Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

tafiti then jadili said:
------
Wakati Rais akijiandaa kuachia madaraka ilitangazwa katika vyombo vya habari kuwa amelipwa takriban dola milioni tatu ambazo ni malimbikizo ya malipo yake akiwa rais kutoka katika mfuko wa serikali CONSOLIDATED FUND.

tafiti.

tafadhali naomba nifahamishe vyombo vya habari vilivyotangaza kuwa BWM alilipwa $3M kama malimbikozo ya malipo akiwa rais. Sikumbuki kusoma/kusikia hayo.
 
tafiti then jadili said:
kabla ya kuanza kulalamika what a shame or not.

Mzee ES nakushukuru kwa spidi kubwa ya kuleta hili lakini tujaribu kuangalia vile vile kama MKAPA hana uwezo wa kununua nyumba AFRIKA KUSINI.

Unaweza kununua nyumba SOUTH AFRICA from as little as 100,000 USD sasa bila kumtetea au kumlinda Rais Mstaafu nadhani ni bora tuangalie je Rais Mstaafu ana uwezo au hana wa kununua hiyo nyumba.

Wakati Rais akijiandaa kuachia madaraka ilitangazwa katika vyombo vya habari kuwa amelipwa takriban dola milioni tatu ambazo ni malimbikizo ya malipo yake akiwa rais kutoka katika mfuko wa serikali CONSOLIDATED FUND.

Sasa Mzee ES tuwekee hapa vifuatavyo kama uthibitisho wako:
1. Kainunua kwa kiasi gani?
2. Ni kwa mkopo au CASH
3.Is there anything fishy katika hilo to deserve a public discussion au ni kwa vile tu huyu mzee ni jina inapaswa tujue, manake kama taratibu zote zimefuatwa na kukamilika na hela halali imetumika sioni kwa nini habari hiyo ije humu.

Naam we are waiting for the story withini six hours!

Hivi wewe ni Mtanzania au Mnyarwanda?Nauliza hivi kwa sababu unatetea kila kitu kinachohusiana na maslahi ya watawala,na sijaona mchango wako wowote katika kutetea maslahi wa WATANZANIA?Kwanini usisubiri yapite hayo masaa sita kabla hujaanza kumtetea Mkapa.Sio bure,kuna manufaa flani unayopata kwa kutetea ulaji wa watu.
 
tafiti then jadili said:
sijaelewa lengo hasa la habari hii kuletwa humu?!

ni kutuambia kuwa mkapa kanunua nyumba tu au kuna jambo sisi hatulijui yaani kavunja sheria fulani ya nchi au nyumba hailingani na fedha alizonazo au kuna sababu gani?

ili kuweza kuwa na michango mizuri humu ndani nadhani kuna haja ya kuangalia mambo ya kuweka hapa manake ikiwa kila kiongozi akinunua nyumba tu basi tunaweka itakuwa ni udaku na sio lengo la mijadala kama hii.

Ningeiona hii habari ya msingi sana kama kungekuwa na utaratibu fulani ambao Rais Mstaafu kaukiuka, au kavunja sheria fulani aidha ya Tanzania au Afrika Kusini au nyingineyo.

Ukweli (not sure) kama Mkapa ana nyumba afrika kusini na inakaliwa na mtoto wa mkewe sioni tatizo so far! Kama kiongozi mstaafu sidhani kama anatakiwa kuifanya hii decision yake public na pia habari ya Mandela kukataa kuuifungua rasmi kama ni kweli ni personal decision yake mwenyewe so what is so wrong here kiasi tumewekewa hii habari humu ndani?

naomba kufahamishwa...

adios

We mwananchi,kwanini usitulize ball hadi data zitakapomwaga ndio uanze kutoa utetezi wako?Maana kwako akisemwa kigogo basi ni kama umechokonelewa macho wewe.Inawezekana ni wakili wa kujitolea kutetea maslahi ya wanaokula nchi yetu.Ungependa habari ya Mkapa kununua nyumba iwekwe wapi kama sio hapa?Suppose habari hii ingekuwa ya kumpongeza Mkapa kwa kununua nyumba ungei-criticise as you're just doing?Kwanini usiTAFITI THEN ukaJADILI kabla ya kukurupuka na your uncalled for defence for the ruling class.
 
Huwa mimi sikurupuki kuleta hapa mambo ya mitaani na ninasisitiza kuwa wanavyongea huko mitaani kuhusu hoteli ina vibwagizo hivi hivi vya hii stori ya mansion. Umeona na mwengine naye anaongelea hoteli Seychelles, je na yeye alikwisha ileta hiyo hapa ikajadiliwa na kuthibitishwa. Niliuliza maswali kutegemea ungeyajibu kuthibitisha ununuzi huo, bali majibu hayatolewi badala yake tunatajiwa jina la mtoto wa Mama Anna ambalo ni rahisi kujuwa majina ya watoto wote wa mama huyu. Majibu kuhusu angalau ni mji gani ilipo hiyo mansion hakuna. Sasa uchangiaji wa mada unakuwa wa kitoto pale mada zenyewe zinapoletwa kitoto, kishabikishabiki na kichukichuki bila ya data za kuzifanya ziwe za kitu kizima.
Mzee Es said:
Hii habari ya hotel ndio mara yangu ya kwanza kuisikia, unless mzee ulishawahi kuitoa huko nyuma, hebu tufafanulie habari ya hotel je walisema na mtoto wake anaishi kwenye hiyo hotel?

Kama vile tunavyojua jinsi watoto wake wawili Nico na Steve, wanavyoishi kule Msasani?

Au kuwa jinsi mtoto wa mama anavyoishi kule South Africa?, Halafu mbona unajikanyaga, at one point unasema "kama ni kweli", meaning kwamba hujui halafu mwishoni unahukumu kuwa "Si kweli", nafikrii the best hoja ilipaswa kuwa sijui,

hatukuisema bure kuwa kijana Peter, mtoto wa mama anaishi kule tayari bila sababu! Na hata yote ya lile "FAILI" yanafahamika, haya ya nyumba ni madogo sana kuliko ambayo hujaambiwa, na kama nilivyosema mwanzoni hatuna mpango wa kubishana kitoto!
 
Assuming hizi habari ni za kweli, kununua majumba namna hii, ni dalili ya ulafi na kupenda kulimbikiza mali, na mwananchi wa kawaida lazima zimkerekete angalau kidogo. Yaani sisi tulipoambiwa 'tufunge mikanda', wenzetu wanaporomosha mijumba! Habari za 'jumba' lushoto nimewahi kuziskia tangu mheshimiwa bado ni rais.

Pia 'hear say' ya jihoteli SA na Mandela kukataa kulifungua ilishasikika before. Binafsi nliichukulia hivyo hivyo, a 'hear say'. It was a bit surprising kusikia kuwa baada ya kununua jumba SA amemuomba Mandela kulifungua, it sounded familiar. Nikajiuliza .. huyu jamaa nyumba yake binafsi ya kuishi (au ya kuishi mwanawe wa kambo) pia mpaka ifunguliwe na Mandela? As if it is something of a historical significance. It must be hell of a Mansion!

To me, either habari ya jihoteli ilikuwa ni ya uongo ... au hii ya mansion ni uongo .. au both.

I've also heard of Mkapa being paid a huge sum (sina uhakika na hiyo $3M figure) out of consolidated funds.. ilisemwa kuwa eti mwanzo alikuwa akizikataa lakini wakamsihi azichukue kwa kuwa ni zake za kihalali ... eti ndio 'akakubali' kuzichukua!

By the way, I must say that tulipoambiwa tusubiri masaa sita ripoti inakamilishwa, I expected a lot more than what came up. Mtu unapoulizwa angalau estimate of the cost (ili wananchi tuone wazi kuwa jamaa hawezi kumudu manunuzi hayo bila ya kutuibia in one way or another), kama hujui ni uungwana kusema tu kuwa sijui. Sijui pia ni jibu... wala halipunguzi heshima.
 
Hey Jizaledo and alike, Tafiti, keep down your adrenaline,
Notwithstanding................ Nyumba ya South Africa, justify hii, this guy parted with USA dollars three millions, and then was being paid USA dollars ten thousands per moth as salary. Presidents have previliges on allowances, they do not use what they own, that money probably was kept in a bank. For ten years, we are talking about USA dollars 1.2 million.
Pamoja na kudau watu walete hivyo vielelezo lakini Tafiti umeshasema hiyo ipo na ni part of "consolidation fund". Lakini benefits zote za rais mstaafu hupitishwa na bunge sasa hizo za consolidation funds mbona mpya.
Another issue vile vile kuna allowance ya kila mwaka ya rais mstaafu. That is too much! The good thing for this country walalahoi wa nchi hii hata hawajui! That is theft for those previleged.
 
Mzee Es,

Kwa nini ninasisitiza kujuwa ukweli usiokuwa na mashaka kuhusu habari hii ya mansion ni kwa kuwa ikiwa ni kweli basi ni nzito kuliko tunavyoichukulia. Mkapa amekwisha kuiathiri nchi vibaya kwa sera zake alizozitekeleza hasa miaka yake mitano ya mwisho baada ya kufariki Mwalimu. Mkapa amewakabidhi mwenyemwenye wageni hasa makaburu rasilmali zetu na nyenjo za uchumi wetu tulizozidundulia kwa miaka mingi na si rahisi nchi kupiga hatua tena kama hazikurudishwa mikononi mwa wananchi: karibu nyanja zetu zote kubwa za uchumi wetu, kuanzia mabenki, breweries, kampuni za umeme, za maji n.k. aliwapa hao, duni thamani. Mimi conviction yangu ni kuwa hakuna binadamu aliyekamilika na kila mmoja wetu hufanya makosa hasa kama anahitajika kufanya maamuzi mazito akiwa kama raisi hivyo raisi yeyote hasingesitaili kushitakiwa au kuchukuliwa hatua kwa makosa ya kibinadamu aliyofanya akiwa madarakani. Inaniwia ngumu hivi sasa kung'ang'ania msimamo huo kuhusu huyu bwana. Mungu anisamehe, kwani ukweli ni kuwa nisingemsikitikia kama angeshitakiwa na kuadhibiwa ipasavyo kutokana na sera zake za hujuma hizo. Tuna kazi kubwa kuyarekebisha matatizo aliyotutia na huwa siridhiki na kasi iliyopo ya kuyatatuwa haya kwani nionavyo mimi mikataba yote ingefutwa mara moja, famalilah, bila ya kuwa na kigugumizi na ajizi, basi kama nikupelekana mahakamani tupelekwe. Matatizo tunayoyalimbikiza athari zake ni kubwa zaidi ya faini ya kotini hata kama faini hizo tutastahili tutozwe.

Hivyo ndio maana ninasema hili la kununua mansion (kama ni kweli) kwa juu juu ni kadhambi kadogo tu ambako kasingeninyima usingizi, bali kwa undani wa tafsiri yake linaweza likawa jambo zito. Anaweza akawa anaandaa mahali pa kukimbilia. Ndio maana kuhitimisha ukweli wa jambo hili ni muhimu sana.

Hey Iterested Observer, I am sorry, but it's you who should control your biased flow of adrenalin. You seem to interpret words differently depending on who uses them!!!!
 
Kinachonikera hapa ni kwamba kwa nini kama Mkapa hakuwekeza nchini kama alivyokuwa akihubiri wakati wa utawala wake? au anajua kuwa he meesed na sasa anatayarisha pa kukimbilia siku mambo yatakapomgeuka?
 
Unajua,

Kwa wale wazee "Wenzetu", kama mnayoyasema ni kweli basi Tanzania hatujawahi kuwa na viongozi wezi hata siku moja!

Mwalimu alipomuita Lowassa kuwa ni mlarushwa na mwizi, je alitoa ushahidi? Tunapoambiwa kila siku kuwa Lowassa ni mlarushwa na mwizi, ni nani ambaye amewahi kutoa ushahidi?

Toka tupate uhuru, tumeambiwa viongozi wangapi kuwa ni wezi, wana mahela mpaka majumba ndani ya nchi yetu, je ni wakati gani tuliwahi kuonyeshwa ushahidi? Tukapewa adress ya nyumba? Na mji zilizoko hizo nyumba?

Sasa hiyo ina maana kuwa Tanzania hatujawahi kuwa na viongozi wezi? Mbona mnageuka kama watoto na hizi hatred mpaka hamuwezi kuuuona ukweli Mkapa hata kwa hela hela zake mwenyewe hawezi kujenga ile nyumba ya Sea View, licha ya hayo majumba yote mengine aliyojenga kwa kipindi cha mwaka mmoja! Watoto alisomeshaje nje, toka vidudu mpaka wamemaliza vyuo vikuu?

Je milishawahi kuziona risiti za nyumba zake za Hapa bongo na kuhakikisha kuwa ni zake kweli? Warioba anpowatukana viongozi wa baada ya Mwalimu kuwa ni wala rushwa na wezi ana maana gani? Alishawahi kututolea ushahidi?

Mrema alipoulizwa na waandishi kama yeye ni clean toka akiwa serikalini, alisema, "......Mimi sio malaika.....", alikuwa na maana gani?

Now back to the point, nimesikia Mkapa amenunua nyumba SA ya kifahari ambayo hata Mandela amekataa kwenda kujihusha nayo, nimewasikia watu wazito wa nchi wakiongea, nkaamua kufuatlia kwa kuwatafuta kwanza watoto wote wa Mkapa, kujua Peter yuko wapi na anafanya nini, nikaambiwa kuwa yuko SA na nikapewa namba yake, nikampigia na kunihakikishia kuwa ni kweli amehamia huko, na the rest of the story ya nyumba,

sasa ninatakiwa kuja hapa na kusema na kusema yote in details, halafu kesho na keshokutwa nisipate info tena? Au nifukuzwe kazi? I mean guys, halafu what is this kuwa akisema Tafiti, basi Kulikoni, Ogmulik, na Jzalendo mnalifahamu na ni sawa sawa, wakisema wengine huyo bwana akiuliza na nyinyi mnauliza? Huyo bwana akikubali na nyinyi mnakubali, mnachotaka hasa kutuambia kwenye hii forum ni nini hasa?

Mnachotaka kuwaambia wananchi hapa ni nini? Eti Mkapa ana hela za kujenga ile Ikulu kule Lushoto, Sea View, Msasani, Majengo ya ku-rent Msasani, majengo ya ku-rent Ilala, na sasa mansion SA, hivi hamuoni hata aibu na maneno yenu? Hii ni wazi kabisa kuwa the man was a thief, na amefanya haya baada ya Mwalimu kuondoka, kumbe alipofariki hawa ndio waliokuwa wanatundanganya,

Kujifanya kilio cha taifa na mambo yote kumbe ni nyoka mbaya huyu, halafu kuna wanaotaka kutudanganya kama kawaida na maneno na mengine ya kizungu, Eti CONSOLIDATE! are you kidding me! Mwalimu angekuwepo angefanya haya maajabu? Sisi tunagawana umeme, magenerator sasa bongo hata usingizi hatulali makelel ya magenerator, mosho ndio hausemeki tena bongo, ni kwa sababu ya hawa kina Mkapa, wezi wakubwa na wanafiki waliomdanganya Mwalimu maisha yake yote akaamini kuwa ni watu wake kumbe wahuni wakubwa, ndio ananunua nyumba huko kujitayarisha kukimbia ikibidi, maana anajua kuwa JK, kwenye hilo hana mchezo maana rafiki yake Sumaye, alimumlilia sana wakati wa uchaguzi asimpe JK, ".....Ben ukimpa huyu kijana atatufunga huyu......Ben Please can you for once listen to me.....",

Baada ya uchaguzi hawa wawili BM na Sumaye walikuwa maadui wakubwa kinachowakutanisha huko Boston sasa hivi ni nini? BM naye anahangaika sana na Malsyia na Singapore anakokwenda kesho kutoka Boston kuna nini?

Ndio maan Mzee JK ameipangua timu yote ya maadili ya CCM, amefukuza wote na alikuwa njiani kufukuza makatibu wote wa mikoa na wilaya, isipokuwa Mzee mmoja akamuwahi na kumbembeleza asifanye hivyo, ama sivyo kimbunga kingewakuta wote, sasa ndugu zangu mnaotetea wezi kaeni chonjo mana tsunami linakuja, ameweka timu mpya ya maadili maana anakuja pole pole, na majuzi amewaita Mtandao wote mmoja bada ya mwingine na kuwapa makali yao kuwa wasifanye mchezo na nchi ya wananchi, atawafukuza wote ikibidi, Wazee BM na Sumaye wanajua kinachokuja, kwenye hilo Mzee JK ninamuamini, na ninaamini kuwa sio muda mrefu hata hayo majumba huko SA yatarudishwa na hela za wananchi zitarudi,

Kwa wale mnaojaribu kuzima issue na maneno ya ushahidi, I hope you are for real kwamba Tanzania hatujawahi kuwa na viongozi wezi, maana hatujawahi kuuona ushahidi in public toka tupate uhuru!

Lakini tunawajua viongozi wote wliotajirikia uongozini, you guys better be right kuwa wote hawa wana condolidated salaries na marupu rupu maana when the day come, tutawatundika plaeee Sanamu Monument, na kumwaga risasi moja baada ya nyingine na tutawalazimisha familia zao kulipia risasi hizo zitaklazonunuliwa kwa hela za wananchi na wakulima!
 
Mzee Es
Hapo umeongea kama ilivyo kawaida yako. Kuna mahali bwana mmoja, kama sikosei FK kasema forum imeingiliwa. Naelekea kuamini. Maana watu wanavyodai ushahidi inaonekana kama Mkapa alivyopuuza kushughulikia rushwa ama wala rushwa akidai aliye na ushahidi aulete.

Ama kweli Bongo kuna mambo! Mzee Es keep it up. Naziona low profiles za akina tafiti and the like. Na wala usipate wasi wasi. You have a legion(army) of followers. We know what you stand for.

ALUTA CONTINUA!
 
Mzee Es hapa kwetu Songea wanaunwa wanathamini sana Chingwaji yaani kiuno walahi nasema ungalikuwa songea ningalikupa mke wa jirani upumzike japokuwa si zawadi nzuri kwa mtu kama wewe .Maana kuna tabia zimefuka ushaidi, Ushahidiiiiiiiiiiiiii mashaidi ama mashahidi what >

Nchi imeliwa kumbuka Mkapa alikuwa mwizi hata kabla hajawa Rais .Mzee Kiraracha alilia sana lakini JK akasema Ben mwanafunzi wangu mambo hayo leo kaamua kutula ,nasikia huyu wanasema ana hotel kuleeeeeeeeeeeeee ushelinishelini Oops ushelisheli nasema nasikia je na nyie mmesha yasikia haya ? Nimevutiwa vijana na michango yenu pasukeni .Tunangoja kuona ukweli wa maneno ya JK kama kweli atarudisha mali zetu na tufungue Mahakama.

Tupe sirini Boston na malasia kunani wewe mjomba Es mzee wa kunyumba wewe ? Umenusa nini wachana na watafiti wa ushahidi bwana wewe .
 
Nimerudi!

Ninaamini kabisa baada ya miaka 30 ijayo kifo chanzo cha kifo mwalimu kitajulikana tu!!!!

wazungu walikuwa wanataka kuja kuchukua madini, wanyama wetu lakini kikwazo kikubwa alikwa ni mwalimu Nyerere!

Mbaya zaidi MKapa alikuwa agaist mwalimu katika uchumi huria!!

kwa hiyo?!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Es,

Ninaona umelijumlisha "jina" langu katika orodha ya unaowadhania kuwa ni wafuasi wa Tafiti na si wako wewe. Kwanza elewa kuwa mimi sipo hapa kumuunga mkono mtu fulani au kumpinga mtu fulani kwa sababu tu yeye ni fulani, si wewe wala si Tafiti au mwengine yeyote. Naomba uelewe hivyo.

Pili, mimi sijasema kuwa Tanzania au mahali popote pengine hakuna viongozi wezi; na pia nimesema waziwazi mambo yanayonikera kutokana na sera na vitendo vya BM alipokuwa madarakani. Hili la nyumba ni dogo na lisingestahili likuzwe kiasi cha kufinika hayo mazito. Kama ulilileta kama changamoto ya kuanzisha mjadala wa hayo mengine basi useme tuanze kuyajadili kwa upana wao, au kama ulilileta lijadiliwe lenyewe kama utangulizi wako ulivyoonyesha basi tulijadili hili kwa mapana na marefu ya uhakika wake, tusiwe tunarukaruka kugusiagusiatu mambo mengi kwa wakati mmoja.

Mwalimu hakumhusisha kila kiongozi katika ulaji rushwa na uovu wao kwa nchi yetu. Aliwataja aliokuwa na uhakika nao na hatukuwa na sababu ya kumquestio kwani yeye vyombo vyote vya habari na usalama wetu vilimuamini, kwa hiyo mtu mwengine yeyote asitarajie kuaminiwa kiasi alichoaminiwa yeye. Katika watu aliopungukiwa na imani kwao mmoja wao alikuwa ni JM, je unalionaje hilo?

Kitu kimoja umenfurahisha kuonyesha kuwa kumbe na wewe pia una imani kuwa JK ataturekebishia mambo. JK anahitaji imani kama hizo ili kazi itendeke. Pia anahitaji support za kweli sio za hoja ya malumbano tu.

Hakuna wa kulindwa wala kulindana tunapoongelea maswala ya nchi yetu kuhusu hatima yake. Kila aliyetufanyia ubaya basi ni haki ashutumiwe na ikibidi ashitakiwe. Hili la kutundika watu hapo askari monument sikubaliani nawe kama maana yako ni kuwa wauwawe. Kama wameamisha mali zetu basi wao waturudishie tu tuangalie ustaarabu mwingine.

Maji ukiyavulia nguo inabidi uyaoge, hivyo tupe tu hivyo vyombo bila ya kuhofu kufukuzwa kazi. Hivi wakati wakutishanatishana kufukuzana kazi kwa kutetea haki bado upo. Nilitarajiya kuwa mambo yamekwisha badilika huko nyumba na usingekuwa bado unaogopaogopa.

Ufikapo Big Apple ( NY) nitumie private message kwenye email yangu.
 
Mzee ES,

Nice piece you have written. I agree with most of it na imenipa moyo ikiwa ni kweli kuna timu mpya ya maadili imeundwa iliyo serious kiasi cha kuwaogopesha 'wezi' mpaka kuwakutanisha wakapiga kambi huko Boston, Malaysia na Singapore kama ulivyoashiria. We look forward to see what comes out of it.

Yeah, hayo majumba ni dalili ya wizi na ubadhirifu, inatufanya tujiulize kama haya ya majumba ndio visible stuff.. hayo yaliyojificha yako vipi?

While kuna walio proud kujinadi kuwa ni 'legion (army) of followers' wako, mimi si follower wako wewe wala wa huyo tafiti (kuna topic tulimpinga mpaka akawithdraw kauli zake) wala wa mwingine. Nitakuwa na wewe ukiwa na opinions/data zinazolingana na zangu au zinazomake sense na ntakupinga ikiwa other wise.. just like any body else. Samahani sisi wengine sio wa kukubali kubali tuuu kwa kuwa amesema mzee ES, au kupinga tuuu kwa kuwa amesema tafiti.

Unless it is your unique style, sioni kwa nini uje juu unapokuwa challenged; na kuanza kuwapa watu majina ya 'hawa jamaa', wale 'wenzetu', 'usalama' na kutugawa as if kuna tafiti alliance na mzee ES alliance. Ikiwa kila ukileta vitu sote tunashangilia tuuu na kukubaliana na wewe ... hata ile 'burudani' aliyoisema mzee mwanakijiji katika sheria alizopendekeza haitokuwepo. Some minds are inquisitive. Tukikuchallenge na ukitoa majibu ya sawa sawa au (kusema sijui.. honestly) ndipo tunapopata confidence zaidi na hizi info, na ukitetereka, ukakwepa maswali basic, kupanic na kubadilisha topic ndio tunapojua kuwa umeropokwa tu huna hakika. Infact hata katika mada hii, zimekuja info nyingi zaidi baada ya challenges za hapa na pale, otherwise tungekuwa tumebakiwa na ile ile mistari michache tuu (not worth the six hours waiting). Na sio kila ukiulizwa swali maana yake umepingwa, some time ni kuchokoza tu ili kama kuna info zaidi zipatikane.
 
Yah blah! blah! blah!, hapana mzee nina familia inahitaji kula, halafu hata siku moja sina wafuasi hapa, na sitetereki hata siku moja katika kuisimamia hoja yangu maana huwa ninafikiri kabla ya kuandika,

Kuhusu JK unless wewe ni mgeni hapa maana wengine wote wanaelewa jinsi ninavyomsiamia hapa siku zote akiwa sawa, lakini kwenye baadhi ya mambo yake ninakataa kuwa sometimes anatuchukulia wa-Tanzania for granted, halafu kizuri ni kuwa ninajua kuwa haya yanayosemwa hapa anayaona kila siku, na ndio hasa sababu ya kuwaita mtandao mmoja baada ya mwingine hivi majuzi,

Halafu naomba niseme kuwa mimi sio Mwalimu, na wala sina ubavu wa huyo Mzee wa kazi!, na rais safari hii anafatana na wajumbe 102!, upo hapo!

At the end of the day, hii ni forum ambayo ni kama Tv, bila umeme havifanyi kazi watu wasivilalie macho sana, meaning kwamba sometimes tunahitaji ku-Relax,

Anyway, guys RESPECT! great debate na tuendelee hakuna noma, the point ni KUMKOMA NYANI GILADI, na mzee wa Songea ninakuja huko Matimila karibuni KUKAYE, RUVUMA mpaka MAPUTO, nintarudi matimila karibuni!

ila tu ninaomba kuwatoka kidogo kwa muda maana sasa shughuli za taifa zimenikaba mno, between shughuli hizo na Forum ninazidiwa kidogo, lakini nipo kila siku hapa na zikipungua I will be right back,

Mzee wa NY, E-mail yangu sio siri ni mtuwameli@yahoo.com,

kwa wale wazee tunaowasiliana kwenye private kumradhini ndugu zangu kidogo nimetingwa lakini sijamsahau hata mmoja na nategemea kuwa hamjakata tamaa, Ishallah tuombe Mungu na mambo yote yatatengemaa tu maana Mungu ndiye yuko kwenye usukani, sisi ni wabebwaji kazi yetu kubebwa na Mungu!

Wasaalm!
 
Duh! kweli kumeingiliwa!.

Sometimes ni afadhali kunyamaza watu wakuone mpumbavu kuliko kujionesha.

Ngoja ninyamaze msijue kama mi ni mpumbavu au?,

Asanteni

FD
 
Mkira,
Welcome back! Haitachukua miaka 30, believe me.
Admin, umeuliza juu ya Vodacom. Unajua Mobitel waliwahi kuingia Tz wakanunua karibu frequencies nyingi za kufunika nchi nzima. Walipokuja Vodacom wakaanza kula na wakubwa na ghafla ikapelekwa bill bungeni kwamba ni hatari kwa usalama wa nchi kwa kampuni moja kuwa na majority ya frequencies. Sasa Mobitel wakanyang'anywa na kupewa Voda. Lakini Voda inakula na wakubwa. Mfano mmoja ni Spika wa zamani wa bunge kuwekwa kwenye bodi ya kampuni hiyo.
 
Mamaaaaaaaaaaa kumbe hii ndiy siri ya majengo ya sirikali kupakwa rangi ya vodacom?Mimi chikujua kabichaaaaaaaaaa.Chacha ni vyema kujua miaka 30 haitafiki ya nini tena ?Vodacom kufa ama Chichiemu kushindwa ?
 
Nikiri kuwa japo nimekuwa nikirambaza ndani ya hili baraza kwa muda sasa, bado najiona kuwa Mwanagenzi kwa kujilinganisha na waliotangulia kujiunga na kwa michango yao mzo mzo katika mada na mijadala mbalimbali.

Mpaka sasa, nadiriki kusema kuwa baraza linavutia kwa mijadala ya wanabodi na pia malumbano, vibwagizo na vijembe vya hapa na pale, ambavyo ni kama chachandu katika pilau.

Pamoja na hayo niseme kuwa bado tuna nafasi ya kuliboresha baraza letu kwani ubora hauna kikomo.

Kwa maoni yangu, tujaribu kuepuka yafuatayo:
1. Kutuhumu na kushutumu kwa nguvu kabisa (siyo kwa namna ya mzaha) baadhi ya waanzilishi wa hoja (wachokozi) au wachangiaji kuwa ni wanachama, wafuasi, wapenzi, wakereketwa, wafurukutwa, au washabiki wa chama fulani cha siasa ilhali wao hawajatuambia hivyo. Daima tuzingatie hoja na si nani katoa hoja.

2. Kutuhumu na kushutumu baadhi ya wachangiaji kuwa "wametumwa" na kikundi cha watu fulani na hata serikali. Hata kama hilo linawezekana, na huenda baraza halina haja wala jinsi ya kulizuia, hoja iwe kuchangia, kukosoa, kupinga, kurekebisha nk "hoja", badala ya kutoa madai ya kijumlajumla. Isitoshe kwa nini mtu uamini kuwa fulani katumwa? Kwani huyo mchangiaji hawezi kuwa na mawazo yake binafsi kama wajumbe wengine? Kwani watoao madai kama hayo wao wanakuwa "wametumwa" na nani? Naamini wengi, kama si washiriki wote, barazani ni wazalendo na wana uchungu na nchi hii. Vinginevyo hatuna kipimo cha kujua nani mzalendo na nani siyo (si hata baadhi ya viongozi wa taifa letu wanaonekana kuwa si wazalendo?).

3. Kujenga dhana kuwa kuna makundi ndani ya baraza, na kwamba hoja hutolewa kwa kufuata makundi, au kuunga mkono hoja za kina fulani tu, na kupinga za wengine. Tuaminiane kuwa washiriki ni watu wazima, wenye uwezo wa kupima mantiki za michango mbalimbali, na kwamba wanashiriki barazani
kwa hiari yao, na wanajiwakilisha wao na nafsi zao.

4. Kama ambavyo imekuwa ikisisitizwa, tuepuke lugha ya matusi, na kumlenga mchangiaji binafsi badala ya hoja yake. Hoja ijibiwe kwa hoja. Kama Mwalimu alivyotuasa, "Tutumie nguvu ya hoja badala ya hoja ya nguvu, na tupingane bila kupigana", kwani sote tuna nia ya kuchangia ujenzi wa Tanzania yetu.

Kwa kumalizia , nadhani ni muhimu tupitishe kanuni na tuziheshimu. Naamini baraza hili ni bora na tusilibomoe kwa mikono yetu wenyewe!

Mungu libariki Baraza,
Mungu Ibariki Afrika,
Mungu Ibariki Tanzania!
 
Back
Top Bottom