Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,987
TAARIFA YA KUSUDIO LA KUPUNGUZA WAFANYAKAZI (BAADHI)
TAREHE 16/10/2023
KWA: VAPI MERKEZI INSAAT VE SANAYI AS TABORA MAKUTOPORA
Rejea kichwa cha habari hapo juu
Baada ya kufikiria kwa uangalifu mwajiri wako YAPI MERKEZI INSAAT VE SANAVI A.S anafikiria kuanza michakato wa kupunguza Wafanyakazi.
Kwa mujibu wa Sheria mazungumzo ama mashauriano yanatakiwa kufanywa kati ya uongozi na Wafanyakazi walenga kupitia uwakilishi watakaouchagua hii ikiwa ni pamoja na Chama cha Wafanyakazi wa Sekta husika.
Uamuzi wa mwisho wa Mwajiri unategemea mapendekezo yatakayofikiwa kwa pamoja kati ya Wafanyakazi walengwa wasio wanachama wa Chama cha Wafanyakazi TAMICO uwakilishi wa Chama cha Wafanyakazi (TAMICO) Mambo muhimu ya kuzingatia:
1. Kwa nini mwajiri anafikiria kupunguza wafanyakazi?
Kumetokea ulazima wa kiutendaji kufunga kambi ya Manyoni na Nyahua na hata tishio la mvua kubwa juu ya wastani kama ilivyotangazwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA)
2. Njia mbadala kabla ya kupunguza
Mwajiri hakupend kuwaachisha Wafanyakazi, alikuja na mapendekezo ya Likizo isiyo na Malipo ila ina nafuu ya kulipiwa 6% yote ya NHIF na 14.28% ya kima cha chini cha mishahara ndani ya kampuni kwa wote wa mkupuo mmoja hili halikuafikiwa na wafanyakazi, limekataliwa.
3. Idadi ya Wafanyakazi wanaoweza kuathiriwa
Zoezi hili linatarajiwa kuathiri wafanyakazi wapatao 525 mara baada ya makubaliano, na upunguza utaendelea hatua kwa tatu hadi kufikia 525.
4 Vigezo vya uteuzi
Kielelezo cha uteuzi ni kama ilivyo kwenye Sheria za kazi.
5. Muda wa kuanza kupunguza
Imekusudiwa kwamba mchakato wa ushauri uweze kukamilika ifikapo tarehe 31/10/2023 au KABLA YA HAPO. 2
Ni kusudi la mwajiri kushauriana na wewe kwanza katika kipindi hiki kabla ya uamuzi wowote wote wa mwisho wa kuchukuliwa. Mwajiri atakuarifu kuhusu tarehe na muda wa mashauriano.
6. Msaada:
Mwajiri atatoa kwa mujibu wa Sheria za ajira na mahusiano kazini.
i. Barua ya kumbukumbu
ii. Cheti cha Utumishi
7. Jumla
Ili kuhakikisha Sheria ya Ajira na Mahusiano mema Kazini inafutwa, mwajiri anakujulisha rasmi kuhusu kupunguzwa kwa Wafanyakazi.
Unaalikwa kutoa uwasilishaji kushiriki kupitia mwakilishi utakaye mchagua akiwakilishe katika kikao cha mashauriano majadiliano juu ya kusudio la kupunguza wafanyakazi (BAADHI).
Inapaswa kusisitizwa kuwa hakuna uamuzi wa mwisho ambao umechukuliwa juu ya suala hili, uamuzi wa mwisho utachukuliwa baada ya mashauri kamili na wewe au mwakilishi wako.
Ikiwa utahitaji msaada wowote zaidi au una maoni yoyote kuhusu yaliyoelezwa hapo juu, tafadhali jisikie huru kuyaleta wakati wa vipindi vya mashauriano.
Imetolewa na
IDARA YA RASILIMALI WATU
YAPI MERKEZI INSAAT VE SANAYI AS
MRADI WA NJIA YA TRENI YA MWENDO KASI
MAKUTOPORA - TABORA
16/10/2023
Pia soma:
Mkandarasi Yapı Merkezi anayejenga Reli ya SGR atoa ufafanuzi taarifa za kushindwa kuwalipa wafanyakazi wake raia wa Uturuki
Waturuki wanaojenga Reli ya SGR wapo katika mgomo, inadaiwa hawajalipwa fedha zao