Mjerumani amchambua Lowassa, awashangaa Watanzania

kama kuna mtu anatazamia kuwa na mabadiliko ktk tanzania kwa kutumia ccm basi anapoteza muda.shida sio mtu shida ni mfumo uliopo ndani ya ccm na sio rahisi kuubadili na jana wapambe tumewaona sisi wenyewe wengine walisimamishwa uenyekiti wa halimashauri fulani kwa rushwa
 
Mbona huyo LOWASSA ajamtaja nani muhusika wa Richmond na aseme hadharan sio kuishia kusema kua ni mpango wa kumchafua tu
Aseme nani alikua pesa
 
Hili ndio tatizo lingine la Wabongo,badala ya kujadili hoja mnakimbilia kumjadili mleta hoja.This is the spirit of simple-mindedness.Watz tuna matatizo makubwa kuliko tunavyodhani,mweh kazi ipo!


Nakubaliana na wewe 100%. Kazi IPO tena si kidogo!!!
 
Ni hatari kama mind ya mtu inanunulika kwa 50000 au 100000 kubadili akili ya kufikiri na kuwa mbumbumbu. Tanzania kuna watu wa ajabu sana
 

ni kweli uadilifu haupimwi kipindi cha kampeni.lakini kwa mgombea wa jana uadilifu wake unatiliwa mashaka toka mwaka 1995.mtu huyu si mgeni machoni mwa watanzania na mambo yake na marafiki zake,na kashfa zake.kipi kinampa sifa ya yeye kuchaguliwa leo hii.yeyote mwenye makandokando hatufai iwe ni lowasa,wasira, mwigulu.wahatever.chama cha mapinduzi hakiwezi kutupatia kiongozi bora kwa sasa.fuull stop.
 

Majibu yako kwa huyo 'mzungu' yanaonesha hata wewe hujitambui na wala ujishughulishi kabisa katika kufikiri.
 
Watanzania wengi wakimuona mzungu lazima wambabaikie wapo radhi kuacha kazi na kuzunguka na mzungu hata kama huyo mzungu ni mwehu.

Sasa wewe kila kitu anachokuambia mzungu kwako sawa tu vipi ameishakuwambia kuhusu uzuri wa ndoa za jinsia moja au mmeishakubaliana kuhusu hilo.

Angalia sana huyo mzungu wako asije kukupoteza.
 

Kama wewe ni mfuatiliaji wa Soka, utajua kuwa Bara la Ulaya linampinga sana Blatter, kura za wala Rushwa wa Africa ndio zinamuweka hapo
 

ulitegemea katika hayo mahojiano Lowassa angekubali kuhusika na hiyo kashfa? ni mahakama tu ndio inayoweza kuthibisha uhusika/kutohusika kwa Lowassa kwenye saga la Richmond!!
 

Kuwa unachukia kupangiwa vitu na wazungu, hilo hata mimi nakuunga mkono na labda niseme mimi sipendi kabisa kabisa. Lakini kuchukia huko nako kunakuja na gharama zake ie: uwajibikaji, ambao umetushinda! Hivyo basi hatuwezi kujifanya kuchukia wakati tunawategemea kwa kila jambo. Lowassa jana ametumia fedha nyingi sana kukusanya watu kwa ajili ya kutaka urais wakati kila mwenye akili anajua huyu anataka kwenda ikulu kufanya biashara na si kumkomboa mtanzania. Sasa anapotokea mtu akausema ukweli kuhusu Lowassa na sarakasi zake, ni lazima tumshukuru na kumuunga mkono bila kuangalia ni mtu wa rangi gani au taifa gani!
 

Umeamua kumu attack mshkaji badala ya kujenga hoja?
 
Kasema kweliii kabisa tutachukua miaka mingi kupata mabadiliko
 
Mbona huyo LOWASSA ajamtaja nani muhusika wa Richmond na aseme hadharan sio kuishia kusema kua ni mpango wa kumchafua tu
Aseme nani alikua pesa

HUMJUI?/ UTU UZIMA DAWA!

TUPENDE KUFIKIRISHA AKILI ZETU!/jr
 

Maalim! Ni bora apotezwa na mzungu kwani hata wenye busara wataelewa lakini si kupotezwa na mwizi anayejulikana ni mwizi na jambazi halafu akamfuata!
 
Hao makatibu wakuu kashindwa kuwadhibiti itakuwa taifa hivyo vimemo vya kuelekeza wafanye nini umesahau asinge kuwa na nakosa angesubili angolewe kama pro Muhongo.
 
Mkuu Gambamala, kiukweli sisi Watanzania ni majitu ma ignorants ajabu na kushindwa kuwa wakweli daima toka kwenye nafsi zetu, na miongoni mwa ma ignorants waliopitiliza ni hawa wanaopenda kujikomba komba kwa wazungu!.

Wewe ulipaswa kuwa mkweli tuu kuwa Lowassa hakujiuzulu kwa tuhuma za rushwa wala hakuna tuhuma yoyote ya rushwa iliyothibitishwa kwenye kashfa ya Richmond ndio maana hakuna kesi yoyote ya rushwa, bali Lowassa alijiuzulu kwa kuwajibika kutokana na madudu ya Richmond yaliyofanyika chini ya dhamana yake kama Waziri Mkuu ili kuiokoa serikali yote isianguke!.

Hii sio mara ya kwanza kwa kiongozi kujiuzulu na kisha kugombea urais!, Mwinyi alikuwa waziri wa mambo ya ndani wakati wa kashfa ya kesi ya Mauaji Mwanza (RIP Andrew Mayalla aliyekuwa RSO wa Mwanza enzi hizo ambaye ndiye mshtakiwa pekee aliyakutwa bila hatia), Alijiuzulu kwa kuwajibika na sio kwa kuhusika!. Vivyo hivyo Lowassa amejiuzulu kwa kuwajibika na sio kwa kuhusika!.

Kama ni rushwa na ufisadi, ungemweleza tuu huyo Mzungu wako kuwa sio siri CCM ndio vinara wa rushwa na ufisadi, ungemwadisia jinsi JK alivyotinga ikulu na mbinu alizotumia!. Precedence ya namna ya kuitafuta ikulu tayari ipo, anachofanya Lowassa ni kufuata nyanyo tuu!.

Na mkiishamaliza mazungumzo yote, muulize hicho ndicho kilichomleta nchini?, akisema sicho, msisitizie ashike kilichomleta na aachana kabisa na mambo yasiyomhusu!.

Pasco
 

Mkono mtupu haulambwi, wazungu wamefanya kila kitu duniani, ni lazima tuchukue mawazo yao kwa sababu kimaendeleo wako sayari nyingine. Waarabu na Wahindi nao wenyewe wakiona mzungu wanatetemeka
 
Eti kipau mbele cha jamaa kitakuwa elimu huo uongo wa mchana kweupe.Ni elimu mbovu ndiyo inayowafanya mpaka leo mheshimike sasa kweli unaweza elimisha watu watambue janja yenu?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…