Wakati vuguvugu la kuwasafirisha,kuwaandalia matamko ya kumsifu na kuwalipa baadhi ya makundi mbalimbali ya kijamii likijadiliwa ndani ya chama kwa hatua za kinidhamu,hali ya marafiki wa EL imekuja na mbinu mpya za kutafuta ushawishi wa nguvu ya pesa ndani ya chama.
Wajumbe wa NEC kutoka mikoa yote ya kanda ya Ziwa wamemiminika Dsm,kwa udhamini na ufadhili wa EL ili kutafuta uungwaji mkono kuelekea Octoba.Wajumbe hao wa NEC walianza kuwasili Dsm toka juzi usiku,wakipokewa na kuwekwa ktk hotel tofautitofauti ndani ya jiji..huku gharama za malazi,chakula,nauli na posho zikiwa chini ya EL.
Wajumbe hao kutoka ktk mikoa ya Mwanza,Geita,Simiyu,Shinyanga,Musoma na Kagera ujio wao umechagizwa na posho ya milioni tano kwa kila mtu,Na kikao kinaendelea na EL ili kutafuta ushawishi kwa wajumbe wa kanda ya ziwa.
Hali hii ya kuanza kuwasafirisha wajumbe kimyakimya na kwa makundi inakuja baada ya ile mbinu ya kuwatafuta watu wa makundi mbalimbali ndani ya nchi kuzuiwa na chama.Lafu hii ya kukiuka kanuni za chama kwa kuwasafirisha na kuwalipa kiasi kikubwa cha pesa wajumbe ni aina mpya ya mbinu ya Team EL baada ya ile ya kwanza kushitukiwa.
Kuelekea uchaguzi Mkuu,EL ameonekana kutumia kiasi kikubwa sana cha pesa ktk kulazimisha ushindi wa kuteuliwa na chama chake kuipeperusha bendera katikati ya vyama vingine vya upinzani hususani UKAWA.
Matumizi haya ya kiasi kikubwa cha pesa si tu ni tishio ndani ya chama chake na kwa mustakabali wa demokrasia safi,bali ni utamaduni unaotaka kupandikizwa ktk siasa za nchi hii kuwapata viongozi nje ya misingi ya uadilifu,nidhamu na uzalendo wa kweli.
Chanzo cha Taarifa hii ni mmoja kati ya wajumbe wa NEC walio ndani ya kikao hicho kinachoendelea sasa Kati ya EL,wapambe wake na wajumbe hao
Ora Et Labora