Unajua,
Kwa wale wazee "Wenzetu", kama mnayoyasema ni kweli basi Tanzania hatujawahi kuwa na viongozi wezi hata siku moja!
Mwalimu alipomuita Lowassa kuwa ni mlarushwa na mwizi, je alitoa ushahidi? Tunapoambiwa kila siku kuwa Lowassa ni mlarushwa na mwizi, ni nani ambaye amewahi kutoa ushahidi?
Toka tupate uhuru, tumeambiwa viongozi wangapi kuwa ni wezi, wana mahela mpaka majumba ndani ya nchi yetu, je ni wakati gani tuliwahi kuonyeshwa ushahidi? Tukapewa adress ya nyumba? Na mji zilizoko hizo nyumba?
Sasa hiyo ina maana kuwa Tanzania hatujawahi kuwa na viongozi wezi? Mbona mnageuka kama watoto na hizi hatred mpaka hamuwezi kuuuona ukweli Mkapa hata kwa hela hela zake mwenyewe hawezi kujenga ile nyumba ya Sea View, licha ya hayo majumba yote mengine aliyojenga kwa kipindi cha mwaka mmoja! Watoto alisomeshaje nje, toka vidudu mpaka wamemaliza vyuo vikuu?
Je milishawahi kuziona risiti za nyumba zake za Hapa bongo na kuhakikisha kuwa ni zake kweli? Warioba anpowatukana viongozi wa baada ya Mwalimu kuwa ni wala rushwa na wezi ana maana gani? Alishawahi kututolea ushahidi?
Mrema alipoulizwa na waandishi kama yeye ni clean toka akiwa serikalini, alisema, "......Mimi sio malaika.....", alikuwa na maana gani?
....Kwa wale mnaojaribu kuzima issue na maneno ya ushahidi, I hope you are for real kwamba Tanzania hatujawahi kuwa na viongozi wezi, maana hatujawahi kuuona ushahidi in public toka tupate uhuru!