Ila huyu mzee, BM, sijui alikuwa anafanya biashara ya nini. Sheria za nchi zinamruhusu rais mstaafu kuhudumiwa kila kitu hadi mwisho wa maisha yake.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amekanusha kumtaja Rais mstaafu Benjamin Mkapa katika ripoti yake ya Mashirika ya Umma kuwa alitumia vibaya mkopo wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Ludovick Utouh, alikanusha habari zilizoandikwa na gazeti la MwanaHalisi la Mei 13 mwaka huu, kwamba Mkapa achota NSSF mabilioni ya shilingi na ashindwa kuyarejesha.
Napenda kukanusha taarifa hii, kwani katika ripoti yangu ya mashirika ya umma kwa mwaka unaoishia tarehe 30 Juni 2008, hakuna mahali nilipomtaja Mheshimiwa Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Katika ripoti yangu hiyo, aya ya 3.2.4 (ukurasa wa 74 hadi 77), nilitaka wakopaji tisa ambao kwa pamoja wamekopa NSSF jumla ya Sh 58,757,794,802 na katika deni lililotajwa na gazeti la MwanaHalisi la Sh 8,127,000,000 linahusu kampuni ya Kiwira Coal & Power Company, alisema.
Aliongeza kuwa kutaja jina la Rais mstaafu Benjamin Mkapa kama mkopaji badala ya mkopaji halali ni kinyume na ripoti yake na huo ni upotoshaji ambao angependa kuukanusha kwa nguvu zote. Ninaomba vyombo vya habari viwe huru kutumia ripoti yangu kama ilivyo na si vinginevyo, kwani kwa kutoa taarifa kama hiyo, kunapotosha umma na kunaweza kuleta mfadhaiko na chuki kwa waliotajwa isivyo halali, alisema.
Alisema lengo la vyombo vya habari ni kutoa taarifa sahihi bila kuongeza maelezo ambayo yanaweza kusababisha taarifa husika ieleweke visivyo na ni imani yake kuwa umma utaendelea kuhabarishwa juu ya ripoti yake kwa usahihi. Pale patakapokuwa hapaeleweki, naomba mje ofisini kwangu kwa ufafanuzi, kabla ya kuchapisha taarifa zinazopotosha na ambazo hazielezi yaliyo kwenye ripoti zangu, alisema Utouh.
Kwanini MKapa asifilisiwe ili kurudisha mikopo aliyokopa ambayo kuna ushahidi wa kutosha kwamba hana uwezo wa kuilipa?
Kwa hiyo alikopa kama kampuni. Habari ya kanuni against kukopesha mtu binafsi inakujaje hapo MwanaHALISI?
Mkopo anaodaiwa Mkapa umedhamiwa kwa asilimia mia moja na serikali. Kwa mujibu wa kanuni za Benki Kuu (BoT), kawaida serikali haidhamini mtu binafsi. Mkapa anahusishwa na umiliki wa mgodi wa mkaa wa mawe wa Kiwira kupitia kampuni yake ya ANBEM anayosadikiwa kumiliki na mkewe, Anna...
Kama hakuna uthibitisho kuwa serikali ilidhamini mkopo, sasa mmejuaje kwamba serikali imedhamini?... kwa kuwa alidhaminiwa na serikali, basi ni serikali itakayolazimika kulipa au kufuta deni. Hata hivyo, CAG anasema hakuna nyaraka zozote zinazothibitisha kuwa serikali ilidhamini mkopo huo.
Mali iliyowekewa dhamana au iliyowekwa dhamana. Na umeshasema serikali ilidhamini huu mkopo, sasa mali gani tena ilitakiwa kuwekwa dhamana kupata mkopo? MwanaHALISI, unaacha ma gap kibao kwenye reports zako.Mkataba wa mkopo huo ulitiwa saini 10 Julai 2007. Hata hivyo kuna udhaifu. CAG hakuona hati miliki ya mali iliyowekewa dhamana, jambo ambalo ni kinyume cha mwongozo wa NSSF juu ya vitegauchumi.
Poleni sana kwani Nyerere hakuwa mkabila na hakujua kuwa BWM ni machinga
Shida tuliyonayo hapa JF kwenye hii the so called vita dhidi ya ufisadi ni lack of strategies,hatujui kipi tushikilie,tuko hohehahe! ........ Mungu mbariki Maximo,JK, Manji, RA na wengine wote wazalendo wenye kulipenda Taifa letu,Simba na bila kusahahu Yanga.
Shida tuliyonayo hapa JF kwenye hii the so called vita dhidi ya ufisadi ni lack of strategies,hatujui kipi tushikilie,tuko hohehahe!
Kabla hata hatuashikilia msimamo wetu kuwa ilikuwa wrong kwa kiongozi mkuu wa nchi kufanya biashara,sasa tunataka kuwa alipe madeni hayo ama afilisiwe kwa kushindwa kuyalipa.
Kiukweli kama hakutakiwa kuwa na biashara akiwa ikulu basi anatakiwa kunyangwanya kila mali aliyojimilikisha isivyo halali ama arudishe mwenyewe kistaarabu.
Ingekuwa afadhali kama hata hiyo biashara ingeendelea na kulisaidia Taifa,wapi,pesa za mikopo zimeliwa na mgodi sijui kama hata unafanya kazi,hivyo huo ni ujambazi,ila hatujui utofauti wake kutokana na vurugu mechi iliyoko...Na ndio maana kuna watu wenye balls za kuufananisha mkopo na wizi wa mchana kweupe ndani ya forum hii,ni maajabu ya mzee Rajabu kuzaa mtoto anaitwa Rajabu.
Cha msingi hapa ni kuwaacha hawa viongozi wetu wastaafu wapumzike,tunachotakiwa kufanya kwa juhudi ni kuhakikisha kuwa Somaiya anatoa hizo miliioni mia nne kwa ajili ya vijana wetu wa uvccm ili waweze kufanya makongamano na kusafiri ili waweze kuona mengi kwa manufaa yetu sote.
Pia tuwe na mshikamano ili tuweze kuifikisha Taifa Stars kwenye kombe la dunia,pia Simba na Yanga,mengine yote tuwaachie viongozi wetu ili tusivunje amani yetu tuliyoizoea kabla hatushinda kombe la Afrika. Mungu mbariki Maximo,JK,Manji,RA na wengine wote wazalendo wenye kulipenda Taifa letu,Simba na bila kusahahu Yanga.
Mangi kama ni mbege umekunywa leo, basi imewekwa molases
Kama Mengi angeendelea kutaja hao anaodai mafisadi papa basi Mkapa angekuwa nambari sita kama si wa kwanza labada Mengi hakuwa na ugomvi nae. Maswali yoote haya huyu jamaa kakaa kimya anafikiri watz wanasogeza muda wasahau? anakinga ya kutoshitakiwa lakini hana kinga ya kunyamazia maswali yanayowakereketa watz wote katika kujua wapi zimekwenda rasilimali zao? kazi kwake...