MABADILIKO HAYAEPUKIKI: Nakubaliana na Lowasa kwa asilimia zote

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
Zaidi ya mara nyingi vyombo vya habari vimemkariri mwanasiasa mwenye historia ya kipekee hapa Tanzania, Ndugu Edward Lowasa kuwa ‘Mabadiliko Tanzania hayaepukiki’.
Ninaanza kumuelewa Lowasa na maana yake anaposema na kulirudia neno hili.

Ameona bila shaka kuwa wapo mahafidhina ndani ya jamii yetu ambao wanashindwa kwenda na mabadiliko. Yeye kama mwanasiasa mwenye ushawishi hana budi kuwaandaa wale mahafidhina kuhakikisha hawabaki nyuma ya mabadiliko ambayo hayana budi kutokea.
Mabadiliko yenyewe anayoyapigia chapuo Lowasa, yameanza kitambo na zaidi kipindi cha uchaguzi.

(Na kama siyo anayoyaongelea basi ana matatizo makubwa). Kuna watu walikuwa wanaamini kuwa lazima rais wa Tanzania atoke CCM. Tena kuna walioamini kuwa Rais wa Tanzania lazima atokane na Mtandao. Siasa zilizotangulia uchaguzi zilibadilisha hilo. Watu walichoshwa na ufisadi, rushwa, ukosefu wa uwajibikaji, na kadhalika. Kelele zilizopigwa zilionyesha kuwa kwa sasa sio lazima Rais atoke CCM au mtandaoni. Tayari watu walishaonja machungu. Walitaka mtu atakayeyashughulikia hayo yanayowaudhi au kuwasumbua. Wakaangalia sera za chama na watu wanaozitangaza sera hizo.

Baada ya uteuzi wa wagombea urais kuna watu (wahafidhina) walitaka kuchanganyikiwa. Hawakuamini kuwa nchi inaweza kupata rais kutoka nje ya CCM na nje ya mtandao. Kumbe CCM yenyewe ilikuwaa imeliona mapema kuwa si kila atakayeteuliwa na CCM lazima achagulike. Ikahakikisha inamteua mtu ambaye hatapita kwa sababu katoka CCM, bali kwa sifa zake za kiutendaji. Kumbe walisoma alama za nyakati na wakapatia.

Wakati wa siasa ya ujamaa na kujitegemea; ujamaa ulikazaniwa na kujitegemea kukasahaulika na kwa kweli kukafutika. Kujitegemea kulifutika miongoni mwa jamii na viongozi wao pia. Watu na viongozi wakazoea misaada. Kila kitu watu wakategemea serikali ifanye. Serikali ikatarajia kila kitu kutegemea wafadhili. Nakumbuka kumsikia jamaa yangu mmoja akilalamikia bei ya madawa. Anasema kupiga picha (X-Rays) shilingi 30,000/= hospitalini ni nyingi. Nikamuuliza mbona juzi ulibadilisha injini ya gari lako kwa hela nyingi na sasa unalalamikia bei ya kurekebisha afya yako mwenyewe?

Watu wakazoea. Ukame kidogo ukitokea wanasubiri chakula cha serikali. Huo ni ukame wa msimu mmoja. Kwa watendaji wa serikali hiyo ikawa neema maana sehemu kubwa watachukua. Watu wakilima mazao wanasubiri serikali iwatafutie, masoko na kwa kweli wako tayari kulaumu kwa nini serikali haijawaletea bei nzuri. Kukuta mtu amelima ekari kumi za mahindi na kuvuna gunia hamsini na anachekelea likawa ni jambo la kawaida.

Hana haja ya kuhakikisha anapata mazao mengi katika eneo dogo. Serikali ipo. Nakumbuka wakati wa awamu ya kwanza uliwahi kutokea ukame. Watu wakalazimika kusaidiwa chakula. Ukiondoa wazee wasio na waangalizi, watu walipewa mbegu ya mihogo na mazao mengine yanayostahimili ukame kama msaada. Ilipolazimika kuwapa chakula utaratibu ulikuwa “Food for Work”. Unafanya kazi ya kulima shamba lako mwenyewe na kupewa chakula.

Tunamkumbuka aliyeilalamikia serikali kwa sababu ngombe wake wamekufa kwa maelfu. Hakuchukua hatua alipoona ng’ombe wanakonda, wanashindwa kutembea mpaka kufikia hatua ya kufa mmoja, mamia mpaka maelfu anasubiri tu kwa sababu anajua kuna msemaji wa upinzani ataitukana serikali apige makofi basi. Katika mabadiliko yasiyoepikika ikitokea atauza mifugo mingine ili kupata mal;isho ya michache inayosalia.

Watu wakasahau na sababu ya uchaguzi. Wakawa na tabia ya kuchagua mtu kwa sababu anatoka chama fulani bila kupima uwezo mgombea huyo; uelewa wake katika matatizo yanayowakabili au hata tabia yake katika maswala anayoyazungumzia katika jukwaa la siasa. Mtu anatoka Dar Es Salaam na kuja kuwanunulia pombe kesho wanampa ubunge. Hawajiulizi atawasaidiaje kwenye bei ya kahawa au pamba yao au mifugo. Havijui na hawajui kuwa wanayemchagua lazima awe anavijua na awe mshirika kwa maana mkulima wa zao wanalolitegemea.

Mabadiliko yakaanza. Baadhi ya walioamini rais lazima atokane na mtandao kwa kuona CCM imemteua mtu asiye na mtandao wakahama ili kuhakikisha mtandao unajitokeza na kutoa rais. Nakumbuka kusoma mahala mtanzania mmoja akisema Sangara hawezi kuishi akishatoka majini na kuonja hewa. Mwisho wa uchaguzi taifa lilimpata rais ambaye hakuwa mwanantandao na hata kama alitoka CCM lakini hakuchaguliwa na watanzania kwa sababu hiyo bali kwa jinsi walivyompima yeye binafsi. Mabadiliko ya kwanza.


Rais akaingia madarakani. Akaanza kutumbua. Wauza unga (madawa ya kulevya) waliokuwa wanafanya kwa uhuru sasa wanajificha. Wamo lupango na wengine wamekimbia. Watu waliozoea kutegemea rushwa sasa wana tahadhali kubwa. Bado wapo na wanaiomba. Lakini si kwa uhuru. Waliozoea kuweka cha juu na kufanya kwa uzembe wakashughulikiwa. Lakini angalau serikalini kuna nidhamu hata kama ni ya woga, huo woga utaisha nidhamu itakuwa tabia. Mabadiliko hayo.

Mabadiliko mengine ndiyo haya tunayoanza kuyashuhudia.
Rais alipotangaza kuwa Mkoa utakaokumbwa na njaa mkuu wa mkoa huo hana kazi watu walishangilia. Hawakujua kuwa maana yake ni wao watakaowajibika kuhakikisha mkoa hauna njaa, na si mkuu wa mkoa.

Watu wachache walimuelewa rais aliposema Misaada iliyotolewa kufuatiwa tetemeko la Kagera itatumika kutengeneza miundo mbinu kama shule na vituo vya afya. Kuna waliojipanga kuifaidi wakati wa usambazaji hata kama hawakuathirika. Sasa wengi wameishajiweka sawa na wamejenga nyumba wanazoweza. Kumbe inawezekana?! Shule ambazo wananchi lazima watazifaidi; zimejengwa. Najua kuna wajinga wachache bado hawajaona na wanaweza kutarajia iwe hoja katika chaguzi zijazo Watu wachache wanamuelewa rais anaposema limeni muuze kwa uhuru bila vikwazo. Mabadiliko hayo.

Si mbali sana watanzania wataanza kuwahoji wabunge na madiwani kuhusiana na barabara ili mazao yao yapite salama. Si mbali sana mkulima atagoma kuuza mpunga kwa sababu anaweza kuuza mchele. Si mbali sana hatutaona mahindi mijini. Utafika unga na mahindi yaliyokobolewa. Hapo hakuna atakayekuwa anauliza viwanda maana vitakuwa vinaonekana. Na huo ndio msingi wa viwanda vya kati na vikubwa. Waliochukua mbegu za mawese yetu walianzia huko.

Fikra za watu sasa zitakuwa kujitegemea badala ya kutegemea kupewa. Usishangae baada ya miaka kumi Magufuli; kama alivyosema Obama; akajitokeza kuwashukuru watanzania kwa kusimamia mabadiliko yao. Ninaamini Lowasa anaposema mabadiliko anamaanisha hayo. Kama hamaanishi hayo basi ajiandae kulalamika 2020.
 
MABADILIKO NI LAZIMA

It depends, ni mabadiliko ya aina gani! Inaweza kuwa mabadiliko ya KUTOKA HALI NZURI KWENDA MBAYA and VICEVERSA..!!!Na kwa utawala huu NINAVYOONA TANZANIA TUNAELEKEA KUBAYA....!!!!Ukweli na uwazi!
 
Tunazidi kutofautiana,. Hali inazidi kuwa mbaya. Jamii inagawanyika. Itafika mahali tutakuwa hatuzikani. Janga likitokea kwa mtu Fulani wanasema yule .ni wa kundi lile. Hawatashiriki. Iliisha Anza. Ndipo tulipo Sasa. Mtu akifa wengine wanafurahi. Wengine wanasikitika. Wa kundi lake.
 
Obama kasema hakuna uhuru wa kujieleza,habari na shughuri za kisiasa lkn jitu linadai limeshinda kwa 98%
 
Back
Top Bottom