Wachangia chupa 53 za Damu Hospitali ya Benjamin Mkapa kusaidia Wagonjwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Katika kusherehekea Kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, leo Januari 12, 2024 watoa huduma za usafi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) wamechangia chupa 53 za damu ili kuwasaidia wagonjwa.
IMG-20240112-WA0086.jpg

Simon Richard, Kiongozi wa wahudumu hao, amesema wanakutana na wahitaji wengi wa damu wanapokuwa wakitekeleza majukumu kila siku Hospitalini.

“Hali hiyo huwa inatuhuzunisha, tukaamua kuhamasishana ili tutoe msaada kwa kuchangia damu” Alisema Simoni.
IMG-20240112-WA0088.jpg

Hatua hiyo imepokelewa kwa furaha na Kucy Kibaja, Mkuu wa kitengo cha Damu salama BMH, akisema kuwa wahudumu hao wameonesha Moyo wa upendo kwa wagonjwa.

“Nimeguswa sana kuona watoa huduma za usafi wakiguswa na mahitaji ya wagonjwa kiasi cha kujitolea damu, ni jambo kubwa na muhimu, ninawashukuru sana” Alisema Kibaja.

Akizungumza baada ya kuchangia, Helena Joseph (37), aliyechangia kwa mara ya kwanza amesema “Ninaona jinsi watu wanavyopata shida kupata damu nikaamua kujitoa” huku Daudi Malongo (32) mchangiaji wa mara kwa mara, akiesema yeye hu changia damu kuokoa maisha ya wengine kwani hajui kesho yake atahitaji nini nani atamsaidia.

Wito umetolewa kwa makundi mbalimbali ya wafanyakazi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa na taasisi nyingine kujitolea kuchangia damu ili kuokoa maisha kwa kuwa damu haitengenezwi wala kuuzwa.
 
Back
Top Bottom