Mkapa above the law?: Allegations

Nyani Ngabu,

Kwanini Wamrushie Mawe,Kwa kosa gani??hakuna aliye juu ya sheria,kama watanzania tunaona ana kosa basi ttumpeleke Mahakamai ili asurubiwe na sio kumuita Mtu fisadi.

Kosa la kuhatarisha Amani.Mathalani kama wangempiga Risasi Rais mstaafu unaju Madhara yake ni yapi.


Mtuhumiwa wa wizi Jijini apigwa hadi kufa

2008-05-03 16:17:34

Je, polisi waliwashika waliomuua huyo kijana au hawana kazi za kufanya?


From Arusha


Anyway watakuja kusema hawa vijana hawakupigania Uhuru na wanatumiwa na mabeberu wa magharibi yaani UK na USA. Wanawasupport wakolomi.
 

Kamanda umesomeka mkuu

Sasa hivi dunia nzima inaelewa jinsi Mkapa alivyofanya biashara, hata polisi waliowakamata vijana wanajua hilo sasa ngoja wataalamu wa mambo ya sheria waanze kuchambua jinsi Mkapa alivyo vunja sheria na kuangalia uhalali wa vijana kukamatwa.

Hili la Mkapa sasa litakuwa big. ishue ni afadhali vijana wamesaidia hili liweze kujulikana dunia nzima.

Itabidi Mkapa sasa anyimwe viza za kuingia nchi mbali mbali.

Naona Mkapa kwa kutaka yaishe aombe polisi wawaachie hao vijana bila masharti yoyote maana inajulikana kwamba yeye na UFISADI ni kama pete na kidole
 
freedom is not free.
Kama uhuru wa siasa haupatikani bure je wa kiuchumi itakuwaje????
Mafisadi yanatumia na yatatumia nguvu zao zote kujilinda. Uhuru wa uchumi ni mchungu sana na utapatikana kwa jasho la damu.

Hawa vijana kukamatwa inaweza kuwa ni chachu ya uhuru wetu dhidi ya mafisadi. je kama wataaamua kuwashikilia na kuwafikisha mahakamani tutafanya nini? tutaandika tu na kusubiri hukumu?

Nchi nyingi duniani zimebadilishwa na watu wachache walioamua kujitoa mhanga. Mkapa ni fisadi inatupasa kupiga kelele nchi nzima. Sasa wakati umefika kuwaonyesha mafisadi tumechoka na ufisadi wao.

Kazi ya usalama wa taifa sio kulinda mafisadi ni kuwafichua mafisadi, sasa kama wameanza kuwalinda usalama wa taifa ubadilishwe jina uwe ni usalama wa mafisadi. Usalama wa raia sasa ni usalama wa mafisadi.

Wote sasa tupige kelele mkapa fisadi ! mkapa fisadi!.........
 
Nyani Ngabu,

Kwanini Wamrushie Mawe,Kwa kosa gani??hakuna aliye juu ya sheria,kama watanzania tunaona ana kosa basi ttumpeleke Mahakamai ili asurubiwe na sio kumuita Mtu fisadi.

So Mr Gembe, tunapopiga kelele mwizi mwizi mwizi, kwani tunakuwa na maana gani? Sin tuna maana tunataka tumkamate tumtie kibano na tumpekele polisi, then mahakamani and then gerezani? In other words do you think it is not fair to call Mkapa so and fair to call vibaka so, is that right?
 
Naelekea Kufikiri kuwa Huyo Bwana(Ben)keshapewa taarifa ya kilichotokea,na atakuwa keshapiga simu kuwa hao Vijana waachiliwe maramoja!!kwani bila ya kufanya hivyo,hatoishi kwa amani hata kidogo.
Kwasababu leo ni pale kijiweni yametokea hayo,hivi Kesho pale uwanja wa taifa:Anaingia Salmin-"Komando,komando",Mwinyi-"Ruksa,ruksa",Mkapa-"Fisadi,fisadi" Je polisi watamkamata nani,wamwache nani??
 
Ni vizuri Watanzania tukaanza kumzomea Mkapa popote atakapoonekana hadharani kwa ufisadi mkubwa alioufanya halafu hataki kujibu tuhuma zozote dhidi yake. Ikitokea bahati mbaya kukutana na fisadi Mkapa popote pale ulimwenguni sintamsalimia, nimsalimie kwanini? kipi alichokifanya Tanzania mpaka nimsalimie. Watanzania natoa wito hawa mafisadi wote akina Mkapa, Chenge, Lowassa, Msabaha, Karamagi, Mramba, Mkono, Mzindakaya na wengineo popote tukiwaona hadharani tuwazomee kwa ufisadi wao dhidi ya nchi yetu.

Sijui hili litakuwa na matokeo gani, lakini mtu mzima kuzomewa hadharani ni aibu ya hali ya juu.
 
Mkapa ni mwizi sawa na wezi wengine, kama wananchi tunaweza kuwachoma moto vibaka wanaoiba simu ya mkononi ya sh 20,000 sioni sababu kwanini wananchi wasifanye hivyo kwa mkapa ambaye kwa kiasi kikubwa sana ametufikisha sehemu hii mbaya tulipo. ametuibia mali zetu nyingi kwa wimbo wake wa sera ya ubinafisishaji wa mashirika ya uma, migodi, alipoambiwa au kuulizwa na wananchi alisema ni wivu wa kijinga. Hawa watu hakuna haja ya kuwalea tuwazomee, tuwaponde mawe na kuwachoma moto.
 
Haya la mgambo likilia ujue kuna jambo NGUCHIRO HAO WAMETOKA MATUNDUNI MWAO NI MAWE TUUUUUUUU!!!!!!!!





 

aaaaaaaaaaaa.... mshkaji unaniangusha TAJA JINA LA HOTEL WE DARE TO TALK OPENLY
 
Hawa wanawaonea, si mkuu Pinda alishasema majuzi Iringa vijana wasisite kumwita fisadi mtu yeyote anayetafuna mali ya umma! sasa hii imekaaje ina maana hawa Polisi wanakiuka maagizo ya mkuu Pinda?
 
Tuandamane una maananisha "FUSADI au FISADI?? Kama ni Fisadi ni mwizi na mdanganyifu. zaidi ilitumika kwa watu wanaoiba wake za watu..lakini mi naamini mwizi ni mwizi tu bila kuangalia haiba ya mtu na alichoiba... Any more clarification please...
 
Yani mtu ukisema ukweli siku izi unakamatwa???dah!!! sijui tatizo liko wapi wakati jamaa ni fisadi kweli..bora wangesema shooga uyoo'' hapo sawa ingekua uzushi wangeamwatwa kwa ku shout uongo na uzushi lakini sio kwa hili.. ila tuache labda sababu haijathibitishwa na mahakama kama ni fisadi kweli au la
 
He will retain the title no matter what. He did it and he deserve the concequences . He can not rub it through police.Hawa vijana ni symbol tu ya what is pending for him. Akumbuke hii ndio itakuwa alama yake ya maisha yaliyobakia. Aliitaka mwenyewe.Inasemekana 666 ni alama ya mpinga Kristo, na FISADI ni alama ya ant Tanzanianism
 
aaaaaaaaaaaa.... mshkaji unaniangusha TAJA JINA LA HOTEL WE DARE TO TALK OPENLY


Ni kweli hiyo Hotel X iko wapi?
Sema hapa openly tujue.
kuna watu majasiri hap[a wanaweza kufanya kile ambacho wengi wanaogopa kukifanya.
Ukitaka kuondoa UFISADI then ondoa Shina lake
 
Gembe amethibitisha tetesi kuwa JK is behind all of these games against his successor. Ni wazi hii iko planned, tokea msafara wake,Dar leo/aka Majira na hata hao polisi walioshiriki ktk ukamataji. Msafara wa kiongozi mara zote hauna hata hiyo nafasi ya kushuhudia makelele ya hao vijana kutokana na maandalizi yake kwa maana ya njia,spidi n.k, hata huyo mwandishi aliyeripoti pamoja na timu yake ya uzomeaji wametuachia maswali mengi sana. Kwanini tunamuona JK kwa sura mpya ambayo FMES alishawahi iandika hapa na BCS? Inakuwaje watu wa usalama ndio wawe chanzo cha vurugu na zile siasa za kiwango cha chini, huu ni mchezo ambao ipo siku wasipojihadhari wajue ipo siku JK atazomewa tena hakutakuwa na maandalizi ya namna hii tuionayo sasa, nadhani wakubwa hawa wanakokwenda si salama, vita hii ya UFISADI ni vema ikapiganwa kisayansi zaidi kuliko hii style ya mediazation na kukodi wazomeaji, naiona hatari ya kukwama kwetu ikikaribia, je tukishazomea mpaka 2015 then wat? Je wakiingia tusiowatarajia ktk game hii itakuwaje? Tumeshamuona Kakobe akikemea hilo na Marando akitoa picha zaidi ya nne ktk story zake na sasa Jaji Warioba naye ktk namna mupya.

Nadhani wasaa umefika wa sisi waTZ kujitizama kwa kina na tutafakari wenyewe nini hatima yetu.
 

hali halisi ni kwamba kuna wanadamu tanzania hii ukisema tu lowassa fisadi au mkapa fisadi unaweza ukaishia hata kupigwa. na wengi wa hawa binadamu hawajafaidi chochote kutoka kwa hawa mafisadi zaidi ya shida.

Mtu unakaa unajiuliza what else can be done kuonyesha kwamba hawa watu ni waovu na wametumia rasilmali za nchi hii kwa manufaa yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…