenizomea? Sijifichi na wala sikimbii kuzomewa, mimi niko ‘busy’ sana na shughuli za kimataifa baada ya kumaliza utumishi wangu serikalini,” amesema Mkapa.

  Ameyasema hayo jana alipozungumza na wadau wanaonufaika na taasisi yake ya Benjamin William Mkapa HIV/AIDS Foundation wilayani hapa.

  Alizungumza wakati wa majadiliano kuhusu hali ya Ukimwi nchini yaliyofanyika katika Ukumbi wa Hospitali Teule ya Wilaya hiyo iliyopo Ilula.

  Mkapa amesema, baada ya kumaliza urais wake amekuwa akijihusisha na shughuli mbalimbali za kimataifa zinazomfanya awe safarini muda mwingi akishughulikia uhusiano na ushirikiano baina ya Tanzania na nchi nyingine; mambo yanayohusu kumbukumbu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na kuimarisha taasisi yake ili ishiriki vizuri zaidi katika mapambano ya Ukimwi unaotishia ustawi wa watu na taifa.

  Amesema, wanaoishi na Virusi Vinavyosababisha Ukimwi (VVU) ni sehemu ya mapambano ya Ukimwi na hivyo wasiwe na hofu,wajiamini na waape kuishi maisha kama wengine.

  Mkapa amesema, nchi inayoendelea ambayo nguvu kazi yake inapungua siku hadi siku kutokana na janga hilo, itakuwa ndoto kwake kupiga hatua za maendeleo.

  “Ili tupambane vizuri na janga hili ni lazima tuwe tayari sasa kama nchi kubeba sehemu ya mzigo wa mapambano unaobebwa na wafadhili mbalimbali duniani kwasababu itafika siku watachoka,” amesema Mkapa.


  CHANZO: Habari Leo
   
 2. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 971
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  Nadhani jibu lipo moyoni mwako kwani kama ulikuwa unasubiri mpaka Jamii ikuzomee ilikhali wajua kabisaa uliyofanya chini ya utawala wako kudidimiza jamii hiyo hiyo, naamini iposiku huyo anayetoa hukumu ya haki bila upendeleo atalidhihirisha hilo mbele ya umma, Jamii ambayo imezingwa na umaskini, ukosefu wa elimu itakuzomeaje?
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,263
  Trophy Points: 280
  Huyu anaonyesha alivyo na upungufu mkubwa wa kupambanua mambo. Yeye anasubiri Watanzania mpaka wamzomee ndiyo aamini kwamba utendaji wake ulijaa ufisadi wa kutisha.

  Kahusika na kufanya biasha Ikulu hadi leo hajatwambia Watanzania biashara hiyo alifanya na nani na ilikuwa ni biashara ya nini. Alilazimisha kununua Rada ambayo sasa imejulikana kwamba ununuzi ule ulijaa ufisadi wa hali ya juu.

  Alilazimisha kuwaingiza makaburu wa Net Group Problems pale TANESCO pamoja na Watanzania kuwapinga na hakuna chochote walichokifanya pamoja na kulipwa mabilioni.

  Miezi michache kabla ya kumaliza muda wake mabilioni chungu nzima yalichotwa kupitia EPA, Meremeta na Mwananchi Gold. Alilazimisha kuuza nyumba za Serikali kwa bei ya kutupa uamuzi ambao umeliingizia Taifa hasara ya shilingi bilioni 200.

  Alilazimisha kununua ndege ya Rais kupitia yule yule wakala wa Rada akiwa amebakisha miezi mitatu tu kumaliza awamu yake na ndege yenyewe sasa hivi iko juu ya mawe.

  Alisaini mikataba ya kuchimba dhahabu ambayo haina maslahi na nchi yetu ambayo tunaambulia 3% tu ya mapato yote. Aliiba Kiwira yenye thamani ya shilingi bilioni 7 na kujiuzia kwa shilingi milioni 700 na kulipa shilingi 70 milioni tu.

  Kachukua mkopo NSSF wa shilingi bilioni 7 ambao hadi leo hii hajalipa hata senti. Sera zake uwazi na ukweli ilikuwa ni changa la macho tu. Sasa sijui anazungumzia utendaji gani alioufanya ambao unastahili sifa toka kwa Watanzania. Mtu mzima..........
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,489
  Likes Received: 190
  Trophy Points: 160
  Hii inanikumbusha hadithi ya mwizi mmoja ambaye alizoea kuiba usiku. Kuna wakati anaiba alipishana na watu njiani lakini kwa sababu ilikuwa giza hakuwa na hakika kuwa wamemfahamu.

  Sasa wakati wa mchana anapotembea anaangalia kila mtu kuona kama kuna mtu amemtambua kuwa ndiye jamaa aliyekuwa anaiba usiku. Alipofika nyumbani kwake akamwambia mkewe, unaona mimi si mwizi, nimepita mji mzima hakuna hata mtu mmoja ameniita mwizi.
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,387
  Likes Received: 5,753
  Trophy Points: 280
  Jasusi nakubali sana mfano wako!!.....BWM anaogopa kivuli chake haki tena ila moyoni ana siri nzito!!!
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,486
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Hata wakimzomea sauti hazitatoka, maana wana ukata wa kimwili na kiakili. Dhufulkhal.
   
 7. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Umesahau kwamba yeye huyu bwana ni mR Clean? Amechagua kwenda Kilolo kijijini kwa makusudi, unajuaje, labda wanyalukolo kule wanadhani bado nkapa anatawala?
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Feb 18, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo kama wangemzomea ingekuwaje?
   
 9. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #9
  Feb 18, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,078
  Likes Received: 4,451
  Trophy Points: 280
  angesema wavivu wa kufikiri!
   
 10. RR

  RR JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,760
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 160
  Hakuna aliyemzomea....
  Hakuna aliyemuuliza kama alijigawia Kiwira
  Hakuna aliyemuuliza kama yeye sasa ana mali kiasi gani....hakuna!
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,831
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  but he is better kuliko wa sasa
   
 12. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #12
  Feb 18, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 25,557
  Likes Received: 26,528
  Trophy Points: 280
  Kesha kuwa msahaulifu huyu jamaa. Miaka kama miwili iliyopita alishazomewa Dar na vijana kwa kumwita Fisadi! mwizi! na serikali na vyombo vyake vya dola ikaingilia kati kuwasaka wale vijana huku wakisema sio heshima nzuri kuzomea viongozi wakaacha.

  Sasa kasahau na anataka waanze upya? Hasira walizonazo sasa hivi ni kubwa kuliko wakati ule, Kama JK na ulinzi wake alipigwa mawe Mwanjelwa yeye itakuwaje? Asiamshe hasira zilizo lala kwa maneno yake ya kebehi. Yeye ajibu hoja alizozikalia kimya muda mrefu
   
 13. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #13
  Feb 18, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,559
  Likes Received: 1,931
  Trophy Points: 280
  Yaani umesema utafikiri umeusoma moyo wa Mkapa unafikiri nini. Ufisadi unamnyima raha, apende asipende. Rekodi yake kubwa ni wizi na ufisadi utamlindaje?
   
 14. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #14
  Feb 18, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kwa nini amekuwa na ujasiri wa kuuliziaa mmeona nimezomewaa???
   
 15. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #15
  Feb 18, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,434
  Likes Received: 2,089
  Trophy Points: 280
  Kwahili I reserve my comment
   
 16. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #16
  Feb 18, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 10,083
  Likes Received: 3,404
  Trophy Points: 280
  Anajilinganisha yeye na mkulu wa sasa!!!
   
 17. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #17
  Feb 18, 2010
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  The Guy is guilty conscious, it seems he doesn't get sleep for his past deeds
   
 18. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #18
  Feb 18, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Anachekesha, anatumia wananchi wa Kilolo kama ndio kipimo? Apite basi kwenye miji aone dawa yake.

  Yaani sijategemea aseme kitu kama hicho, huyu jamaa pamoja na ufisadi wake na kila kitu huwa na muona kama ana principles flani.
   
 19. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #19
  Feb 18, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160

  Mkapa, anajokes sana, lakini jeuri yake ni kule kulindwa na serikali....
  kuna jamaa waliwahi kumzomea mwaka mmoja nyuma, wakakamatwa na POLICE, Mara hii Ben kasahau, anazeeka sasa, usahaurifu unaongezeka.
   
 20. M

  Mkombozi JF-Expert Member

  #20
  Feb 18, 2010
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 628
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Jamani nimesoma maoni yote ya watu humu, kwa kusema kweli na pia tuache unafiki, Mkapa alifanya kazi kubwa sana ambayo huwezi kulinganisha. Mimi namkubali sana jamaa, ukianzia kuinua mapato ya serekali, hazina ya fedha za kigeni BOT, ubinafsishaji ambao umeongeza ajira, barabara, Uwanja mkuu wa Taifa, Daraja kubwa la Rufiji, utendaji kazi masaa mengi ofisini na safari chache za nje, alipambana na mfumuko wa bei (mkate haba Dar ulikua TShs 150,sasa zaidi ya 700, Unga wa sembe ulikua Tshs 250, sasa 900, Daladala ilikua 150 kwa 50 kwa muda mrefu. Amepunguza madeni ya nje
  Tumwache apumzike jamaa alifanya kazi kubwa Sana, ila hamna mtu ambaye ni Mungu au Malaika asiye na makosa. Kama swala ni kufanya biashara je ni wangapi wanafanya kwa kupitia migongo ya ndugu zao? Si afadhali huyu alifanya mwenyewe? Mimi nakwambia Tanzania ni kubwa sana, kwa hiyo alifanya mambo mazuri sana jamaa.

  Unajua performance ya mtu inabidi uipime kwa kulinganisha na tulikotoka, Mkapa alipokea nchi ikiwa katika hali mbaya sana, vijana walikua hawataki shule, serekali ilikua haina hela, shule ilikua haithaminiki, hospitali dawa kulikua hamna, yeye alipambana kufa na kupona. Vyote tunavyojivunia sasa vimetoka kwenye uongozi wake.
  Swala hapa ni kuchambua kwa upeo wa mpana wa kiuchumi na sio kuleta siasa, unayesema mkapa hakufanya kitu je ni nani aliyefanya? Hamna aliyemsafi 100%

  Wanaoamini biblia, Yesu aliletewa mwanamke moja mzinzi na watu wengi. Ila kwa sheria ya kiyahudi ilimpasa kupigwa mawe hadi kufa. Yesu akawaambia makutano, kwa yeyote anayejiona hana dhambi yeyote awe wa kwanza kumpiga jiwe, Yesu akainama chini akawa anachora kwa kidole chini, hapo alikua anandika amri za Mungu. Aliponyanyua kichwa hakumkuta mtu hata mmoja, na akamwamuru yule mama aende zake na asirudie tena dhambi. Kwa mfano huu, anayejiona hana dhami yeyote awe wa kwanza kumyooshea mkapa kidole.
  Amefanya makubwa sana, tumwache apumzike
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...