The Fixer
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 1,365
- 567
Ndugu zangu wana JF !
Mkapa hamuelewi Kikwete, unaweza ukaona ni kama mchezo flani wa kuigiza lakini ukweli ni kwamba yanaendelea huko nyuma ya pazia ni mazito kuliko yale ambayo tunayaona na kuyasikia hata pale Habari maelezo na hali ni ya kutoaminiana hadi leo hii !
Wakati Rais Kikwete, Anaingia madarakani si kwamba alikuwa mgeni na serikali aliyokuwa anaifanyia kazi na ambayo angekuwa ndio kiongozi wake muda ule alipoingia rasmi kama Rais wa nchi, Hakuwa mgeni alikuwa anayaelewa mambo ya kifisadi yote yaliyokuwa yanaendelea hata kama naye atakuwa ni mmoja wa wahusika kama ambavyo mnyororo unavyoonyesha ! Ili kuendelea na Serikali yake safi na kutoa mambo yote ya kifisadi ambayo Watu wake wa karibu walikuwa wanamweleza kuhusu Mkapa na kama mlivyokuwa mnajua kuwa Kikwete hakua chaguo la Mkapa basi aliamua kuunda kikundi chake cha siri ambacho kilianika mambo yote ya Mkapa na kumletea kila Data za Mkapa na Kikwete akaa nazo !
Katika hali ambayo hata mwenyewe Mkapa alishangaa ni pale ,Alipomuita yule Mama Anna Mkapa siku moja pale Ikulu na kumuonyesha utitiri wa malimbikizo ya mali ambayo yule Mama pamoja ama kwa kutumia cheo cha Mumewe Mkapa aliamua kutumia kila njia na kuikamua nchi ,Ikiwa ni pamoja na sakata zima la makabidhiano la TASAF ! Baada ya Mama Anna Mkapa kukataa kuiacha pale Ikulu ,Kikwete alituma Jamaa wake waifuatilie na kuifumua kwa kuifanyia "ODITING" ya nguvu hadi walipogundua kuwa yule Mama alikwisha kuumaliza ule Mfuko na masurufu yake !
Alipomuita alimuonyesha kila kitu kuhusu TASAF, na yule Mama wa watu akabaki hana la kusema ,kwani aliombwa tu aendelee na safari zake na kumuachia jamaa afikirie namna ya kufanya ! Aliyomuonyesha yalimtoa yule Mama jasho Achilia yale Magorofa ya Kariakoo aliyonayo, wala ile hotel ya Lamada aliyojinyakulia pale Ilala karibu na Msimbazi center, Alionyeshwa ubadhirifu wote alioufanya kwa kutumia cheo cha Mumewe kama Rais.