Mjadala wa Sheria Mtaani: Kufanya kazi za ndani nyumbani ni jukumu la mume siyo mke

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Hivi karibuni kulikuwa na picha zenye maneno kadhaa zilikuwa zikisambaa mitandaoni zikielezea kuhusu masuala mbalimbali ya sheria.

Kuna moja hii nikaiona ikisambaa kwa kasi ikiwa na kichwa cha habari:

Kwa Mujibu wa Sheria ya Ndoa Tanzania
KUFANYA KAZI ZA NDANI NYUMBANI NI JUKUMU LA MWANAUME

Andiko hilo lilielezea mambo ambayo mwanaume aliyeoa anatakiwa kuyafanya kwa mkewe kwa mujibu wa sheria ikiwemo kufanya kazi za ndani, na ikaelezwa kuwa mwanamke akifanya hizo kazi basi ni anafanya tu kwa kumsaidia mume wake lakini siyo majukumu yake kisheria.

Wakati mjadala huo ukiendelea kuwa mkali kutokana na wanaume wengi kuonekana kupinga, kuna andiko lingine la kisheria nalo lipo mtandaoni likielezea kupinga kiasi fulani kile kilichoelezwa katika andiko la kwanza.

Andiko la kwanza ni hili hapa…..
f9af4236-5651-4ca4-b21d-ecc2e2395226.jpg


Andiko la pili ni hili hapa…

WAKILI: MJIHADHARI NA WATU WENYE NIA YA KUPOTOSHA MAANDIKO YA SHERIA
Bashir Yakub, WAKILI.
+255 714 047 241.

Kwenye hicho kipeperushi chake anasema Kifungu cha 63 cha Sheria ya Ndoa (S. 63 LMA) kinasema kuwa:

- Kazi za ndani kama kuosha vyombo, kufua, kudeki, kupika, kufagia ni jukumu la mwanaume katika familia.

- Sheria inamtaka mwanaume kumpa mkewe chakula kilichopikwa au ampikie na sio kumpa vitu vya kupika.

- Mume amfulie mke nguo za kuvaa zilizopo au amnunulie nyingine.

- Na kuwa kisheria mwanamke hana wajibu wa kufanya kazi za ndani.

Sasa nakinukuu na kukiweka hapa hicho Kifungu cha 63 Sheria ya Ndoa (S 63 LMA) neno kwa neno kama kilivyo halafu ninyi msome muone hayo maneno kama yamo.

Nitakikopi na kuki-paste kama kilivyo kwa Kiingereza na nitakitafsiri kwa Kiswahili chini.

"63. Duty to maintain spouse

"Except where the parties are separated by agreement or by decree of the court and subject to any subsisting order of the court—

(a) it shall be the duty of every husband to maintain his wife or wives and to provide them with such accommodation, clothing and food as may be reasonable having regard to his means and station in life;

(b) it shall be the duty of every wife who has the means to do so, to provide in similar manner for her husband if he is incapacitated, wholly or partially, from earning a livelihood by reason of mental or physical injury or ill-health".


KISWAHILI.
K. 63 Wajibu wa Kumtunza Mwanandoa.

Isipokuwa kama wahusika wametengana kwa makubaliano ama kwa tuzo ya mahakama, au amri nyingine yoyote ya mahakama:-

(a) Itakuwa ni wajibu wa kila mume kumtunza mke wake au wake zake kwa kuwapa malazi, makazi na chakula kadri itakavyowezekana kwa kuzingatia namna yake ya maisha.

(b) Itakuwa wajibu wa kila mke ambaye ana uwezo wa kufanya hivyo, kumtunza mume wake katika namna sawa ikiwa mume huyo ni mlemavu jumla au sehemu, kutoka katika kipato chake lakini iwe ni kwa sababu tu ya matatizo ya akili, ulemavu au ugonjwa.


Kifungu Kimeishia Hapo.
Sasa, NI WAPI, kazi za ndani kama kuosha vyombo, kufua, kudeki, kupika, kufagia ni jukumu la mwanaume katika familia.

NI WAPI, sheria inamtaka mwanaume kumpa mkewe chakula kilichopikwa au ampikie na siyo kumpa vitu vya kupika.

NI WAPI, mume amfulie mke nguo za kuvaa zilizopo au amnunulie nyingine?

NI WAPI, kuwa kisheria mwanamke hana wajibu wa kufanya kazi za ndani.

Mjihadhari
 
Back
Top Bottom