Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Mzee Tafiti Tena Ujadili,

Vipi hli nalo la mzee wetu mahiri? Hebu tafiti huko halafu tuje tujadili hapa?
 
Uwazi ndilo neno Mzee wetu Mkapa alikuwa akilitumia muda wote . Juzi Mzee JK alipokuwa ziarani kujitambulisha alikusanya kidogo . Aliporudi tu kesho yake kila mmoja alisikia kupita Mambo ya nje kwamba kiasi fulani kilikusanywa msaada . Sasa huyu kaondoka bila kutueleza ni kiasi gani alipata huko na kimetumika wapi ndiyo maana tunauliza .tafiti upo ama napo bado hujafanya utafiti?
 
Mimi ni mgeni kabisa kwenye forum. Nimevutiwa na hii taarifa ya Mkapa kununua/kujenga mansion South Africa. Ukweli ukoje?
 
kabla ya kuanza kulalamika what a shame or not.

Mzee ES nakushukuru kwa spidi kubwa ya kuleta hili lakini tujaribu kuangalia vile vile kama MKAPA hana uwezo wa kununua nyumba AFRIKA KUSINI.

Unaweza kununua nyumba SOUTH AFRICA from as little as 100,000 USD sasa bila kumtetea au kumlinda Rais Mstaafu nadhani ni bora tuangalie je Rais Mstaafu ana uwezo au hana wa kununua hiyo nyumba.

Wakati Rais akijiandaa kuachia madaraka ilitangazwa katika vyombo vya habari kuwa amelipwa takriban dola milioni tatu ambazo ni malimbikizo ya malipo yake akiwa rais kutoka katika mfuko wa serikali CONSOLIDATED FUND.

Sasa Mzee ES tuwekee hapa vifuatavyo kama uthibitisho wako:
1. Kainunua kwa kiasi gani?
2. Ni kwa mkopo au CASH
3.Is there anything fishy katika hilo to deserve a public discussion au ni kwa vile tu huyu mzee ni jina inapaswa tujue, manake kama taratibu zote zimefuatwa na kukamilika na hela halali imetumika sioni kwa nini habari hiyo ije humu.

Naam we are waiting for the story withini six hours!
 
Hata kama ni haki yake kuishi kokote yeye alikuwa rais wa Watanzania why SA? Nani ali staafu Urais akaja kununua jumba Tanzania ? Ina maana gani yeye kununua jumba huko ?What sort of a message is he sending ? tafiti tulia bwana wacha habari zije .

tafiti mbona hujasema zile pesa za Vyandarua toka kwa akina Sharon Stone kazipeleka wapi je ndiyo hizo kaongezea kahama nazo kwenda SA ?

Speaker SS kama habari ni kweli inaa maana zitakuwa hazikuanza jana mbona ulimletea longo longo bwana Zitto alipo sema juu ya jumba la Mkapa la SA . Je ni hili hili alilosema Zitto bungeni ama hili ni la pil la kwanza ilikuwa la 10 % asante kwa kuuzia Nchi yetu kwa wa SA ?
 
nadhani tunatwist ukweli, natulia habari zije kwa kufuata ushauri wako bwana mugishagwe lakini habari ya awali ni kuwa kanunua nyumba SA sasa kusema kwamba anahamia huko ni kupotosha habari.

Inawezekana ameamua kununua nyumba hiyo kwa vile ana safari nyingi za huko, ndio his chosen holiday destination au hata kwa business interest zake.Yeye ni retired president na hajavunja sheria yoyote kununua nyumba SA.

Hela za Sharone Stone nasikitika sijui lakini ni rahisi kuulizia kwa kina Mzee Herman Lupogo kama zilikabidhiwa kwao, kama unajua kitu hatujui mzee mugishagwe naomba uweke hapa.

i submit with a promise ya kungojea habari zije.
 
Rais wetu wa zamani Mzee Mkapa, amenunua nyumba mpya ya kuishi ambayo tayari inakaliwa na mtoto wa mkewe mama Anna,

Mzee Mkapa baada ya kuinunua alimuomba rasmi Mzee Mandela aifungue rasmi nyumba hiyo, Mzee Mandela alishtushwa sana na habari hizo hivyo akaaamua kwanza kuwatuma watu wake kuiona hiyo nyumba kwanza,

waliporudi na kumfahamisha waliyoyaona kuhusu hiyo nyumba, Mzee Mandela alisema kuwa "...Hata sisi wa-South Africa huwa hatununui nyumba za namna hiyo.......", akamfahamisha mzee wetu Mkapa kuwa hataweza kujihusisha na shughuli za nyumba hiyo na aendeleee salama!

So far ndio uchunguzi wetu ulipoishia na tutanendelea kusema as we get more info,

kwa wale wazee wenzetu ambao tayari mmeanza ushabiki ninasema safari hatuna huo muda na wala hatutishiki na kama tulivyoahidi kuwa kwenye TAIFA LETU, hatuna compromise na mtu yoyote hata kama anatumwa na usalama, maana sisi tunatumwa na wananchi!
 
sijaelewa lengo hasa la habari hii kuletwa humu?!

ni kutuambia kuwa mkapa kanunua nyumba tu au kuna jambo sisi hatulijui yaani kavunja sheria fulani ya nchi au nyumba hailingani na fedha alizonazo au kuna sababu gani?

ili kuweza kuwa na michango mizuri humu ndani nadhani kuna haja ya kuangalia mambo ya kuweka hapa manake ikiwa kila kiongozi akinunua nyumba tu basi tunaweka itakuwa ni udaku na sio lengo la mijadala kama hii.

Ningeiona hii habari ya msingi sana kama kungekuwa na utaratibu fulani ambao Rais Mstaafu kaukiuka, au kavunja sheria fulani aidha ya Tanzania au Afrika Kusini au nyingineyo.

Ukweli (not sure) kama Mkapa ana nyumba afrika kusini na inakaliwa na mtoto wa mkewe sioni tatizo so far! Kama kiongozi mstaafu sidhani kama anatakiwa kuifanya hii decision yake public na pia habari ya Mandela kukataa kuuifungua rasmi kama ni kweli ni personal decision yake mwenyewe so what is so wrong here kiasi tumewekewa hii habari humu ndani?

naomba kufahamishwa...

adios
 
tafiti nadhani wewe una lako jambo. Tumewasikia marais wana staafu lakini hubakia wazalendo na Nchi zao . Sijawahi kusikia wanana nunua majumba Nje ya Nchi zao . Hivi Mkapa majumba yote haya kwa mwaka mmoja ina mana hatakuwa na pesa ya kula sasa ama ndiyo kula state house hata akiwa nje ya mdaraka ? Ana nunua majumba haya ili iweje ana sababu gani ya msingi hata kama mapesa na uamuzi ni wake ? Je majumba yote haya yana thamani gani wakati akina Rashid JK anaokoa maisha baada ya wazazi kushindwa kumpa matibabu ? Sikatai mzee BM kuishi kokote lakini yeye si kama mimi . Yeye ni Rais wa Nchi huyu jamani vipi hapa ??OK majumba kila kona na yote ni ma Mansion ana watoto ngapi hao na kununua nyumbani huko na kuweka watoto wake huko pia kuna maana gani ?bado tuna hoji hata kama pesa ni zake yeye ni Rais wa Nchi .
 
Mzee Es said:
Ni uamuzi wa wananchi kuamua kama ni sawa kwa rais wao wa zamani, kujenga Mansion Lushoto, kujenga upya ile mansion Sea View, Mansion Mpya kule Msasani, na kununua mansion South Africa kwa kipindi cha mwaka mmoja tu, alio-retire!

Mungu amrehemu Mwalimu Julius Kambaraga Nyerere, kwani huyu alikuwa ni a TRUE LEADER NA MKOMBOZI WA WANANCHI!

Aluta Contunua, na Stay Tuned................Tunaendelea!

Dah..

Hiyo ya lushoto ikoje.. Hebu nipe breif kidogo.. hiyo sijaisikia

ya msasani siijuii na hiyo brief yake nipe kama unayo..

Ila Sea view si hoteli au pia kule anayo nyumba..
 
Ya Lushoto, iko karibu na rafiki yake Mzee Ngwilizi, mzee pita kwa nje ujioneeee, mimi nimeingia mpaka ndani yaani sina la kusema,

Kule Sea View, ni pembeni ya Hotel ya Sea View ukipita utaona FFU kwa wingi upende wa kulia kama unaelekea baharini, yaani nayo siwezi kusema ukarabati iliyofanyiwa nayo pia nimeingia ndani,

Kule Msasani kuna watoto wake Nico na Steve, mzee pitia nako uone, halafu kabla hujafika huko kuna magorofa ya ku-Rent ya mama, na serikali ikalazimishwa kujenga lami ya kufika huko, huko pia nimefika mpaka ndani,

Wallahi Wallah!, mzee Mkapa msalie mtume kidogo!
 
mimi issue yangu ni ndogo tu kwenye hili,hii Consolidated Fund aliyotaja Mh Tafiti nilikuwa sijawahi kuisikia...kwani mshahara wa rais ni kiasi gani,na hayo ni malimbikizo yapi? Maana kwa kusema ukweli sidhani kama Mwalimu (ambaye nina uhakika angekuwa na malimbikizo zaidi) au Mwinyi walipata hata nusu ya hizo pesa,na jamani 3 million Dollars IS A LOT OF DOUGH! In other words,a poor president becomes a millionaire after his term has expired! Poverty alleviation in the real sense of the word! But in all honesty,Tafiti please shed some light
 
Kwa kwa kweli sidhani hata kiongozi wa nchi zilizoendelea anaweza kupata pesa nyingi kiasi hicho.

Kuendana na habari za ndani Mshahara wa Rais ni U$8000 kwa mwezi (kama haujabadilishwa bila bunge kuambiwa (this was as of 2002). Kwa hiyo ukiongeza allowance and other marupurupu utafikia $10,000 kwa mwezi.
Hence for a year Rais hujipatia $10,000 x 12 = $ 120,000. Mkapa alikuwa Rais kwa miaka 10, therefore $120,000 x 10 = $1,200,000.

Kuna ambao watasema alikuwa kwenye bodi na kamati za kimataifa, pamoja na hilo ni vigumu kuwa kwenye kamati hizo na kupata mshahara unaozidi mshahara unaolipwa kama Rais.

Swala la kujiuliza je anaweza kununu hayo majumba sembuse kujenga Hekalu hapa Lushoto (utadhani ni ikulu).

Nadhani kuna haja ya kumchunguza yeye na Mkewe. Tunahitaji majibu ya TAKURU kuonesha alipoingia madarakani alikuwa na mali kiasi gani na akiwa anaondoka madarakani ana kiasi gani.

Inabidi tuwaige wenzetu wa Malawi.
 
hakuna haja ya kuwalipa maraisi wetu mapesa yote hayo. taifa bado linawagharamia hata wanapoondoka madarakani. mtu mwenye maadili, uzalendo kwa tanzania, na huruma kwa wananchi wake, anapaswa kuukataa mshahara huo. haulingani na hali halisi ya watanzania.

kama hizi habari za kununua nyumba huko afrika kusini ni kweli basi sababu yake inaweza kuwa ni hayo mapesa tunayowalipa maraisi wetu. yanawatia ulimbukeni na uwendawazimu.

mkapa alikuwa akihimiza wasauzi waje kuwekeza tanzania. vipi leo awe wa kwanza kuchomoka tanzania kwenda kuwekeza sauzi? moja ya kauli mbiu ya mkapa ilikuwa kuwahimiza watanzania kununua bidhaa za ndani, leo anakwenda kununua bidhaa za sauzi. kwanini asirudishe mabilioni aliyolipwa kwa kuwekeza katika uchumi wa tanzania?
 
Kitendo cha Raisi mstaafu Mkapa kununua mansion Afrika Kusini (kama ni kweli) kinaweza tukakakiona ni cha maana au si cha maana tukiyachambua mazingira yote ya ununuzi wa mansion hiyo hasa vile tunavyoambiwa kuwa mtoto wake anaishi kwenye mansion hiyo. Lile la kumhalika Raisi mstaafu Mandela kuifunguwa nyumba hiyo ndilo linalozuwa maswali mengi ya kujiuliza, "kulikoni?"

Wakati jambo hili la kumhusisha Mkapa na umiliki wa jengo huko Afrika Kusini linaonekana kama kitu kipya kwa baadhi yetu, mbona amekwisha semwa sana kuhusu sio tu kununuwa mansion bali kujenga jihoteli la haja na kifahari huko Cape Town. Stori hiyo inamwelekeo uleule wa hii ya sasa kuwa alimualika Mandela afunguwe hoteli hiyo na Mandela akakakataa hivyo hivyo kama alivyofanya hapa. Haiingi akilini kuwa kama ile ya awali ni kweli, Mkapa huyo huyo amualike tena Mandela huyo huyo kumfungulia mansion yake baada ya kukataa kumfungulia jihoteli lake! Aidha moja la haya ni kweli au yote mawili ni uzushi tu na kama lolote ni kweli pia inawezekana jina la Mandela limeingizwa kutia chumvi tu.

Kama nilivyosema, mtu unaweza ukamshutumu au kumsifu Bwana Mkapa kwa kununuwa mansion hiyo kama kitendo hicho kweli amekifanya kwa kuchambuwa sababu za kufanya na kuzipima. Lakini kufuatana na hizo habari za hoteli na hizi za sasa kufananafanana inawezekana habari zote mbili ziwe si kweli. Ingetupa nyenzo za kuujadili huu ununuzi wa nyumba wa huyu bwana ughaibuni wakati hapa nyumbani bado tunahitaji kuboresha vibanda vyetu kama tungepewa data za uhakika za kitendo hicho: i) aliinunua lini? ii) kwa thamani gani? iii) iko mji gani na pia anwani (physical address) yake ni ipi? iv) aliinunua kutoka kwa nani na kwa mpangilio gani wa malipo? v) ina ukubwa gani? na data nyingine kama hizi.

Habari mbili za kuvuma kama hizi ambazo zinafananafanana mara nyingi zinaelekea kwenye uzushi tu usiokuwa na ukweli.

By the way, mimi sihafiki sera za uwekezaji bandia (yaani uvamizi) aliouruhusu ufanywe na hao makaburu aliowapalilia njia watuhujumu na kututia kwenye tindiga la kurudi nyuma kimaendeleo. Bali siwezi kuchangia apachikwe mizigo mingine ambayo pengine hakujibebesha. Hadi hapa, lawama anazozibeba kwa vizazi vijavyo zinamtosha kama kuna za ziada ziwe ni ukweli sio uzushi.
 
Hii habari ya hotel ndio mara yangu ya kwanza kuisikia, unless mzee ulishawahi kuitoa huko nyuma, hebu tufafanulie habari ya hotel je walisema na mtoto wake anaishi kwenye hiyo hotel?

Kama vile tunavyojua jinsi watoto wake wawili Nico na Steve, wanavyoishi kule Msasani?

Au kuwa jinsi mtoto wa mama anavyoishi kule South Africa?, Halafu mbona unajikanyaga, at one point unasema "kama ni kweli", meaning kwamba hujui halafu mwishoni unahukumu kuwa "Si kweli", nafikrii the best hoja ilipaswa kuwa sijui,

hatukuisema bure kuwa kijana Peter, mtoto wa mama anaishi kule tayari bila sababu! Na hata yote ya lile "FAILI" yanafahamika, haya ya nyumba ni madogo sana kuliko ambayo hujaambiwa, na kama nilivyosema mwanzoni hatuna mpango wa kubishana kitoto!
 
Nasikia huyu mzee BM ana hotel ule ushelisheli nazo hizi je ni kweli ama uongo ? Mana huyu Mzee kweli alikuwa mpoke rushwa kama mambo ni haya .Maana tukisema kula basi unashiba unalala yeye alikuwa anapokea tu .
 
DU!!!!!!!!

hii ni kali!

Huyu BWM ameisha laaniwa siku nyingi!


Na wewe tafiti then jadili mbona uko hivyo!!!!!!!!!!

yaani wewe ni kupinga tu!!!!!!!

Sasa Mkapa hizo hela za kununua nyumba SA amezitoa wapi? na kama anazo ni kwa nini asiwekeze Tanzania??

Ni huyu huyu aliyeruhusu madini yetu kuuzwa Thailand, India. Leo nimesikia viwanda vya kukata madini(tanzanite nk) huko India vimeajiri zaidi ya watu laki moja!!

Hizo zote zingekuwa ajira za watanzania!

Thailand kuna ajira 2000 zote hizo zingekuwa ajira za watz!!

Sasa huyu BMW aliyiwaona wote hawajui bali yeye, huwezi kuona kuna maslhi yake binafsi humo!! Kwa maana kuna wakati ilitakiwa tuwe tunakata(process) madini yetu. Lakini Mwaka jana India wakaja wakabembelaza na kupewa kibali kuendelea kununua madini raw!


Ni huyu BMW aliyewatetea Vodacom na makampuni ta simu kuendelea kutukamua kwa viwango vya juu vya matumizi ya simu!!

Tume ya mawasiliano ilishamua siku nyingi kupunguza viwango. Lakini hawa jamaa ilibidi wamfuate Mkapa akiwa likizoni huko Mtwara na matokeo yake alidikiteti kuwa viwango vya juu viendelee!!

Jiulize ni kwa nini viongozi wote wa serIkali wanatumia VODACOM?!
Na ndiyo maana anathamini nje tu! akina Blair, waandishi wa habari wa nje nk!

anyway inasiktisha sana!
 
Back
Top Bottom