Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Ripoti ya ufisadi EPA yavuja

Habari Zinazoshabihiana
• Balozi Mwapachu azidua ripoti ya maendeleo 28.04.2006 [Soma]
• Sakata la ufisadi Wizara yashindilia lawama Muhimbili 06.03.2008 [Soma]
• Bunge halijaona ripoti ya ubadhirifu BoT 16.01.2008 [Soma]

*Yadai Utawala wa Mkapa ulishindwa kuuzuia
*Kampuni zenye fedha zao zatinga mahakamani

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI ya Awamu ya Tatu chini ya Rais Mstaafu, Bw. Benjamin Mkapa, ilishtukia harufu ya ufisadi kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), iliyokuwa kwenye Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tangu mwaka 1997 lakini ikashindwa kuizuia.
Makosa hayo ya utawala wa Mkapa ndiyo yaliyoendelea kuruhusu mwanya wa ufisadi kwenye akaunti hiyo hadi Januari, mwaka juzi ulipoingia utawala wa Rais Jakaya Kikwete. Hayo yamo kwenye ripoti ya ukaguzi iliyofanywa na kampuni ya Ernst & Young ambayo gazeti hili limenasa nakala yake.
Katika kipindi cha wiki kadhaa, ripoti hiyo iliyokuwa siri kubwa, imekuwa ikisambazwa kwa kasi miongoni mwa watu mbalimbali baada ya kuvuja kutoka serikalini. Ripoti hiyo ndiyo iliyosababisha Rais Kikwete kumfuta kazi aliyekuwa Gavana wa Benki hiyo, marehemu Dkt. Daud Balali na kuingia Profesa Benno Ndulu.
Utata wa malipo ya EPA Ripoti hiyo inaanika kuwa tangu mwaka 1997 Serikali ya Mkapa ilianza kubaini utata katika uendeshaji wa akaunti ya EPA na kuanza kuihoji BoT ikitaka maelezo ya kina kuhusu akaunti hiyo.
"Tume ya Ukaguzi imebaini kuwa kupitia barua ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hazina (Raphael Mollel) ya Oktoba 17, 1997, Wizara ya Fedha ilianza kuwa na shaka kuhusu uendeshaji wa akaunti ya EPA," inasema ripoti ya Ernst & Young na kukariri sehemu ya barua hiyo ya Mollel kwenda BoT iliyoandikwa:
"Hazina ingefurahi kama ingeweza kupata hesabu halisi ya fedha zilizoko kwenye akaunti ya EPA, ili iweze kuweka sera nzuri zaidi katika matumizi ya fedha hizo."Kama unavyojua Hazina imekuwa ikipata tetesi zinazotofautiana kuhusu hali halisi ya akaunti hiyo. Wakati fulani iliashiriwa kwamba hakuna pesa yoyote kwenye akaunti hiyo na kuwa madeni yangepaswa kulipwa kupitia raslimali za nchi."Uchunguzi huo hata hivyo umebaini kuwa pamoja na barua hiyo, uongozi wa BoT haukuwa tayari kutoa ushirikiano huo, jambo ambalo sasa linazidi kuiongezea nguvu dhana, kwamba ufisadi kwenye akaunti hiyo ulianza kufanyika siku nyingi.
Baada ya miaka mingi ya ukimya, hatimaye katika barua yake ya Julai 2005, kwenda kwa Katibu Mkuu wa Hazina, Bw. Gray Mgonja, Gavana wa Benki Kuu wakati huo, Dkt. Ballali, aliashiria kuwa isingekuwa rahisi wao kutoa hesabu halisi ya fedha zilizokuwa kwenye akaunti ya EPA. Akataja tatizo la mfumo wa kompyuta."Ifahamike kuwa ni vigumu kwa sasa kutoa hesabu halisi za akaunti ya EPA, kwa sababu malipo yote yanafanyika kadri maombi (ya wadai) yanavyokuja na hakuna muda maalumu. Hata hivyo pindi matatizo ya kiufundi katika mfumo wetu wa kompyuta yatakapokuwa tayari, tutakuwa katika nafasi nzuri ya kutoa mchanganuo," ilisema barua hiyo. Tofauti na maelezo hayo ya Dkt. Ballali, hesabu za wadai zilizo sahihi na zilizokuwa na utata zilikwishawekwa bayana kupitia ripoti ya Lazard iliyokamilika mwaka 2004 na zaidi, wakati BoT wakisingizia mtandao wa kompyuta kuwa mbovu, mtandao huo huo ndio mwezi mmoja uliofuata, uliotumiwa na watendaji wa Benki hiyo kuidhinisha malipo kwa kampuni 22.
Uchunguzi unaonesha kuwa wakati Dkt. Ballali akiieleza Serikali kuwa kulikuwa na tatizo la kompyuta, lakini malipo yakaendelea kupitia orodha zilizokuwa kwenye mtandao huo, hadi mauti yanamfika jijini Washington, Marekani, hivi karibuni. Hakuwahi pia kuipa Serikali taarifa rasmi kuhusu EPA kama alivyoahidi na kama ilivyoombwa tangu mwaka 1997 na Serikali nayo ilionekana ghafla kuondoa wasiwasi wake juu ya akaunti hiyo."Timu ya ukaguzi haikupata ushahidi wowote kuwa mchanganuo huo uliwahi kuwasilishwa kwenye Wizara ya Fedha," inakariri Ernst & Young katika ukurasa wa 19 wa ripoti yake. Mchanganuo mgumu?Wakati viongozi BoT wakishindwa tangu mwaka 1997 kuonesha mchanganuo wa fedha za EPA, uchunguzi wa kikaguzi umedhihirisha kuwa katika akaunti ya fedha hizo namba 9991 509 101 ambayo awali ilikuwa NBC kabla ya kuhamishiwa kwenye akaunti namba 9924 191 011 iliyokuwa BoT, ushahidi kadhaa uliopatikana umehitimisha kuwa mfumo wa kompyuta ya akaunti hiyo haukuwa na hitilafu yoyote na ulikuwa ukiendelea kutumika. Kwa mfano, hadi mwaka 2004 takwimu halisi kuhusu akaunti ya EPA zilikuwa hivi:
Madeni yaliyohakikiwa na kulipwa dola milioni 228,
madeni ambayo wadai waliruhusu yafutwe (ikiwa sehemu ya msaada) dola milioni 216. Jumla ndogo dola milioni 444.
Hesabu zaidi za akaunti hiyo zinaonesha kuwa sehemu kubwa ya deni hilo iliyosalia ilikuwa haijalipwa kwa sababu mbalimbali kama ifuatavyo:
Madeni yaliyokuwa na utata/kesi dola milioni 25, wadeni waliokataa masharti (ya mkusanya madeni) dola milioni 14,
deni lisilokidhi viwango (cha mkusanya madeni) dola milioni tatu, wadai ambao hawakujitokeza kabisa dola milioni 48, deni ambalo ilishindikana kuhakikiwa, dola milioni 143, jumla ndogo dola milioni 233 na jumla ya deni lote (lililolipwa na lililobaki na utata) dola milioni 677. Kwa mujibu wa mapendekezo ya Mkaguzi wa Kimataifa M/S Lazard aliyefadhiliwa na Benki ya Dunia, BoT ilishauriwa kutolipa deni lililosalia lenye utata la dola milioni 233, kutokana na utata ulioanishwa hapo juu na ushauri huo ulikuja kutiliwa nguvu baadaye na ripoti nyingine ya wakaguzi wa PriceWaterhouseCoopers ya Ufaransa. Lakini mwaka mmoja baadaye, BoT hiyo hiyo ikaibuka, katika mazingira tata na kuanza kuwalipa waliojiita mawakala wa kampuni hizo za nje. Kipindi chote hicho Serikali iliyokuwa imekwishaona utata na iliyokuwa ikinyimwa ripoti za akaunti hiyo, haikuonekana kuwa na wasiwasi tena."Ripoti (ya wakaguzi kutoka M/S Lazard) ilihitimisha kuwa sehemu kubwa ya madeni yalishapitwa na wakati na ikaishauri Wizara ya Fedha kutoyalipa," inasema ripoti ya Ernst&Young, Wizi wa kisomi Huku zikitumia mihuri ya mawakili wenye majina na maelezo hewa, nyingi kati ya kampuni 22 zilizopitishiwa malipo kutoka akaunti ya EPA, sasa imebainika kuwa zilighushi nyaraka mbalimbali. Ernst & Young wanaonesha kuwa kati ya sh. 133,015,186,220 zilizochotwa kutoka EPA, nyaraka zilizowasilishwa na zile kampuni 22 zinazotuhumiwa kuchota sh. 90,359,078,804, 13 zilibainika kuwa za kughushi. Ripoti ikaeleza zaidi kuwa kiasi kilichosalia cha sh. 42,656,107,416.61 haikuweza kubainika mara moja usahihi au ubatili wake, kwa sababu mbalimbali ikiwamo kukosekana nyaraka zozote au sehemu ya fedha hizo kuwa na kesi mahakamani. Serikali kizimbani Hivi sasa pamoja na kuwapo kesi za awali, imebainika kuwa baadhi ya kampuni ambazo majina yao yalitumika katika ulaghai wa fedha za EPA ikidaiwa kuwa yalitoa ruhusa madeni yalipwe kwa niaba yao, yamekana kufanya hivyo na baadhi pamoja na mambo mengine, yakilalamikia uzembe wa Serikali ya Tanzania kupitia BoT kwa kuwalipa watu ambao wao kamwe hawakuwa na mikataba nao. Majira Jumapili ilijaribu kuwasiliana na baadhi ya kampuni zilizoingizwa katika utapeli wa EPA kwa fedha zao kulipwa mawakala hewa, karibu zote ziliamua kutolizungumzia suala hilo, huenda zikisubiri hatua za kisheria.Watendaji wa kampuni za Mirrlees Blackstone ambayo kuanzia mwaka 2002/03 ilibadili jina na kuitwa Man B & W Diesel Limited, Metsopaper na Iveco ambazo ni miongoni mwa wahanga wa majina na mihuri yao kughushiwa, hawakupenda kulizungumzia sana suala hilo kwenye vyombo vya habari walipotakiwa na gazeti hili kulizungumzia. Sakata la EPA kwa kifupi Kati ya mwaka 1970 na 1980, Serikali ya Tanzania ilipokea huduma mbalimbali kutoka kampuni na taasisi za nje, lakini kushuka kwa thamani ya shilingi kulikochangiwa na vita ya Kagera kunaifanya Serikali ishindwe kulipa madeni hayo kutokana na ukosefu wa fedha za kigeni.Kati ya mwaka 1985 na 1995, Benki ya Dunia iliona haja ya kuisaidia Tanzania kulipa madeni hayo kupitia mikakati mbalimbali ukiwamo wa kuyanunua (Debt Buy Back).
Mwaka 1985 Akaunti ya EPA ilihamishwa kutoka NBC kwenda BoT.Mwaka 1994, ili kuhakiki wadai halisi, Tanzania ilitangaza kwenye vyombo vya habari vya kimataifa wenye madai wajitokeze. Kampuni chache sana zikaitikia mwito huo.

Its pay back time.Too many corrupt case its like releasing a pack of rabbits infront of hunters-you dont know which to target.
 
Fisadi huyu atasema kuhusu ulafi wake alioufanya kujilimbikizia utajiri wa kupindukia? Kawa Bubu siku hizi.

CUF challenges Mkapa to declare his wealth

2008-07-03 10:29:19
By Correspondent Austin Beyadi

The Supreme Governance Council of the Civic United Front (CUF) has challenged former president, Benjamin Mkapa, to disclose his wealth and answer various allegations leveled against him.

Addressing a news conference yesterday in Dar es Salaam, CUF national chairman, Prof Ibrahim Lipumba, said Mkapa should declare all his properties and wealth he acquired during his ``truth and transparency`` ten-year rule.

Lipumba said that when the former leader came to power, he disclosed his wealth, including two houses-one in Masasi and the other in Dar es Salaam, 100 trees of cashew nuts and an undeveloped land located on the outskirts of Dar es Salaam.

``If Mkapa was able to disclose his wealth and properties that time why is it becoming too hard for him to disclose what he has after serving as president.

This is a clear indication that there is something wrong with the way he acquired the wealth,`` said Lipumba.

He said that Mkapa`s statement which he issued at his home village of Lupasso in May this year where he called those who issued allegations against him, as liars and people with personal hatred, was not enough to save him from the deep rooted accusations.

Additionally, Lipumba challenged former Attorney General and Minister for Infrastructure Development, Andrew Chenge, to issue a clarification to Tanzanians on how he was able to secure USD1m which was discovered by UK`s serious fraud office in Jersey`s offshore account.

``Even if he had never used a single cent of his salaries which he was receiving since he became a public servant, he could have not made enough to have a bank account of more than 1bn/-,`` he said.

In 2005, Mkapa allegedly `fast tracked` privatisation and ultimate sale of the government-owned Kiwira Coal Mine at a knock-down price of USD700,000.

Out of the USD700,000 purchase price, Mkapa`s Tanpower Resources is said to have made a down payment of only 70m/- for a majority stake in the coal mine.

It has also been reported that in 2004, Mkapa, former Energy and Minerals minister Daniel Yona, and their close relatives jointly registered another private company under the name of Tanpower Resources Ltd.

While still in office, Mkapa and former First Lady Anna Mkapa, allegedly registered a private company, ANBEM Ltd in 1999 listing themselves as sole directors and entrepreneurs.

With ANBEM Ltd operating from within State House, Mkapa and his wife are said to have obtained loans of up to USD75m from different local banks.

SOURCE: Guardian

Comment on this article
 
Fisadi huyu atasema kuhusu ulafi wake alioufanya kujilimbikizia utajiri wa kupindukia? Kawa Bubu siku hizi.

Kawa BUBU ANAYETAKA KUSEMA.
UMESAHAU.."UONGO UONGO UONGO"-BW MKAPA
 
Mkapa avishukia vyombo vya habari
Mwandishi Wetu
Daily News; Sunday,July 06, 2008 @00:01

Leadership Challenges" –Kuibadilisha Tanzania: Changamoto za Uongozi (1985-1995), alisema wakati alipoingia madarakani alikuwa na jukumu la kuleta mabadiliko ya uchumi na siasa.

Sema kweli kwamba wakati ulipoingia madarakani ilikuwa na nia ya kufanya ufisadi na hata ikibidi kuwaibia Watanzania mchana kweupe.
 
Sijaelewa.

1985-1995?

Hilo jukumu anaendeleza wa Sasa!
 
Na kweli ameibadilisha maana biashala mpaka ikulu haijawahi kutokea duniani. Hongela Che Nkapa.
 
Ukweli wa Kiwira kutobolewa leo
Mwandishi Wetu, Dodoma
Daily News; Tuesday,July 08, 2008 @00:01

Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, leo anatarajiwa kutoa ufafanuzi wa sakata la mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira ambao umekuwa ukidaiwa kuuzwa kwa bei ya ‘chee’ kwa kampuni yenye uhusiano na Rais mstaafu Benjamin Mkapa.

Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia gazeti hili, hatua hiyo imefikiwa kutokana na agizo alilolitoa Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akihitimisha mjadala wa Bajeti ya Ofisi yake bungeni.

Kabla ya kutolewa kwa agizo hilo la Waziri Mkuu yamekuwapo madai yaliyowahi kutolewa ndani na nje ya Bunge kuwa kuna utata katika ununuzi wa hisa za kampuni ya Kiwira Coal and Power Ltd (KCP) inayomiliki mgodi wa Kiwira, huku Rais mstaafu Mkapa na mkewe, Anna, wakitajwa kuwa ni miongoni mwa wamiliki.

Hata hivyo, hivi karibuni uongozi wa KCP ulitoa maelezo kwamba kampuni ya ANBEN inayomilikiwa na Mkapa na mkewe ambayo awali ilikuwa sehemu ya Tanpower, ilijitoa baada ya baadhi ya wanahisa wenzake kuwa na mpango wa kununua mgodi wa Kiwira.

Yamekuwapo malalamiko kwamba KCP ilinunua mgodi huo kwa Sh milioni 700 wakati umejengwa na Serikali kwa Sh bilioni nne. Lengo la baadaye ni kuwezesha mgodi huo kuzalisha umeme na kuuuza kwa Kampuni ya Umeme Tanzania (Tanesco).

Maelezo ya Kiwira yanatarajiwa kutolewa wakati Wizara ya Nishati na Madini itakapowasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha wa 2008/2009, huku masuala ya madini na mafuta, yakitarajiwa kuendelea kuwa kinara katika mjadala wa wabunge kwa wizara hiyo.

Waziri, William Ngeleja anatarajiwa kuwasilisha makadirio hayo baada ya kipindi cha maswali na majibu katika kikao cha 20 cha Mkutano wa 12. Suala la madini limekuwa moja ya matatizo makubwa katika sekta ya nishati na madini, kiasi kwamba Serikali ya Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete, imeamua kulivalia njuga.

Hali hiyo ilimlazimu Rais Kikwete kuteua Kamati ya kufuatilia masuala hayo ya madini ambayo iliongozwa na Jaji Mark Bomani, na hivi karibuni ilikabidhi ripoti yake kwa Rais. Tayari ripoti hiyo imekabidhiwa kwa Waziri Ngeleja kwa ajili ya utekelezaji na inategemewa kwamba mapendekezo yake yatakuwa miongoni mwa masuala ya kipaumbele katika hotuba yake leo.

Sekta ya madini imekuwa ikilalamikiwa na wananchi wengi kwa madai kuwa kampuni za kigeni zimekuwa zikipata faida kubwa kutokana na rasilimali hiyo, lakini Watanzania wamebaki kuwa masikini kwa kuambulia kiasi kidogo kinachotokana na rasilimali hiyo.

Katika mikutano ya Bunge iliyopita, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), aliibua hoja kuhusu mradi wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, kiasi cha kusababisha kusimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa madai ya kulidanganya. Baadaye Rais Kikwete aliunda Kamati ya Madini ambayo miongoni mwa wajumbe wake, alikuwa ni Mbunge huyo kijana wa Chadema.

Mbali ya madini, eneo jingine linalotarajiwa kuchangiwa na wabunge ni nishati hasa mafuta ambayo kwa sasa bei yake imekuwa ya kutisha. Wabunge mara kwa mara, wamekuwa wakipendekeza serikali kurudisha utaratibu wa kudhibiti nishati hiyo ili kuzuia mfumko mkubwa wa bei, ingawa kwa sasa tatizo limekuwa kupanda kwa kiasi kikubwa kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kunakochangiwa na sababu mbalimbali.

Bei ya dizeli na petroli kwa sasa imefikia Sh 1,790 na 1,970 kwa lita nchini. Kwa mujibu wa ratiba ya mkutano huu wa 12 wa Bunge, makadirio ya Wizara ya Nishati na Madini yatajadiliwa kwa siku mbili kabla ya kesho Waziri Ngeleja kuhitimisha mjadala wake kwa kujibu hoja za wabunge, kabla ya kuamua kuyapitisha au kutoyapitisha makadirio hayo.

Tayari wabunge wamekwisha kujadili hotuba ya Bajeti ya Serikali iliyowasilishwa Juni 12, mwaka huu na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. Pia mijadala ya Wizara zilizokwisha kujadiliwa ni Ofisi ya Waziri Mkuu; Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma); Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu na ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
 
Leo Waziri wa Nishati na Madini Bw. Willliam Ngeleja atasoma bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake. Wizara hii kama mnakumbuka ndiyo iliyozua kasheshe la Buzwagi na ndiyo ambayo imegubikwa na kashfa nyingi na za ajabu. Je leo wataleta jambo jingine jipya, je leo watatoa majibu ya maswali ya watanzania wengi?

Maswali muhimu

Kati ya majibu ambayo yanatarajiwa kutolewa leo ni kuhusu kampuni ya Meremeta na makampuni mengine ya madini ambayo yamegubikwa na kashfa kubwa. Nani anamiliki Meremeta? Kwanini mahesabu ya Meremeta hayachunguzwi na Mkaguzi Mkuu kama kampuni hii ni ya serikali? Leo kutakuwa na kasheshe na kuna mtu katupiwa kamba ameambiwa ajinyonge!

Lakini kati ya maswali muhimu ni hasa kuhusu Kiwira na uhusiano wa kampuni hiyo na viongozi waliokuwepo madarakani wakati inauzwa kwa Tanpower kwa bei ya chee. Leo inatarajiwa Bw. Ngeleja atatoa maelezo kuhusu Kiwira na kuhalalisha ushiriki wa namna yoyote ile wa Rais na Waziri wake wa Madini.

Kwa vile serikali inatabia ya kusahau, nimeona niwakumbushe jambo moja:

Katika hotuba yake kwenye Bunge la Bajeti la mwaka 2004/2005 aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Bw. Daniel Yona alisema hivi kuhusu mgodi wa Kiwira:

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2003, mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira ulizalisha tani 54,610 za makaa yaliyosafishwa ikilinganishwa na tani 79,210 mwaka 2002. Hali ya uzalishaji inazidi kuzorota kutokana na uchakavu wa vifaa na mitambo iliyoanza kutumika takriban miaka 20 iliyopita. Kwa kuwa mgodi ulijengwa kwa teknolojia, msaada na mkopo kutoka serikali ya China, juhudi za kumtafuta mbia ili aweze kuufufua mgodi huo zimekuwa zikielekezwa kwa makampuni kutoka China. Hata hivyo, kwa kuwa jitihada hizo za muda mrefu hazijazaa matunda, sasa PSRC imefungua milango kwa wawekezaji wengine watakaojitokeza.

Katika kifungu hicho tunaweza kuona mambo makubwa matatu; a) Kiwira ina mitambo iliyochokaa, b) Mbia alikuwa anatafutwa kutoka China, c) Jitihada hizo hazikuzaa matunda d)PSRC imefungua milango kwa "wawekezaji wengine".

Umuhimu wa hoja hii:

Kwa mtu yeyote mwenye kuelewa utendaji kazi ataona kwamba Waziri Daniel Yona alikuwa na taarifa za ndani za hali ya Mgodi wa Kiwira na alijua maendeleo ya utafutaji mbia yalivyokwama na alijua milango "imefunguliwa". Kwa maneno mengine, Daniel Yona alikuwa na "inside information" ya hali ya Kiwira ambayo (kama nitakavyoonesha dakika chache baadaye) alizitumia kufanikisha malengo yake ya kibiashara.

Mawasiliano na Mkapa:

Ni kutokana na ujuzi huu Waziri Yona alimwambia Rais wake kuhusu hali ya mgodi wa Kiwira na jinsi gani "milango imefunguliwa" katika uwekezaji. Wawili hao (mmoja mkuu wa nchi na mwingine waziri wa sekta husika) walipokubaliana kushikiriana. Mantiki inalazimisha kuamini kuwa Yona asingeweza kwa namna yoyote kujiingiza katika biashara ya makaa ya mawe hususan kuanzisha kampuni ya madini na kuweza kuchukua mgodi wa Kiwira kiulaini. Ni lazima angemshirikisha Rais wake. Kama Rais Mkapa angetaka kujitoa angeweza lakini nafasi ya fedha na hali ya nishati nchini lilikuwa ni jaribio ambalo alishindwa kulishinda na kama nzi anayefia kidondani akaingia kichwa kichwa.

Kampuni kuundwa:
Ni kutokana na ujuzi huo miezi chini ya sita baada ya hotuba hiyo Waziri Yona Na Rais wake Mkapa wakaanzisha kampuni yao ya madini tarehe 29 Disemba 2004. Kampuni hii ndiyo inaitwa Tanpower Resources Limited. Wakati wa kuandikishwa kwake wahusika wakubwa walikuwa ni Daniel Yona(waziri wa sekta), Anna Mkapa (mke wa Rais), Nicholas Mkapa (mtoto wa Rais), Joseph Mbuna (Baba Mkwe wa Niko), na Evans Mapunda. Rais Mkapa mwenyewe alikuwa ni mwanahisa kupitia kampuni yake ya ANBEN iliyoanzishwa mwaka 1999.

Cha kushangaza:

Jambo kubwa la kushangaza ni kuwa kampuni ya Tanpower Resources ilianza mawasiliano na serikali kuhusu Kiwira tarehe 15 Disemba, 2004 karibu wiki mbili kabla ya kuandikishwa rasmi. Kujitoa kwa kampuni ya ANBEN katika Tanpower kulikuja miezi miwili baadaye baada ya mazungumzo ya kuchukua Kiwira yalipoanza na si kabla yake.

Kampuni hiyo ya Tanpower ilifanya mawasiliano na Yona (ambaye pia yumo Tanpower) na akijua kinachoendelea kuhusu Kiwira jinsi ya kuweza kuichukua Kiwira. Kwa maneno mengine, Yona alienda mtumbani, kajua nini kinauzwa, kina hali gani, na amekubaliana na dalali, halafu wakati bei zinarushwa ananyosha mkono na kusema ana nia ya kununua kitu fulani ambacho ni yeye pekee anayejua ubora wake na hali yake!

Bomu:

Wakati mipango ya kuchukua Kiwira ikiwa imepamba moto huku Yona, Mkapa na kampuni zao wakijua nini kinaendelea waliweza hatimaye katikati ya 2005 kampuni hiyo ya Tanpower ikaingia makubaliano na serikali (yaani Yona -raia- anaingia mkataba na Yona-Waziri)! Hata Profesa Ndumba Nangae asingeweza kufanya mazingaombwe ya namna hiyo.

Matokeo yake ya kuingia ubia huo kununua hisa za Kiwira
Kwa vile serikali na wabunge wanaweza kusahau, nimejivika jukumu la kuwakumbusha. Kwamba katika hotuba yake ya Bajeti ya Wizara hiyo hiyo mwaka 2005/2006, Waziri Yona hakugusia kabisa Kiwira na maendeleo ya hali yake. Hii ingemshangaza mtu yeyote anayefuatilia suala la Kiwira. Kama alitoa taarifa ya hali mbaya ya mgodi huo na ya kuwa jitihada za kutafuta mwekezaji mwingine zinaendelea na ya kuwa milango imefunguliwa kwanini asitoe taarifa ni kina nani wamepita kwenye "milango" hiyo?

Of course asingeweza kufanya hivyo, kwani mlango walikuwa wamebanana, yeye, Rais wake, familia zao na jamaa zao! Ni aibu na hofu ya kusutwa Bw. Yona hakugusia suala la Kiwira Bungeni kwenye bajeti yake ingawa alijibu maswali ya juu na reja reja ambayo hayakugusia mchakato wa kutafuta mwekezaji!

Kimsingi Daniel Yona na Mkapa kwa kutumia nafasi zao wamelipora Taifa mgodi na sidhani kama Ngeleja atakuwa na ujasiri wa kusema hivyo.

Wamevunja sheria?
Sheria ya maadili ya viongozi wa umma ya mwaka 1995 (na mabadiliko ya 2005) inasema hivi na ninaamini ni baadhi ya vipengele ambavyo Yona na Mkapa wamevivunja:
12. A public leader shall be considered to have breached the Code
if he knowingly acquires any significant pecuniary advantage, or assists in the acquisition of any pecuniary advantage by another person, by:
(a) improperly using or benefiting from information which is obtained in the course of his official duties and which is not generally advantage available to the public.

Ni wazi kuwa kutokana na nafasi zao Yona na Mkapa walikuwa na nafasi ya kujua mambo ambayo hadhara ya jumla haikuwa nayo. NI kutokana na ujuzi huo ndio waliweza kuanzisha kampuni ya madini ambayo inataja kabisa lengo la kujishughulisha na "makaa ya mawe" katika articles zake. Ni wao pekee waliokuwa na uwezo wa kujua hali ya Mgodi wa Kiwira na ni wao pekee ambao waliweza kujua kwa kina maendeleo ya mchakato wa kutafuta mwekezaji mwingine. Kimsingi walichangamkia tenda waliyoitengeneza wenyewe! Walitangaza wenyewe Biashara, na wakajjitokeza wenyewe kama wanunuzi! Goli la Mkono!

Je wana njia ya kutokea:

Katika kutafakati kwangu naona njia ambayo ipo na wanaweza kuitumia kutokea. Nayo ni kuunda nyaraka kuonesha kuwa yeye Yona na Mkapa walitangaza nia yao ya kununua mgodi kwa Kamishna wa Maadili ya Umma. Watafanya hivyo kwa kutumia Ibara ya 14 ya sheria hiyo.

Ngeleja atajikaanga au atawakaanga?
Hilo ndilo swali la leo!

NB: Taarifa zangu zinaniambia kuna uwezekani Mhe. Zitto asihudhurie mkutano huu aliokuwa anausubiri kwa hamu. Hili litafahamika baadaye leo, kama ataweza kuhudhuria.

M. M. M.
 
Hii Serikali inaweza kushughulikia petty issues yaani mambo madogo madogo. Mambo makubwa ambayo wananchi wanahitaji kuyasikia ili wapate majibu serikali inakaa kimya. Habari ya Kiwira inatakiwa iongelewe na Raisi kwa Wananchi. Lakini kwa kuwa samaki huoza kuanzia kichwani yaani serikali inaoza kuanzia kwa raisi mwenyewe. Raisi ni bubu sasa kwa mambo ya maana. Yeye anaweza kuongelea Sullivan tu; lakini wizi wa kiwira hapana, Meremeta hapana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Solution ni kumwaga damu tu
 
MMM
Thanks for the reminder. It is true they may attempt a cover up. It is going to be short lived. There are so many other aspects they will underrate, and this will certainly get them by their necks. By the way, "itakuwa ajabu akijaribu kujibu leo wakati Kamati ya Bomani inasema wazi katika mapendekezo yake kuwa ubinafsishwaji huu unatakiwa kuchunguzwa kwa kina". Ngeleja atapaswa kuwaeleza Watanzania uchunguzi huo wa kina ulifanyika lini wakati wiki chache zilizopita haukuwepo, na watu wake walikuwepo kwenye Kamati ya Bomani. In any case thanks once again for the reminder. Watanzania tutaendelea kupiga kelele hadi kieleweke.
 
unaweza ukashangaa mwanakijiji huyu waziri anavyoweza kubadilisha maneno na kuuficha ufisadi wa wenziwe.

masuala ya shutuma kwa rais mstaafu nafikiri ni pahala pa rais kikwete kusimama na kueleza ukweli ili kutupa imani wananchi kwa viongozi hao kutoka chama kimoja.

kikwete anapo nyamaza kimya ni sawa na kutuambia kuwa hayo madai ni ya ukweli na mimi nimeyakubali na mie naweza kufanya kama hayo na isiwe kitu
 
Mh.Dr.Slaa naamini kuwa 'opposition camp' mmejipanga vilivyo kukabiliana na blah blah za ccm kuhusiana na sekta ya madini ambayo viongozi wake wameitumia kujitajirisha kiharamu.
Naamini kuwa lazima Ngeleja atakuwa ameandaliwa utetezi wa hali ya juu dhidi ya Mkapa na washirika wake.Ngeleja pia ataendeleza kile alichokianzisha waziri mkuu mizengo pinda kutetea ufisadi wa meremeta kwa kisingizio cha usalama wa taifa.
Mkiwa wabunge pekee katika bunge letu mlio na uchungu wa kweli kuona rasilimali zetu zinatufaidisha wote na wale walafi wachache wanawajibishwa, tunategemea leo kuwaona mkiwasha moto mkali kama ilivyo kawaida yenu.
Mungu awabariki sana wabunge wote anti-fisadiz!
 
Leo Waziri wa Nishati na Madini Bw. Willliam Ngeleja atasoma bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake. Wizara hii kama mnakumbuka ndiyo iliyozua kasheshe la Buzwagi na ndiyo ambayo imegubikwa na kashfa nyingi na za ajabu. Je leo wataleta jambo jingine jipya, je leo watatoa majibu ya maswali ya watanzania wengi?

Maswali muhimu

Kati ya majibu ambayo yanatarajiwa kutolewa leo ni kuhusu kampuni ya Meremeta na makampuni mengine ya madini ambayo yamegubikwa na kashfa kubwa. Nani anamiliki Meremeta? Kwanini mahesabu ya Meremeta hayachunguzwi na Mkaguzi Mkuu kama kampuni hii ni ya serikali? Leo kutakuwa na kasheshe na kuna mtu katupiwa kamba ameambiwa ajinyonge!

Lakini kati ya maswali muhimu ni hasa kuhusu Kiwira na uhusiano wa kampuni hiyo na viongozi waliokuwepo madarakani wakati inauzwa kwa Tanpower kwa bei ya chee. Leo inatarajiwa Bw. Ngeleja atatoa maelezo kuhusu Kiwira na kuhalalisha ushiriki wa namna yoyote ile wa Rais na Waziri wake wa Madini.

Kwa vile serikali inatabia ya kusahau, nimeona niwakumbushe jambo moja:

Katika hotuba yake kwenye Bunge la Bajeti la mwaka 2004/2005 aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Bw. Daniel Yona alisema hivi kuhusu mgodi wa Kiwira:

Katika kifungu hicho tunaweza kuona mambo makubwa matatu; a) Kiwira ina mitambo iliyochokaa, b) Mbia alikuwa anatafutwa kutoka China, c) Jitihada hizo hazikuzaa matunda d)PSRC imefungua milango kwa "wawekezaji wengine".

Umuhimu wa hoja hii:

Kwa mtu yeyote mwenye kuelewa utendaji kazi ataona kwamba Waziri Daniel Yona alikuwa na taarifa za ndani za hali ya Mgodi wa Kiwira na alijua maendeleo ya utafutaji mbia yalivyokwama na alijua milango "imefunguliwa". Kwa maneno mengine, Daniel Yona alikuwa na "inside information" ya hali ya Kiwira ambayo (kama nitakavyoonesha dakika chache baadaye) alizitumia kufanikisha malengo yake ya kibiashara.

Mawasiliano na Mkapa:

Ni kutokana na ujuzi huu Waziri Yona alimwambia Rais wake kuhusu hali ya mgodi wa Kiwira na jinsi gani "milango imefunguliwa" katika uwekezaji. Wawili hao (mmoja mkuu wa nchi na mwingine waziri wa sekta husika) walipokubaliana kushikiriana. Mantiki inalazimisha kuamini kuwa Yona asingeweza kwa namna yoyote kujiingiza katika biashara ya makaa ya mawe hususan kuanzisha kampuni ya madini na kuweza kuchukua mgodi wa Kiwira kiulaini. Ni lazima angemshirikisha Rais wake. Kama Rais Mkapa angetaka kujitoa angeweza lakini nafasi ya fedha na hali ya nishati nchini lilikuwa ni jaribio ambalo alishindwa kulishinda na kama nzi anayefia kidondani akaingia kichwa kichwa.

Kampuni kuundwa:
Ni kutokana na ujuzi huo miezi chini ya sita baada ya hotuba hiyo Waziri Yona Na Rais wake Mkapa wakaanzisha kampuni yao ya madini tarehe 29 Disemba 2004. Kampuni hii ndiyo inaitwa Tanpower Resources Limited. Wakati wa kuandikishwa kwake wahusika wakubwa walikuwa ni Daniel Yona(waziri wa sekta), Anna Mkapa (mke wa Rais), Nicholas Mkapa (mtoto wa Rais), Joseph Mbuna (Baba Mkwe wa Niko), na Evans Mapunda. Rais Mkapa mwenyewe alikuwa ni mwanahisa kupitia kampuni yake ya ANBEN iliyoanzishwa mwaka 1999.

Cha kushangaza:

Jambo kubwa la kushangaza ni kuwa kampuni ya Tanpower Resources ilianza mawasiliano na serikali kuhusu Kiwira tarehe 15 Disemba, 2004 karibu wiki mbili kabla ya kuandikishwa rasmi. Kujitoa kwa kampuni ya ANBEN katika Tanpower kulikuja miezi miwili baadaye baada ya mazungumzo ya kuchukua Kiwira yalipoanza na si kabla yake.

Kampuni hiyo ya Tanpower ilifanya mawasiliano na Yona (ambaye pia yumo Tanpower) na akijua kinachoendelea kuhusu Kiwira jinsi ya kuweza kuichukua Kiwira. Kwa maneno mengine, Yona alienda mtumbani, kajua nini kinauzwa, kina hali gani, na amekubaliana na dalali, halafu wakati bei zinarushwa ananyosha mkono na kusema ana nia ya kununua kitu fulani ambacho ni yeye pekee anayejua ubora wake na hali yake!

Bomu:

Wakati mipango ya kuchukua Kiwira ikiwa imepamba moto huku Yona, Mkapa na kampuni zao wakijua nini kinaendelea waliweza hatimaye katikati ya 2005 kampuni hiyo ya Tanpower ikaingia makubaliano na serikali (yaani Yona -raia- anaingia mkataba na Yona-Waziri)! Hata Profesa Ndumba Nangae asingeweza kufanya mazingaombwe ya namna hiyo.

Matokeo yake ya kuingia ubia huo kununua hisa za Kiwira
Kwa vile serikali na wabunge wanaweza kusahau, nimejivika jukumu la kuwakumbusha. Kwamba katika hotuba yake ya Bajeti ya Wizara hiyo hiyo mwaka 2005/2006, Waziri Yona hakugusia kabisa Kiwira na maendeleo ya hali yake. Hii ingemshangaza mtu yeyote anayefuatilia suala la Kiwira. Kama alitoa taarifa ya hali mbaya ya mgodi huo na ya kuwa jitihada za kutafuta mwekezaji mwingine zinaendelea na ya kuwa milango imefunguliwa kwanini asitoe taarifa ni kina nani wamepita kwenye "milango" hiyo?

Of course asingeweza kufanya hivyo, kwani mlango walikuwa wamebanana, yeye, Rais wake, familia zao na jamaa zao! Ni aibu na hofu ya kusutwa Bw. Yona hakugusia suala la Kiwira Bungeni kwenye bajeti yake ingawa alijibu maswali ya juu na reja reja ambayo hayakugusia mchakato wa kutafuta mwekezaji!

Kimsingi Daniel Yona na Mkapa kwa kutumia nafasi zao wamelipora Taifa mgodi na sidhani kama Ngeleja atakuwa na ujasiri wa kusema hivyo.

Wamevunja sheria?
Sheria ya maadili ya viongozi wa umma ya mwaka 1995 (na mabadiliko ya 2005) inasema hivi na ninaamini ni baadhi ya vipengele ambavyo Yona na Mkapa wamevivunja:

Ni wazi kuwa kutokana na nafasi zao Yona na Mkapa walikuwa na nafasi ya kujua mambo ambayo hadhara ya jumla haikuwa nayo. NI kutokana na ujuzi huo ndio waliweza kuanzisha kampuni ya madini ambayo inataja kabisa lengo la kujishughulisha na "makaa ya mawe" katika articles zake. Ni wao pekee waliokuwa na uwezo wa kujua hali ya Mgodi wa Kiwira na ni wao pekee ambao waliweza kujua kwa kina maendeleo ya mchakato wa kutafuta mwekezaji mwingine. Kimsingi walichangamkia tenda waliyoitengeneza wenyewe! Walitangaza wenyewe Biashara, na wakajjitokeza wenyewe kama wanunuzi! Goli la Mkono!

Je wana njia ya kutokea:

Katika kutafakati kwangu naona njia ambayo ipo na wanaweza kuitumia kutokea. Nayo ni kuunda nyaraka kuonesha kuwa yeye Yona na Mkapa walitangaza nia yao ya kununua mgodi kwa Kamishna wa Maadili ya Umma. Watafanya hivyo kwa kutumia Ibara ya 14 ya sheria hiyo.

Ngeleja atajikaanga au atawakaanga?
Hilo ndilo swali la leo!

NB: Taarifa zangu zinaniambia kuna uwezekani Mhe. Zitto asihudhurie mkutano huu aliokuwa anausubiri kwa hamu. Hili litafahamika baadaye leo, kama ataweza kuhudhuria.

M. M. M.

MMM,

Umesema kuna uwezekano Zitto asihudhurie kikao hiki cha bunge, je kuna sababu za msingi?! Au ni hujuma kwa wananchi wake wengi ambao wanahitaji mchago wake katika hili ukizinga yeye Zitto ni miongoni mwa watu wachache wanaolijua hili kwa undani, kwa vile alihusika kwenye kamati ya Bomani.
 
Mkuu Mwanakijiji,

Umenena Ya liyo ya kweli ,ila nachokwambia na walichoamua baada ya kikao kilichopita cha Baraza la Mawaziri,wameweka msimamo wa Serikali.Ni Pinda alishatoa Muungozo wa nini Kitakachojiri leo.na Mambo ambayo wameamua kufanya kwa kifupi

Wameshindwa kutuzuga na wameamua kutulazimisha tukubali
Rejea kauli ya Pinda kuhusu suala la Meremeta,walishatuzuga sana kipindi kile kuhusu Kampuni hii,alijaribu karamagi akashindwa na njia ambayo wametumia sasa ni kutumia Ubabe wa kutulazimisha tukabalia hata kaam hatutaki.Ndiyo maana Pinda akapindisha kwa kusema Merermeta ilikuwa ni mali ya Jeshi na Usalama.Sian uhakika ni lini Nchii hii ilishaanzisha Vyombo vya Usalama kwa Ajili ya Biashara.

Na hili la leo watatulazimisha tukubali kile ambacho hatukitaki na tunakijua kwamba walihujumu na kuchukua mali zetu.Kama Jana Ulimsikia Ngeleja akitoa Muhtasari utajua ni nini leo atazungumza

Kuhusu DOWANS na Richmond
Leo tutegeme mambo ambayo hatukuwahi kabisa kujua ila tutalazimishwa kuyameza,Jana Ngeleja akihojiwa na TBC! alisema seriklali haiikuwahi kuwa na Mkataba na Dowans na wameuvunja,cha kujiuliza hapa ni hiki

1.Je serikali ambayo tunaiamini iliwezaje kulipa pesa nyingi kiasi hicho bila ya kuwa na mkataba na kampuni hii.Kama ni hivyo ina maana hata malipo yaliyofanyika haijulikani yalilipwa kwa nani.Huku ni kutulazimisha kwa nguvu baada ya uzugaji kushindikana

2.Mkataba ulivunjwa na TANESCO,ila ukiangalia mwanzoni serikali ilikuwa ya kwanza kufanya nao mazungumzo,ilikuwaje TANESCO haikufanya hivyo ila baadaye waje wavunje mkataba.

3.Dr. Idrisa Rashid Alisema kwamba Wamevunja Mkataba,Serilai inasema kulikuwa hakuna Mkataba,sasa tumuelewe nani?Leo tutapata Majibu

Tumuachie Ngeleja azungumze Msimamo wa Serikali,ila siyo mawazo yake na hii ndiyo mbinu mpya ya serikali iliyobuniwa ili kujibu mapigo.Ndiyo maana hata Rais kwa sasa hatoi Hotuba za mwisho wa Mwezi na kamuachia Rweyemamu ambaye atakuwa akipewa maelekezo kutoka kikao cha Baraza la mawziri na makatibu wakuu.

Naomba nijibiwe leo,Msimamo wa serikali ni kitu Gani,Je Serikali imechaguliwa na Nani,Bila sisi kuna Serikali??Ikiwa Kama ni sisi tunasababisha inakuwapo serikali Je Msimamo wetu ni upi?
 
M.M.M

Mkuu Zitto yuko wapi?zitto soma PM yako kama uko online
 
Gembe, Zitto hayupo Dodoma, nadhani ana matatizo. Leo ilikua siku muhimu sana kwake kuwapo Dodoma, lakini nimeambiwa hayupo kabisa na hajaonekana hata viwanja vya Dodoma, tokea asikike kule Tanga akimsema Wangwe!!!
 
Back
Top Bottom