William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,466
Hitimisho: Hapa suala ni kwamba, Kikwete and his inner circle wameshaona kuwa wamechemsha big time, hivyo wanachokifanya ni kumchafulia mzee Ben jina ili watu wasipate fursa ya ku-compare utawala wake (mtalii Kikwete) na ule wa mzee Ben (mtu safi).
..ukisema mtu ni msafi unamaanisha nini?
Labda ana maanisha...Anayeoga mwili na kupiga mswaki kila siku..!!
Mnafiki huyu alipokuwa serikalini alitaka tule majani tulipomwambia mambo yaliyo na mashiko ndani yake. Yaani pesa ya kununua ndege ifanye kazi nyingine.Mramba amlipua Mkapa!
2008-08-13 15:47:06
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Katiaka kile ambacho pengine hakikutazamiwa kutokea, Waziri wa zamani katika Serikali ya Awamu ya Tatu ya Rais Benjamin Mkapa na ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rombo, Mheshimiwa Basil Mramba, amemlipua kiaina Rais Mstaafu Mkapa kwa kuiponda Serikali yake kuhusu sera ya viwanda.
Mheshimiwa Mramba amesema Serikali hiyo ya awamu ya tatu ( iliyokuwa ikiongozwa na Rais Mkapa), kamwe haikuwahi kutekeleza sera ya viwanda.
Akizungumza bungeni jana wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Mheshimiwa Mramba akazidi kueleza kuwa kwa kasi iliyokuwepo katika serikali ya awamu ya tatu, nchi ingechukua muda mrefu sana kuwa na viwanda.
``...Nina tatizo. Najua watu watauliza, si (nawe) ulikuwepo. Lakini wacha niseme,`` ndivyo alivyoanza kueleza Mheshimiwa Mramba kabla ya kuchangia zaidi.
Aidha, Mheshimiwa Mramba aliwageukia wajumbe wa Halmashauri ya CCM ,NEC na kuwahoji kuhusu sera ya viwanda vidogovidogo.
``Simuoni Bw. Yusuf Makamba, Katibu Mkuu wetu wa CCM... lakini nawaona wajumbe wengi wa Halmashaurii Kuu ya Taifa. Nauliza, hivi CCM ina Sera ya viwanda vidogo vidogo?`` Akahoji Mheshimiwa Mramba ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.
Akasema viwanda vilivyopo sasa ni matokeo ya sera za Serikali ya Awamu ya Kwanza iliyokuwa ikiongozwa na Rais wa wakati huo, Marehemu Mwalimu Nyerere.
Akasisitiza kuwa viwanda vingi vilivyopo leo ni vya Nyerere na kwamba sera yake ilikuwa ni viwanda vya awali, ambayo amesema kamwe haijatekelezwa katika serikali ya awamu ya tatu (ya Rais Mkapa).
Hata hivyo, Mheshimiwa Mramba akasema anafurahia kuona Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko ameipeleka bungeni, huku akishauri kuwa Serikali ya sasa ya awamu ya nne, ijielekeze katika jitihada za kuchochea uanzishaji wa viwanda.
Pia akaishauri serikali kusamehe kodi kwa viwanda vidogo vidogo kama inavyofanya kwa viwanda vikubwa ambavyo vimekuwa vikipata msamaha.
Aidha, ametaka kuanzishwa kwa benki maalum kwa ajili ya viwanda vidogo ama kuziagiza benki kutenga fungu maalum kwa ajili ya kuwakopesha wanaoanzisha viwanda hivyo.
SOURCE: Alasiri
Tuma Maoni Yako
Nilitaka kuuliza the same... wakati yuko madarakani (kwa serikali ya mpaka!) muda wote huo hakujua kuwa hilo na kushauri ipasavyo?... hebu atuondolee usanii wake huko!. Leo ndo anajua kuwa hatuna sera?
Hakika kama Mramba kamkandia Mkapa mimi naketi chini na kutafakari kwamba kwanini ametoa kauli kama hizo. Jibu ninaloweza kupata ni kwamba lazima kuna kitu kisicho cha kawaida kati ya Mramba na Mkapa kinatokota hili si bure. Mramba "Mla majani" mradi ndege ya Rais Mkapa inunuliwe leo unamsaliti Rais wako???
Yaelekea ukuwahi kumalizia sentensi yako hapo juu, naona kifungo kilikupata wakati unaendelea kuchangia hapa... Anyway siku saba sio nyingi... ukitoka huko uje kumalizia mstari wako...jamani tuwe watu wa kukubali ukweli sio kum
Anakosoa nini mnafiki huyu? sisi tunachopingana naye huyu fisadi Mramba si kupinga sera za serikali ambazo kahusika kuzibuni na kuzitunga tu bali pia ni kulamba matapishi.Kama Mtanzania anahaki ya kukosoa anachokiona hakiendi sawa, na mara nyingi mtu huona makosa anapokaa nje kuliko aliyeuwanjani. mimi naona ni sawa yeye kusema hayo. Pia unapokosea wewe haimaanishi uendelee kukubali makosa ya wenzio!!!!, ni lazima watanzania tubadilike, askari anapomkamata mlarushwa tusiulize mbona yeye jana kapokea/kadai rushwa. kila mwenye nafasi ya kurekebisha na afanye jukumu lake bila kujali alikosea lini na wapi.
Tulisema pole pole, wataanza kutemana wenyewe kwa wenyewe, walete hao ndio tatizo la kuwa fisadi huwezi kumuamini fisadi mwenzako hata siku moja!
mnafiki Huyu Alipokuwa Serikalini Alitaka Tule Majani Tulipomwambia Mambo Yaliyo Na Mashiko Ndani Yake. Yaani Pesa Ya Kununua Ndege Ifanye Kazi Nyingine.
Leo Atatuambia Nini Mwizi Mkubwa Huyu?