TAJIRI MKUU WA MATAJIRI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 5,720
- 10,215
KUMBUKUMBU: JE, WAJUA? KWAMBA HAITI NDILO TAIFA LINALOSEMEKANA KUONGOZA KWA UCHAWI DUNIANI?
Rais wa zamani wa Haiti, Dikteta François "Papa Doc" Duvalier, aliyechaguliwa na wananchi wa taifa hilo kuwa rais wa 32 wa Jamhuri ya Haiti, kuanzia mwaka 1957 hadi mwaka 1971, anasemekana kuwa mchawi kuliko marais wote wachawi duniani wa wakati wote.
Kwa mujibu wa makala ya runinga ya Evolution of Evil (),
Rais François Duvalier wa Haiti ndiye anayesemekana kusababisha kifo cha Rais John F. Kennedy wa Marekani kwa njia za kishirikina.
Kilichotokea ni kwamba Papa Doc alipoanza kufuja fedha za misaada za walipa kodi wa Marekani, akizitumia fedha hizo kuendesha nchi kichawi na kidikteta, kupitia kikosi-kazi chake cha Tonton Macoute, Rais Kennedy aliamua kusitisha misaada yote kwa taifa hilo kongwe ulimwenguni. Kitendo hicho kilimuudhi sana Duvalier, kiasi cha kuamua kuweka nadhiri ya kumuondoa Kennedy madarakani na duniani kwa msaada wa mungu wake aitwaye Bondye.
Tarehe 22/11/1963, siku moja tu baada ya Rais Kennedy kutangaza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Haiti, Dikteta Duvalier alifanya tambiko akiwa nchini mwake la kumroga Kennedy kama alivyodhamiria. Siku hiyohiyo, yaani tarehe 22/11/1963, J. F. Kennedy aliuwawa na mtu asiyejulikana huko Dallas nchini Marekani.
Nchini Haiti Papa Doc alionekana kwenye vyombo vya habari akisherehekea kifo cha hasimu wake kwa kunywa shampeni na kucheza muziki na Tonton Macoute, kikosi chake maalumu kilichotesa au kuua mtu yeyote aliyepingana na Rais, huku akitamba kuwa yeye ndiye aliyemuua Kennedy.
Rais aliyefuata huko Marekani baada ya Rais Kennedy, Rais Lyndon B. Johnson, aliondoa mara moja vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Haiti. Uhusiano kati ya Marekani na taifa hilo la Kikaribi, lililojipatia uhuru wake toka Ufaransa mnamo mwaka 1804, ukaendelea tena kama kawaida.
Haiti ina asilimia 70 ya Wakatoliki, asilimia 30 ya Waprotestanti, na asilimia 100 ya wachawi.