Mjali mama kijacho wako

Mjali mama kijacho wako

MJALI MAMA KIJACHO WAKO

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

1. Hakikisha unauhakika Mimba ni yako. Usiwe mpumbavu.
Kitendo cha kuhakikisha Mimba ni yako ndio kujali kwenyewe

2. Mpe Maneno matamu mama kijacho wako

3. Msaidie kazi za nyumbani au mtafutie Msaidizi wa Kazi hapo Nyumbani

4. Hakikisha anakula mlo Kamili( balance diet)

5. Fanyeni kwa pamoja mazoezi madogomadogo kulingana na Hali ya ujauzito wa mama kijacho wako.

6. Hakikisha anakunywa Maji ya kutosha kulingana na maelekezo ya wataalamu

7. Muogeshe mama kijacho wako hasa Mimba ikiwa Kubwa

8. Mkatie Bima ya afya tangu Mimba ikiwa changa ili imsaidie wakati wa kujifungua

9. Wekeni utaratibu wa maombi kila siku tangu siku ya Kwanza ya Mimba Mpaka siku ya mwisho akijifungua.

10. Nunueni vifaa vya kujifungua na vya mtoto kidogokidogo kujiandaa na tukio kubwa zuri la kumpokea mtoto.

11. Usimgombeze Mama kijacho lakini hiyo haimaanishi mwanamke akupelekeshe kwa kisingizio cha Mimba.
Mwanamke anaowajibu wa kukuheshimu wakati wote angekuwa na Mimba ya mapacha Saba.

Hakunaga kisirani cha Mimba. Huo ni utapeli na utovu wa Nidhamu kwa baadhi ya wanawake wasio na Adabu

12. Hakikisha mnaishi vizuri na mama kijacho wako ili mtoto akizaliwa awe na utulivu wa Kihisia na kiakili

13. Epuka Washauri ambao sio wataalamu wa mambo ya kina mama wajawazito.

14. Epuka Imani za kishirikina.

15.. Mpeleke Mama kijacho Kliniki awamu zote zinazohitajika.
Usimuache aende pekeake.

Omba ruhusa kazini ukifika Kliniki watampa Mkeo kipaombele mtawahi kuondoka.

Acha nipumzike sasa

Robert Heriel Tz
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
No3❌️❌️
No7❌️❌

Nakuomba uzifute
 
Nipe hoja Mkuu
No3:-Nimsaidie kazi kwa sababu gani? Tangu lini mimba ikawa ugonjwa?

No7:-Hadi inafikia hatua ya kumuogesha ina maana hajiwezi kiasi ambacho anahitaji msaada kama mgonjwa mahututi sio?

Mimi mke wangu huwa anaoga mwenyewe hafi siku ya kwenda kujifungua.

Wewe ninachokiona hapa ni kwamba unataka sasa hadi kazini nisiende nifanye hadi kazi za nyumbani kitu ambacho sicho.

Na ukimuendekeza hivi utaimba wimbo mpya kabla hujafika mbinguni
 
No3:-Nimsaidie kazi kwa sababu gani? Tangu lini mimba ikawa ugonjwa?
Kumtunza Mkeo ni jukumu Lako.
Kumsaidia Kazi iwe kwa kumpa Msaidizi wa Kazi za nyumbani, au kumnunulia mashine za kumrahisishia Kazi za nyumbani au kumsaidia wewe mwenyewe hizo Kazi ni jukumu lako kama Mume.

Mwili wa mwanamke ni tofauti na Sisi Wanaume. Ukimfanyisha mikazi mingi mwanamke anapoteza ule utukufu wa kike na inakuwa aibu kwako na Kwa watoto wako.
Mkeo kachoka, kazeeka na watoto watamuona Mama Yao kajichokea Hana utukufu wowote.

No7:-Hadi inafikia hatua ya kumuogesha ina maana hajiwezi kiasi ambacho anahitaji msaada kama mgonjwa mahututi sio?

Kwani watu wanaogeshwa wakiwa wanaumwa?
😃😃
Kumuogesha Mkeo ni mapenzi sio Mpaka Aumwe.
Yeye anaweza kukuogesha nawe unaweza kumuogesha.

Kama unaweza Kulala naye uchi kipi cha ajabu kuogeshana?

Mimi mke wangu huwa anaoga mwenyewe hafi siku ya kwenda kujifungua.

Wewe ninachokiona hapa ni kwamba unataka sasa hadi kazini nisiende nifanye hadi kazi za nyumbani kitu ambacho sicho.
Kwamba kumuogesha Mkeo inachukua siku nzima?
Ule Muda unaenda kuoga si muende wote wawili bafuni!

Mbona mnakula pamoja,
Mnalala pamoja,
Mnafanya mambo mengi pamoja,
Why kuoga uone ni Jambo Kubwa.

Na ukimuendekeza hivi utaimba wimbo mpya kabla hujafika mbinguni

Kumpa Mkeo mapenzi sio kumuendekeza Bali ni wajibu wako namba Moja kama Mume wake.
 
Jf uongo muhimu...

Si unajua hatupo Sirius saana humu just changamsha genge

Karibu Eid kesho
Khaaah! Ko nawee ni muongo? Hili limeniliza sana.
Na kwa kuthibitisha uongo, EID ni leo, sio kesho.
 
Khaaah! Ko nawee ni muongo? Hili limeniliza sana.
Na kwa kuthibitisha uongo, EID ni leo, sio kesho.
Wenzetu wanakula Leo, tunawatakia sikukuu njema saana.

Sisi tunakula kesho insha'Allah
 
Kheeeh kumbe?! Hii EID mbna kivuruge. Lol
😂😂😂😂
Hamna kivuruge hapo.

Sawa tuu na wale wakusali jumamosi na wengine jumapili

Different perception but the same goal

Unajua mambo ya mapokeo
 
Hamna kivuruge hapo.

Sawa tuu na wale wakusali jumamosi na wengine jumapili

Different perception but the same goal

Unajua mambo ya mapokeo
Sidhani km inashabihiana na hilo, nweiii EID Mubarak.
 
Sidhani km inashabihiana na hilo, nweiii EID Mubarak.
Vina shabishiana sana, yaan watu wanatofautiana namna wanavyo yapokeoa maandiko na tafsiri zake.

Kutofautiana Katika tafsiri ndio huleta tofauti za siku ya kuabudu as well Kula Eid

Anyway haya yote yaliletwa na watu wamashariki ya Kati..

Kikubwa mwezi umeisha Turudi kwenye Kula kimasikhara
 
Una visa weyee, haya sawa. 😂😂😂😂
 
Kumtunza Mkeo ni jukumu Lako.
Kumsaidia Kazi iwe kwa kumpa Msaidizi wa Kazi za nyumbani, au kumnunulia mashine za kumrahisishia Kazi za nyumbani au kumsaidia wewe mwenyewe hizo Kazi ni jukumu lako kama Mume.

Mwili wa mwanamke ni tofauti na Sisi Wanaume. Ukimfanyisha mikazi mingi mwanamke anapoteza ule utukufu wa kike na inakuwa aibu kwako na Kwa watoto wako.
Mkeo kachoka, kazeeka na watoto watamuona Mama Yao kajichokea Hana utukufu wowote.

Kwani watu wanaogeshwa wakiwa wanaumwa?
😃😃
Kumuogesha Mkeo ni mapenzi sio Mpaka Aumwe.
Yeye anaweza kukuogesha nawe unaweza kumuogesha.

Kama unaweza Kulala naye uchi kipi cha ajabu kuogeshana?

Kwamba kumuogesha Mkeo inachukua siku nzima?
Ule Muda unaenda kuoga si muende wote wawili bafuni!

Mbona mnakula pamoja,
Mnalala pamoja,
Mnafanya mambo mengi pamoja,
Why kuoga uone ni Jambo Kubwa.

Kumpa Mkeo mapenzi sio kumuendekeza Bali ni wajibu wako namba Moja kama Mume wake.
Hii kwangu ni hapana Nina kazi nyingi sana za kufanya mkuu
 
Back
Top Bottom