Mkakati: Lowassa kuhamia UKAWA

Mkakati: Lowassa kuhamia UKAWA

Ndio maana akina Dr Slaa wakaamua kustaafu siasa kama vijana tegemeo kwa ukombozi ndio hawa ....Mbowe alivyobadili gia angani wakala matapishi yao ....

Kuna jamaa mmoja anajiita Tindo wangalau ndio aliyebakia na msimamo wake toka zamani kuhusu huyo Lowassa. Maana huyo jamaa naye ni king'ang'anizi. Ila kwa makamanda wengine kama kina Erythrocyte wakiona huu uzi umeibuliwa wanaweza shindwa kula xmas kwa jinsi wanavyomnyenyekea Lowassa. Kweli nimeamini pesa ni mwanaharamu.

CC: Okw boban Sunzu, Godbless J. Lema
 
Hahahahahahaaaa! Lowassa hana ubavu wa kubaki CCM kama atatoswa kwenye kuwania Urais. Kwa sababu anajua hawezi tena kusubiri miaka kumi ijayo kama alivyokubali kumsubiri Kikwete hadi atakapomaliza ungwe yake. Akitoshwa Urais atatoka tu CCM, na kuna kila dalili kuwa CCM hawatampa nafasi ya kuwania Urais mwakani.
Ova

Ndugu yangu uliona mbali sana!
 
Lowasa akija UKAWA mimi natoka , amechafuka , hana na wala hajawahi kuwa na fikra mpya , ndio maana hadi leo anaamini kwamba rushwa itampeleka ikulu .

Bado yupo Ukawa kwa sababu aliekuja Ukawa ni Edward Ngoyai si hayati Mzee Lowassa si ndio? Hahahahaahha
Kufukua Makaburi kuna ladha yake
 
Ndio maana akina Dr Slaa wakaamua kustaafu siasa kama vijana tegemeo kwa ukombozi ndio hawa ....Mbowe alivyobadili gia angani wakala matapishi yao ....

Halafu walivyo Watu wa Ajabu, Yule aliebaki na Msimamo wao wa awali kumkataa Lowassa anaitwa Msaliti halafu waliobadilika ndio sio Wasaliti, kuwaelewa Hawa Wadudu inabidi nawe uwe mdudu
 
UKAWA hakuna nafasi ya mafisadi aende zake huko. UKAWA hawawezi kufanya makosa ya kipumbavu ya kumkaribisha huyu fisadi.
Wewe Ulikuwa hujui kuwa Jukumu lako linaishia kwny kukunja ngumi hewani na kusema pipoooz, Chama kina wenyewe na wakiamua kufanya Maamuzi huulizwi chochote !
 
hatutaki viongozi waliowahi kuliingizia taifa hasara ndo waje huku never on earth, labda awe mwanachama wa kawaida tu na sio kugombea nafasi yoyote ya uongozi vinginevyo arudi huko huko kwa chama chake cha mashetani
Mambo vip
 
ana nini cha zaidi? hatutaki majizi huku. alifukuzwa kwa escro no1 epa leo anaendelea kugawa hela ili awe rais.mwe nafuuu kuwa bila na kiongozi
Pesa za mamvi hazijawah kumuacha salama mwenyekiti cha chama kikuu cha upinzan Tanzania.
 
Naam na mimi si bendera hufuata upepo hivyo chochote watakachoamua nikipigie makofi, kukiunga mkono na kubaki kukenua. Mie najitambua Mkuu huwa sikurupuki kwenye kufanya maamuzi yangu na hadi hii leo sijajutia kuupinga uamuzi wa kumkaribisha huyu kwani sijaona mchango wake wowote wa kukiimarisha chama zaidi ya kupiga kimya kwa kipindi kirefu.

Wewe Ulikuwa hujui kuwa Jukumu lako linaishia kwny kukunja ngumi hewani na kusema pipoooz, Chama kina wenyewe na wakiamua kufanya Maamuzi huulizwi chochote !
 
UKAWA haihitaji Sub-dakika ya 90, timu imeshakamilika, tunachosubiriwa ni KIPENGA tu ili mshuhudie timbwili.

Hahahahahah!
Mshabiki Maandazi ukajipa Kazi ya Ukocha, ona Sasa ulivyoumbuka!
 
Labda agombee ubunge jimbo la Monduli kupitia UKAWA
Aligombea ubunge jimbo la serikal ya muungano wa Tanzania, ila kura hazikutosha hivyo atajarib kutupa karata yake ya mwisho kwa mara ua pili kupitia chama letu pendwa
 
Back
Top Bottom