Mie sishangai watu wanaomtetea Ben, nae ana wapambe wake, na pengine nae yumo humu kajisajili. sheria au sio sheria, hatuhitaji kwenda shule kujua kuwa raisi wa nchi kuomba mkopo na kununua mali akiwa bado katika ofisi yake ya uraisi huko ni kutumia madaraka yake vibaya: aa; wanaotoa mikopo wanapitisha document zake bila hata kuuliza swali kwa kuwa ni raisi; bee; yeye kulipwa mshahara mkubwa, na mkewe kulipwa mshahara wa ufirst lady ni ili kuwafanya wasiangalie pembeni: chee; hata kama kapata kihalali, tujiulize, kwanini mzee kifimbo hakuwa na hata kibanda cha maana hadi akajengewa na serikali wakati kastaafu? ye ndo hakuviona? tena alikuwa na nafasi nzuri sana maana enzi zake hata tulikuwa twapishana na almasi/dhahabu/tanzanite bila kujua thamani yake; mzee wa watu aliweka maslahi ya wananchi mbele hadi kifo kikamfika kwa mapenzi yake mema,; hawa wezi alowaachia nchi ndo wanaifilisi kwa kasi na ari mpya; Ben anamiliki mali ambazo hata hawezi kuzitumia, huyo bibie Anna na tamaa yake ya mzee fisi ndo kanunua kila kitu, bora alirudisha zile nyumba za serikali alizo nunua(or so am told), kabakiza nyingine hata kazisahau, mama mwizi yule!