Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Kaka huko serious na hili, hivi anaruhusiwa na sheria kuanzisha kampuni ndani ya ikulu, ofisi takatifu ya nchi yetu, hiyo kampuni aliyoanzisha ilifanya biashara gani, kwanini tenda ya kuuza kiwira haikutangazwa, be serious sometimes acha ukada usiokuwa na msingi.

TUSAIDIE WEWE NI SHERIA IPI INAYOMNYIMA RAIS KUTOKUWA NA KAMPUNI HAPA TANZANIA AU DUNIANI, JANA BELUSCONI KAJIUZURU URAIS WA AC. MILAN LAKINI HAIMAANISHI KUWA WA-ITALIANO HAWAJUI KUWA YEYE NDIYE MWENYE HISA NYINGI PALE SANSIRO, TUNAHITAJI ZAIDI HOJA ZINAZOLINDWA NA SHERIA KULIKO UTASHI AU FIKRA YA MWENYEKITI KUDUMU KTK AKILI ZETU NA KUSAHAU WAJIBU WETU KAMA WANADAMU.

SOTE TUNAJUA SI WATOTO WOTE WA MWALIMU WALIOISHI KAMA TUNAVYOTAKA SISI IWE, MADARAKA NI MMILIKI WA MAKAMPUNI MBALIMBALI YENYE KUFA NA KUZALIWA KILA KUKICHA TENA WAKATI BABAKE NDIO ANAJIANDAA KUONDOKA IKULU NA HATA ALIPOKUWA M/KITI WA CHAMA MPAKA 1990 ALIPONG'ATUKA,JE MAKAMPUNI HAYO HAKUYAFAHAMU MWALIMU? AU NDIO SAINT ASIYEGUSWA,ABBAS MWINYI NI MMOJA WA WAFANYABIASHARA MAARUFU BY THEN MZEE YUKO IKULU MBONA HATUKUMBUSHANI HUMU?

AU TUJIULIZE SUKITA YA MWALIMU NA MWINYI NI KAMPUNI ILIYOANZISHWA NA KUTOKOMEA BILA TAARIFA! FEDHA ILIPATIKANA TOKA WAPI KWA AJILI YA KAMPUNI HII? KIWIRA INAYOZUNGUMZWA HAPA NI IPI MAANA KILA MTU AMEKOMAA NA KIWIRA, TUNATAKA DATA ZA KUTOSHA NA SIYO KUCHAFUANA HUMU NDANI WAKATI SISI WENYEWE WANA JF HATUONYESHI SPIDI SAWIA YA KUUSAKA UKWELI WA KIWIRA, 1995 KIWIRA ILINGIA KTK MACHAFUKO MAKUBWA YA KIUTAWALA NA HATIMAYE WAFANYAKAZI WASIOPUNGUA 1500 WALIPELEKWA LIKIZO PASIPO KWA ZAIDI YA MIAKA SABA.

ILIKUWA NI MWAKA 2003 SERIKALI IKAAMUA KUWAACHISHA KAZI WAFANYAKAZI HAO AMBAO WALILIPWA MAFAO YAO INGAWAJE HAYAKUFAA MAISHA YA WAHANGA WALE WA MGODI, WAKATI HILO LINAFANYIKA SHUGHULI YA UZALISHAJI ILIKUWA INAENDELEA PALE BELOW 50% NA NI WASAA HUO NDIPO SERIKALI ILIPOWARHUSU WACHINA WAZALISHE UMEME, HUKU GEOGOLIST ADAM AKIKAIMU UMENEJA WA KIWIRA COAL MINE AMBAYO TAYARI IMESHAPOTEZA MUELEKEO TANGU 1995.

JK KNOWS KIWIRA KULIKO WANA JF MNAVYOIFAHAMU, YEYE PIA NI MMOJA WA MAJERUHI WA KIWIRA KWA NAMNA FULANI, KIWIRA CRISIS ILIANZA WAKATI AKIWA NISHATI NA MADINI,ALIJITAHIDI SANA KUTATUA MIGOGORO YA MGODI ULE LAKINI ALIKWAMISHWA NA MAOFISA WA WIZARANI KWAKE NA STAMICO, KUNA MMASAI LESHANGI NA TIMU YAKE ILIYOKUWA HUKU MAKAO MAKUU AKINA GEMBE, BUGAISA, HANGI NA WENGI WA NAMNA HIYO CHINI YA KAMISHINA MWAKALUKWA JK AKAKWAMA NA ALIJIKUTA AKIIACHA KIWIRA INATOWEKA NA KIJANA ALIYEKUWA MENEJA WA MGODI HUO WAKATI YEYE AKIWA WAZIRI ANANG'OLEWA NA KUPELEKWA KTK KA MGODI KALIKOKUWA KAMEKUFA PALE KISARAWE.

YULE BWANA ALIONDOLEWA KIWIRA KWA ZENGWE LA AKINA LESHANGI KWA MSAADA WA WAKUU STAMICO LAKINI LAANA HAIKUWAACHA MAANA MIEZI 6 BAADA YA MENEJA WA MGODI KUBALISHWA ULIFUATIA MGOMO WA KUTISHA ,THEN MISHAHARA IKATA NJIA THEN MABADILIKO TENA YA UONGOZI WA MGODI THEN LIKIZO 1995-2003,HII NDIYO KIWIRA JAMANI,KISAYANSI KIWIRA ILITEGEMEA SANA WATEJA WAKE WAKUBWA WAWILI,MBEYA CEMENT NA SPM MGOLOLO,KUFA KWA SPM KULIITETERESHA KIWIRA,KUTETEREKA KWA ZIMBABWE KIUCHUMI KULIFUTA SOKO LA KIWIRA.

WAKUBWA KIWIRA SI HABARI MPYA KWA JAKAYA ILA NI JINAMIZI AMBALO KURUDI KWAKE NI MSUKULE AMBAO NIONAVYO HATOUPENDELEA SANA, PENGINE NIMKUBUSHE JK KUWA YULE KIJANA WAKE WA KIWIRA YUPO JIJINI ILA HANA NURU YA MAISHA , NI MBANGAIZAJI KWA UFUPI BADO NI MAJERUHI WA SIASA ZA KIWIRA MPAKA SASA.
 
1. PRESSURE is mounting now within the National Assembly for an official investigation against Benjamin Mkapa who is accused of serious allegations of corruption and abuse of office during his tenure as president of the United Republic of Tanzania.

2. The ex-president has opted to keep mum even after new demands are being made by legislators for an official corruption inquiry against him and his former energy and minerals minister, Daniel Yona.

3. The two public officials were allegedly involved in the dubiously-conducted privatization and buy-out of the formerly state-owned Kiwira Coal Mine in Mbeya Region at a ridiculously cheap price of 700m/-.

4. These allegations on the part of the former president must not be ignored for the sake of the future of the country. Instead, they should be determined through the forthright and rigorous application of the relevant provisions of the laws of the land.

Baho! Baho! Mwanangu, sasa ni mpaka kieleweke halafu watajisema wenyewe nani alimpa nani, mwaka huu mpaka mafisadi wote wasafishwe na kurudisha mali za wananchi, wanaanza hawa kujisema!

Duh! I love JF where we dare kumkoma nyani mchana kweupeee!
 
Sababu kubwa ni mapato duni yaliyoko kwenye mkataba wa ubinafsishaji wa Kituo cha Kontena ambacho ndicho kilikuwa mhimili wa mapato ya Mamlaka, kuongezeka kwa gharama zisizoepukika, na uzito wa madeni ya Mamlaka kwa Serikali.

KAZI IPO..ndio haya haya tunayolilia bungeni leo.....kumbe yalitajwa tangu 2002 hatukuyaona jamani?
 
Pinda wewe si fisadi, tunajua unakotoka, hauna hata barabara wala umeme, kweli serikali yako itaweza kupambana na matajiri hawa? kweli unajipa hope, but what matter tujipange upya, siamini kama hawa hawa ccm wanaweza kujikana wenyewe, hizi hadithi za kuchekesha,
 
Huyu mzee Luhigo kanikosha sana na hii spichi yake, naona aliamua kumkoma nyani giladi, mchana kweupe na tena hadharani! A rarity in Tanzania! Yuko wapi Samson Luhigo siku hizi?



Alistaafu mwaka juzi.

Sasa hivi ukimwona kachoka.
 
Huyu mzee Luhigo kanikosha sana na hii spichi yake, naona aliamua kumkoma nyani giladi, mchana kweupe na tena hadharani! A rarity in Tanzania! Yuko wapi Samson Luhigo siku hizi?

Nasikia Mzee kastaafu yupo anafanya consulting.Alivyotoka THA Rostam Aziz ali-offer a lucrative contract jamaa aka decline kwa sababu ya machale yake.
 
Luhigo alipatikana na kasha ya kubambikiziwa ya matibabu ya familia yake kama sikosei, aliikosa kazi immediatelly baada ya hii scandal. Manake ilizua joto kwa muda kiasi, kama nakumbuka vizuri.

Haika unafahamu unachosema au unajisemea tu?

Tafadhali kama huna hakika na unachosema fanya research kwanza, huyu Mzee anaheshima yake bongo.Alistaafu bada ya kufikisha umri wa kustaafu.
 
TUSAIDIE WEWE NI SHERIA IPI INAYOMNYIMA RAIS KUTOKUWA NA KAMPUNI HAPA TANZANIA AU DUNIANI


FDR Jr,

Naona unafananisha Kunguru na Meza , hakuna sheria inayomnyima Rais kuwa na kampuni kwani hiyo ni haki yake ya kikatiba kwa Tanzania. Ila watu wanachokipinga hapa ni yeye kutumia offisi yake kupata hiyo kampuni ! Nadhani unakubalina na mimi ya kuwa Rais atakuwa na advantage kubwa sana kupita watu wengine katika upatikanaji wa hiyo kampuni , pia Rais anapata inside information ambazo zinampa yeye " unfair advantage"

Sijui ni nini haswa unachochotetea hapa ? jee simply kwa kuwa Madaraka anafanya kitu fulani basi ndio watu wengine wafanye?
 
haya yalizungumzwa kweli au ni tahariri?

Kweli nimeamini watanzania ni wepesi wa kusahau au kubisha tu.

Tutaendelea kuwa na maisha duni hadi yesu aje!

Haya Luhigi aliyasema sana na hotuba nzima iliandikwa kwenye h=gaezi maaruifu la RAI wakati huo.

Na alisema yuko alikuwa amejianda kurudi kwao shinyanga?


Alikuwa ni shujaa sana aliyeweza kummwabia ukweli DR. MKAPA bila wogoa wowote! Na ilikuwa ni kweli tupu!

Lakini kwa kuwa DR. MKAPA MSOMI ALIYEJIONA ANA UELEWA MKUBWA KULIKO WATANZANIA WOTE HAKUWA TAYARI KUMSIKILIZA.
 
"Kosa si kutenda kosa bali kurudia kosa" is logically inconsistent kwa sababu each time kosa linatendeka litakuwa looped back in an endless iteration.

Mfano

Kosa1= Si Kosa

Kosa2=Kosa (limerudiwa from Kosa1)

but Kosa2 halijarudiwa (kurudiwa kosa hakujarudiwa)

Therefore Kosa2 becomes Kosa1= Si Kosa

Repeat ad infinitum with no escape

KAVERSION KENGINE, MALIZIA KWA KU DEBURG PROG TUU MKUU,

IF (Kosa1= Si Kosa) THEN

((Kosa2=Kosa (limerudiwa from Kosa1)

(but Kosa2 halijarudiwa (kurudiwa kosa hakujarudiwa))

WHILE (Kosa2 becomes Kosa1= Si Kosa)

ELSE

END
 
[/COLOR]


Alistaafu mwaka juzi.

Sasa hivi ukimwona kachoka.


Kachoka maana yake ni nini hasa? Kauli kama hizi ndio zinakatisha tamaa baadhi wa watu serikalini wenye nia ya utumishi wa kweli na wasiopenda ufisadi. Ni akili za namna hii ambazo zinaamini maisha ni hela tu na ukimuona mtu hana Escudo basi unafikiri amechoka. Mshindwe kabisa na mawazo ya namna hii!
 
Kachoka maana yake ni nini hasa? Kauli kama hizi ndio zinakatisha tamaa baadhi wa watu serikalini wenye nia ya utumishi wa kweli na wasiopenda ufisadi. Ni akili za namna hii ambazo zinaamini maisha ni hela tu na ukimuona mtu hana Escudo basi unafikiri amechoka. Mshindwe kabisa na mawazo ya namna hii!

Kabisa Mkumbo,
Fikra hizi ndio hufanya viongozi wale rushwa kwani wanaogopa kuambiwa "umemwona Mkumbo, kachokaaa'. Ni hulka mbaya sana.
 
Wanachoka kwa sababu wakwenda kuishi maisha alisi ya mtanzania,kwani wanapokuwa ktk utumishi wao huwa hawajui maisha yako je uraiani,
Sasa anapokuta kila kitu ni shida basi wewe mpe mwaka tu.atakuwa anajua hata bei ya kipimo cha mafuta ya taa,muhimbili ikoje,polisi wetu wakoje,kulinda sungusungu kukoje na mengine mengi ambayo alikuwa anayaona kama simulizi tu.
 
Kabisa Mkumbo,
Fikra hizi ndio hufanya viongozi wale rushwa kwani wanaogopa kuambiwa "umemwona Mkumbo, kachokaaa'. Ni hulka mbaya sana.

SASA HUYO ANAESEMA MWNZIE KACHOKA MANAKE HANA HELA EE??? MULIZE KAMA ALIJUA KAMA cHENGE ANGEKEWA NA VIJISENTI VILE, UKIMWANGALIA SI KACHOKA TUU
 
Yuko wapi Samson Luhigo ]siku hizi?au yalitimia.
kwa imani yangu namshukuru mungu kwa kukuongoza angalau kwa kusema ukweli kwa hili
god bless yu
 
Collective rensponsibility mnaikumbuka?? Hivi bado ipo?
Wakati Kamati ya chama bungeni inapokaa kukubaliana kupitisha miswada ya ajabuajabu na hakuna mtu kupinga, la sivyo utakumbuka CCM makao makuu ilikupa sh ngapi wakati wa kampeni, na inakufichia maovu yako mangapi.
Hivi walikuwa wanapata sitting allowance sh ngapi?
 
Tuandamane umenikumbusha miaka ya 90 nilipokuwa nasoma Pascal pale FOE chini ya Ishengoma , sijui yuko wapi yule mtu ...
 
Huu mgodi wa makaa nafikiri uko wilaya ya Kyela na wala sio Rungwe.

Hapa tusije tukageuka kuwa kama ile ya Kilamanjaro kuwa Tanzania au Kenya.
 
laana kubwa iliyo wakumba wana CCM akiwemo Chenge ni kwenda Butiana na kuzuru kaburi la Mwalimu wakiajiamini kwamba kafa hana madhara kwao tena .They made a huge mistake na madhara ni haya .Nakwambia huu ni Mwanzo tu .Mengi utayasikia .

Mr Lunyungu, umewakilisha kauli pana na yenye kina. "Wakiajiamini kwamba kafa hana madhara kwao tena" ...

Ndio uzuri wa Wapumbavu! Hawana maono! Hawana kina cha tafakari! Muda wakutosha ukipita wataonyesha upupu, wanadhibitisha ujinga wao. Wanajitokeza wazi na kujidhihirisha kwa kile wanachotaka kujificha..huku wakifkiri wamekificha kwa ujanja mkubwa na hawaonekani..Thanks God the principal works.

Falsa aliyoiishi na kuifundisha Mwalimu...Technicaly speaking inahitaji solid about 40 years kujikita ndani ya jamii ili iibuke kwa nguvu zote yenyewe.

Mbegu ilishaoteshwa...ndio kosa mafisadi walilolifanya. Kwa upofu wao wangezuia Mwaimu asifanye vile vitu vyake alivyovifanya.

Watu wengi hawakumuelewa kabisa wakati huo... but Now they r crinying for the principals and facts alizoziamini Mwalimu. Kila mwananchi analilia MIIKO YA UONGOZI...Thamani ya UTU nk ambayo basicaly ndio wimbo kulilia kuondoshwa kwa mafisadi!

Ukikiuka kwa kasi kabisa dhana na falsafa ya Mwalimu unachopata ni Ufisadi unaoendelea kwa kasi nchini.

Unapolilia kwa nguvu zote kuuondosha ufisadi... kwa namna fulani unamfanya Mwalmu kuwa Hai kuliko alipokuwa hai kimwili.

Kama mtu sio kipofo anawezakuona kuwa TAIFA LA TANZANIA KWA KIWANGO KIKUBWA SASA HIVI LINAELEKEA KUTAWALIWA NA FALSAFA ZA MWALIMU TENA KWA VITENDO ZAIDI YAALIPOKUWA HAI KIMWILI.

Kile alichokuwa anakiwaza na kutaka kila mwanchi akitekeleze..ni KILIO NDANI ya haya maandamamano na makelele yanayosikika bunguni na kwenye vyombo vya habari.

Neno "RUKSA" basicaly haliendani na dhana ya "UTU" na kujitegemea. Kusitiri utu wako,wa familiia yako na wa Taifa Kila kitu hakiwezi kuwa ruksa. MIIKO NA MAADILI na hata wakati mwingine maadili kuwa makali ndio chimbuo la Kutunza na kujenga Utu. Hapa Rais Mwinyi ajutie alichokifanya kama mwanzo wa jahazi kuyumba.... Hii Mbegu itakuja kuwa na kukomaa na kuwa jambo kinyume na utu na madili yake.

Kimsigi MKAPA, atajilaumu kuingia kichwa kichwa kwenye kuvunja Dhana nzima Ya UTU wake, wa Familia Yake na Ya Taifa..alipoibeba na kuitumia Dhana ya RUKSA iliyo antidote ya UTU...Bila kuisaili.

Ruksa Ikakomaa na kukamilikia pale Zanzibar Kwa Kuua MIIKO ya UTU WA VIONGOZI NA kuwa RUKSA katika kukiuka na kuvunja Maadili kwa viongozi....!

Hapo ndipo Mkapa akonyesha Ruksa katika Kutumia madaraka Kufanyia YOTE YANAYO MSUTA LEO HII, HILO LIKAZAA wote hao waliojiuzulu na watakao jiuzulu...karibni!

But Yote haya yatatibiwa kwa kilio kikuu cha Watanzania kwa MIIKO YA UTU ndani ya Taifa...ambayo ndio Kanuni kuu ya UTANZANIA.

Kwa mfano..Nani anaona Kitu kinyume na utu kwenye azimio la Arusha....Nauliza.Lilikikua nini katika kulinsda utu na Ubinaadamu.

Na atakaye pinga kanuni ya UTU amejikana utanzania ahame au ataumbuliwa tu.....Mbegu inakomaa alikuwa na tumuulize alikuwa wapi wakati mbegu inakuwa na kukomaa! Ukifanya ufisadi kama hua unaofanywa hapatanzania sasa ndani ya nchi nyigi za kiafrika unaweza usipate matatizo kama haya hapa nyumbani kwani hawana "Mbegu inayokomaa" ya kuwasuta na kuwaangamiza kama inavyotoke hapa Tanzania

Kuna wengi wameona hilo na wanarejea kwenye mstari!

Ole wa wale wasioona na wanaendelea kukiuka UTU na maadili yake katika Uongozi, elimu, afya, uchumi, makuzi ya kifalia nk. Yote haya yana kauli mbiu kwenye falsafa ya Mwalimu.

Leo hii yanahitaika kama Mvua kwenye ukame wa kiangazi kikali!

Mtu Ayapinge haya hadharani tumuone atakavyo sambaratika!!!!

Na walivyo wapuuzi hawatakubaliana na haya tunayosema hapa, Hivyo ni hakika watasambaratika na ndio ushindi tunao usubiri karibuni!
 
Back
Top Bottom