Mkakati wa Team Lowassa huu hapa

Mkakati wa Team Lowassa huu hapa

Wakati vuguvugu la kuwasafirisha,kuwaandalia matamko ya kumsifu na kuwalipa baadhi ya makundi mbalimbali ya kijamii likijadiliwa ndani ya chama kwa hatua za kinidhamu,hali ya marafiki wa EL imekuja na mbinu mpya za kutafuta ushawishi wa nguvu ya pesa ndani ya chama.

Wajumbe wa NEC kutoka mikoa yote ya kanda ya Ziwa wamemiminika Dsm,kwa udhamini na ufadhili wa EL ili kutafuta uungwaji mkono kuelekea Octoba.Wajumbe hao wa NEC walianza kuwasili Dsm toka juzi usiku,wakipokewa na kuwekwa ktk hotel tofautitofauti ndani ya jiji..huku gharama za malazi,chakula,nauli na posho zikiwa chini ya EL.

Wajumbe hao kutoka ktk mikoa ya Mwanza,Geita,Simiyu,Shinyanga,Musoma na Kagera ujio wao umechagizwa na posho ya milioni tano kwa kila mtu,Na kikao kinaendelea naTeam EL ili kutafuta ushawishi kwa wajumbe wa kanda ya ziwa.

Hali hii ya kuanza kuwasafirisha wajumbe kimyakimya na kwa makundi inakuja baada ya ile mbinu ya kuwatafuta watu wa makundi mbalimbali ndani ya nchi kuzuiwa na chama.Lafu hii ya kukiuka kanuni za chama kwa kuwasafirisha na kuwalipa kiasi kikubwa cha pesa wajumbe ni aina mpya ya mbinu ya Team EL baada ya ile ya kwanza kushitukiwa.

Kuelekea uchaguzi Mkuu,EL ameonekana kutumia kiasi kikubwa sana cha pesa ktk kulazimisha ushindi wa kuteuliwa na chama chake kuipeperusha bendera katikati ya vyama vingine vya upinzani hususani UKAWA.

Matumizi haya ya kiasi kikubwa cha pesa si tu ni tishio ndani ya chama chake na kwa mustakabali wa demokrasia safi,bali ni utamaduni unaotaka kupandikizwa ktk siasa za nchi hii kuwapata viongozi nje ya misingi ya uadilifu,nidhamu na uzalendo wa kweli.

Chanzo cha Taarifa hii ni mmoja kati ya wajumbe wa NEC walio ndani ya kikao hicho kinachoendelea sasa Kati ya Team EL,wapambe wake na wajumbe hao
Ora Et Labora
Kwa Musoma nadhani anapoteza muda na fedha yake bure. Kule Vincent Nyerere amefanikiwa kufuta CCM.
 
Kama kawaida porojo zimeanza, tangu lini wajumbe wa NEC wakasafirishwa na mtu binafsi, tangu lini wajumbe wa NEC (CCM) wakapokelewa na mtu binafsi, tangu lini posho za wajumbe wa NEC zikalipwa na mtu binafsi halafu chama kikae kimya, Kama CCM iliwafunga luku wale walioonekana kuanza kampeni mapema kabla ya wakati ni kwa vipi CCM hiyo hiyo leo ikae kimya mtu binafi anapowahudumia wajumbe wa NEC kwa staili inayoonekana kama rushwa? That is porojo at work.
 
Nimebahatika kuona/kupata bandiko hili nyuma ya gari likisomeka: TEAM LOWASSA (PICHA YA LOWASSA) "Tuhuma za Kipuuzi Zisitunyime Raisi Bora 2015"

Sasa sijajua ni tuhuma zipi pengine zingetajwa tukazijua la sivyo nipo/tupo gizani na tuhuma hizo.

Binafsi: Kwa mwendo huu na nilivyokwisha kuona anayoyafanya ndugu Edward Lowassa, ngonjera nyingi tutaona - time will tell!

dc578b9e7d92083853c58d40953097fe.jpg

efbb6b2b5819d951e29240eadc524a52.jpg

7ae2fc32a8a135ed02dc62f97ed4d624.jpg
 
hiyo picha/bandiko unaiona wewe mwenyewe tu,kiukweli sisi wengine hata hatuioni.nimetumia darubini lakini wapi.
 
kweli kabisa mkuu,kipi EL alikosea ilihali hadi sasa tunalipa mamilioni kwa dowans kiss kuvunja mkataba kijuha? tuhuma za kipuuz zisitukoseshe raisi bora 2015 TEAM lowassa
 
Last edited by a moderator:
Nimebahatika kuona/kupata bandiko hili nyuma ya gari likisomeka: TEAM LOWASSA (PICHA YA LOWASSA) "Tuhuma za Kipuuzi Zisitunyime Raisi Bora 2015"

Sasa sijajua ni tuhuma zipi pengine zingetajwa tukazijua la sivyo nipo/tupo gizani na tuhuma hizo.

Binafsi: Kwa mwendo huu na nilivyokwisha kuona anayoyafanya ndugu Edward Lowassa, ngonjera nyingi tutaona - time will tell!

Ni CCM imetukanwa!
 
Hakuna jipya...bila ya EL hakuna ushindi au labda wajitoe kwenye kinyanganyiro waanze kujipanga upya na warudi baada ya 5 yrs (maoni yangu tu)kwani hizi kambi ni kiboko,akiteuliwa wa kambi yoyote balaa,hata asiye na kambi ndiyo balaa zaidi.
 
Manina chama kitakacho msimamisha huyu kijiandae kabisa kupata mapingamizi kwa kuanza kampeni kabla ya wakati.
 
Hofu yangu ni je?akikosa kupitishwa kwenye kamati kuu kwenye kura za maoni itakuwaje???nguvu inayotumika ni kubwa mno mpaka anafanya tuanze kuamini baadhi ya tuhuma.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom