- Feb 10, 2006
- 4,553
- 16,911
Mengi tutayajua. Tena kafanya vema kufungua kinywa!Hizo tetesi pia zina sikika na kule kwenye kiwanda cha sukari turiani. ila yeye na sumaye wana mashamba makubwa sana ya miwa tuna yako barabarani kabisa kama unaelekea turiani (hii ya mashamba si tetesi)
Kwanza tunatakiwa kufahamu neno kusingiziwa alipoliongea Mheshimiwa Rais Mstaafu Mjasiliamali alikuwa anamaanisha nini!
kafanya nini huyo mkapa
This man is a liar. He should be in jail. Amewadanganya Watanzania na kuwaangusha wote waliokuwa na matumaini ya kupambana na ufisadi.
Naombeni msaada, hivi hii habari ya kiwira imeshaundiwa tume au ndo itakuwepo ndani ya repoet ya madini?? au ndo itachunguzwa toka tamko la Pinda alililitoa kuwa hizo shutma zote zitachunguzwa???
Tume ya nini? Suala la Kiwira linaweza kuwekwa wazi bila ya kuwa na tume. Kinachihitajika ni hiki:
1. Kwenda Brela/Wizara ya Nishati na Madini kuangalia nyaraka za umiliki wa mgodi huu.
2. Kama ni kweli Mkapa ndio mmiliki, Je, alifanya hivyo akiwa madarakani? Muda aliokaa madarakani tunaujua.
3. Je taratibu za manunuzi zilifuatwa?
Sasa maswali haya matatu yanahitaji tume kweli au ni njia nyingine za ubadhirifu wa fedha za umma?
Tuandamane,
Hii issue ya Kiwira ni skandali nyingine inapikwa taratibu na itakuwa inajitegemea. Linakuja moja baada ya jingine mpaka wananchi wachoke kabisa na kinachoendelea huko serikalini.
Nimefurahi sana kwa huyu bwana kuanza kusema. Sasa hana kisingizio tena cha kukataa kusema eti amestaafu. Ameamua kusema na sasa ajibu hoja zote zilizo mbele yake.
1. Kampuni anazomiliki hati zake ziko kwa msajili - hilo halina ubishi
2. Kwamba kampuni alizianzisha wakati akiwa ikulu, halina ubishi maana tarehe alizoingia ikulu na kutoka na tarehe alipoadikisha hizo kampuni zinajulikana.
Sasa hapa anakanusha vipi.
Kuna maswali ya kujiuliza hapa
a. Kwa nini ametafuta soft target ya kujitakasia. Wanakijiji yawezekana hawajui hizo kampuni zake - si angewaita waadishi wa habari ili nao wamuulize maswali?
b. Kwa nini amesubiri mpaka Balali amekufa ndipo naye anajitokeza kusema?
kwa nn kaongelea kwa wanakijiji wasio jua kuhoji maswali???na kwa nn ajibu tuhuma akiwa BUsh.........