TANZIA Muongoza filamu maarufu Iran, Dariush Mehrjui na Mkewe wauawa

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Mkurugenzi maarufu wa filamu nchini Iran pamoja na mke wake wameuawa wakiwa nyumbani kwao nje kidogo ya Mji Mkuu wa nchi hiyo, Tehran.

Taarifa kutokea kwenye vyombo vya habari vya nchini Iran zinasema kuwa Dariush Mehrjui (83) na mkewe Vahideh Mohammadifar (54) aliyekuwa Mwandishi wa vitabu na mbunifu wa mavazi walikutwa wakiwa na majeraha ya visu.

Katika wiki za hivi karibuni mke wa Mehrjui alilalamika kupata vitisho vya kuchomwa visu katika mitandao ya kijamii. Binti yao Mona Mehrjui aliikuta miili yao alipoenda kuwatembelea jana usiku.

Mauaji hayo yanaweza kuleta tuhuma juu ya kuhusika kwa Mamlaka kwani hivi karibuni kumekuwa na ukandamizwaji mkubwa dhidi ya wanaoupinga utawala wa Tehran.

Kwa miaka mingi Mkurugenzi huyo alikuwa mkosoaji wa Serikali na mwaka jana alipinga kwa hasira uamuzi wa serikali wa kupiga marufuku filamu yake mpya.

Mehrjui aliyesomea masuala ya Filamu katika Chuo Kikuu cha California nchini Marekani amepokea tuzo nyingi za Kimataifa kutokana na kazi zake.

Mamlaka nchini humo zinafanya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo na hadi sasa hakuna taarifa zaidi.

1697530581087.jpg
 
Mkurugenzi maarufu wa filamu nchini Iran pamoja na mke wake wameuawa wakiwa nyumbani kwao nje kidogo ya Mji Mkuu wa nchi hiyo, Tehran.

Taarifa kutokea kwenye vyombo vya habari vya nchini Iran zinasema kuwa Dariush Mehrjui (83) na mkewe Vahideh Mohammadifar (54) aliyekuwa Mwandishi wa vitabu na mbunifu wa mavazi walikutwa wakiwa na majeraha ya visu.

Katika wiki za hivi karibuni mke wa Mehrjui alilalamika kupata vitisho vya kuchomwa visu katika mitandao ya kijamii. Binti yao Mona Mehrjui aliikuta miili yao alipoenda kuwatembelea jana usiku.

Mauaji hayo yanaweza kuleta tuhuma juu ya kuhusika kwa Mamlaka kwani hivi karibuni kumekuwa na ukandamizwaji mkubwa dhidi ya wanaoupinga utawala wa Tehran.

Kwa miaka mingi Mkurugenzi huyo alikuwa mkosoaji wa Serikali na mwaka jana alipinga kwa hasira uamuzi wa serikali wa kupiga marufuku filamu yake mpya.

Mehrjui aliyesomea masuala ya Filamu katika Chuo
Kikuu cha California nchini Marekani amepokea tuzo nyingi za Kimataifa kutokana na kazi zake.

Mamlaka nchini humo zinafanya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo na hadi sasa hakuna taarifa zaidi.

View attachment 2784328
Ndugu Mhaya , mkurugenzi imetafsiriwa kutoka kwenye "director" ambayo kiusahihi kwenye tasnia ya kiwanda cha filamu ni "muongozaji".
 
Asante sana ndugu Residentura...

Residentura limetokana na Resident, maana yake Mkazi
 
Back
Top Bottom