Bukyanagandi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2009
- 11,626
- 18,223
!kiongozi makini hatakiwi hata kutuhumiwa kwa rushwa achiambali kuitoa au kupokea.
Lowasa Hana uthubutu wa kuikemea kwasababu sio msafi.
Mkuu umenikumbusha kisa kimoja kwenye biblia kilihusu Mfalme, katika himaya ya Mfalme kulitokea minongono ya hapa na pale kwamba mkewe alikuwa anatembea nje ya ndoa! Mfalme alikasirishwa sana na taarifa hizo, alikata shauri ya kumtariki mkewe.
Haikuchukua muda Mfalme kampa taraka mkewe na kuambiwa aondoke kwenye Kasri ya mfalme fasta! Baadae kabisa, wapambe wake wakaja kwa mfalme na kumweleza kwamba mkewe watu walimsingizia hajawahi kujihusisha na uzinzi, Mfalme kawasikiliza kwa umakini sana alfu kawapa jibu la kishindo! Kasema hivi: "Yeye kama Mke wa Mfalme hatakiwi hata kutuhumiwa/kuhisiwa na kosa lolote" i.e hata kuhisiwa tu kunatia DOA UFALME/Taifa lake.
Viongozi wetu wa ngazi za juu wakijitahidi ku-emulate uongozi wa Mfalme huyo wa Agano la kale mbona Taifa letu litashamiri na raia wapenda kula/kutoa bribes watafikilia mara mbili kabla ya ku-commit kitu kama hicho. Sasa hivi TAIFA letu limeghubikwa na kasumba ya kuwasifia mafisadi, wala rushwa na wezi utasikia raia wanasema yule jamaa "kuchangamka sijuhi ana AKILI" Personally sita kaa hata siku moja nikamsifia mwizi/mla rushwa/fisadi hata akijenga mahekalu ntamuona hafai hata kidogo.