China yaungana na Afrika katika mapambano dhidi ya UKIMWI kwa kutoa mafunzo kwa wataalamu wa Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG111466238038.jpg

Ikiwa tarehe Mosi Disemba ni siku ya Ukimwi duniani, mbali na kwamba dunia inakumbwa na majanga ya magonjwa mengine lakini janga la Ukimwi bado halijasahauliwa. Nchi mbalimbali zimekuwa na mipango ya kuhakikisha zinatokomeza kabisa ugonjwa huu. Wanasayansi wa sehemu mbalimbali wamekuwa wakikuna vichwa ili kupata chanjo ama hata dawa ya kumaliza janga hili.

China kwa sasa imepata ufanisi mkubwa katika kutibu virusi vya Ukimwi, na kwa mujibu wa ripoti ya viwango vya vifo vya VVU/Ukimwi iliyotolewa na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha China, ufanisi huu umezidi asilimia 90. Kwa upande wa pili kiwango cha vifo vya ugonjwa wa Ukimwi kimepungua kwa kiasi kikubwa, huku makadirio ya muda wa kuishi wa wagonjwa yakiongezeka kwa udhahiri. Mafanikio haya yote hayakuja bure tu, bali yanatokana na kuongezeka kwa hamasa inayotolewa na serikali kwa watu kwenda kupima virusi vya ukimwi pamoja na matokeo ya teknolojia mpya katika matibabu ya Ukimwi.

Juhudi hizi za China katika kuhakikisha inatokomeza ugonjwa huu hatari duniani, hazikuishia ndani ya China tu, bali ziliendelea na kuvuka mabonde, milima na bahari na kufika hadi Afrika. Katika dunia ya utandawazi inayoongezeka kwa kasi mabadiliko ya afya na udhibiti wa magonjwa, jamii ya kimataifa imekuwa mstari wa mbele pia. Hata hivyo ufanisi wa mipango ya afya inayotolewa na jamii ya kimataifa unategemea na ufanisi wa ushirikiano wa kikanda na kimataifa juu ya changamoto na masuala ya afya. Lakini ikiangaliwa kwa ujumla ni kwamba kuna taarifa chache za msingi na ukosefu wa maarifa kuhusu ushirikiano na shughuli za kimataifa zinavyoweza kutumika vizuri kama nyenzo za usimamizi wa afya ya kimataifa na kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Kwa hiyo mipango ya maendeleo ya afya ya China na Afrika, inaonekana kuja kwa wakati muafaka kwani imeweza kushughulikia pengo la utafiti wa afya na la afya ya umma. China imekuwa ikitoa mchango wa moja kwa moja na usio wa moja kwa moja katika juhudi za Afrika za kupambana na VVU/UKIMWI, kifua kikuu na malaria barani humo. Mchango wa China katika Mfuko wa Dunia, ambao ni wa kupambana na magonjwa hatari, ni mojawapo ya maeneo yasiyo ya moja kwa moja ya kusaidia katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI katika bara la Afrika.

Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema VVU vinaendelea kuwa tatizo kubwa la afya ya umma duniani. Na kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na UNAIDS Julai mwaka huu, kuna njia ya wazi ya kuweza kumaliza UKIMWI. Njia hii pia itasaidia nchi kujiandaa na kukabiliana na janga la siku zijazo. Ripoti hiyo imekadiria kuwa katika mwaka 2022, watu milioni 39.0 duniani walikuwa wanaishi na virusi vya Ukimwi, huku watu milioni 1.3 wameambikizwa virusi vya Ukimwi, ambapo Afrika bado linabaki kuwa bara lenye kiwango kikubwa cha watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi.

Pamoja na mchango usio wa moja kwa moja kupitia Mfuko wa Kimataifa, China iliunda ushirikiano mzuri na Umoja wa Afrika wenye wanachama 55, kwa kutoa msaada, ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa wataalam ambao wana jukumu muhimu katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI. Wataalamu hao wamekuja China kupata mafunzo juu ya udhibiti wa VVU.

Tunafahamu kuwa bado maambukizi ya virusi vya Ukimwi ni makubwa katika Afrika, lakini juhudi zinazochukuliwa na bara hili haziwezi kupuuzwa. Tukiangalia mifano michache namna nchi za Afrika zinavyojitahidi kutokomeza ugonjwa huu, nchi kama Botswana imefanikiwa kuondoa kabisa maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Vilevile Rwanda itadhibiti VVU, kama mpango wa Afya ya Umma, kabla ya mwaka 2030.

Jitihada hizi mara nyingi huwa zinakabiliwa na changamoto kadha wa kadha, zikiwezo fedha na usugu wa dawa, huku mifumo ya afya pia ikiingia kwenye changamoto hizi katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI.
 
Back
Top Bottom