Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Ana ubavu? akae tu anaimba ngonjera siku zake zikiisha aondoke.
 
Kwani Ben Mkapa akiwa na share au hata pesa kuna mbaya gani? Kama kuna ushahidi kuwa ameiba fedha alizo nazo, au alitumia madaraka vibaya, basi utoeni hapa ili tumhukumu nao.

Kumhukumu bila ushahidi ni kinyume cha haki. Kuwa na mali si dhambi. Na kufanya kazi ya Uwaziri miaka nenda rudi, na baadaye Urais, kisha usiwe umehifadhi (save) fedha kiasi ni kosa. Utakuwa umetapanya malipo yako yote? Huo ni utumiaji mbaya wa fedha, na unaleta umasikini.

Tuache kulalamikia utajiri. Si kosa kuwa tajiri. Kama utajiri umepatikana kwa wizi basi utolewe ushahidi, na Polisi waarifiwe.

Kuwa "clean" ni synonymous na kuwa "poor"?

Augustine Moshi

Mh Augustine Moshi,

Kiongozi kuwa na hisa kwenye kampuni siyo dhambi, inakuwa dhambi/kosa pale anapotumia nafasi yake ya uongozi serikalini katika kujinufaisha yeye na kampuni yake alikowekeza hisa zake. Na hapo ndipo inapoingia dhana ya ETHICS za uongozi, kiongozi mzuri wa serikalini hatakiwi kuchanganya uongozi na biashara maana ni ngumu kutenganisha yapi ni maslahi ya biashara zake na yapi ni maslahi ya nchi/wananchi.

Kumbuka kwamba mfanya biashara yeyote nia yake ni kutengeneza faida kubwa kadri awezavyo, kwa hiyo ni rahisi sana kwa mtendaji serikalini kutumia mwanya huo kujitengenezea faida kwa kuwa na mikataba mibovu kama hiyo ya Kiwira Coal Power Project. Sidhani kama mkataba huo ulikuwa na maslahi kwa wananchi, TANESCO wala serikali, bali kulikuwa na maslahi ya watu binafsi (shareholders wa kampuni ambao ni pamoja na BWM kupitia kwa kampuni ya mwanae na kupitia kampuni ya familia ANBEM).

Kama umekuwa ukifuatilia hiyo skendo, malalamiko ni kwamba nguvu ya ziada ilitumika katika kuwalazimisha TANESCO kusaini huo mkataba, na nguvu hiyo ilitoka kwa kigogo mmoja kutoka serikali ya awamu ya tatu. Ni waziri gani anaweza ku-block ulaji wa Rais? Au mtendaji gani serikalini anaweza ku-block ulaji wa Rais?

Ndiyo maana nchi za wenzetu mtu akishachaguliwa/teuliwa kuingia serikalini anatakiwa kuachana na biashara zake ili asije akatumia nafasi yake ya uongozi serikalini kwa manufaa ya kampuni au biashara zake. Utamaduni huo hapo kwetu Bongo haupo tangu lilivyokufa Azimio la Arusha mwaka 1992 na kuanzishwa kwa Azimio la Zanzibar ambalo linaendelea kuitafuna nchi yetu mpaka leo hii.

Sidhani kama watu wana tatizo na utajiri wa BWM, tatizo ninaloliona mimi ni kwamba kuna uwezekano kwamba alitumia nafasi yake ya Urais kwa manufaa ya kwake binafsi. Iko wazi kwamba ofisi ya ANBEM ilikuwa IKULU, unategemea nini kwenye mazingira kama hayo? Tayari hapo kuna kosa la pili kutumia public ofisi kwa biashara zake binafsi.

Kwa mtazamo wangu watanzania tuna haki ya kujua na wala hatumuonei wivu ila tunasikitika kwamba kuna dalili nyingi zinazoonyesha kwamba BWM na familia yake walitumia Ofisi ya Rais kufanya biashara. Nakumbuka zama za uhai wa Baba wa Taifa Mwalimu JKN (wakati Mzee Ruksa akiwa madarakani na wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea urais kupitia CCM mwaka 1995), aliwahi kusema IKULU ni mahali patakatifu na kilichomkera zama hizo ni jinsi wafanya biashara walivyokuwa wakitumia IKULU kwa manufaa yao na alipiga kelele sana. Leo hii mtu aliyetupatia ndiye amekuwa mfano mbaya wa matumizi mabaya ya IKULU mpaka anageuza ofisi za IKULU kuwa ofisi ya kampuni yake! It is so sad, I wish Nyerere siku moja angeamka akaona huu uchafu!

Swali la mwisho kwa Mh. Augustine Moshi ni hili, kwanini uchafu huo wa ANBEM, Radar, Ndege ya Rais, Net Group Solution na uchafu wa mikataba mibovu imeibuka sana after 1999?????
 
Ni juzi tuu huyu Raisi wa Nigeria alifuta mkataba kwa makampuni mawili ya kusafisha mafuta ambayo ni ya washikaji zake Obasanjo na sasa kafuta tena huu wa vitua vya Afya hii ni hatua nzuri ila sidhani kuwa Muungwana anaweza kufanya haya maaana alishasema publicly kuwa hana nia ya kuwachunguza waliomtangulia, issue ya BOT nayo iko kima, watu walitemea mikataba ya madini itapitiwa upya, mikataba ya uuzaji wa nyumba za serikali itapitiwa upya, mikataba ya Tanesco na ubinafisishaji itapitiwa upya kwa kasi mpya, ari mpya na nguvu mpya ila hizo ni ngonjera tuu hayawezi tokea Tanzania.
 
Kosa la kiufundi la kwanza alilolifanya JK katika uongozi wake ni kushindwa kuishungulikia RICHMOND (RDC) na hiyo itam-cost kwenye uongozi wake wote na ndiyo maana ameshindwa hata kuwawajibisha wengine. Kitakachofuata itakuwa ni kuulizana ilikuwaje wahusika wa RDC akashindwa kuwashughulikia halafu aje awashughulikie wengine? Matokeo ya RDC ilikuwa ni kutolewa kafara kwa Dr Msabaha kwa kuhamishiwa wizara nyingine. Bunge na kamati yake vikabaki gizani na hakuna aliyenyenyua mdomo kutaka RDC ijadiliwe bungeni. Kila kikao kikija utasikia wanasema this time hoja binafsi itatolewa kuhusu RDC, matokeo yake kadhia ya RDC imekufa natural death na sasa tunaendelea kuwaangalia hao waarab waliopewa huo mradi na RDC wakati watu walishakomba hela tayari na PCCB imeishasafisha hiyo kashfa and life goes on as usual!

Kwa mantiki hiyo hata akina Twin Tower, Mali Asili na Utalii, Fedha za Nje za BoT na mengineyo tutaishia kupewa report kwamba kila kitu kilikuwa swafi na hakukuwa na harufu ya rushwa. Maana kama Muungwana alikaa kimya kwenye kasheshe ya RDC itabidi akae kimya kwenye kashfa zote zinazowagusa marais waliotangulia kwa kuchelea kujimaliza yeye mwenyewe na chama chake. I know ndani ya CCM bado kuna watu ambao ni pro-BWM na hivyo lolote atakalofanya ambalo litamgusa BWM kuna hatari ya kujiongezea maadui ndani ya chama na huwezi kujua wako sehemu zipi. Ndiyo maana hizi kashfa kila kukicha tunazisoma kwenye magazeti which means zinavuja toka serikalini.
 
Matokeo ya RDC ilikuwa ni kutolewa kafara kwa Dr Msabaha kwa kuhamishiwa wizara nyingine
mkuu hii sio kafara mbona? kila mara mtu akiharibu mahali huwa kunatabia ya kumwamisha ili aende sehemu nyingine kuharibu tena. Kwani watu wengi si walijua kuwa Mramba hapati potifolio? Hatuna utamaduni wa kuwajibisha walioharibu.
 
Mze AM,
Mwenye dada hakosi shemejiwe!!!
Tunakuelewa na walala hoi wote hata JK anajua ni jinsi gani Malo desiny walivyohujumu uchumi bila hala huruma mpaka mtoto Steve anadiliki tutuita wapayukaji,but don't forget history ni mwalimumzuri hata akina Bokasa,Mobutu,and Iddi Amin walifanya hivyobut the day will come sheria itachukua mkono kama siyo kwake basi Steve anaye wavarau watanzania atajua nguvu za umma.
Mungu Ibariki Tanzania na watu wake
 
Kwani Ben Mkapa akiwa na share au hata pesa kuna mbaya gani? Kama kuna ushahidi kuwa ameiba fedha alizo nazo, au alitumia madaraka vibaya, basi utoeni hapa ili tumhukumu nao.

Tuache kulalamikia utajiri. Si kosa kuwa tajiri. Kama utajiri umepatikana kwa wizi basi utolewe ushahidi, na Polisi waarifiwe.

Kuwa "clean" ni synonymous na kuwa "poor"?

Augustine Moshi

AM.
The way unavyomtetea BWM kwa nguvu zote tangu BCS really makes me wonder WHY?? Nakufananisha na MM kwa serikali ya TZ!
 
Kwani Ben Mkapa akiwa na share au hata pesa kuna mbaya gani? Kama kuna ushahidi kuwa ameiba fedha alizo nazo, au alitumia madaraka vibaya, basi utoeni hapa ili tumhukumu nao.

Kumhukumu bila ushahidi ni kinyume cha haki. Kuwa na mali si dhambi. Na kufanya kazi ya Uwaziri miaka nenda rudi, na baadaye Urais, kisha usiwe umehifadhi (save) fedha kiasi ni kosa. Utakuwa umetapanya malipo yako yote? Huo ni utumiaji mbaya wa fedha, na unaleta umasikini.

Tuache kulalamikia utajiri. Si kosa kuwa tajiri. Kama utajiri umepatikana kwa wizi basi utolewe ushahidi, na Polisi waarifiwe.

Kuwa "clean" ni synonymous na kuwa "poor"?

Augustine Moshi
__________________

Kwanza Augustine Moshi, naamini kama kweli unampenda mzee wetu Ben, ungenyamaza na si kumtetea kwa jambo usolijua, huko si kumtetea bali kumkandamiza.. Sisi tunaompenda kwa jinsi alivyosaidia kukua kwa uchumi wetu (japo sehemu aliimega) tunanyamaza na kuacha mambo yaendelee kuibuka na kumuombea Mungu kama atashitakiwa akute Magereza yametengenezwa na kuwekwa magodoro na kuomba Mungu, kama ataugua kama Chiliba, basi Mungu ampe tahfifu na serikali imsaidie na kumpa matibabu.. Tumuombe Mungu aendelee kumsaidia apate haki zake zote... Yaani kama alitenda memama, apewe haki yake kwa mema yake na kama alitenda maovu apewe haki kwa maovu yake..

Lakini hebu angalia... Ukweli hakuna ubaya kwa kiongozi kufanya biashara (baada ya Kuzikwa Azimio la Arusha, kule ZNZ), lakini je ni sawa kulazimisha Kiwira isimamiwe na Wizara ambayo Daniel Yona alikua Waziri wake? Je, ni sawa Ben na Yona na familia zao kumiliki hisa katika Kiwira? Huoni mgongano wa KIMASLAHI HAPO? Tafadhali utetezi wako unamuangamiza KAKA BEN, ni bora ukanyamaza, usiwape watu faida..

Hebu soma THISDAY ya leo ambayo nashangaa hapa katika net halipo.. Niko Dodoma naliona hapa likiwa na headline... KIWIRA COAL PROJECT OWNERSHIP: The Mkapa-Yona link, A TALE OF TWO POWERFUL FAMILIES AND THEIR INTERTWINING INTERESTS

Ikianza na maneno, "Former cabinet Minister, Daniel Yona, who held energy and mineral potfolio in the final years of the third phase government unde Benjamin Mkapa, has been identified as a major shareholder in the $271.8m Kiwira Coal-fired Project along with te ex-presidenr and his familiy."
 
Naona wameweka

http://www.thisday.co.tz/News/2497.htmlKiwira coal power project ownership:The Mkapa-Yona link

-A tale of two powerful families and their intertwining interests

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

FORMER cabinet minister Daniel Yona, who held the energy and minerals portfolio in the final years of the third phase government under Benjamin Mkapa, has been identified as a major shareholder in the $271.8m (approx. 340bn/-) Kiwira coal-fired power project along with the ex-president and his family.

Latest findings by THISDAY now indicate that both Yona and his son, Danny Yona, are also prominent shareholders of Kiwira Coal and Power Limited under the umbrella of Tanpower Resources Company Limited.

They are represented in the little-known but apparently high-powered Tanpower Resources through a private company called DEVCONSULT Limited, in which Yona senior owns 90 per cent of the shares while Yona junior holds the remaining 10 per cent.

THISDAY investigations have already established that Mr Mkapa and the former first lady, Mrs Anna Mkapa, have shares in the Kiwira company through their own private company ANBEM Limited, which was registered in 1999 with the couple as sole shareholders while they were still at State House.

Before being appointed minister for energy and minerals, Yona held a number of other key portfolios in the Mkapa government from 1995, including minister of state in the president's office (planning), and minister of finance.

Apart from the shares held by ANBEM Limited, it has also been established that Mr and Mrs Mkapa's son Nicholas Mkapa also has his own shares in the same Kiwira company through another company going by the name of Fosnik Enterprises Limited.

It is understood that Mkapa junior owns Fosnik Enterprises on a 50-50 basis with his wife, Ms Foster (Mbuna) Mkapa.

At the same time, Nicholas Mkapa's father-in-law Joseph Mbuna has also been discovered to be one of the shareholders and major figures in Kiwira Coal and Power Limited, which is based in Mbeya Region.

Mbuna, whose stake in the company is under the name of Choice Industries Limited company in which he is the majority shareholder, currently serves as chairman of the Kiwira Coal and Power Limited board of directors, whereby Nicholas Mkapa is one of the directors.

Like ANBEM Limited, DEVCONSULT Limited and Fosnik Enterprises Limited, Choice Industries Limited also falls under the umbrella of Tanpower Resources.

To put it in a nutshell, it has now been verified that Nicholas Mkapa and his father-in-law both sit on the Kiwira Coal and Power Limited board of directors, while former president Benjamin Mkapa and his wife are also among the company's listed shareholders through ANBEM Limited.

Other shareholders of the Kiwira company have been identified as Evans Mapundi and Wilfred Malekia through the Universal Technologies Limited company, which is also under the Tanpower Resources umbrella. Mapundi and Malekia also sit on the six-member Kiwira board of directors.

Tanpower Resources is now understood to own up to 85 per cent of shares in Kiwira Coal and Power Limited, with the remaining 15 per cent of shares being formally held by the government of the day.

The government is currently represented on the Kiwira company's board of directors by the Deputy Permanent Secretary in the Ministry of Infrastructure Development, Omari Chambo, while the Mbeya Regional Administrative Secretary, Ms Asumpta Ndimbo, also sits on the Kiwira board.

Serious questions have begun to be raised within government circles about the multi-billion shilling contract signed between Kiwira Coal and Power Limited and the Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) in March last year for the supply of 200 megawatts of electricity into the national power grid.

Impeccable sources privy to the contract details are now hinting at the growing possibility that the deal could eventually turn out to be another expensive trap for the national economy, along the same lines as the infamous 1995 IPTL affair.

According to THISDAY's sources, the signs of potentially disastrous discrepancies in the contract have started to emerge as delays continue to hamper the still-pending launch of the project ? more than 16 months since the signing.

The sources have already revealed that at least one 'big hand' in the Mkapa administration was responsible for exerting undue pressure on TANESCO officials to sign the contract with the Kiwira investors, and strongly hinted that the pressure came via the ministry of energy and minerals.

The controversial, 20-year power purchase agreement (PPA) which, among other things, gives the owners of Kiwira Coal and Power Limited enough discretion to calculate future power tariffs at will, was signed between the government, TANESCO and the private investor company.

Our sources now say TANESCO could end up being liable to pay Kiwira Coal and Power Limited a staggering $6m (approx. 8bn/-) each month once the firm starts delivering on the agreed 200MW of electricity.

This would bring TANESCO?s monthly obligations to three independent power producers (IPTL, Songas and Kiwira) to a figure exceeding $20m (approx. 26bn/-), which is well beyond the estimated $19.35m (around 25bn/-) per month that TANESCO currently earns from its revenues.
 
Kiwira coal power project ownership:The Mkapa-Yona link

Source: http://www.thisday.co.tz/News/2497.html
 
Augustine Moshi,
Na hapa je? Nadhani hata JK pamoja na utetezi wake hapa yamezidi!
 
Looh!!! mwanzoni nilikuwa siamini kwamba tumeibiwa mno, inaekea
jamaa wamechota kweli kweli.

Wale jamaa wa pale Kiwira, hawana hata share moja?
 
Mze AM,
Mwenye dada hakosi shemejiwe!!!
Tunakuelewa na walala hoi wote hata JK anajua ni jinsi gani Malo desiny walivyohujumu uchumi bila hala huruma mpaka mtoto Steve anadiliki tutuita wapayukaji,but don't forget history ni mwalimumzuri hata akina Bokasa,Mobutu,and Iddi Amin walifanya hivyobut the day will come sheria itachukua mkono kama siyo kwake basi Steve anaye wavarau watanzania atajua nguvu za umma.
Mungu Ibariki Tanzania na watu wake

.. you meant Maro Dynasty didn't you!
 
MASWALI KWA SERIKALI NA TANESCO:

Mkataba ulisainiwa March 2006. Kwanini Kikwete,Msabaha,Masha,na Mwanasheria Mkuu, walishindwa kunegotiate mkataba mzuri zaidi?

Je, serikali inaweza kuwahakikishia wananchi kwamba mkataba huu hautakuwa mzigo kwao na Tanesco?

MASWALI KWA GAZETI LA THIS DAY:

This day Magazine said:
It has lately been made apparent that the content details of the official 20-year power purchase agreement (PPA) signed by the three parties to the contract � the government, TANESCO, and Kiwira Coal and Power Limited � give the owners of the private company enough discretion to calculate future power tariffs at will - based on their own computations of final construction and production costs.

This, say our sources, could very well lead to a fall-out even worse than the infamous Independent Power Tanzania Limited (IPTL) affair of 1995, for which TANESCO is still forced to pay through its nose. They state that according to the terms of the PPA, Kiwira Coal Power Ltd would be allowed to periodically adjust upwards some of its key charges based on its operational costs and the future price of coal. According to the sources, TANESCO could well end up having to pay Kiwira Coal Power Limited � being owners of both the coal mine and power plant - a staggering $6m (approx. 8bn/-) each month once the firm starts delivering

Nadhani kilichoelezwa hapo juu ni kitu cha kawaida. Hakuna kampuni inayoweza kusaini mkataba ya kutoa huduma yoyote ile at a FIXED RATE for 20 yrs.

Mfano mdogo ni bei ya mafuta. Makampuni ya mafuta hupandisha bei kila wakati bei ya mafuta katika soko la dunia inapoongezeka. Bei ya mafuta inapaswa kupungua kwa watumiaji ikiwa kutakuwa na unafuu ktk soko la dunia.

Nitashangaa sana ikiwa SERIKALI na TANESCO na wao hawakuweka kipengele kinachowawezesha kuteremsha kiwango wanachowalipa Kiwira Coal & Power ikiwa bei ya makaa ya mawe itateremka ktk soko la dunia.

Mwandishi pia analalamika kwamba gharama za Tanesco zitakuwa kubwa sana. Haelezi kwamba baada ya kununua umeme toka kwa Kiwira Tanesco itakuwa inausambaza kwa watumiaji. Je, Tanesco itakuwa haipati mapato yoyote?

Ninavyoelewa mimi umeme wa makaa ya mawe ni bei rahisi kuliko umeme unaozalishwa kwa kutumia mafuta. Je, hakuna uwezekano kwamba Tanesco itapunguza gharama zake kwa kubadilisha source ya umeme from mafuta to makaa ya mawe?

MASWALI KWA MKAPA & YONA:
1.Wamewekeza kiasi gani ktk kampuni ya Kiwira?
2.Fedha walizowekeza zimepatikana kwa shughuli halali?
3.Je fedha na mali zao walikuwa wakiziorodhesha ktk daftari la Msajili wa Maadili ya Viongozi?

MASWALI KWA WANA JAMBO FORUMS:
1.Raisi,Makamu,Waziri Mkuu,Mawaziri,Makatibu Wakuu, by estimate wanapata mshahara na marupurupu kiasi gani?

2.Ideally, Raisi,Makamu,Waziri Mkuu, au Waziri, aliyetumikia miaka 10 anatakiwa awe na mali kiasi gani? At what point should we start questioning?
 
JokaKuu,
Good questions. Hata mimi nasubiri kuelimishwa.
 
Joka Kuu, Maswali mazuri sana na yanatoa changamoto kwa wahusika wote wakuu pamoja na kuwa yanaweza kutumika vibaya katika kukwamua wahusika.

Mkataba ulisainiwa March 2006. Kwanini Kikwete,Msabaha,Masha,na Mwanasheria Mkuu, walishindwa kunegotiate mkataba mzuri zaidi?

Je, serikali inaweza kuwahakikishia wananchi kwamba mkataba huu hautakuwa mzigo kwao na Tanesco?

Huu ni mfano hai wa jinsi serikali ya JK ilivyokua haijajiandaa kutawala na kujikuta inakamilisha na kutekeleza mambo yaliyokwisha kamilishwa na Ben. Mchakato wa Kiwira ulianza kipindi cha mwisho cha Ben na Baraza la Mawaziri chini ya Ben (japo JK na EL walikuwamo)na kwamba mbali ya THISDAY kuandika, kuna taarifa kwamba katika hali ya kushangaza Kaburu wa NET GROUP alikataa kusaini hadi akagombana na Msabaha na TANESCO wallilazimishwa kusaini. Kaburu huyo anaelezwa alianza kuwageuka waliomleta Tanzania hata katika kukataa kuagiza vifaa toka Afrika Kusini ambavyo vinaweza kupatikana Tanzania. Mwezi Machi ni kipindi ambacho bado WANAMTANDAO walikua wamelewa USHINDI WA KISHINDO na kwamba baadhi walijipa likizo baada ya kazi mpya na wengine walikua wakijipanga kushika nyadhifa mbalimbali na kupeana ulaji. Hapo ndipo wenye kujua michezo waliitumia nafasi hiyo na kuchangamkia zabuni hiyo.

MASWALI KWA MKAPA & YONA:
1.Wamewekeza kiasi gani ktk kampuni ya Kiwira?
2.Fedha walizowekeza zimepatikana kwa shughuli halali?
3.Je fedha na mali zao walikuwa wakiziorodhesha ktk daftari la Msajili wa Maadili ya Viongozi?

Naomba kuongezea maswali kwa Mkapa &Yona.
1. Je, walikabidhiwa mradi huo kwa tenda halali? na kulikua na ulazima gani kwao kulazimisha PSRC iachie mradi ili uende Wizarani alikokua Yona?
2. Je, walipokua wakijadili katika Baraza la Mawaziri, Mkapa na Yona waliwaambia wenzao kwamba wana hisa? Je Walitoka katika kikao ili kupisha wanaojadili wasiwaonee haya?

Kwa wana JF na THISDAY Tusaidiane kujua,
1. Je, Edgar Maokola-Majogo, aliondoka Nishati na Madini kwa sababu zipi?
2.Je, kampuni ya Kichina iliyoonekana awali katika mradi huo imepotelea wapi?
3. Je, Kiwira wataweza kweli kuzalisha 200MW?
4. Je, Kuna fedha nyingine zilizochukuliwa katika Taasisi za Fedha za Umma kwa ajili ya miradi hiyo?
5. Mwinyi na Marehemu Baba wa Taifa, JK Nyerere, wana vitega uchumi sawa na Mkapa? Vipi kuhusu Sumaye naye ana vitega uchumi gani vya wazi ukiachia mashamba ya Mvomero na Kibaigwa? Ili tuweze kulinganisha mafao yao maana nao wamekaa madarakani kwa miaka mingi hasa MWalimu Nyerere
 
Siamini kama JK atatoa tamko lingine kumtetea Ben
 
Back
Top Bottom