Katika miaka 17 yote ya uwanja wa Benjamin Mkapa, ni lini umetumika kwa mashindano ya kimataifa ya riadha?

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,246
8,108
Mwaka huu uwanja wa Benjamin Mkapa unatimiza miaka 17 toka kuzinduliwa kwake. Katika kipindi hicho chote uwanja umetumika kwa shughuli nyingi za soka, serikali na dini.

Moja ya eneo muhimu la uwanja ambalo limekuwa na matumizi madogo sana ni "running tracks" au eneo la kukikimbilia kwenye michezo ya riadha/mbio. Katika matengenezo yanayosemekana kufanyika hivi sasa katika uwanja ule, mojawapo ni kutumia pesa nyingi ili kulijenga upya eneo hilo la kukimbilia.

Tunapopima mafanikio ya uwanja ule kwa miaka hii 17, tujiulize pia ni lini Tanzania iliwahi kuwa mwenyeji wa mashindano ya kimataifa ya riadha kwenye uwanja huo?

Nimewahi kushauri tunapojenga viwanja vya soka, tuepuke sana kuweka hizi "running tracks" hasa kama hakuna mipango yoyote iliyo thabiti ya kutumia mara kwa mara kwa mashindano ya riadha yanayoweza kuleta faida za moja kwa moja za kiuchumi maana sehemu zile zinachakaa haraka na gharama zake za kuzitengeneza upya ni kubwa sana.

Kwa nyongeza, soka linanoga sana pale mashabiki wanapokuwa karibu zaidi na sehemu ya kuchezea, yaani pale uwanja unapokuwa hauna "running tracks". Mfano viwanja vingi vya soka kwenye ligi ya Uingereza na Ulaya kwa ujumla havina "running tracks". Ni kama tumekariri hivi kwamba uwanja lazima uwe na sehemu za kukimbilia, au labda zinajengwa mahsusi ili iwe rahisi magari ya viongozi kuingizwa kwenye shughuli za serikali. Ukiangalia viwanja vyote vikubwa nchini vimetengewa sehemu za kukimbilia ila kwa ufahamu wangu ni uwanja wa Mkapa tu ndiyo uliwahi kujengewa "lami" ya kisasa.

Kwa mitazamo hii, sikuona umuhimu wa kuweka "running tracks" kwenye uwanja mpya wa Arusha wakati huu wa Mkapa tumeshindwa kabisa kuzitumia hizo tracks kwa miaka hii yote 17.
 
Viwanja vya club ndio vinapaswa kutokuwa na hizo running tracks... ila kwa Uwanja unaomilikiwa na serikali ni vizuri uwe multpuporse hakuna hasara jui ya hilo ,Mashindano ya Riadha ya kimataifa nakumbuka yalishawahi kufanyika pale kwa mkapa.sikumbuki mwaka ila niliyafuatilia sana kipindi kile
 
Mtoa mada nakukumbusha pamojana kua na mada nzuri ila viwanja unavyolenga sio vya Club ni vya serikali hivyo naona ni sawa kujengwa vile ili kuondoa usumbufu. Umeona Azam complex hauna sehemu ya kukimbili kwa sababu hauna hayo matumizi. Mwisho wahimizwe wenye vilabu watengeneze viwanja vyao.
 
Mwaka huu uwanja wa Benjamin Mkapa unatimiza miaka 17 toka kuzinduliwa kwake. Katika kipindi hicho chote uwanja umetumika kwa shughuli nyingi za soka, serikali na dini.

Moja ya eneo muhimu la uwanja ambalo limekuwa na matumizi madogo sana ni "running tracks" au eneo la kukikimbilia kwenye michezo ya riadha/mbio. Katika matengenezo yanayosemekana kufanyika hivi sasa katika uwanja ule, mojawapo ni kutumia pesa nyingi ili kulijenga upya eneo hilo la kukimbilia.

Tunapopima mafanikio ya uwanja ule kwa miaka hii 17, tujiulize pia ni lini Tanzania iliwahi kuwa mwenyeji wa mashindano ya kimataifa ya riadha kwenye uwanja huo?

Nimewahi kushauri tunapojenga viwanja vya soka, tuepuke sana kuweka hizi "running tracks" hasa kama hakuna mipango yoyote iliyo thabiti ya kutumia mara kwa mara kwa mashindano ya riadha yanayoweza kuleta faida za moja kwa moja za kiuchumi maana sehemu zile zinachakaa haraka na gharama zake za kuzitengeneza upya ni kubwa sana.

Kwa nyongeza, soka linanoga sana pale mashabiki wanapokuwa karibu zaidi na sehemu ya kuchezea, yaani pale uwanja unapokuwa hauna "running tracks". Mfano viwanja vingi vya soka kwenye ligi ya Uingereza na Ulaya kwa ujumla havina "running tracks". Ni kama tumekariri hivi kwamba uwanja lazima uwe na sehemu za kukimbilia, au labda zinajengwa mahsusi ili iwe rahisi magari ya viongozi kuingizwa kwenye shughuli za serikali. Ukiangalia viwanja vyote vikubwa nchini vimetengewa sehemu za kukimbilia ila kwa ufahamu wangu ni uwanja wa Mkapa tu ndiyo uliwahi kujengewa "lami" ya kisasa.

Kwa mitazamo hii, sikuona umuhimu wa kuweka "running tracks" kwenye uwanja mpya wa Arusha wakati huu wa Mkapa tumeshindwa kabisa kuzitumia hizo tracks kwa miaka hii yote 17.
Serikali inajenga viwanja vya olimpiki, kuna mjinga mmoja humu niliwahi kumwambia FIFA huwa inaleta siasa tu kusema serikali isiingilie mpira wakati serikali ndio wenye facility za huo mpira.
 
Tusipoweka running tracks kwenye viwanja vya CCM commodore wetu watavutia wapi magari na kupasua matofali
 
Back
Top Bottom