CV ZA WANAOJIITA TEAM LOWASA AMBAO SASA WANASEMA CCM ITAPASUKA KAMA MGOMBEA WAO HATAPITISHWA-
MGEJA-Ni mwenyekiti wa ccm mkoa wa shinyanga,Chini ya uenyekiti wake-CCM Shinyanga imepoteza majimbo Matatu, Ni huruma tu ya vikao,ccm haikustahili kumteua kutetea tena kiti chake maana alizungukwa na tuhuma lukuki za kuusahau mkoa wake na kujikita katika siasa za magazeti Dar es salaam.
MAHANGA-Ni mbunge wa Segereq ambaye siri ya ushindi wake ndani ya ccm na nje ya ccm anaijua mwenyewe kama mtu mzima,ni maajabu ya Musa kama kweli Mahanga anao uthubutu wa kusema leo anatetea jimbo lake la ubunge.
SERUKAMBA-ni dhahiri ushindi wake wa ubunge mwaka 2010 ni siri ya mtungi anayeijua ni yeye mwenyewe,haishangazi kwa kuujua ukweli kusikia leo anataraji kuhama jimbo lake la awali na kuhamia jimbo la Kigoma Kaskazini
Wengine katika Team Lowasa ni MATHAYO-huyu ni mshindwa wa ubunge Musoma Mjini
MASHA,ni mshindwa ubunge Nyamagana
MBUZI ni mshindwa ubunge Meatu
CHEGENI-mshindwa ubunge Busega
MGANA MSINDAI -Mshindwa ubunge Singida hukoo.
Chenge na Karamagi uhai wa siasa zao na biashara zao ni sababu ya
"hekima" za mfumo huu,sii sura ambazo CCM inatakiwa kujivunia kuwa nazo hadharani.
KIUFUPI MZEE LOWASA AMEAMUA AUNGWE MKONO NA -COALITION OF FAILURES IN POLITICS,AMBAO SASA WANA-GANG UP KUSEMA WANATISHIA VIKAO KUWA MGOMBEA WAO ASIPOPITISHWA CCM INAPASUKA,NIULIZE SWALI,KATIKA HIYO LIST NI NANI MWENYE UWEZO WA KUIPASUA CCM KAMA AKIAMUA KUONDOKA??
PILI;LIPO KUNDI LA MATAPELI,WACHONGA MADILI NA MAJIZI YA KIBIASHARA AMBAYO YAMEUKWAA UNEC WA CCM,HUO UNEC NA BENDERA YA CCM NDIZO NGAO ZA BIASHARA ZAO NA UBABAISHAJI WAO,LEO NAO WANAJIAPIZA KUWA ETI CCM ITAMEGUKA KWA KUWA MAJIZI NA MATAPELI HAYA YATAJIONDOA CCM,NAAMINI HUU NI MWAKA WA CCM KUZALIWA UPYA,NI MWAKA AMBAO MAJIZI,NA MATAPELI AMBAYO YALIAMINI CCM NI KICHAKA CHAO YAKAKIMBILIA MADARAKA NA UONGOZI WA CCM ILI IWE KINGA MWAKA HUU YATAUMBUKA,MILANGO IPO WAZI KUONDOKA ILI PLACENTA YA UCHAFU HUU ISAFISHIKE KABISA
Leo wezi wa serikali,Drug Dealers,Matapeli,vibaka,wote mtu wao awe EL???!!!CCM laweza kuwa kweli dodoki,lakini hata dodoki hufika mahala likasafishwa uchafu wake ili liaminike kutumiwa tena na muogaji,huu ni mwaka wa kusafisha dodoki ili waogaji waiamini tena CCM,uchafu utawekwa jalalani.
NIMALIZIE KWA KUOMBA JAMBO MOJA-NITAFUTIENI MSAFI MMOJA TU ANAYEMUUNGA MKONO EL MAANA NAWAONA WOTE WANAOMUUNGA MKONO WANA NAKISI YA KUTILIWA SHAKA,AMA KWENYE JAMII AU HATA HUKO CCM KWENYEWE,FUMBA MACHO UNIAMBIYE MTU MMOJA TU AMBAYE ANAMUUNGA MKONO EL AMBAYE NI KIELELEZO CHA WEMA KATIKA JAMII.
"Kuelekea Magogoni 2015 ni kishindo kikuu"
