Kuna mawazo mengi ya msingi yametolewa hapa. Shukrani kwa waliyoyatoa. Viko vipengele vingine vinahusu hii ishu ambavyo bado havijatajwa.
Umeme wa mafuta ni ghali sana. Kwetu sisi tusio na mafuta, umeme huo hautufai hata kidogo.
Tuna hydroelectric potential kubwa, gesi na mkaa wa mawe. Hatuna sababu ya kutegemea umeme wa mafuta. Unatumalizia forex, na unachangia sana kuyumbisha dhamani ya shilingi yetu.
We have not exhausted our hydroelectric potential. Tutafute wawekezaji (sio lazima watoke nje) wa upande huo. Wajue kabisa Watanzania wenye mitaji (kama wenye NICO) kwamba unaweza kujenga bwawa ukauza umeme. Ikibidi tutalazimisha TANESCO wanunue huo umeme wako.
Ni vizuri kwamba tunazalisha umeme wa gesi, lakini tulikosea sana pale tulipokubali kupewa ruzuku badala ya kuwa wamiliki washiriki. Kama atatokea Mtanzania mwenye fedha nyingi (wapo, na mikopo ipo) akainunua kabisa SONGAS tungeshangilia sana. Kwa sasa, inatugharimu FOREX nyingi kuzalisha huu umeme wa gesi, kwani SONGAS wanahamishia fedha zao nje. Wakina Mkapa, Mengi, etc, tunaomba mtafute mbinu ya kununua hiyo kampuni iwe ya Watanzania. Tutawashangilieni.
Kama Umeme wa Kiwira ni wa Wamakonde na Wapare, basi tutaupata bila kutumia forex nyingi. Hiyo ni AHUENI kubwa. Ni sababu ya kufurahi, si ya kulalamika.
Wako Watanzani wenye mtaji wa kutuwezesha kupunguza kasi ya utumiaji wetu wa FOREX kwenye nishati. Tukipata ushahidi kwamba fedha walizo nazo ni za wizi, basi tutaujadili. Kabla ya hapo, tuwapongeze.
Tumezoea mno kuona biashara ya Mtanzania ni ya baa ya kuuza sanduku nne na kuku sita, au daladala mbili na lori moja. Akitokea anayefanya uwekezaji wa kikweli, asitukoseshe raha. Si lazima awe ameiba. Mbona wanapokuja wageni kuwekeza hatusemi wameiba?
Kuhusu Mwalimu kutokuwa na fedha, naomba niseme hivi: Mwalimu alipunguza hata mshahara wake. Kuna watu hawapendi fedha, period. Sasa sio lazima kila mtu awe kama Mwalimu. Rais ambaye anahudumiwa kila kitu na serikali kwa nini asiwe na savings? Lazima awe na savings za mamilioni mengi tu. Kwa vingine ni mpuuzi. Msisahau hawa watu wana marupurupu mengi sana. Badala ya kulalia hayo mapesa ni vema hawa wastaafu wanunue makampuni wazalishe mali na kuinua uchumi wetu.
Augustine Moshi
Ndugu yangu AM
Kuna key issue ambazo ziko wazi, moja ni mgongano wa ki-maslahi.
Inakuwa kama kesi ya nyani umpeleke tumbili.
Au let me put it like this u r the prosecuter na Judge at the same time. Sasa hapo haki itakuwepo?
Tumia akili yako ya kawaida tu sio ya kwenda Shule.
Pili ukitumia ya kwenda shule, sasa bahati mbaya sijui fani yako, lakini kila fani inataratibu zake ili ku-uphold high standard za utendaji kazi na kuweka heshima ya hiyo Profession.
Na hata ukiwa mfanya biashara yule ambaye hakwenda shule, anajua the basic principle ya Biashara ni kuweka undugu ktk biashara inaweza kuwa moja, nyingine ni kukopesha bila kuji-shield na uwezekano wa kutolipwa, au ule utaratibu wa kumjua mtea wako.
So hata ukienda Bar ya mtu yoyote, unless u r are regular customer, ndio anaweza kukukopesha kwa dharura au atakwambia acha saa yako au simu.
Tukirudi kwa Kaka Ben etc kuna issue ya kuwa kiongozi unapitisha sera na maamuzi kwa faida ya watu sio ya kwako.
Kampuni unajiuzia mwenyewe, then tarriffs una set mwenyewe, kweli kutakuwa na haki kwa wengine?
Tatu nitakupa mifano ya Hotel zetu za kitalii zilivyo kufa sababu hiii hiii ya wa conflict of interest, Hotel ina stock nzuri tu ya kuku, lakini kwa sababu waziri au mjumbe wa Board au ndugu au rafiki, ana kuku wameisha kuwa na hawezi kuendelea kubeba cost ya kuwalisha , anaiuzia hii hotel, matokeo yake wanakaa saana kwenye fridge, then kinakuwa chakula cha staff kabla hawajaharibika, hasra kwa hotel, matokeo yake hao hao wajomba zetu, dada zetu na kaka zetu ambao walikuwa wana kazi kwenye hizo hotel wakawa hawana kazi.
so ukiwa mtu mzima na akili zako timamu usifurahie furaha ya dakika tatu wakati mbele ni mauti.
wasio na kazi ambao huko nyuma walikuwa na kazi ni wengi, angalia kwenye textile mill , NMC, Ugawaji , TWICO etc. mifano ni kingi na wewe mwenyewe unaijua.
Usiwe na ile sera ya mkuki kwa nguruwe ni sawa kwa binadamu ni mchungu. Hope umenielewa.
wa