Jamani nimesoma maoni yote ya watu humu, kwa kusema kweli na pia tuache unafiki, Mkapa alifanya kazi kubwa sana ambayo huwezi kulinganisha. Mimi namkubali sana jamaa, ukianzia kuinua mapato ya serekali
, hazina ya fedha za kigeni BOT, ubinafsishaji ambao umeongeza ajira, barabara, Uwanja mkuu wa Taifa, Daraja kubwa la Rufiji, utendaji kazi masaa mengi ofisini na safari chache za nje, alipambana na mfumuko wa bei (mkate haba Dar ulikua TShs 150,sasa zaidi ya 700, Unga wa sembe ulikua Tshs 250, sasa 900, Daladala ilikua 150 kwa 50 kwa muda mrefu. Amepunguza madeni ya nje
Tumwache apumzike jamaa alifanya kazi kubwa Sana, ila hamna mtu ambaye ni Mungu au Malaika asiye na makosa. Kama swala ni kufanya biashara je ni wangapi wanafanya kwa kupitia migongo ya ndugu zao? Si afadhali huyu alifanya mwenyewe? Mimi nakwambia Tanzania ni kubwa sana, kwa hiyo alifanya mambo mazuri sana jamaa.
Unajua performance ya mtu inabidi uipime kwa kulinganisha na tulikotoka, Mkapa alipokea nchi ikiwa katika hali mbaya sana, vijana walikua hawataki shule, serekali ilikua haina hela, shule ilikua haithaminiki, hospitali dawa kulikua hamna, yeye alipambana kufa na kupona. Vyote tunavyojivunia sasa vimetoka kwenye uongozi wake.
Swala hapa ni kuchambua kwa upeo wa mpana wa kiuchumi na sio kuleta siasa, unayesema mkapa hakufanya kitu je ni nani aliyefanya? Hamna aliyemsafi 100%
Wanaoamini biblia, Yesu aliletewa mwanamke moja mzinzi na watu wengi. Ila kwa sheria ya kiyahudi ilimpasa kupigwa mawe hadi kufa. Yesu akawaambia makutano, kwa yeyote anayejiona hana dhambi yeyote awe wa kwanza kumpiga jiwe, Yesu akainama chini akawa anachora kwa kidole chini, hapo alikua anandika amri za Mungu. Aliponyanyua kichwa hakumkuta mtu hata mmoja, na akamwamuru yule mama aende zake na asirudie tena dhambi. Kwa mfano huu, anayejiona hana dhami yeyote awe wa kwanza kumyooshea mkapa kidole.
Amefanya makubwa sana, tumwache apumzike