Mjadala: Side Comments: Tathmini ya Utawala wa Rais Kikwete (2005-2012)

Mjadala: Side Comments: Tathmini ya Utawala wa Rais Kikwete (2005-2012)

Zomba,sina kumbukumbu sahihi kuhusiana na kamati aliyowekwa Iddi Simba.Nafikiri nimeconfuse na ile ya madini ambayo Zitto naye alikuwemo na baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi?Bottomline pointi yangu ni kwamba hakuna ushahidi wa kutosha wenye kusonyesha kuwa serikali inapambana na ufisadi,sana sana ni usanii tu.Watu wanaotakiwa wachunguzwe,wanawekwa kwenye tume za kujichunguza wao wenyewe,is that the way to handle corruption issues?
 
Mkuu ni kweli siyo dagaa,hukunipata vyema,dagaa kivipi na alipigiwa kampeni na mkulu?isitoshe,wale wote waliotajwa kuhusika,kumweka mramba na wale wahindi mahabusu kwa siku kadhaa iyo changa la macho?Style ya JK inajulikana,mbona alimweka Iddi Simba kwenye kamati ya uchunguzi wa EPA eti kukusanya ushahidi na wakati pesa zenyewe zilipotoka yeye alikuwa muhusika mkuu akiact kama mwenyekiti wa ccm wazazi?

Nadhani mantiki ya kuuliza kama Mramba ni kidagaa hujaijuwa bado. Isitoshe nilikuwa siongelei kesi ipi, nilikuwa naonesha kuwa hapana si dagaa tu wanaokumbwa na safisha safisha ya Kikwete ni yeyote anaekutikana na tuhuma na kuna taasisi za kuchunguza na kuamuwa hapa kuna kesi ya kujibu au hakuna.

Kumbuka Kikwete anafanya kazi kwa utawala bora na kufata kanuni na shria za nchi na si kwa kuamrisha shika huyu, shika yule. hapana, lazima kuwe kuna system kamili na hiyo ndiyo anaiweka Kikwete. Na tunaiona kila siku ikizidisha ubora. hata huyo Iddi Simba unaemtaja unamuweka fungu lipi? kidagaa? Jee, hujui kama ana kesi ya kujibu iko mahakamani hivi sasa? Jee unajuwa wakati wa Mkapa alikuwa na shutuma nzito lakini hakufikishwa mahakamani? Fikiri.

Listi ni ndefu kuna kina Yona, kina Mahalu, kina Simba, kina Mramba, hao wote huwezi kusema ni vidagaa, Kuna mpaka wa Mbunge wa cCM ana kesi ya kujibu na wengi sana waliokwisha hojiwa na taasisi mbali mbali za kupigana na ubadhirifu.

Nachelea kuita ufisadi kwani uafisadi ni mpana zaidi ya kuiba serikalini, kuna ufisadi wa ngono, ufisadi wa madaraka, ufisadi wa ubaguzi wa kijinsia, ufisadi wa udini. Ufisadi ni mpana sana kuliko tunavyotaka uwe.
 
Zomba,sina kumbukumbu sahihi kuhusiana na kamati aliyowekwa Iddi Simba.Nafikiri nimeconfuse na ile ya madini ambayo Zitto naye alikuwemo na baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi?Bottomline pointi yangu ni kwamba hakuna ushahidi wa kutosha wenye kusonyesha kuwa serikali inapambana na ufisadi,sana sana ni usanii tu.Watu wanaotakiwa wachunguzwe,wanawekwa kwenye tume za kujichunguza wao wenyewe,is that the way to handle corruption issues?

Unaweza ku copy na ku paste ndio maana hizo features ni muhimu sana kwa dunia ya leo, tuko kwenye kasi zaidi na usitegemee kuna anaeyajuwa yote kwa kichwa na wala sitegemei nawe utayajuwa yote kwa kichwa , use the technology.
 
Nadhani mantiki ya kuuliza kama Mramba ni kidagaa hujaijuwa bado. Isitoshe nilikuwa siongelei kesi ipi, nilikuwa naonesha kuwa hapana si dagaa tu wanaokumbwa na safisha safisha ya Kikwete ni yeyote anaekutikana na tuhuma na kuna taasisi za kuchunguza na kuamuwa hapa kuna kesi ya kujibu au hakuna.

Kumbuka Kikwete anafanya kazi kwa utawala bora na kufata kanuni na shria za nchi na si kwa kuamrisha shika huyu, shika yule. hapana, lazima kuwe kuna system kamili na hiyo ndiyo anaiweka Kikwete. Na tunaiona kila siku ikizidisha ubora. hata huyo Iddi Simba unaemtaja unamuweka fungu lipi? kidagaa? Jee, hujui kama ana kesi ya kujibu iko mahakamani hivi sasa? Jee unajuwa wakati wa Mkapa alikuwa na shutuma nzito lakini hakufikishwa mahakamani? Fikiri.

Listi ni ndefu kuna kina Yona, kina Mahalu, kina Simba, kina Mramba, hao wote huwezi kusema ni vidagaa, Kuna mpaka wa Mbunge wa cCM ana kesi ya kujibu na wengi sana waliokwisha hojiwa na taasisi mbali mbali za kupigana na ubadhirifu.

Nachelea kuita ufisadi kwani uafisadi ni mpana zaidi ya kuiba serikalini, kuna ufisadi wa ngono, ufisadi wa madaraka, ufisadi wa ubaguzi wa kijinsia, ufisadi wa udini. Ufisadi ni mpana sana kuliko tunavyotaka uwe.
Zomba,hakuna mtu yuko jela,yote ni usanii tu,waliokamatwa walichaguliwa chaguliwa tu,eti wizi ulitokea kwenye instituion ya serikali (BOT),halafu rais akaja kusema wananchi wapeleke ushahidi kwenye tume yake aliyoiunda.Si vichekesho hivi ni kitu gani?Kiukweli alitaka ajue issue imelikia wapia na si kuwakamata wahusika.Na baadaye hata Mwema na Pinda wakasema mafisadi wana nguvu sana,na wakikamatwa,basi nchi itayumba,ama umesahau?Pia usipate sana shida sana kuhusu ufisadi,tunazungumzia rushwa hapa,sasa unaweza kuniambia ni kwakiasi gani mmepambana na rushwa ngono?ama uanzungumzia kitu gani unaposema ufisadi wa ngono?Na wa madaraka je?nani kaiba kura?mafumbo ama vijembe kwa viongozi na vyama vya upinzani?Naomba urudi kwenye hoja,kama JK amepambana na ufisadi wa ngono weka ushahidi hapa,otherwise jibu maswali mkuu.
 
zomba hebu tuwe wakweli hapo kwenye red kwa msaada wa chama chetu ripoti ya CAG ilibainisha nini hapa? hihi wataka kusema kwamba ilikosewa? kodi gani ambayo serikali hii imekusanya? FYI uliza watu wa TRA serikali hii inategemea kodi kutoka kwa wafanyakazi tu na ndio maana kila mwaka kodi pay as you earn inapanda. hii ndio kodi pekee ambayo ni reliable kwa serikali hii. ila wafayanbiashara ndo kabisaa wengi wao ni wakwepa kodi na hta ripoti ya CAG ilisema hili. sasa unataka kusema nini zaid hapo?

njia mbadala gani zaid? kumbuka hata maswala ya kukopeshwa wakulima pembejeo ulianza enzi za Ben huku kafanya kuendeleza tu. trekata zenyewe zilizokusudiwa ndio hizo mchina type ipeleke nchi yenye mawe kama iringa uone kama itasembua. pia ni wakulima wangapi ambao wana wakusudia peasant ama farmers? peasants wetu wanatafuta for subsistance na surplus ni ndogo sana hao wakulima wakubwa wanakopesheka ndo akina METL sui dewj ambao kwanza hawana nia thabiti ya kulima bali kuwa na mashamba ili wakakopeshwe na mabenki hivi wafikiri watu hawayajui haya?

Naona unachanganya mada, unachangaya kodi na unachanganya kazi za CAG. Hebu tulia kidogo na ulete moja moja tulichambuwe. CAG analeta ripoti na inajadiliwa bungeni na madudu yake, kitu ambacho ilikuwa hakuna kabla ya Kikwete, jamani hamjui kuwa Kikwete ndiye aliyefanya mabadiliko ya sheria na kanuni za CAG na kumpa wigo mpana zaidi na kufikishwa ripoti yake bungeni kwa haraka zaidi.

Soma hapa kidogo ujuwe mambo ya CAG; allAfrica.com: Tanzania: Bankers, Councils Cited in Massive Swindling Scams

Na hapa: Tanzania: Ministers quizzed over CAG report - In2EastAfrica - East African news, Headlines, Business, Tourism, Sports, Health, Entertainment, Education
 
Zomba,hakuna mtu yuko jela,yote ni usanii tu,waliokamatwa walichaguliwa chaguliwa tu,eti wizi ulitokea kwenye instituion ya serikali (BOT),halafu rais akaja kusema wananchi wapeleke ushahidi kwenye tume yake aliyoiunda.Si vichekesho hivi ni kitu gani?Kiukweli alitaka ajue issue imelikia wapia na si kuwakamata wahusika.Na baadaye hata Mwema na Pinda wakasema mafisadi wana nguvu sana,na wakikamatwa,basi nchi itayumba,ama umesahau?Pia usipate sana shida sana kuhusu ufisadi,tunazungumzia rushwa hapa,sasa unaweza kuniambia ni kwakiasi gani mmepambana na rushwa ngono?ama uanzungumzia kitu gani unaposema ufisadi wa ngono?Na wa madaraka je?nani kaiba kura?mafumbo ama vijembe kwa viongozi na vyama vya upinzani?Naomba urudi kwenye hoja,kama JK amepambana na ufisadi wa ngono weka ushahidi hapa,otherwise jibu maswali mkuu.

Nakushangaa sana unaposema hayo, ina maana haupo kabisa kwenye hii dunia ya Tanzania na mabadiliko anayoyafanya Kikwete, soma hizi halafu useme wapo jela au hawapo jela:

Tanzania jails two over central bank corruption scandal - Central Banking

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...an-car-thief-now-linked-to-epa-scandal-2.html

Soma na hii uone mambo yanavyokwenda: Tanzania: Ministers quizzed over CAG report - In2EastAfrica - East African news, Headlines, Business, Tourism, Sports, Health, Entertainment, Education
 
Karibu tena,unaweza kutuambia kama kiwango cha elimu nacho kimepanda?uwingi wa shule(nadhani ni za kata)unatakiwa uambatane na data za kukuwa kwa kiwango cha elimu nchini,hapo ndo ita make sense,otherwise,ni sawa na ile issue ya umeme alipozungumzia JK kuwa toka awe rais uzalishaji wa umeme umeongezeka kuliganisha na awamu zilizopita,ila hali inazidi kuwa mbaya na umeme ni wa mgawo,so ongezeko la uzalishaji halikuendana na matumizi ama hitaji,mifano hiyo inalingana.Hii ina maana kuwa kuattribute ongezeko la shule kama sifa,basi matokeo kama ni mabaya ie kiwango cha elimu kimeshuka,lazima pia yawe attributed to the leadership as a total failure in an overall issue of education accordingly...

Wala sina tatizo na hoilo, jisomee mwenyewe, Takwimu hazidanganyi:

1. Kuongezeka kwa fursa ya utoaji wa elimu ya awali kwa kuhakikisha kuwa kila shule ya msingi ina darasa la Elimu ya Awali

  • Uandikishaji katika elimu ya awali umeongezeka kutoka wanafunzi 638,591 kwa mwaka 2005 hadi 896, 146 mwaka 2010.(wav 445,867, was 450,279)
2. Kuongezeka kwa ubora wa Elimu

  • Uandikishaji wa Wanafunzi katika shule za msingi umeongezeka kutoka wanafunzi 7,541,208 mwaka 2005 na kufikia 8,441,553 mwaka 2010
  • Uwiano wa mwanafunzi katika darasa umeboreshwa kutoka 1:80 mwaka 2005 na kufikia 1:54 mwaka 2010
  • Uwiano wa kitabu kwa mwanafunzi umeimarika kutoka 1:7 mwaka 2005 na kufikia 1:3 mwaka 2009.
  • Idadi ya walimu wa shule za Msingi imeongezeka kutoka 151,882 mwaka 2006 hadi 157,185 mwaka 2010.
  • Idadi ya shule za msingi imeongezeka kutoka 14,700 mwaka 2006 na kufikia 15,727 mwaka 2009.
  • Kuongezeka kwa uandikishaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalum(walemavu) kutoka wanafunzi 18,982 mwaka 2005 hadiwanafunzi 27,422 mwaka 2009.
3. Idadi ya wanafunzi wanaoendelea na na elimu ya sekondari imeongezeka

  • Wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi na kuendelea na elimu ya sekondari wameongezeka kutoka wanafunzi 493,636 mwaka 2005 na kufikia wanafunzi 999,070 mwaka 2009.
  • Kuongezeka kwa wanafunzi wanaogharamiwa na serikali kutoka katika familia zenye kipato duni na yatima , kutoka wanafunzi 16,345 na kufikia wanafunzi 58,843 mwaka 2009
4. Mafanikio ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari(MMES)

  • yamefanikisha kujengwa na kuongezeka kwa Shule za sekondari za serikali na zilizojengwa kwa nguvu za wananchi kutoka shule 1,745 ( 1,202 za serikali na shule 543 zisizo za serikali) mwaka 2005 hadi shule 4,102 ( 3,283 za Serikali na zisizo za Serikali ni 819) mwaka 2010.
  • Uandikishaji wa wanafunzi wa Elimu ya Sekondari umeongezeka kutoka wanafunzi 524,325 mwaka 2005 hadi wanafunzi 1,466,402 mwaka 2010.
  • Nyumba 4,087 za walimu zimejengwa kuanzia mwaka 2005 hadi 2009 kupitia MMES.
  • Serikali ya awamu ya nne imefanikiwa kujenga Shule za kata 3,131 katika kata 2,575 mwaka 2005-2010.
  • Vitabu nakala 35,6000 vya masomo ya hisabati na sayansi vimesambazwa katika shule 81 za sekondari katika halmashauri 31 ili kuongeza uelewa wa masomo hayo kwa wanafunzi.
  • Vitabu 266,032 vya Sayansi na vitabu 203,824 vya hisabati kutoka USAID vilisambazwa katika shule za sekondari 1,259
5. Kuongezeka na upanuzi wa Mafunzo ya walimu katika shule za msingi na sekondari ambapo vyuo 16 vimefanyiwa ukarabati

  • Vyuo vya ualimu vimeongezeka kutoka vyuo 32 mwaka 2005 na kufikia 34 mwaka 2009.
  • Idadi ya wanafunzi katika vyuo vya ualimu imeongezeka kutoka 14,00(2005) hadi kufikia wanafunzi 21,846 mwaka 2010.
  • Walimu waliohitimu stashahada wameongezeka kutoka 3,148 mwaka 2005 na kufikia 5,476 mwaka 2009.
  • Walimu waliohitimu Shahada wameongezeka kutoka walimu 2,843 mwaka 2005 na kufikia walimu 5,331 mwaka 2009.
  • Jumla ya wahitimu wote ni 5,985 mwaka 2005 walimu 10,807 mwaka 2009
  • Jumla ya walimu kwa sasa ni 19,000
6. Mafanikio ya elimu ya Juu ni pamoja na

  • kuongezeka kwa udahili katika vyuo vikuu ambapo udahili wa wanafunzi umeongezeka kutoka wanafunzi 40,993 mwaka 2005 na kufikia wanafunzi 111,078 mwaka 2010.
  • Idadi ya vyuo vikuu imeongezeka kutoka vyuo 23 mwaka 2005 hadi kufikia vyuo vikuu 31, 2010.
  • Kuweza kujenga chuo kikuu cha Dodoma chenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 40,000 kwa mwaka na kwa sasa kuna wanafunzi 17,282.
  • Kumekuwepo na Ongezeko la utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu kutoka wanafunzi 42,729( sh. 62.5) mwaka 2005 na kufikia wanafunzi 58,841 ( Sh. 140 bilioni) mwaka 2009.
  • Programu za vyuo vikuu zimepanuka na kuboreshwa ambapo vyuo vikuu vya Sokoine, Mzumbe na Dodoma vinatoa shahada ya Elimu.
7. Kuongezeka kwa upanuzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi

  • kuongezeka kwa nafasi za mafunzo kutoka wanafunzi 78,586 mwaka 2005, hadi kufikia wanafunzi 125,359 mwaka 2009.
  • Ujenzi wa vyuo 10 vya ufundi umekamilika katika mikoa ya Kigoma, Kilimanjaro,Mtwara, Pwani, Dar es salaam, Manyara na Kagera(karagwe).
8. Kuongeza fursa ya upatikanaji wa Elimu ya Watu wazima

  • Walimu 940 na Maafisa Elimu watu Wazima487 wa Halmashauri zote nchini wamepatiwa mafunzo kuhusu uanzishwajio wan a uendeshaji wa vituo na vikundi vya MUKEJA
  • Moduli 2,280 za MUKEJA zilichapwa na kusambazwa
  • Wanafunzi 7,290 wa Mpango Elimu ya Msingi kwa Walioikosa( MEMKWA) walimaliza Elimu ya Msingi na kati yao wanafunzi 2,363 walichaguliwa kuendelea na Elimu ya Sekondari
 
Ok,
Je wafikiri hata hiyo 40% ya utegemezi tuliyonayo ni sahihi kwetu?
Nafikiri tuache sana ku-refer previous leadership kwani comparison yaweza kua "vertically"au "horizontally", what about other countries?

Be realistic, Unaamini resources tulizonazo + geographical boundaries zinatu-favor kua na "competitive advantages" ambazo tumeshindwa kuzitumia.

Nyerere alikua na falsafa ya kuyaacha madini yetu huko chini yalipo mpaka tutakapopata uwezo wetu wenyewe kwa Imani kwamba "hayaozi",

Walifuata wakaja na falsafa kua bora yatolewe na wageni huko chini japo tuambulie kidogo. Leo Makampuni ya kigeni yanagombania "njia/mikanda" na wachimbaji wadogo huko chini na kuishia kupiga raia risasi.

Tuna vivutio vingi sana vya utalii ikiwemo uwindaji ambapo Mawaziri wanaishia kujinufaisha wenyewe, huku wakipumzishwa kupisha wengine pale wanapobainika bila kuchukuliwa hatua.

Unakiri liko tatizo hapa ambalo one of the course ni Kikwete as Chief in charge of ruling Government??

Utegemezi sio sahihi kabisa kwetu au kwa mwingine yeyote yule kumbuka kutoka 60% mpaka kufikia around 40% ni achievement kubwa sana. Ina maana tuneelekea kuzuri na malengo ni kuwa ifikapo mwaka 2020 tuwe tuna budget isiyotegemea donors. Kwa sasa bado lakini tunafanya vizuri, inawezekana tusifike 2020 (nadhani unakumbuka vision 2020). Na hizi Gas kwa wingi tulizovumbuwa na misamaha ya kodi ya wawekezaji kwenye migozi na kwingine inavyoanza kwisha na kufikia kuanza kulipa kodi, kuna migodi na uwekezaji mwingine umeshaanza kulipa kodi zilizosamehewa natumai mpaka 2015 tutakuwa tunaongea mengine.
 
Wala sina tatizo na hoilo, jisomee mwenyewe, Takwimu hazidanganyi:

1. Kuongezeka kwa fursa ya utoaji wa elimu ya awali kwa kuhakikisha kuwa kila shule ya msingi ina darasa la Elimu ya Awali

  • Uandikishaji katika elimu ya awali umeongezeka kutoka wanafunzi 638,591 kwa mwaka 2005 hadi 896, 146 mwaka 2010.(wav 445,867, was 450,279)
2. Kuongezeka kwa ubora wa Elimu
3. Idadi ya wanafunzi wanaoendelea na na elimu ya sekondari imeongezeka
4. Mafanikio ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari(MMES)
5. Kuongezeka na upanuzi wa Mafunzo ya walimu katika shule za msingi na sekondari ambapo vyuo 16 vimefanyiwa ukarabati
6. Mafanikio ya elimu ya Juu ni pamoja na
7. Kuongezeka kwa upanuzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi

  • kuongezeka kwa nafasi za mafunzo kutoka wanafunzi 78,586 mwaka 2005, hadi kufikia wanafunzi 125,359 mwaka 2009.
  • Ujenzi wa vyuo 10 vya ufundi umekamilika katika mikoa ya Kigoma, Kilimanjaro,Mtwara, Pwani, Dar es salaam, Manyara na Kagera(karagwe).
8. Kuongeza fursa ya upatikanaji wa Elimu ya Watu wazima

Nashukuru,ila naona hujalipata swali langu la msingi.Je unaweza kunipa details kama vile ni wanafunzi kiasi gani wamefaulu vs fail, pamoja na waliofanikiwa kumaliza vs walioshindwa,maana hapo ndo tunapima ukuaji wa kiwango cha elimu.Kweli umeweka listi ndefu hapo,lakini mazingira ya watoto kusoma unayajuwa na quality ya elimu yenyewe.Otherwise inaonekana kama mnafanya vitu ili munekane mnafanya kazi,kweli wanafunzi wanakaa chini na pia matatizo mengine mengi tu kuhusiana na elimu.Hayo mambo yanafurahisha kuyasoma lakini reality kitaa ni waay opposite.
 
Mkuu udagaa tunaozungumzia hapa,sidhani kama una anything to do with previous powerfull positions.Nadhani kama hujaelewa,mimi nazungumzia proximity to the case ndo inaonyesha udagaa ama upapa!Kwasababu Mramba alikuwa waziri,haina maana kwamba kwenye dili ndo alipata panga kubwa,mpira walitupiana sana na ikulu kama umesahau yeye ndo alikuwa waziri kipindi hicho serikali ya Ben inamalizia ngwe yake,na vimemo vilitembea from Balali to state house to ministry of finance.Hao wengine mliowataja hata hakuna mtu anawafahamu,hao ni dagaa tu,na unajuwa howm much money has been embezzled so far?possibly nyingi kuliko zile zinazopelekewa kwenye miradi ya wananchi.
 
Ni mafanikio ya rais omba omba kwenye nchi yenye rasilimali za kutosha. Rasilimali zimetusaidiaje? Rushwa ushikaji tumewasadia wanaotusaidia wakati wa kutembeza bakuli badala ya kujisaidia.

Mimi naomba niwaulize hawa wawili tulimchagua JK kwa ajenda ipi? Sababu ya swali langu huko juu kwenye mjadala inasemekana issue ya mabarabara ni mwendelezo wa mipango ya Mkapa. Tuliahidiwa kupigwa vita Rushwa na ufisadi tumefikia wapi?

Rasilimali za nchi zinaanza kukusaidia unapozitumia na si unapozikalia. Huwezi kuanza kuchimba dhahabu leo kwa sururu uone tija kwa nchi, utaiona tija kwa mchimbaji ataebahatika kuipata hiyo dhahabu.

Leo Rasilmali ya Tanzania imeanza kutumika na matokeo tunaanza kuyaona, rasilmali Ardhi ambayo ni bora kuliko dhahabu na almasi ndio kwanza tunaona ikianza kutolewa katika kutumika kwa kulima kwa mkono kwenda kwenye kilimo cha mashine. Hapa ndio kwenye tija kwa Watanzania 80% na ndio kwanza tumeanza uwekezaji wa hali inayoridhisha wakati wa Kikwete na matokeo mazuri tunayaona; Jisomee kidogo:

Kilimo kimeendelea kukua kwa asilimia 5.1, kinachangia asilimia 25.7 katika Pato Ghafi la Taifa, kinachangia asilimia 95 ya chakula na kinatoa ajira kwa zaidi ya asilimia 80 ya watanzania kutokana na kutekeleza kwa ufanisi Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (Agricultural Sector development Programme –ASDP) na Programu ya Mageuzi na Modenaizesheni ya Ushirika (Cooperative Reform and Modernisation Programme –CRMP)
Matumizi ya pembejeo za kilimo yameongezeka kutokana na serikali kutoa ruzuku kwenye mbolea za viwandani, mbegu bora, miche bora na madawa. Kwa mfano mbolea yenye ruzuku imeongezeka kutoka tani 51,629 mwaka 2005/06 hadi tani 141,050 mwaka 2008/09. Katika mwaka 2009/2010 ruzuku ya pembejeo kwa mfumo wa vocha imelenga kuwanufaisha jumla ya wakulima 1,500,000 ikilinganishwa na wakulima 737,000 mwaka 2008/2009.
Huduma za ugani zimeendelea kuboreshwa kutokana na Wizara kuongeza idadi ya wataalam wa kilimo wanaohitimu kutoka katika vyuo vya kilimo na kuajiriwa kwa lengo la kutoa utaalam kwa wakulima vijijini. Kwa mfano, Idadi ya wanafunzi waliojiunga na vyuo vya kilimo nchini imeongezeka kutoka 1,460 mwaka 2007/2008 hadi 3,498 mwaka 2009/2010. Aidha idadi ya Wagani imeongezeka kutoka 3,379 mwaka 2007/2008 hadi 4,437 mwaka 2010.

Ukija kwenye sekata nyingine nayo ni utalii:

3.1. Mchango wa Utalii katika pato la taifa umeongezeka

  • Utalii ni Sekta inayokua kwa kasi na mchango wake kwenye pato la Taifa umekuwa ukiongezeka kila mwaka na kwa sasa ni zaidi ya asilimia 17.5. Aidha, sekta huchangia asilimia 25 ya mapato ya fedha za kigeni.
  • Kutangaza utalii wa Tanzania katika vituo vya Televisheni vya WABC – TV, CNN – America, ‘CNN headline News’ na tovuti ya CNN.
  • Ili kukuza mchango wa Sekta ya Utalii katika pato la Taifa, Wizara iliendelea kupanua wigo wa Mazao ya Utalii kwa kuanisha aina nyingine za utalii kama vile utalii wa mikutano, fukwe za bahari, ikolojia na malikale. Baadhi ya mikutano iliyofanyika ni kama ule wa Sullivan na “African Travel Association-ATA.

Juhudi za dhati na za makusudi zinaendelea kuonekana wakati wa Kikwete kwenye utalii. Jee, unaijuwa Sangita? unajuwa Hoteli bora duniani imetoka Tanzania? kama siyo jitihada makusudi za kukuza utalii wenye tija ungeyaona hayo?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Mkuu udagaa tunaozungumzia hapa,sidhani kama una anything to do with previous powerfull positions.Nadhani kama hujaelewa,mimi nazungumzia proximity to the case ndo inaonyesha udagaa ama upapa!Kwasababu Mramba alikuwa waziri,haina maana kwamba kwenye dili ndo alipata panga kubwa,mpira walitupiana sana na ikulu kama umesahau yeye ndo alikuwa waziri kipindi hicho serikali ya Ben inamalizia ngwe yake,na vimemo vilitembea from Balali to state house to ministry of finance.Hao wengine mliowataja hata hakuna mtu anawafahamu,hao ni dagaa tu,na unajuwa howm much money has been embezzled so far,possibly nyingi kuiko zile zinazopelekewa kwenye miradi ya wananchi.

Tatizo bado unaongelea kesi, huongelei system iliokuwepo na mapungufu yake na vipi yanaboreshwa. Kikwete ameliona hilo na ameboresha wigo wa CAG, wigo wa TAKUKURU, wigo wa sheria na kanuni za jinai. Ujuwe mfumo mzima ulikuwa mbovu na ndio huo unaoshughulikiwa uendane na wakati. Mimi siongelei kesi ila nakuonesha kuwa ulisema hakuna aliyefungwa, mimi nakuonesha kuwa wapo. Ukitaka tuchambuwe kesi moja moja hatutomaliza leo. Na unaweza pia kufanya hivyo kwa kufunguwa mjadala kwenye jukwaa la sheria, huko tutakuja tuchambuwe kesi moja moja.
 
Nashukuru,ila naona hujalipata swali langu la msingi.Je unaweza kunipa details kama vile ni wanafunzi kiasi gani wamefaulu vs fail, pamoja na waliofanikiwa kumaliza vs walioshindwa,maana hapo ndo tunapima ukuaji wa kiwango cha elimu.Kweli umeweka listi ndefu hapo,lakini mazingira ya watoto kusoma unayajuwa na quality ya elimu yenyewe.Otherwise inaonekana kama mnafanya vitu ili munekane mnafanya kazi,kweli wanafunzi wanakaa chini na pia matatizo mengine mengi tu kuhusiana na elimu.Hayo mambo yanafurahisha kuyasoma lakini reality kitaa ni waay opposite.

Ukipitia huko juu utaona kuwa "kuongezeka kwa udahili katika vyuo vikuu ambapo udahili wa wanafunzi umeongezeka kutoka wanafunzi 40,993 mwaka 2005 na kufikia wanafunzi 111,078 mwaka 2010."

Hiyo itakuonesha ni kiwango gani kimeongezeka, sidhani kama kuna wanaoingia vyuo vikuu bila kufaulu.

Ukipenda usipende hiyo ni big achievement kwa miaka 5. Kwa miaka 44 ya Nyerere, Mkapa na Mwinyi tumefikisha wanafunzi 40,993 wa vyuo vikuu kwa mika 5 tu ya mwanzo ya Kikwete kaipita hiyo idadi kwa zaidi ya 100%. bado sijapata data za uhakika za mwaka 2012 nilizopata (not verified) zinaonesha ni zaidi ya mara mbili ya hiyo ya 2010.
 
quote_icon.png
By Mr Rocky

Kuongeza fedha katika Mfuko wa Uwezeshaji Kiuchumi wa wajasiriamali wadogo (Mfuko wa JK) kiasi cha Shilingi bilioni 10.5 kupitia benki ya NMB. ilitoa kiasi cha Shilingi bilioni 10.5 kupitia benki ya NMB (Shilingi bilioni 5.25) na CRDB (Shilingi bilioni 5.25). Kiasi hiki kiliwezesha kutolewa kwa mikopo ya Shilingi bilioni 37.17 ikiwa in asilimia 118 ya Shilingi 31.5 zilizotengwa kutolewa na benk hizo mbili.

Qn;
Zomba tueleze nani alipata hizi bilions ulizotaja katika aya yako hii Sio kusifia tuu na kusema kuwa mkopo huu ulisaidia nani alizipata na zimesaidia nini na kwa nini hadi sasa hata marejesho hayaonekani Mikopo hii ililengwa kuwasaidia wale wajasiriamali wadogo klujikwamua na kufanya biashara katika hali nzuri ila zilitolewa na kuishia kwenye mikono ya watu ambao mnawajua ninyi ila mmekaa kimya wala hamtaki kutujuza ni akina nani. Na wala hamjasema lolote kuhusu kurejeshwa kwa mkopo huo ili uwasaidie wengine ambao wanauhitaji.

Benki zinazotoa mikopo ya mfuko wa uwezeshaji zimeongezeka na kwa sasa si hizo mbili tu kama ifuatavo, nilitaja hizo mbili tu kwa kuwa nilikuwa naonesha kuwa kazi inafanyika, kwa kuwa umelirudia swali naomba nikupe darsa la kina zaidi, swali lako la kuhusu "nani alipata hizo billions" nimeli highlight kwa rangi nyekundu chini hapo:

Economic Empowerment and Job Creation Programme (J.K. Fund)
1.0 Introduction During the financial year 2006/2007 the Government committed a total of shillings 21 billion to establish the Economic Empowerment and Job Creation Programme in order to promote, support and empower small and medium Tanzanian citizen entrepreneurs engage in productive activities to access loans. The main objective of the programme is to increase incomes of small and medium entrepreneurs and to create new jobs for Tanzanian citizens. The programme was planned to be implemented in to two phases and each phase was allocated with shillings 10.5 billion as loan Fund. Two different windows were disigned to channel the Fund to entrepreneurs:- one window was as a "guarantee facility" and the other one as "an on lending facility". In the case of the on lending facility, it was agreed that banks and other financial institutions participating in the programme would issue loans to entrepreneurs amounting to exactly the same amount of Fund deposited by the Government.

Banks that agreed to use the "guarantee facility" window in Phase II include the following:-

  1. CRDB Bank
  2. Tanzania Postal Bank
  3. Akiba Commercial Bank
Whereas, banks and financial institutions that opted for the "on lending facility window" are as follows:-
  1. Kilimanjaro Cooperative Bank LTD,
  2. Kagera Farmers Cooperative Bank,
  3. SCCULT (1992 LTD),
  4. Mbinga Community Benk,
  5. Pride Tanzania,
  6. Mufindi Community Bank,
  7. Azania Bank,
  8. Shirika la Dunduliza,
  9. Uchumi Commercial Bank,
  10. Presidential Trust Fund, and
  11. Mwanga Community Bank
1.1 Implementation of Phase I The implementation of phase I started in November 2006 when the Government deposited shillings 5.25 billion to the CRDB Bank and shillings 5.25 billion to the NMB Bank as guarantee. According to the agreement between the Government and the two banks (CRDB and NMB), the banks were obliged to issue loans to entrepreneurs three times as much the amount deposited by the Government which is equivalent to shillings 31.5 billion. In this phase CRDB issued loans to SACCOS, where as NMB was issuing loans to individual entrepreneurs.

Reports show that by December 2010 a total of shillings 37.169 billion were issued as loans to 44,224 entrepreneurs. Credits amounting to Tshs. 20.939 billion were issued by the CRDB and Tshs. 16.230 billion were issued by the NMB.
1.2 Implementation of Phase II
The implementation of phase II started in December 2007 and concentrates mainly in the 78 districts that were either not at all reached or inadequately funded during Phase I. The Government issued shillings 10.5 for the implementation of Phase II and out of that amount shillings 9.9 billion were allocated to Tanzania Mainland and the remaining shillings 600 million to the Revolutionary Government of Zanzibar for a similar programme.

From the shillings 9.9 billion allocated to Tanzania Mainland, shillings 8.947 billion were disbursed to 12 Financial Institutions to cater for both, as "guarantee facility" and "on lending facility".
By December 2010 a total of Tshs. 9.7 billion was disbursed to 27,973 entrepreneurs.

2.0 Application for credit facilities
Loan application forms are available at the participating Banks and Financial Institution. Application forms are available free of charge i.e. there are no application fees.

Unaweza kusoma zaidi hapa kuhusu mpango mzima:
http://www.uwezeshaji.go.tz/economic/mwananchi.php#
 
Tatizo bado unaongelea kesi, huongelei system iliokuwepo na mapungufu yake na vipi yanaboreshwa. Kikwete ameliona hilo na ameboresha wigo wa CAG, wigo wa TAKUKURU, wigo wa sheria na kanuni za jinai. Ujuwe mfumo mzima ulikuwa mbovu na ndio huo unaoshughulikiwa uendane na wakati. Mimi siongelei kesi ila nakuonesha kuwa ulisema hakuna aliyefungwa, mimi nakuonesha kuwa wapo. Ukitaka tuchambuwe kesi moja moja hatutomaliza leo. Na unaweza pia kufanya hivyo kwa kufunguwa mjadala kwenye jukwaa la sheria, huko tutakuja tuchambuwe kesi moja moja.
Ha ha ha!mkuu tunajuwa mahakama ni kama "shield", si unajuwa tena ie "mambo yako mahakamani so haturuhusiwi kuyazungumzia"?ndo maana sasa huzungumzii tena mambo ya dagaa,sasa unasema kuna waliofungwa na wewe huchambui kesi.What the way to dispise someone and to insult their intelligences!madharau to the fullest.Mkuu mabaya hayajafunika mazuri kweli?umenishangaza kweli kusema kama JK alishindwa kuwachukulia mafisadi hatua basi nifungue thread nyingine kwenye jukwaa la sheria kuchambua kesi moja moja.What a joke!
 
quote_icon.png
By Mr Rocky
Qn;
Kuhusu sheria na utawala, kwa mara ya kwanza Tanzania tumeona ingezeko la mahakimu, majaji, na kupunguwa kwa kesi kwa kiasi kikubwa sana mahakamani.

Je ongezeko hilo linareflect hali halisi ya mahamaka zetu na mlundikano wa kesi? je hao mahakimu na majaji walioongezeka kuna vitendea kazi kuwawezesha kuhimili hali ya nchi yetu? Maana kuna wilaya ambhazo hazina mahakama za mwanzo au hata majengo kuendeshea kesi mbalimbali. Au inabidi hakimu aendeshee kesi zake kwenye ghala (refer Magu)?

Je budget ya kuendesha shughuli za mahakama inatolewa kwa wakati kukidhi uhalisia na mahitaji ya hizo mahakama? Au ni kuongeza tuu majaji na mahakimu bila kujali kama kuna majengo au vitendea kazi kuendesha hizo kesi?

Napendaa uelewe kuwa katika kipindi cha Kikwete kuna mabadiliko ya mfumo wa upelelezi na uendesha mashtaka uliofanyika, zamani ilikuwa wapelelezi ndio haohao waendesha mashtaka, kwa sasa mfumo huo umedilishwa na soma hapa uone unavyoendelea: FULL SHANGWE: WATAALAMU WA JESHI LA POLISI, MAGEREZA NA TAMISEMI WAKUTANA NA MWENDESHA MASHITAKA!!

Kuhusu swali lako la bajeti, nna uhakika mpaka sasa bajeti yetu haikidhi mahitaji yetu na ndio maana kuna mpango wa vipaumbele ulioanzishwa na Kikwete, bajeti ya kila mwaka, kubwa zaidi huenda kwenye sekta na wizara iliyopewa kipaumbele kwa mwaka huo na mpango huo unaonesha kuleta mafanikio makubwa sana.

Mlundikano wa kesi kwa sasa unapunguwa sana, si tu kwa kuongeza majaji na mahakimu bali kama utavyosoma hapo, kesi zinapitia kwanza kwa waendesha mashtaka na hapo huchujwa kesi zinazofikishwa mahakamani na ambazo hazifai kufikishwa mahakamani, Kikwete anafanya kweli hakisii.
 
Ha ha ha!mkuu tunajuwa mahakama ni kama "shield", si unajuwa tena ie "mambo yako mahakamani so haturuhusiwi kuyazungumzia"?ndo maana sasa huzungumzii tena mambo ya dagaa,sasa unasema kuna waliofungwa na wewe huchambui kesi.What the way to dispise someone and to insult their intelligences!madharau to the fullest.Mkuu mabaya hayajafunika mazuri kweli?umenishangaza kweli kusema kama JK alishindwa kuwachukulia mafisadi hatua basi nifungue thread nyingine kwenye jukwaa la sheria kuchambua kesi moja moja.What a joke!

Huo ni unazi usio na mantiki. Kesi za chadema zinaposhinda huwa ni hakimu na sio mahakama? kesi zingine eti ni "shield".

Huwezi kumchukulia mtu hatua kwa kuwa fulani tu kasema huyu ni fisadi, ni lazima uwe na ushahidi kamili la sivyo unapigwa chini vibaya sana. Tunatakiwa tuamini kuwa mfumo wetu unakwenda vizuri sana kwa sasa, isitoshe tuna katiba mpya inakuja kama kuna mapungufu huu ni wakati muafaka wa kuyainisha yawekwe sawa, au unaonaje?

Msikilize Nyerere anasemaje: "'I have sufficient powers under the Constitution to be a dictator." - Nyerere

Hapo hauna hoja unaanza viroja.
 
bottomline ni kwamba hamwezi kuji prosecute,tutajuwa yote tu mkiondolewa madarakani.Ndo mtajuwa uongozi ni dhamana ni si usanii.The day is coming,ndo mtajuwa nani mwenye nguvu za kuuliza nani anahujumu taifa.Na uhalali wa mapato hayo kama viongozi wa umma,vyote vitakuwa ni ushahidi na si hizi tumba hapa za eti hakuna ushahidi na lazima muwe makini!Hizi ni kesi zinazohusu mali za wananchi,mali za taifa.
 
Kilimo kimeendelea kukua kwa asilimia 5.1, kinachangia asilimia 25.7 katika Pato Ghafi la Taifa, kinachangia asilimia 95 ya chakula na kinatoa ajira kwa zaidi ya asilimia 80 ya watanzania kutokana na kutekeleza kwa ufanisi Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (Agricultural Sector development Programme –ASDP) na Programu ya Mageuzi na Modenaizesheni ya Ushirika (Cooperative Reform and Modernisation Programme –CRMP)

Ukisoma kwa haraka haraka unaweza kupiga vigelegele. But let's look at the numbers, shall we?

1. Pamoja na cosmetic efforts za kupata number 'nzuri' kilimo kinakuwa kwa 5.1% (FY 2010/11). From 2005 -2010 growth rate kwenye agriculture ilikuwa around 4.4% kwa hiyo kuna increament of just 1.1%! Yote tisa, kumi, ukiangalia figures za MKUKUTA, by 2010 mipango inaonesha kuwa kilimo kilitakiwa kikuwe na kufikia 10%. 2011 tuko 5.1%., kwa hiyo tuko off MKUKUTA target.

2. Kilimo kinachangia 25.7% ya GDP. Tanzania's GDP ni USD 23bn. Hivyo 25.7% X 23 = USD 5.29. Sasa, leta figures za watu walio kwenye kilimo, 70-80% ya watanzania (aprox 30m people) wako vijijini na wanajishughulisha na kilimo. Kwa maana hiyo basi, 70-80 ya watazania kupitia shughuli kubwa wanayofanya -kilimo wanachangia only 25.7% ya GDP! Hapa tuna kilimo kwanza? and how much we've spent on this kilimo kwanza? return on investment iko wapi hapa?

3. Tanzania tuna 44 million hectares of land suitable for agriculture, lakini only 23% is utilized. Na pia tuna 29.4 million hectares suitable for irrigation, but 289,245 hectares (1%) ndio ziko under irrigation. Hali ilikuwa hivi 2000, ikawa hivyo 2005 na iko hivyo 2011.

Swali la muhimi kujiuliza hapa, Tanzania tunajenga uchumi gani? agricultural based economy? how? matrekta yako Dar, bank ya wakulima iko Dar, mamlaka za hali hewa wako busy kuwataadharisha wakazi wa Dar kuhusu mvua, eduaction system hainekani kuandaa watoto to take a meaningful part kwenye aina ya uchumi unaoongelewa!
 
quote_icon.png
By Edson

swali 1. ni kwa nini utawala wa raisi kikwete umegubikwa na hsutuma za rushwa na ufisadi? na je kwa mtizamo wa zomba ni kweli kikwet kama raisi hana makucha ya kuwadhibiti hawa wala rushwa? kama anayo kwa nini hali iko hivi na kama hana kwa nini asiachie ngazi

Utawala wa Kikwete haujagubukwa na shutuma za rushwa na ufisadi, utawala wa Kikwete unazishughulikia tuhuma za rushwa na ufisadi za tawala zilizopita na kung'oa mizizi iliyowachwa ikuwe kwa miaka 44. NDIO maana leo wakati wa Kikwete unaona kesi nyingi za ufisadi na zinajadiliwa wazi kwenye vyombo vya habari. Ukitazama kesi zote za rushwa na "ufisadi" utakuta ni za tawala iliyopita, mfano EPA, BOT, KIWIRA, MAHALU, RADAR, NDEGE YA RAIS, ATC. Yote hayo ni madudu ya tawala iliyopita. Kikwete anayaibuwa na kuyashughilikia ipasavyo ki kanuni na sheria bila kukiuka haki za mtuhumiwa na tunaona watu wakifikishwa mahakamani na wengine kufungwa na wengine kesi zinaendelea tena nyingi sana. Na bado anaendelea na kufumuwa madudu, tutayaona na kusikia mengi kabla ya muda wake kuisha. Huoni kuwa hiyo ni faraja kubwa kwa Watanzania leo hii?

Tunaona wakati wa Kikwete alivyobadili mfumo wa ukaguzi wa hesabu za Serikali na kumpa wigo mpana CAG na CAG kwa mara ya kwanza ukaguzi wake unajadiliwa kwa kina bungeni na kamati za udhibiti alizozianzisha bungeni. Hivi huuoni mfumo wake mpya unavyoibuwa madudu? na watu kufikishwa mahakamani na kukosa nyadhifa zao. Bado una mdomo wa kusema Kikwete ajiuzulu. Jiulize hao wa kabla yake walikuwa wapi? wakiyalea haya madudu?
 
Back
Top Bottom