Mkapa above the law?: Allegations


Vipi mbona sijamsikia yule Katibu wa CCM wa zamani,Mh. P. Mangula akiongea kuhusu hali aya Mwenyekiti wake (Mstaafu) Fisadi Mzoefu na Mwongo Mtukuka Mtukufuru Benjamin W. Mkapa?
 
Mutu vipi?
Naomba uelewe kuwa wote wanaochangia, ni watu tofauti kwa majina yao , hata kwa tabia zao pia.
.....watu wanauchungu Mutu......,katika hilo nipo pamoja na hao wanaostahili kupigwa risasi kambini na kuwa siri ya jeshi kama unavyosema.
.....hata siku moja usiamini kuwa tutakapo wapeleka mahakamani watapona kutokana na matusi yetu tunayowatukana.
.....nafikiri wanastahili kutukanwa matusi yote yaliyopo kwenye kamusi ya matusi ya uswazi.
WAMESHINDWA KUTUHESHIMU HIVYO HAWASTAHILI KUHESHIMIWA.
....Mutu....tunapoteza wazazi wetu kwa kukosa huduma bora kwenye zahanati zetu,
watoto wetu wanakosa quality education,barabara mbovu...
THEN YOU COME HERE AND TELL PEOPLE TO BEHAVE THEMSELVES?
....MUTU...OH HOO
NAKUHESHIMU.
 
Yaani wamehamishia hisa zao kwa mkwe wao na sasa wanajidai hawana kitu Kiwira?
 
Hatimaye mapambano ya kifamilia yataamia mahakamani.
Nadhani hii ni hatua nzuri tutajua ukweli uko wapi. Najua hayo magazeti yatakuambia ushahidi wao wameupata kwenye familia gani. Wengine wametuambia humu kuwa wamepewa habari na rafiki zake Mkapa.
 
Yaani wamehamishia hisa zao kwa mkwe wao na sasa wanajidai hawana kitu Kiwira?
Mzee kuna tofauti kati ya sheria na haki. Binadamu tumeamua kuishi kwa sheria na kama hutambui hilo kila siku utaona unaonewa.
 
wametengeneza cinema imekamilika:

Balali kafa

Kiwira mambo yameshakaa sawa

sasa lililobaki na kufunga midomo magazeti ili wasibugudhiwe kamwe

I can see the link between Mkapa-EPA-Balali
but I can not see the link between Mkapa-Kiwira-Balali... kama una nafasi naomba ufafanuzi kidogo.
 
Huko nyuma tumesoma kuwa kuna mfanyakazi aliyepewa nyumba ya serikali kama zawadi kwa kufanikisha kuharibu rekodi za kampuni ya RICHMOND huko BRELA. Hizi nguvu anazopata Mkapa sasa hivi zinanishawishi niamini kuwa naye kaamua kucheza game walilocheza RICHMOND !
 
baada ya balai kufa sio? je, JOSEPH MBUNA si mkwe wake mkapa? na hapa atakataa nini?
na MBUNA hapo alibebwa tu'. hiyo ni dili ya mzee mkapa mwenyewe asitake kututisha hapa
 
mazingaombwe ni sanaa ya kuwafanya watu waamini kitu ambacho kilikuwepo hakipo! - M. M. Mwanakijiji Original
 
aliyejengewa nyumba anafahamika. jamani si REHEMA wa hapo BRELA?
 
Nadhani hii iunganishwe na ile ambayo ya Kiwira yamsafisha Mkapa na ya Sofia Somba kusema tuhuma dhidi ya Mkapa ni uzushi mtupu, ili watu wasipoteze muelekeo na hoja zisiparaganyike. Nasema hivyo kwa kuwa muda si mrefu "WATU WATAMWAGA RADHI" humu JF na Mkapa mwenyewe atachanyikiwa. HUKU NI KUJIFANYA MBUNI NA KUWADHARAU WATANZANIA. JANA SUMAYE ALISEMA, "WATANZANIA WAMECHANGAMKA SANA" si wale wa zamani, japa hakuna mtu wa kuzugwa labda kina mwanakijiji huko kijijini kwao, maana alituambia "Waache watuzuge tu......" tunasubuiri what next..... Five, four, three.........!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Soo itapigwa preeeeeeeeeeeeeeee!!!!
 
Nadhani hii iunganishwe na SUmaye amtosa Mkapa, then watu wajadili, maana kuna contradictions
 
Nadhani hii iunganishwe na SUmaye amtetea Mkapa, then watu wajadili, maana kuna contradictions
 
Inanikumbusha wakati mzee FTS alisema shamba sio lake.....ni la mke wake!
Mgodi wa Kiwira sio wa BWM ni mkwe wake!
 
Hebu angalia Tanzania Daima ambaoa katika kichwa chao cha habari sehemu ya chini wamesema, Sumaye amtetea Mkapa, lakini ndani ya habari yenyewe kuna sentesi inayosema "mimi si mtoto wake, siwezi kumsemea". Nilikuwapo katika huo mkutano na niliongea na Sumaye baada ya mkutano, akasema sasa hivi ukimtetea mtu unaweza kupata matatizo makubwa, ni bora ukajitetea mwenyewe na ukawa mkweli hata kama unamuudhi mwenzako. Kwa ujumla Sumaye alitetea SERIKALI YA MKAPA AKIWA WAZIRI MKUU WAKE." na alipoulizwa kuhusu tuhuma za viongozi akiwamo Mkapa, alisema, "UNATAKA MIMI NIMSEMEE? ALISHASEMA KULE LUPASO, LAKINI KWANI MIMI NI MTOTO WAKE NIMSEMEE?" sasa hao wanaoandika amemtetea wapi kuna quotation? Mbona quotation zote wameandika serikali ya awamu ya tatu blah!!! Blah!!!

umaye amtetea Mkapa

2008-06-02 09:39:20
Na Mashaka Mgeta

Waziri Mkuu mstaafu, Bw. Frederick Sumaye, ameibuka na kuutetea utawala wa Rais wa Awamu ya Tatu, Bw. Benjamin Mkapa, kuwa uliharakisha maendeleo ya nchi na watu wake.

Kauli hiyo ya kwanza kutolewa na Bw. Sumaye, imekuja huku kukiwa na tuhuma nyingi zinazomkabili Bw. Mkapa, kutokana na madai ya matumizi mabaya ya madaraka alipokuwa rais.

Baadhi ya tuhuma hizo ni kuingia mikataba `feki` na makampuni ya uwekezaji, hasa katika sekta ya madini huku naye akidaiwa `kujiuzia` mgodi, ufisadi kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ununuzi unaotia wasiwasi wa rada na ndege ya Rais, na madai ya kuwa na mkono katika menejimenti ya kigeni iliyokuwa inaendesha Tanesco, Net Group Solutions.

``Utawala wa Mkapa ulileta maendeleo kwa kasi kubwa sana, na nchi ilikwenda mbele kweli kweli,`` alisema Bw. Sumaye, alipozungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana.

Mkutano huo uliandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tanzania Leo Limited, inayochapisha gazeti la Tanzania Leo, Bw. Venance Rwegoshora, kukanusha taarifa iliyochapishwa na gazeti hilo, toleo la Machi 31 hadi Aprili 6, mwaka juzi, kuwa Bw. Sumaye, anamiliki akaunti iliyopo nje ya nchi, ikiwa na Sh. Trilioni 10.

Bw. Rwegoshora, alisema baada ya mchakato wa hoja kati ya kampuni hiyo na Bw. Sumaye kushindikana kupitia usuluhishi wa Baraza la habari, suala hilo lilifikishwa mahakamani, ilipobainika kuwa habari hizo zilikuwa za uongo, zilitungwa, zikapotosha na kutokuwa na msingi wowote.

Kutokana na hali hiyo, Mahakama Kuu iliamuru kufanyika kikao cha usuluhishi kati ya pande mbili hizo, na kukubaliwa masuala kadhaa, ikiwemo Tanzania Leo kumlipa Bw. Sumaye fidia ya Sh milioni 100, zitakazolipwa kuanzia kipindi cha kabla ya Desemba Mosi mwaka huu hadi juni mwaka ujao.

Bw. Sumaye, alisema utendaji wa Serikali ya Mkapa, ulikuwa makini, uliozingatia maslahi ya nchi, ingawa kuna uwezekano wa kuwepo viongozi binafsi, waliokiuka misingi na maadili ya utumishi wao.

``Kama kuna viongozi waliokiuka maadili ya utumishi, hawawezi kuwa sababu ya kusema serikali ilishindwa. Tumeambiwa kuna uchunguzi unafanyika, tusubiri matokeo yake na wahusika watashughulikiwa,`` alisema.

Alisema uchunguzi unaofanyika dhidi ya vitendo vya ufisadi vinavyodaiwa kufanyika wakati wa utawala wa Bw. Mkapa, ambapo (Sumaye), alikuwa Waziri Mkuu, unawahusu watu binafsi na si utendaji wa iliyokuwa serikali ya awamu ya tatu.

Miongoni mwa hatua za kiutendaji alizozitetea Bw. Sumaye, ni ununuzi wa rada, iliyoligharimu taifa kiasi cha Sh. bilioni 70.

Alidai kwamba kabla ya ununuzi wake, ndege za kimataifa zilitishia kukatisha safari zake kutokana na kulazimika kuzunguka angani, ili zionekane na waongozaji ndege, kabla ya kuruhusiwa kutua.

``Kwa hiyo ununuzi wa rada ile ulikuwa uamuzi wa msingi na muhimu, sasa kama kuna watu walifanya madudu yao, wanapaswa kushughulikiwa,`` alisema.

Hata hivyo, watanzania wamekuwa hawapingi ununuzi wa rada hiyo, isipokuwa kilichowashangaza ni gharama kubwa ya rada hiyo ya kijeshi, huku ikisemekana kuwa Tanzania ilihitaji rada ya kawaida yenye gharama ndogo.

Licha ya kutoa tathmini hiyo kuhusu utendaji wa serikali ya Bw. Mkapa, waziri Mkuu mstaafu Sumaye, alikataa kuzungumzia utendaji wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete, kwa madai kuwa hana utaalamu wa kufanya hivyo.

``Kwa bahati mbaya, nilipokwenda kusoma Marekani, sikuchukua somo hili la tathmini, hivyo suala hilo tuziachie taasisi kama zile za Chuo Kikuu,`` alisema wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari.

Muda baada ya kumaliza kipindi cha uongozi akiwa Waziri Mkuu, Bw. Sumaye alijiunga katika Chuo Kikuu cha Harvard, nchini Marekani, ambapo alisomea masuala ya uongozi wa umma.

Akizungumzia fidia atakayolipwa na kampuni ya Tanzania Leo, Bw. Sumaye, alisema baada ya kutoa gharama zilizotumika kudai haki yake, sehemu ya `vijisenti` vitakavyobaki atavikabidhi kwa Jukwaa la Wahariri ili kufanya semina ya maadili ya uandishi kwa vyombo vya habari.

Alisema fedha nyingine atazipeleka kufanikisha miradi ya kuwawezesha wasichana wa kabila la Kimasai, kupata fursa zaidi za kujiendeleza kielimu.

Wakati huo huo, Bw. Sumaye, amesema hajiandai kuwania urais, baada ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete.

Bw. Sumaye ni miongoni mwa wanachama 10 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), walioshindana na Rais Kikwete kuwania nafasi ya kuteuliwa na chama hicho, kuwania urais mwaka 2005.

Wakati Bw. Sumaye akitoa tamko hilo, habari za ndani ya CCM zilinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari hivi, zikidai kuwapo wanasiasa waandamizi, wakiwemo waliowania uteuzi wa kugombea Urais mwaka 2005, kujipanga kushindana na Rais Kikwete, katika uteuzi wa kuwania kiti hicho mwaka 2010.

``Sijiandai kuwa Rais, kwanza sasa hivi tunaye Rais Kikwete tuliyemchagua, sasa hadi atakapotoka madarakani mwaka 2015 mimi niingie tena, yaani kama ni urais nikae miaka 10 mingine, nitapona kweli,`` alihoji bila kufafanua.

Alisema hivi sasa, anakamilisha mipango itakayofanikisha azma yake ya kuwa mwanaharakati wa kuwasaidia viongozi waliopo madarakani katika nchi za Afrika, kupambana na umaskini.

Aidha, Bw. Sumaye, alisema katika kipindi alichokuwa madarakani, hakuwahi kujihusisha na biashara za kimataifa wala kufungua akaunti nje ya nchi.

``Sikuwahi kuwa na akaunti hata ya Dola moja, ama isiyokuwa na fedha kabisa nje ya nchi, ndani ya kipindi chote nilipokuwa Waziri Mkuu,`` alisema wakati akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari.

Hata hivyo, alisema hivi sasa anamiliki akaunti moja nchini Marekani, aliyoifungua wakati alipokwenda kusoma katika Chuo Kikuu cha Harvard nchini humo.

Alisema bado anaendelea kuihudumia akaunti hiyo, kutokana na kuwa na shughuli mbalimbali anazozifanya na Chuo Kikuu hicho nchini Marekani, ambazo hata hivyo hakuzitaja.

Pia Bw. Sumaye, alisema hana hofu kuhusishwa na vitendo vya ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa umma, akiwa msaidizi wa karibu wa Bw. Mkapa wakati wa utawala wa awamu ya tatu.

``Mkiniandika kama mnavyomwandika (Mkapa) andikeni tu, ali mradi muwe na taarifa za kweli, vinginevyo, hivi sasa mimi ni raia wa kawaida. Mkifanya hivyo kwa kunichafua, tutafikishana mahali pa kusafishana,`` alisema.

Bw. Sumaye, alitetea usiri unaoainishwa katika Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kwamba unasaidia kulinda utu wa mtu.

``Dunia hii kila mtu ana privacy yake (mambo binafsi), kama kuna wasiwasi na kiongozi fulani kuna vyombo vya uchunguzi kupata na kutumia zile taarifa, vinginevyo ukisema iwe kwa kila mtu, itakuwa vurugu,`` alisema.

Hata hivyo, alisema bado kuna haja ya kuangalia mapungufu yaliyopo katika sheria hiyo na kuyarekebisha kwa maslahi ya umma.

Tayari Spika wa Bunge, Bw. Samuel Sitta, ameiagiza Kamati ya Kudumu ya Katiba, Sheria na Utawala, kuipitia sheria hiyo na kutoa mapendekezo ya uboreshaji wake.

Kwa upande mwingine, Bw. Sumaye alisema tuhuma dhidi ya ufisadi, zinazowakabili wanasiasa, zina athari kubwa katika maisha yao binafsi.

Alisema athari zake ni kubwa zaidi inapotokea tuhuma hizo `zimepandikizwa` na watu kwa maslahi yao binafsi.

``Hali ikiwa hivyo unaweza kujikuta kila unapopita unazomewa na pengine kupigwa mawe... Watu wakikuona wanasema huyo alikula fedha zetu,`` alisema.
 
If I were Nzee Nkapa I wouldn't have this plan. Why??? It is the people who have the power, the right and evidence. Hawawezi kusema tu. Yangu macho....
 
Lazima uelewe, Kikwete sio mwenzako hapa. Ukishangaa watu anaowateu Kikwete ni kutokumuelewa Kikwete!

Actually, inatakiwa tumshangae mtu anayemshangaa Kikwete na wale wanaotegema makubwa kutoka kwa huyu mheshimiwa. Kwangu mimi, akiweza hata kukamilisha barabara ya Sam Nujoma vizuri atakuwa ame-perform beyond my expectations!
 

Inasikitisha sana kuona kwamba watu wamekazania kuandika kuhusu mapungufu ya serikali ya awamu ya tatu na kusahau makali ya maisha yalipo sasa tangu serikali ya awamu ya nne iingie madarakani. Imeshindwa kutimiza ahadi lukuki zilizotolewa wakati wa kampeni za uchaguzi. Mfumuko wa bei umeongezeka sana, watu wanazidi kuishi maisha duni zaidi kuliko awali, shule bado hazina walimu wala madawati ya kutosha, mahospitalini watu bado wanalala chini. Ajira milioni moja ziko wapi? Umeme ni wa kusuasua kutokana na ufisadi, barabara wala hazijengwi tena kwa kasi kama ile iliyokuwapo katika awamu ya tatu, na zile zilizopo hazifanyiwi ukarabati kwa wakati unaostahili.

Tumekuwa na viongozi wa kwenye taarifa za habari za TV na magazetini! Tunakwenda wapi? Tujiulize, mpaka sas serikali ya awamu ya nne ikiulizwa imefanya nini kikubwa itajibu nini? Kumleta George Bush au Mkutano wa Sullivan?

Magazeti yageuke jamani, tuangalie hali halisi ya sasa nchini kwetu, mambo yanazidi kuwa magumu kila kukicha....!!! Na je hivi Richmond zile Milioni 152 kwa mwezi bado wanalipwa au zilshasitishwa?
 
!... Nadhani tuna tatizo kubwa la umakini wa waandishi wetu na hata baadhi ya wanasiasa. Kwa mfano issue ya Mkapa na Kiwira sasa, THISDAY walishaandika yote kuhusu ANBEM kujitoa katika hisa za Kiwira lakini baada ya proscess kuwa katika hatua za mwisho na nyaraka zipo, angalieni achaives za JF. THISDAY HAWAJAWAHI kusema "KIWIRA ni ya MKAPA" wanasema siku zote, yeye ndiye mwanzilishi na waziri wake Yona na kwa sasa iko chini ya familia zao, Nicholus Mkapa na baba mkwe wake Advocate.Mbuna. Ni lazima waandishi na hata wanasiasa wawe makini hasa wanapojadili watu matata kama kina Mkapa. Wanasiasa nao walidaakiwa na kuanza kusema, "KIWIRA NI YA MKAPA". in direct yess ni ya Mkapa maana ni ya familia yake. Huyo mwanae kapata wapi fedha? yeye alilipwa kiasi gani kuondoa hisa zake? Na kwa mara ya kwanza wamekiri kuwa Ben anahusika na Kiwira ila sasa wanasema alijitoa kabla... its good starting na kwa mara ya kwanza mbali ya magazeti kunatokea taarifa za kukiri kwamba ANBEM ni ya Mkapa na mkewe, sasa kuanzia hapo ndio tuandelee mbele, wametupa pa kuanzia...
 
Great work Mwanahalisi, Inabidi tuanze mashinikizo ya kumkataa huyu mama na kumwomba aachie hiyo nafasi, ameliaibisha taifa, ni kama vile amenogewa penzi la Nkapa. Sikutegemea kwa kweli!!


Hivi tutaelewa lini kwamba CCM ni wamoja? Kwa hiyo wewe unafikiri kwamba haya ni mawazo yake na siyo ya wana CCM wenzako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…