Kitila,
Swali gumu sana hili. Nimekuwa napiga vita swala la polisi kutumiwa na viongozi wa serikali (hata wastaafu) kwa mambo ya ajabu kama haya kwa muda sasa hapa.
Ni makosa makubwa, inaonekana walitaka hao vijana wasifie tu na kupiga vigelegele kuwa mkubwa kapita.
Pambaffff kabisa!
Hata kama Mzee Mkapa ni Mwizi(Hapa mahakama haijaamua) ila jua ya Kwamba bado ni Rasi Mstaafu tu..other thing reamin Constant.
Wewe unadhani kama angepita kiongozi mstaafu wa upinzani watu wakaanza kumzomea,viongozi wa juu wanatembea na mtoto wako huku wakimghasi..Polisi wakikaa kimya unadhani italeta picha nzuri??
Msaada mwingine kwa wanasheria, yapasa kusaidia hao vijana walishitaki Jeshi la vibaraka kwa kuwaweka kizuizini pasi kosa lolote! Wakileta kisingizio cha uzururaji then watuambie wametoa ajira ngapi baada ya kusababisha maisha ya vijijini kuwa magumu?!
Tatizo hivyo vijitu vya usalama na polisi ni kama vijibwa fulani vikipewa amri vinakurupuka tu na kukamata watu sijui ndio shida ya kazi au ujinga waliofundishwa huko wanakofundishwa...Inatakiwa wajue zama za wa-tz kushangilia hata mambo ya kipuuzi zimepita siku nyingi sana nina imani vijana watatoka tu sana watawarusha kichura waseme kama wametumwa au ni wao wenyewe maana mafisadi wengi hawaamini kama wa-tz wameamka...
Ndio malipo ya matendo maovu hayo Mzee Ben.....alijifanya kamanda wa miavuli kudadadeki anatutia mchanga wa macho nadhani leo atagundua angalau kidogo kuwa watu wako serious...
Wananchi wameshaamua. Wamechoshwa na ufisadi. Huwezi kumhemshimu kiongozi aliyekuibia. Angalia yaliyompata Moi shambani kwake baada ya Dec 27. Ilibidi akimbilie Ngurdoto.
Hayo hayo yatampata Mkapa na viongozi wa aina yake, hata kama wanasindikizwa na msururu wa magari mangapi.
Naomba kuuliza wakuu:
Bara barani wana pita watu wengi na wengine wanakuwa wamekaa au kusimama, Polisi walijuaje kuwa anayezomewa ni Mheshmiwa Mkapa?. Vipi nikisema alikuwa anazomewa kijana mmoja aliyeketi au kusimama upande wa pili wa barabara na sio Mheshmiwa?
Ni kuuliza tu, NISAIDIENI majibu.
Naomba kuuliza wakuu:
Bara barani wana pita watu wengi na wengine wanakuwa wamekaa au kusimama, Polisi walijuaje kuwa anayezomewa ni Mheshmiwa Mkapa?. Vipi nikisema alikuwa anazomewa kijana mmoja aliyeketi au kusimama upande wa pili wa barabara na sio Mheshmiwa?
Ni kuuliza tu, NISAIDIENI majibu.
Aaaahhhh!!! Big Ben huo ndio utamu wa utandawazi bwana....Baba ukifanya utumbo ndani ya nyumba kuna siku watoto wako mwenyewe watakuzomea ndio mambo yalivyo...Polisi si just watch dogs ni lazima kuna kibaraka wa huyo fisadi kawapa amri kukamata then kesho hao hao wanalia lia mishahara haitoshi mara nyumba za full suit (bati kila mahali) zina joto kumbe wanaosababisha hali ngumu wanawalinda wenyewe... Bravo na ni mwanzo mzuri message was sent and delivered correctly!!!Poleni vijana ndio gharama za mapambano hizo na sisi tutamzomea hata humu JF...
safi sana hebu ibold hii....Nasikitika kwa yaliyotokea maana ni kinyume kabisa na kauli aliyoitoa RAIS KIKWETE siku chache zilizopita mkoani Singida
namquote "VIONGOZI MSIOGOPE KUITWA MAFISADI...." unaweza kusoma hii thread http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=12939
So vijana waachiwe mara moja kwa kuzingatia kauli halali ya RAIS JK.
Kikwete toa agizo mara moja na wape karipio KALI vijana wa Mwema waache kujikomba.
Vipi kama walikuwa wanamzomea mmoja wa aliyekuwapo kwenye msafara na sio Mheshimiwa Mkapa?