Zanzibar 2020 CCM Zanzibar kunaanza kufuka moshi

Gavana

JF-Expert Member
Jul 19, 2008
33,233
8,779
Urais Zanzibar 2020: Makundi yanavyohaha kuzuia mabadiliko!

1 July 2020

Oktoba mwaka huu wapiga kura wa Zanzibari tutamchagua Rais mpya, akiwa ni Rais wa nane tangu Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964.

Uchaguzi wa Rais Zanzibar mwaka huu pengine utaingia katika rekodi ya namna yake kwani kwa upande wa CCM, mpaka sasa makada zaidi ya 30 wamejitokeza na kuchukua fomu. Hii ni idadi kubwa na sehemu ya makala hii itaelezea kwa nini hili limetokea.

Kwanza lazima tukubaliane kwamba kuijadili CCM na mgombea toka ndani ya chama hicho ni jambo muhimu kwani ndicho chama chenye dola kwa sasa na kina nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi ujao. Hivyo basi hatuwezi kujadili mustakabali wa Zanzibar ama Tanzania kwa ujumla wake pasi kujadili kinachoendelea ndani ya CCM.

Hali ilivyo Zanzibar

Sarakasi za sasa ndani ya CCM Zanzibar hasa za nani ateuliwe kuwa mgombea Urais ni kati ya makundi makubwa mawili. Kundi la kwanza ni lile ambalo kwa upofu limejiaminisha kuwa limehodhi mfumo wa dola Zanzibar na kwamba ndilo lenye haki ya kuendeleza mfumo huo.

Hiki ni kikundi cha watu wachacge walojichotea fedha na mali kwa hila na ufisadi wakitumia nafasi zao ndani ya SMZ au CCM.

Mfumo wa uongozi wa CCM Zanzibar umekuwa katika kazi ya kujisafisha hasa toka aingie madarakani Mwenyekiti mpya wa CCM, Rais Magufuli. Hata hivyo kundi hilo linaamini Magufuli inabidi azungushiwe ukuta na kufungwa kidhibiti mwendo (speed governor) ili yale alofanya bara hasa kufurusha walioneemeka kwa hila ndani ya serikali na CCM yasitokee Zanzibar kwani yatakuwa anguko kubwa kwao. Kundi hili lina watu kama Dk Khalid Salum Mohamed (aliyekuwa Waziri wa Fedha kisha kutimuliwa kwa ufisadi na Rais Dk Shein), Katibu Mkuu wa Fedha Zanzibar Khamis Mussa Omar, Issa Gavu, Katibu Mkuu Kiongozi Dk Abdulhamid Yahya Mzee, Mahmoud Thabit Kombo, Mohamed Raza, Naushad Mohamed Suleiman na Haroon Zakaria, Hassan Turky na wengine.

Ili kufahamu kwa nini kundi hili linataka mtu wao kuwa Rais Zanzibar tutazame japo kwa ufupi watu hawa ni kina nani.

Dk Khalid Salum Mohamed.

Huyu alifutwa kazi akiwa Waziri wa Fedha katika serikali ya Dkt Shein. Khalid alidhihirika kujilimbikizia mali akikusanya rushwa za mabilioni toka kwa wawekezaji na wafanyabishara hasa wa China.

Vyombo ya usalama vikamnasa, Rais Dkt Shein akamfuta kazi. Mbali na hilo akiwa Waziri Khalid ana madudu lukuki na yote sasa yako katika faili lake Kamati ya Maadili CCM na vyombo vya Usalama. Mfano akiwa Waziri alishinikiza mpwawe, Sabra Issa Machano kuajiriwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF).

Mwanamama huyo akiwa ZSSF akashirikiana na Khalid na washirika wao kuweka mipango mahsusi ya kuifisadi SMZ kwa miradi ya ujenzi wa mabilioni isiyo na tija stahiki kwa Wazanzibari. Katika hilo familia hiyo na washirika wao wamechota zaidi ya shilingi bilioni 10 fedha ya walalahoi wa Zanzibar kwa kuzidisha gharama za miradi maradufu.

Video za Sabra Issa Machano akiimbiwa taarabu, kugawa fedha na kuonyesha mali zake alizopata ndani ya kipindi cha muda mfupi zinapatikana katika mtandao wa YouTube .

Khamis Mussa Omar

Huyu ni Katibu Mkuu Fedha SMZ. Kajichotea mabilioni toka enzi za Karume akiwa madarakani. Anaungwa mkono na wafanyabishara janja janja waliojipatia neema yenye laana kwa ulanguzi na ukwepaji kodi mkubwa katika historia ya Zanzibar wakiwemo Salim Hassan Abdullah Turky (Mr. White)na Mohamed Raza.

Kinyume na kiapo chake, Khamis Mussa katumia ofisi ya umma kuendesha biashara tena zisizo haki kwa walipa kodi wa Zanzibar. Kwa kificho, yeye na mkewe ni wamiliki halali wa kampuni Exotic Tours & Safaris.

Nyaraka zinaonesha kampuni hiyo imekuwa ikitumika kama wakala wa tiketi zote za ndege za wasafiri waloajiriwa SMZ huku ikivuna mamilioni ya shilingi kwa mwaka kinyume na utaratibu wa manunuzi serikalini. Wao wanakula asilimia fulani (cha juu) kwa kila tiketi ya ndege ya mfanyakazi wa serikali.

Kama ilivyokuwa kwa Khalid, Khamis Mussa naye bila haya wala soni katumia nafasi yake ya utumishi wa umma kuweka ndugu zake lukuki kwenye ajira za SMZ akiacha vijana mahiri wa Kizanzibari wenye ujuzi kusota mtaani. Mfano yeye ndiye kalazimisha mkewe (Bi Nasra) aajiriwe katika kitengo cha kupokea marejesho kwenye Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRB).

Mbali na hilo, yeye, mkewe huyo na nduguze wanamiliki vitega uchumi vingi maeneno ya Forodhani tofauti na kipato chao cha utumishi wa umma jambo ambalo baadhi ya makachero wamekuwa wakilifanyia utafiti tangu Januari 2020 na sasa tayari wamekabidhi taarifa yao Kamati ya Maadili CCM Taifa.

Duru za kiuchunguzi zinaonesha Khamis Mussa ana utajiri kupindukia, fedha yake kubwa akiwa amechota ndani ya SMZ kupitia miradi ya ZSFF kama ule wa Mnara wa Kisonge ambao bajeti yake ilizidishwa mara mbili.

Katika uchunguzi wa uadilifu wake, kikosi kazi kilihoji zilipo fedha za SMZ shilingi karibu bilioni 7 ambazo zilipatikana kupitia uwekezaji wa Jumba la Mambo Msiige. Katika sakata hilo ambalo Khamis Mussa ameshiriki na kunufaika kwa asilimia mia, Jengo la Mambo Msiige lilikabidhiwa kwa mwekezaji ambaye sasa ni Hoteli ya Park Hyatt, na mwekezaji huyo ASB Holding alilipa dola za Kimarekani milioni 3 (karibu shilingi bilioni saba), katika akaunti iliyofunguliwa PBZ kwa jina la serikali.

Baadaye akaunti hiyo ilifungwa na fedha haikuingizwa kwenye hazina ya serikali na inaelezwa zilichotwa na Khamis Mussa akisaidiana na washirika wake.

Jumba la Mambo Msiige sasa Park Hyatt Hotel ambapo Khamis Mussa na wenzake walichota shilingi bilioni 7 za uwekezaji wake
Jumba la Mambo Msiige sasa Park Hyatt Hotel ambapo Khamis Mussa na wenzake walichota shilingi bilioni 7 za uwekezaji wake

Kwa kuwa tumbo la mlafi halishibi chochote bali vumbi ya kaburi, akiwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Khamis Mussa amehusika kuidhinisha miradi mikubwa zaidi ya kifisadi kuwahi kutokea katika historia ya Zanzibar kwa kutumia fedha za walipo kodi masikini za Shirika la Maendeleo ya Hifadhi ya Jamii (ZSFF).

Mradi kama ule wa apartments za ZSSF Mbweni kautilia saini na kuzidisha gharama maradufu, akala cha juu yeye na washirika wake akiwemo Waziri Issa Gavu. Sehemu ya fedha hizo ndizo zinatumika sasa kwenye kujaribu kupata Urais 2020.

Itoshe kwa ufupi kusema, serikali mpya ijayo Zanzibar lazima si tu imuondoe mtu huyu na watu wa aina yake SMZ na CCM bali pia achunguzwe na kufunguliwa mashtaka haraka. Amekuwa sehemu ya watu wanaoididimiza Zanzibar kwa kutanguliza tumbo zao mbele na hata kwa makusudui kushauri vibaya viongozi wetu wakuu wa nchi kuanzia Amani Karume hadi Dkt Shein.

Sisi wananchi wanyonge wa Zanzibar tunaamini inawezekana, tumeona Magufuli akitapisha fedha mafisadi bara, hilo nalo tunaamini litafika Zanzibar na hakika wanatetemeka na kukosa usingizi kila wakiwaza hilo.

Issa Gavu

Huyu ni Waziri kijana ndani ya serikali ya sasa. Mtu mjanja mjanja, wa kuunganisha na kuchezesha mambo. Katika sakata la ufisadi wa ZSSF yeye ndiye aliyenishikiza fedha za walalahoi wachangiaji ZSSF kutolewa, na ni mnufaika mkubwa ufisadi mwingi wa Khalid na ule wa Khamis Mussa. Gavu pia ni mtu wa karibu wa wafanyabiashara walotajwa katika makala hii.

Katika mbio hizi yeye anatumika kama mjumbe kwenye vikao vya kupanga mikakati wakiamini “kuweka mtu wao” Ikulu ya Zanzibar baada ya Dkt Shein kutamnusuru na madudu yalopita na kumpa nafasi kuendelea kuwa na umuhimu kwenye siasa za Zanzibar. Baadhi ya wazee wa Zanzibar wanamtaja kama mwanasiasa kijana aliyekwenda kasi bila breki na kuponzwa na tamaa.

Wengine

Wengine katika kundi hili ni Mwanasheria Mkuu Zanzibar Said Hassan Said, Katibu Kiongozi Abdulahimd Mzee, Waziri wa Utalii Mahmoud Thabit Kombo, wafanyabiashara janja janja Mohamed Raza, Naushad Mohamed Suleiman na Haroon Zakaria. Said Hassan Said kapitisha uozo mwingi SMZ na hata kumuongopea Rais huku akijikusanyia mabilioni.

Hivi sasa yuko mbioni kukamilisha jumba lake jipya la makazi binafsi. Kombo yeye kajimilikisha utalii Zanzibar akiandaa matamasha na wafanyabishara kama Javedi Jafferji na kuchota maelfu ya dola za Kimarekani bila kulipa mapato yoyote SMZ.

Kundi hili linataka yeyote kati ya watu wao awe Rais Zanzibar alimradi asiwe Mhandisi Hamadi Masauni, Dkt Hussein Mwinyi au Profesa Makame Mbarawa. Watatu hawa wanaonekana kama watu wa mabadiliko na wasio na fadhila yoyote kuulipa mfumo wao huo wa kifisadi.

Mbinu gani zinatumika?
Mbinu ya kwanza ni ile ya kutuma makada wengi kuchukua fomu. Hii inatajwa kuwa na malengo mawili, moja ni kumuonesha Mwenyekiti wa CCM Rais Magufuli kuwa tunao wagombea wa kutosha wenye sifa hapa Zanzibar hivyo tunaweza kuchagua tunayemtaka. Ni kama kukitisha chama jambo ambalo ni kosa kinidhamu. Nasema kukitisha chama sababu uko ushahidi kwamba baadhi ya walochukua fomu wamehongwa na timu hiyo ya kina Khamis Mussa na wenzake, na kuwapa hadi shilingi milioni 5 kwa Mgombea.

Wao wanaamini kila kitu kina bei na kinaweza kununulika. Tunaamini baada ya mchakato huu hili litajadiliwa kinidhamu ndani ya CCM kwani ni udhalilishaji mkubwa kwa chama na wanachama. Baadhi ya waliohongwa na kukubali wamerekodiwa na kukiri kuwa wamehongwa kwenda kuchukua fomu.

Mmoja ya watu hao ni Mussa Aboud Jumbe ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya pili Zanzibar, hayati Mzee Aboud Jumbe.

Mbinu ya pili ni ile ya ugeni wa siasa za Zanzibar. Hii inatumika kuwalenga makada wale wale watatu yaani Masauni, Mwinyi na Mbarawa. Hata hivyo ugeni unaotajwa hapa ni ule wa kutokuwa sehemu ya mfumo wa kifisadi ambao sasa CCM imekusudia kuusafisha.

Mfumo ambao alianza kuusafisha Dkt Shein pale alipomfuta kazi ya Uwaziri wa Fedha Dk Khalid Salum Mohamed kutokana na ufisadi.

Mbinu ya tatu ni ile ya usultani ambayo inamlenga hasa Mwinyi. Wajumbe wengi NEC CCM wanashangaa hoja hii kwani watu hao hao wanaotaja usultani sasa ndio waliomuunga mkono Amani Karume mwaka 2000 na 2005. Wachambuzi wanarudi pale pale kwamba suala si “Usultani” bali “Ulaji”.

Kwa hali ilivyo mambo yanakwenda kombo kwa kundi hili la kina Khamis Mussa, Dk Khalid, Issa Gavu na wenzao na katika kutapata tutaona propaganda mufilisi kama hizo ambazo kinadharia tunaweza kuziita unafiki dhidi ya visiwa vyetu hivi vitukufu na watu wake. Hakika jina sahihi ni unafiki.

Kundi hili pia linajinasibu kuwa katika sarakasi zao hizo wanazo baraka za Rais wa sasa Dkt Ali Mohamed Shein. Hata hivyo uchunguzi wa kina unaonesha kuwa jambo hilo si kweli kama ilivyo kawaida yao, kundi hilo linatumia vibaya jina la Rais Dk Shein na Kiti cha Rais, kama ambavyo wamekuwa wakifanya mara kwa mara kwa maslahi yao.

Pengine hakuna jina jengine zaidi ya kusema huu ni unafiki kulinda matumbo binafsi, wakisahau kuwa hakika tumbo la mja asotosheka halishibi kwa lolote bali mavumbi ya kaburi lake mwenyewe. Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema alama za mnafiki ni tatu:

Moja anapozungumza husema uongo, badala ya kusema huyu ataharibu ulaji wetu wanasema huyu analeta Usultani. Kwa kuwa Amani Karume alikuwa ulaji wao mwaka 2000 hawakusema usultani.

Mbili, mnafiki anapotoa ahadi hukhalifu (hatimizi). CCM inataka siasa safi, kiapo cha utumishi wa umma SMZ kinataka utumishi safi. Watumishi hawa wa umma na wana CCM wanapata wapi fedha kununua binadamu wenzao?

Biashara gani wamefanya katika utumishi wao? Kweli watu hawa wametunza viapo vyao vya chama na ndani ya serikali?

Tatu, mnafiki anapoaminiwa hufanya khiyana/haaminiki. Tuwaamini vipi kwa uongozi watu hawa wasotunza viapo vyao vya chama na utumishi?

Watu hawa wenye ndimi mbili za kuongopa ili kulinda maslahi yao? Utumishi wa umma tumewapa ila wao badala ya kutumikia umma wakenda kujitumikia wao na mabwana zao. Tuwaamini kwa lipi?

Yoyote iwavyo, CCM ni imara, inatazama haya wanayofanya kwa makini na itavuka salama katika mtego huu ambao kwa hakika ni mdogo ukitazama chama hiki kikongwe kilipotoka. Ukweli pia unabaki kwamba muda ukifika umefika, pengine sasa ni muda wa wanaodhani wameihodhi Zanzibar kwa manufaa yao na matumbo yao waamke kwani kushakucha na hakika muda ushawadia.
 
Mada yako nimeona umejaa chuki na majungu tu kusema vitu visivyo na ushahidi ikiwa ni muendelezo wa siasa za kimaskini za maji taka na kuchafuana!!ona sasa ninavyoihamisha direction hapa chini!!

Jecha ni chaguo letu wabara! ndie afaa kuwa rais kwa uzoefu, hekima na busara yuko nazo japo washamba waliojazana visiwani mnamzingua pliz enyi wazenji mliojaa damu ya ubaguzi mjazieni Jecha form zake za udhamini, ni mtu jasiri kuliko wote na mwenye akili kuliko wote Zenji.

Kamati kuu CCM nawashauri mpitisheni huyu Jecha kuwa rais kwa kuwa tayari alijitoa mhanga kuulinda muungano kwa kumtangaza rais akiwa jeshi la mtu mmoja mafichoni, Jecha ndie anafaa rais kwa maslahi mapana ya Muungano sababu wazenji wote wanamchukia huyo ndie anafaa kuwa rais na kuwanyoosha na kuwakomesha wazenji, siku zote mwalimu mkali wanafunzi humchukia ila ndie bora kwa hujenga nidhamu na kuleta matokeo bora ya mitihani!!
 
Zanzibar mnachezea sharubu za Magufuli.

Msomage alama za nyakati-Magufuli hapendi siasa za majitaka, mizengwe, rushwa na kung'ang'ania uongozi

Anaweza kuusitisha na kufuta huo mchakato mzima, akaanzisha mwingine, na kuwaondolewa sifa za kuomba tena wale waliohusika na mchakato wa awali
 
Zanzibar mnachezea sharubu za Magufuli

Msomage alama za nyakati-Magufuli hapendi siasa za majitaka, mizengwe, rushwa na kung'ang'ania uongozi

Anaweza kuusitisha na kufuta huo mchakato mzima, akaanzisha mwingine, na kuwaondolewa sifa za kuomba tena wale waliohusika na mchakato wa awali

Acha kumpaka mafuta mwenyekiti wa chama kwa mgongo wa chupa! Jeuri yake atufanyie tu sisi Watanganyika Wanyonge! Zanzibar ni Nchi Huru! Hivyo akitaka kuwaletea ubabe wake alio uzoea, atasababisha tu machafuko kama yale ya 2001.
 
Usitupotezee muda wako hapa tafadhali Rais wa Zanzibar tunajua kama siyo Makame Mbarawa basi atakuwa ni Mkongwe Shamsi Vuai Nahodha.
 
Acha kumpaka mafuta mwenyekiti wa chama kwa mgongo wa chupa! Jeuri yake atufanyie tu sisi Watanganyika Wanyonge! Zanzibar ni Nchi Huru! Hivyo akitaka kuwaletea ubabe wake alio uzoea, atasababisha tu machafuko kama yale ya 2001.
Unamchukulia poa Magufuli, basi ngoja waendeleze huo upuuzi uone
 
Zanzibar mnachezea sharubu za Magufuli

Msomage alama za nyakati-Magufuli hapendi siasa za majitaka, mizengwe, rushwa na kung'ang'ania uongozi

Anaweza kuusitisha na kufuta huo mchakato mzima, akaanzisha mwingine, na kuwaondolewa sifa za kuomba tena wale waliohusika na mchakato wa awali
Mkuu kwa hali ya siasa ilivyo hivi sasa huko Zanzibar kunahitajika Hekima na Busara kumpata Kiongozi na sio ubabe wala vitisho. Zinzibar kwa sasa inahitaji Kiongozi wa kuwaleta pamoja Wazanzibari na sio wakwenda kuwatawanya kwa maslahi ya Viongozi wa Tanz Bara.
 
Mapambio mengi wakati kila mtu anajua kuna chaguo la Chamwino na chaguo la Kisiwandui, kila kundi linapigania maslahi yak
 
Mada yako nimeona umejaa chuki na majungu tu kusema vitu visivyo na ushahidi ikiwa ni muendelezo wa siasa za kimaskini za maji taka na kuchafuana!!ona sasa ninavyoihamisha direction hapa chini!!

Jecha ni chaguo letu wabara! ndie afaa kuwa rais kwa uzoefu, hekima na busara yuko nazo japo washamba waliojazana visiwani mnamzingua pliz enyi wazenji mliojaa damu ya ubaguzi mjazieni Jecha form zake za udhamini, ni mtu jasiri kuliko wote na mwenye akili kuliko wote Zenji.

Kamati kuu sisiem nawashauri mpitisheni huyu Jecha kuwa rais kwa kuwa tayari alijitoa mhanga kuulinda muungano kwa kumtangaza rais akiwa jeshi la mtu mmoja mafichoni, Jecha ndie anafaa rais kwa maslahi mapana ya Muungano sababu wazenji wote wanamchukia huyo ndie anafaa kuwa rais na kuwanyoosha na kuwakomesha wazenji, siku zote mwalimu mkali wanafunzi humchukia ila ndie bora kwa hujenga nidhamu na kuleta matokeo bora ya mitihani!!
Ina onyesha huu ndio ule ule kuendelezo wa fitna ndani ya matumbo ya Ccm. Mbona haya ya kuchafua kundi moja ili tumbo lako lijae upande wa Usultan
 
Kama vijana wa CCM Sasa Tumebadilika Chini ya Mwenyekiti Wetu Mwadilifu JPM.

Duuuuh tumeyasoma
YALIYOANDIKWA na tunaendelea kutafakari Maana Kuna ule usemi adhimu usemao "pindipo inapokufikia hoja ichunguze Kwanza ili usije ukadhuru wasio na hatia".

Nitasema Kweli,fitina Kwangu Mwiko.

Siempre Siempre CCM
Hasta la Victoria CCM
Aluta Continua CCM
 
Dah!...hawa jamaa wameigeuza Zanzibar Mali yao, yaani wanatafuna nchi bila aibu wala huruma. Vyombo vya usalama na taasisi ya kupambana na rushwa wapo wapi?
 
Back
Top Bottom