Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 65
vijana wa kileo wamekuwa hawana adabu.
huo ndio ukweli na tukishindwa kukaza kamba kwenye malezi taifa litaelekea kubaya
Vipi kama walikuwa wanamzomea mmoja wa aliyekuwapo kwenye msafara na sio Mheshimiwa Mkapa?
Nyani Ngabu,
Sikuhizi hapa Mbagala vijana humtania kila anayeendesha gari la thamani kama GX, VX etc kuwa ni FISADI. - ni utani tu.
Je unajuaje hakuwepo mtu wa aina hiyo jirani kapaki?
Wanajuaje kama haikuwa coincedence tu?
Kosa la kuhatarisha Amani.Mathalani kama wangempiga Risasi Rais mstaafu unaju Madhara yake ni yapi.
Mzee Mwanakijiji said:a. Kama walikuwa kwenye msafara wakaona watu wanapiga kelele "Fisadi" "Fisadi" wanapoteremka na kufanya msako, wanajuaje walioawakamata NDIYO waliosema "fisadi"?
b. Je kama vijana hawa wangesimama na kupiga kelele "Mtukufu" "Mtukufu" ni hatua gani wangechukuliwa au zawadi gani wangepewa?
c. Uhuru wa maoni ni pamoja na uhuru wa maoni ya kijinga. Katiba haisemi mahali popote kuwa maoni yatakayotolewa na wananchi lazima yawe mazuri au yanayopendeza ili yakubaliwe.
d. HIvi wanazojela za kutosha? Maana tukianza hii movement ya "Fisadi" "Fisadi" wataweza kweli kuwasweka watu ndani au watalazimika kutumia njia "kali" zaidi... ?
teh teh teh... ndio ujue vibaraka hawajishughulishi kujua sheria maana wamewekwa na mafisadi!!naomba kuuliza nani ata washtaki wale vijana polisi au mkapa??
msumali wa moto kuonyesha walivyo wapumbavuhao mapolisi wakamkamate basi na Mbunge Aloyce Kimaro
au kama vipi atumie vijisenti vyake kununua chopper/'copter ya kumpingisha misele hapo mjini.......maana inaonekana huu ndio mwanzo tu, watu watazidi kumzomea kila aendako!!
Naomba kuuliza wakuu:
Bara barani wana pita watu wengi na wengine wanakuwa wamekaa au kusimama, Polisi walijuaje kuwa anayezomewa ni Mheshmiwa Mkapa?. Vipi nikisema alikuwa anazomewa kijana mmoja aliyeketi au kusimama upande wa pili wa barabara na sio Mheshmiwa?
Ni kuuliza tu, NISAIDIENI majibu.
au kama vipi atumie vijisenti vyake kununua chopper/'copter ya kumpingisha misele hapo mjini.......maana inaonekana huu ndio mwanzo tu, watu watazidi kumzomea kila aendako!!
Kosa la kuhatarisha Amani.Mathalani kama wangempiga Risasi Rais mstaafu unaju Madhara yake ni yapi.
madhara ni kuwa angekuwa amepigwa risasi! haihitaji utaalamu wa kufikiria madhara ya mtu kupigwa risasi.
But, hatuwezi kuanza kukamata watu kwa mawazo yao. Kwamba labda wangefanya kitu fulani au wangefanya jambo fulani vinginevyo kuna watu wengi wenye mawazo machafu kweli kuhusu viongozi wao.
Hawa wamedaiwa kufanya jambo moja tu na tusianze kurundika possible crimes; wao walisikika wakizomea (even that is questionable) "fisadi"! Ni hilo tu ndilo liwe msingi wa majadiliano yetu kwani kujaribu kuingia kwenye mawazo yao ni kujaribu kufanya lisililowezekana. Walikutwa na silaha? walikutwa na maandishi ya kichochezi?
So far sijaona mahali popote kwamba walikuwa na lengo lolote la kumdhuru Rais mstaafu. Kama wangedaiwa kufanya jambo kama hilo bila ya shaka mimi ningekuwa wa kwanza kulaani vitendo vya kujichukulia sheria mikononi. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na mambo yanaweza kumalizwa kwenye sanduku la kura, mahakamani, au barazani!
Kuna uwezekano mkubwa (ukizingatia uchumi wa Tanzania) mtu anayeendesha GX, VX, etc. kuwa fisadi. Sasa, hata katika ufisadi kuna viwango. Kuna mafisadi wa small scale, medium scale, na kina Mkapa na Chenge ambao hamna hata daraja la kuwaweka. Kwa hiyo sishangai kabisa kwa walalahoi wasukuma mikokoteni, watembea kwa miguu, waendesha baiskeli, na wapiga debe kuwaona waendesha magari ya thamani kuwa ni mafisadi. Disparity iliyopo ni ya ajabu sana kiasi kwamba huwezi kuamini mtumisha wa serikali kuwa tajiri kupindukia.
Halafu kama ni utani kwa nini sasa watu wakamatwe? Na kama walikuwa hawamzomei Mkapa, ina maana na mimi Ngabu nikikuzomea wewe Fikiraduni nitakamatwa? Or in other words siku hizi kuzomea limekuwa kosa linalo-warrant kukamatwa na polisi?
Nyani..huwa hatuonani eye to eye kule kwenye ile "thread nyingine" lakini hapa kaka ume drive point nyumbani. Tatizo ni kwamba Polisi wetu wamezoea ku abuse haki za wananchi, na wananchi japokuwa wameanza kuamka sasa hivi, wengi hawajui haki zao. Watanzania kwa kipindi kirefu tumejengwa kwenye tamaduni za kuwa submissive, obedient, na "shikamoo mzee" towards viongozi wetu. Nafikiri huko kwenye Police Academy wabadilishe curriculum..waanze kuwa train Police kutumia akili zaidi kuliko misuli.
Problem ya kesi kama hii ni kama ile kesi ya waandamanaji Buzwagi 3 weeks ago. Wataswekwa rumande, kupoteza hela za walipa kodi bure, kisha baada ya miezi miwili kuachiwa huru.
What a waste of resources and human rights violation!
you are not serious, are you?vijana wa kileo wamekuwa hawana adabu.
huo ndio ukweli na tukishindwa kukaza kamba kwenye malezi taifa litaelekea kubaya
Kwa anayejua ratiba ya Ben, please nipatieni, na mimi nataka kutia timu kwenye msafara wake nipayuke MKAPA FISADI!
Niende mahakamani ku-prove yeye ni FISADI, vielelezo vyote ninavyo, na yeye (ANBEN) aitwe kuja kukanusha, akisaidiwa na rafikize vijisenti, yona, pesambili, tluway!!