Mjadala: Side Comments: Tathmini ya Utawala wa Rais Kikwete (2005-2012)

Mjadala: Side Comments: Tathmini ya Utawala wa Rais Kikwete (2005-2012)

Aisee ndugu zangu mimi ningependa kuwa pamoja nanyi lakini majukumu yananifanya nilale muda huu, kwakuwa Zomba namuona yuko hewani hebu tuwasiliane kwa inbox ili tumalizie Debate yetu.
 
Ukisoma kwa haraka haraka unaweza kupiga vigelegele. But let's look at the numbers, shall we?

1. Pamoja na cosmetic efforts za kupata number 'nzuri' kilimo kinakuwa kwa 5.1% (FY 2010/11). From 2005 -2010 growth rate kwenye agriculture ilikuwa around 4.4% kwa hiyo kuna increament of just 1.1%! Yote tisa, kumi, ukiangalia figures za MKUKUTA, by 2010 mipango inaonesha kuwa kilimo kilitakiwa kikuwe na kufikia 10%. 2011 tuko 5.1%., kwa hiyo tuko off MKUKUTA target.

2. Kilimo kinachangia 25.7% ya GDP. Tanzania's GDP ni USD 23bn. Hivyo 25.7% X 23 = USD 5.29. Sasa, leta figures za watu walio kwenye kilimo, 70-80% ya watanzania (aprox 30m people) wako vijijini na wanajishughulisha na kilimo. Kwa maana hiyo basi, 70-80 ya watazania kupitia shughuli kubwa wanayofanya -kilimo wanachangia only 25.7% ya GDP! Hapa tuna kilimo kwanza? and how much we've spent on this kilimo kwanza? return on investment iko wapi hapa?

3. Tanzania tuna 44 million hectares of land suitable for agriculture, lakini only 23% is utilized. Na pia tuna 29.4 million hectares suitable for irrigation, but 289,245 hectares (1%) ndio ziko under irrigation. Hali ilikuwa hivi 2000, ikawa hivyo 2005 na iko hivyo 2011.

Swali la muhimi kujiuliza hapa, Tanzania tunajenga uchumi gani? agricultural based economy? how? matrekta yako Dar, bank ya wakulima iko Dar, mamlaka za hali hewa wako busy kuwataadharisha wakazi wa Dar kuhusu mvua, eduaction system hainekani kuandaa watoto to take a meaningful part kwenye aina ya uchumi unaoongelewa!

Hayo unayoyasema jibu lake ni Kilimo Kwanza. Hujui kazi za SAGCOT iliyoanzishwa na Kikwete? hujui kuwa tunaalika wawekezaji wakubwa kwenye kilimo? Hujui Kikwete juzi juzi katoka kwenye mkutano alioalikwa USA na G8 ulikuwa kuhusu nini?

Unajuwa leo Singida wanalima strawberries tunda ambalo hakuna Mnyaturu wala Mnyiramba aliyekuwa analijuwa kama linaweza kulimika Singida? Nenda sokoni Singida ukaone strawberries zinavyouzwa kuliko Morogoro (lilikuwa tunda la matajiri tu). Leo bwerere sokoni Singida. Ni ajabu lakini kweli.

Soma hapa uone mapinduzi ya kilimo: Southern Agricultural Corridor of Tanzania: home
50250670dc.jpg

​

Jiulize wa kabla ya Kikwete walikuwa wapi? wamelala?
 
Aisee ndugu zangu mimi ningependa kuwa pamoja nanyi lakini majukumu yananifanya nilale muda huu, kwakuwa Zomba namuona yuko hewani hebu tuwasiliane kwa inbox ili tumalizie Debate yetu.

Wewe pumzika tu, Ni raha tukiongea nje ya inbox, kama tuko hai tuta endelea kesho na kesho kutwa na siku zote, si unaona nipo JF toka 2007. InshaAllah tuwe hai na tutaendelea na mjadala, hakuna haraka.

Wacha mimi nijibu haya maswali mengi yaliyoibuka humu kadri ya uwezo wangu.
 
bottomline ni kwamba hamwezi kuji prosecute,tutajuwa yote tu mkiondolewa madarakani.Ndo mtajuwa uongozi ni dhamana ni si usanii.The day is coming,ndo mtajuwa nani mwenye nguvu za kuuliza nani anahujumu taifa.Na uhalali wa mapato hayo kama viongozi wa umma,vyote vitakuwa ni ushahidi na si hizi tumba hapa za eti hakuna ushahidi na lazima muwe makini!Hizi ni kesi zinazohusu mali za wananchi,mali za taifa.

Bado upo dunia ya zamani sana ndugu yangu, leo kila kitu kipo wazi na Tanzania tuna tuzo za utawala bora, Ni moja katika nchi yenye uongozi wa kuigwa.

Dunia ya leo "you're either with us or you are against us" hachekewi mtu ambae hafai kuwepo. Kikwete analijuwa hilo na ndio maana unaona yupo na anafanya vizuri sana tena sana ukilinganisha na Rais yeyote wa kabla yake kwenye nyanja zote. Ntaendelea kutoa ushahidi humu kila muda unavyokwenda.
 
Wewe pumzika tu, Ni raha tukiongea nje ya inbox, kama tuko hai tuta endelea kesho na kesho kutwa na siku zote, si unaona nipo JF toka 2007. InshaAllah tuwe hai na tutaendelea na mjadala, hakuna haraka.

Wacha mimi nijibu haya maswali mengi yaliyoibuka humu kadri ya uwezo wangu.
zomba huu ni mwanzo wa kuijenja JF upya mimi na wewe tunapaswa kuondoa na kukemea religion hatred hapa JF. Historia itatuhukumu au itatulinda mimi na wewe kama tutasimaia katika ukweli.

Nakutakia daku njema , nadhani utapata msg kutoka kwa Bi Roulette, maana hata mimi nmsubili yeye kabla sijalala.
 
Last edited by a moderator:
Hayo unayoyasema jibu lake ni Kilimo Kwanza. Hujui kazi SAGCOT iliyoanzishwa? hujui kuwa tunaalika wawekezaji wakubwa kwenye kilimo?

Unajuwa leo Singida wanalima strawberries tunda ambalo hakuna mnyaturu wala mnyiramba aliyekuwa analijuwa kama linaweza kulimika Singida? Nenda sokoni Singida ukaone strwaberries zinavyouzwa kuliko Morogoro (lilikuwa tunda la matajiri tu). Leo bwerere sokoni Singida. Ni ajabu lakini kweli.

Soma hapa uone mapinduzi ya kilimo: Southern Agricultural Corridor of Tanzania: home
​
Jiulize wa kabla ya Kikwete walikuwa wapi? wamelala?

Swali langu lilikuwa hapo hapo kwenye kilimo kwanza, return on investment ikoje? Wakati Kilimo kwanza kinaanza 70-80 ya watanzania walikuwa kwenye kilimo cha mkono na growth rate kwenye hii sector ilikuwa 4.4%. Leo hii tunajadili hapoa still ni ile ile, 70-80% kwenye kilimo - subsistence faminig. SAGGOT ni manamba, and worse ni GM (Genetically modified).
Monsato nao wamo.

Lakini kama kweli kilimo kimekuwa, kwanini wakubwa hao hao wanaendelea kulia kila siku kuwa Inflation inachangiwa na uzalishaji mdogo wa chakula? We know inflation rate ilikuwa 5% 2006, sasa hivi tuko 18%, na sababu tunazopewa ni mbili, hali ya chakula nchini & umeme. Kilimo kwanza....




​
 
quote_icon.png
By Edson

swali la 2. raisi kiwkte kwa kiwango kikubwa ameshindwa kuboresha sekta ya afya na kwa kuzingatia mvutano uliopo na na madaktari na hivyo wengi wameamua kuondoa na kwenda nje ya nchi. Nini maoni ya zomba katika hili. ni kweli haiwezekani kuboresha mazingira na malipo ya wafanyakazi wa sekta ya afya?

Ndugu yangu unataka nicheke kwa swali lako. Sekta ya afya Tanzania wakati wa Kikwete, imeboreshwa kiasi hata "life expectancy" ya Mtanzania imeongezeka kutoka miaka 40 wakati wa Nyerere, miaka 48 wakati wa Mkapa mpaka kufikia miaka 58.2 wakati wa Kikwete na inazidi kupanda. Bila Kikwete kuwa na sera nzuri ya Afya ungeona life expectancy ya Mtanzania inapanda hivyo na kuwa record kwa Afrika Mashariki?

soma:

[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Tanzania's life expectancy rises [/TD]
[TD="class: buttonheading, align: right"] [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Thursday, 03 November 2011 22:59
By Ludger Kasumuni
The Citizen Reporter
Dar es Salaam. Tanzanians now have higher life expectancy fixed at 58.2 years at birth than the rest of the citizens of East African Community (EAC), the 2011 Human Development Report (HDR) released by the United Nations Development Programme (UNDP) shows.

Source: Tanzania

Hilo la madakatari kalishughulikia vizuri sana mpaka kakutana nao, kawaachiswa kazi wote waliotka madaktari yote hiyo hawasikii, ulitaka awalambe miguu? kawapa ultimatum, wakae au waondoke. Ni vyema sana alivyofanya wala lisikupe shida.

Soma mafanikio ya Kikwete kwenye sekata ya afaya Takwimu hazidanganyi:

1. Kuongezeka kwa jitihada za kupambana na magonjwa ya mlipuko;Elimu juu ya magonjwa ya kuambukkiza na yasiyo ya kuambukiza ikiwa ni pamoja na kuelimisha jamii juu ya kujikinga na magonjwa mapya yanayojitokeza kama vilel ebola, marbug, Homa ya bonde la ufa na Homa ya mafua makali ya nguruwe.
Wizara imeendelea kuhamasisha jamii juu ya magonjwa milipuko kwa kutoa vipeperushi zaidi ya laki moja kwa nchi nzima pia imetoa elimu kwa umma kupiti vyombo mbalimbali vya habari kama vile radio, televion, magazeti na mabango ambayo yamebandikwa barabarani yakieleza mbinu za Kukabiliana na magonjwa ya milipuko.
2. Kupungua kwa vifo vya watoto wachanga na Mama wajawazito;

  • Chanjo zimeendelea kutolewa kwa watoto wote bila malipo. Chajo mpya imeongezwa aina ya ‘HiB Vaccine' chanjo hii ianajumushwa na chanjo nyingine 4 zilizokuwa zinatolewa kwa pamoja sasa zimekuwa tano na kuitwa chanjo ya Pentavalent (DPT –HB-Hib). Katika mwaka 2009 watoto waliopata chanjo ya surua ni asilimia 93%, DPT-HB3 asilimia 85%, OPV asilimia 88%.
  • Huduma za kliniki zimeboreshwa kwa ununuzi wa vifaa vya kupima mimba, uzito, upatikanaji wa dawa, kufundisha watoa huduma
  • Huduma kwa wajawazito na huduma za kujifungua pamoja na huduma kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano zimeendelea kutolewa bila malipo aktika vituo vya Serikali.
  • Vifaa mbalimbali vya huduma ya uzazi na kliniki wakati wa ujazito vimepelekwa katika hospitali 86 na vituo vya afya 50 kwenye mikoa 20. Aidha machakato wa kupeleka vifaa vya uzazi na kuhudumia watoto katika vituo 200 vya vya afya unaendelea.
  • Ununuzi wa pikipiki za miguu mitatu (ambulance) kwa ajili ya usafiri wa kina mama wajawazito unaendelea na pikipiki 400 zitanunuliwa.
  • Ujenzi wa Zahanati katika kila kijiji unaendelea kupitia Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM). Kati ya mwaka 2008/09 hadi 2009/10 zahanati 400 na vituo vya afya 78 vimejengwa.
3. Kuimarika kwa vita dhidi ya UKIMWI na Malaria;

  • Hali ya maambukiza nchini kiwango cha asilimia 5.7.% ya watu wenye umri wa miaka 15 – 49 (THMIS 2007 – 2008). Hali hii ni pungufu ukilinganisha kiwango na kiwango cha 7.7.% cha watu wenye umri kama huo iliyotolewa (THIS 2003 – 2004). Hii imechangiwa kwa kiasi kikubwa na Kampeni ya upimaji iliyozunduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Mh. Dr. J. K. Kikwete Julai 2007.
  • Hadi 2009 Disemba Kliniki 909 zinatoa Dawa za kupunguza makali ya UKIMWI. Watu waishio na virusi vya UKIMWI 632,086 wamesajiliwa katika kiliniki hizo na 322,783 katik ya hao wanapata dawa za kupunguza makali ya viruasi vya UKIMWI.
  • Huduma za kupunguza maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto inatolewa katika vituo vya Tiba 3,626
  • Jamii inaendelea kuelimishwa kupitia vyombo mbali mbali vya upatikanaji habari ikiwa ni pamoja na machapisho, sinema vipindi vya radio, Televisheni na sanaa.
Ugawaji wa vyandarua vyenye viuatilifu

  • Mwaka 2008 ni takribani 50% ya kaya hapa nchini zilikuwa na vyandarua vyeneye dawa ya kudumu (NGAO). Ili kuongeza kasi Serikali imeamua kugawa bila malipo ili ifikapo mwishoni mwaka mwaka 2011 killa sehemu ya kulaala iwe chandarua chenye dawa ya kudumu. Mwaka 2008 Serikali ilianzisha kampeni ya kugawa bila malipo vyandarua kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5. Hadi kufikia mwezi Aprili (2010) watoto takriban milioni 9 wamegawiwa vyandaru vyenye dawa ya kudumu. Kampeni hii imekamilika katika mikoa yote.
  • Kuanzia mwezi wa nane mwaka huu 2010 kuna kampeni ya pili ya kugawa bila malipo vyandarua 14.6 milioni kila kaya itapewa vyandarua viwili au zaidi,
Upuliziaji wa Viuatilifu Ukoko katika Kuta

  • (indoor Residual Spraying)
  • Kampeni hii imeanzia mkoa wa Kagera mwaka 2007 katika Wilaya ya Muleba, na Wilaya ya Karagwe 2008. Mwaka 2009, afua hii ilitekelzwa katika wilaya zote za mkoa wa Kagera kuanzia mwaka huu (mwezi Agosti, 2010 kampeni itaendelea itajumuisha pia mikoa ya Mara na Mwanza.
  • Kampeni hii imeanzia mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa kuwa mikoa hii ndiyo inaongoza kwa maambukizi ya malaria ifuatatiwa na mikoa ya Kanda ya Pwani
Tiba ya malaria kwa dawa mseto

  • Dawa mseto kama Alu ndiyo dawa bora za kutibu malaria kwa sababu ufanisi wake wa kuponya uko juu (aslimia 95%)
  • Hapa nchini wagonjwa wa malaria wanaokwenda kutibiwa katika vituo vya huduma ya afya vya Serikali wanatibiwa bila malipo au huchangia gharama kidogo kama Sera ya uchangiaji ilivyo.
4. Kutolewa kwa huduma za upasuaji wa moyo nchini;

  • Wagonjwa 168 wamefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo
  • Wataalam wa upasuaji wa moyo wameongezeka, WAUJ ilipelekea jumla ya wataalam 27, nchini india na Israel kusomea upasuaji wa moyo na sasa wote wamerudi nchini wakiendelea na kutuoa huduma katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
  • Ujenzi wa kituo maalum cha matibabu ya moyo umeanza kaktika hospiotali ya Taifa Muhimbili, WAUJ inashirikiana na Mh. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Mrisho J. Kikwete, na unatarajiwa kumalizika miezi kumi na nne ijayo. Kitakuwa ni kituo bora katika Afrika Mashariki na kati.
5. Kukamilika kwa ukarabati wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na upatikanaji wa vifaa vya kisasa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini

  • Karibu majengo yote ya Hospitali ya Taifa Muhimbili yamekarabatiwa na vifaa vya kisasa vimekwea vifaa hivyo ni CT Scan ya Kisasa, Magenet Resonance Imaging (MRI) ya kisasa, Digital, radiograph Sysytem, USS na Fluroscopy. Mashine za kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo zimeshafungwa.
  • Vifaa vya kisasa vimewekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
  • Idara ya Huduma za magonjwa ya Dharura imeimarishwa kwa kuwa na wataalam na vifaa tiba vya kisasa
  • Vituo vingi vya kutolea huduma za afya hapa nchini vimepatiwa vifaa vya kutibu wagonjwa
6. Kuimarishsa upatikanaji wa haki za watoto

  • Kukarabati majengo na kutoa vifaa katika mahabusi za watoto na shule ya maadilisho Irambo.
  • Kukamilisha ujenzi wa mahabusu ya watoto Mtwara.
  • Kukarabati chuo cha Walezi wa Watoto Kisangara.
  • Kutoa mafunzo kuhusiana na haki za watoto katika jamii.
  • Kuimarisha utaratibu wa utojai huduma kwa watotot walio katika mazingira hatarishi.
  • Kutoa huduma kwa watoto walio katika mazingira hatarishi
  • Kuweka viwango vya utoaji wa hududma kwa toto walio katika mazingira hatarishi.
7. Kuimairisha upatikanaji wa haki kwa watu wenye ulemavu na wazee

  • Kukamilika kwa sera ya wazee
  • Kukamilisha sera ya watu wenye ulemavu
  • Kupitishwa kwa sheria ya walemavu 2010
  • Kukarabati nyumba za vyuo vya ufundi kwa watu wenye uelemavu.
  • Kukarabati majengo ya makazi ya wazee
  • Kuhamasisha jamii kuhusiana na utoaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu na wazee.
  • Kutoa nyenzo (vifaa) za kujimudu kwa watu wenye ulemavu na wazee.
  • Kuwajengea uwezo wazee na watu wenye ulemavu kwa kuwapa mitaji midogo midogo.
Source: Afya | Kikwete 2010
 
Swali langu lilikuwa hapo hapo kwenye kilimo kwanza, return on investment ikoje? Wakati Kilimo kwanza kinaanza 70-80 ya watanzania walikuwa kwenye kilimo cha mkono na growth rate kwenye hii sector ilikuwa 4.4%. Leo hii tunajadili hapoa still ni ile ile, 70-80% kwenye kilimo - subsistence faminig. SAGGOT ni manamba, and worse ni GM (Genetically modified).
Monsato nao wamo.

Lakini kama kweli kilimo kimekuwa, kwanini wakubwa hao hao wanaendelea kulia kila siku kuwa Inflation inachangiwa na uzalishaji mdogo wa chakula? We know inflation rate ilikuwa 5% 2006, sasa hivi tuko 18%, na sababu tunazopewa ni mbili, hali ya chakula nchini & umeme. Kilimo kwanza....




​

Nakushangaa sana wakati hata wakuu wa dunia wanayaona mafanikio ya kilimo kwanza wewe huyajui. Sitoshanga kuwa watu kama wewe mko hapa Tanzania lakini hujawahi kwenda hata Ngorongoro.

Soma:

Kilimo Kwanza ch aibeba Tanzania

obama.jpg


Fidelis Butahe RAIS Barack Obama wa Marekani amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi tatu barani Afrika zinazonufaika na mpango wa pamoja wa Kilimo lengo likiwa ni kuongeza na kulinda usalama wa chakula na lishe kwa wananchi wake.

Taarifa ya Ikulu iliyopatikana jana imeeleza kuwa katika hotuba yake ya ufunguzi wa kongamano kuhusu kilimo na usalama wa chakula lililoandaliwa na Kituo cha Masuala ya Kimataifa cha Chicago, jijini Washington juzi, Rais Obama alitangaza ushrikiano huo mpya wa nchi hizo ambazo ni Tanzania, Ghana na Ethiopia.

"Kuna umuhimu wa kuangalia changamoto zinazoikabili dunia, changamoto ya usalama wa chakula, tutatangaza ushirikiano mpya na nchi hizi tatu zitakuwa za mwanzo kuanza ushirikiano huu ambao tutatangaza zaidi kwenye kushughulikia usalama wa chakula," alisema Rais Obama mbele ya viongozi wakuu wa nchi hizo tatu. Alisema kuwa ushirikiano huu mpya utatangazwa rasmi katika kikao cha nchi nane tajiri duniani G8 uliofanyika jana katika eneo la wageni wa Rais wa Marekani, Camp David.

Alisema kuwa kikao hicho cha nchi tajiri duniani kimeweka katika agenda yake suala la chakula duniani kutokana na umuhimu wake katika kipindi hiki.

"Tumeliweka suala la kupiga vita njaa, Marekani ina wajibu wa kupiga vita njaa na pia suala la usalama wa chakula ni suala la kiuchumi," alisema Rais Obama huku akifafanua, "Bara la Afrika linaweza kujitosheleza kwa chakula na pia kuuza nchi nyingine". Ushirikiano huo utakaotangazwa na nchi nane tajiri utahusisha serikali, watu binafsi na wafadhili.

Katika kikao cha mwaka huu, Tanzania imealikwa kuhudhuria kutokana na mpango wake wa Kilimo Kwanza, ambapo nchi tajiri zimeuchukua kama mfano na mikakati iliyomo katika Kilimo Kwanza itatumika kwa ajili ya kuendeleza nchi zingine barani Afrika.

Rais Obama alisema nchi hizo tatu zimechaguliwa katika ushirikiano huo kwa kuwa zimeonyesha kujikita katika kilimo cha usalama wa chakula.

Rais Jakaya Kikwete, tayari yuko jijini Washington kuhudhuria kikao hicho ambapo anatarajiwa kueleza mwelekeo wa Tanzania katika ushirikiano huo.

Akizungumza katika kongamano hilo la siku moja, Rais Kikwete alieleza umuhimu wa ushirikiano huo unaohusisha Serikali, wafanyabiashara binafsi na wafadhili.

"Tunahitaji msaada zaidi katika kilimo na pia kilimo hakiwezi kuachwa kwenye mikono ya Serikali na wafadhili peke yake, hata sekta binafsi ina mchango mkubwa," alisema Rais Kikwete.

Source: Kilimo Kwanza ch aibeba Tanzania

Dodoma

THE Ministry of Agriculture and Food Security has said Kilimo Kwanza programme in the country has been a success despite major challenges still facing the sector.

​
The Deputy Minister for Agriculture, Food Security and Cooperatives, Mr Adam Malima, said areas under irrigation farming have risen from 264,388 hectares in 2006/2007 up to 345,690 hectares in 2010/2011. He said there has been an increase in use of improved seeds due to subsidy programme and extension officers have more been doubled in the last six years.

The Minister was responding to a question posed by Ms Suzan Anselm Lyimo (Special Seats-CHADEMA) on the matter. He said the initiative was being implemented through Agricultural Sector Development Programme (ASDP), also the Southern Agriculture Growth Corridor of Tanzania(SAGGOT).

Mr Malima said other successes were the construction of Ward Resource Centres, use of agro machines and power tillers. The Deputy minister mentioned the challenges as low productivity, unreliable markets, drought, climate change and poor infrastructure.
The Deputy Minister clarified that the government's desire was to deal with the challenges step by step through reviewing implementation of Tanzania Agricultural Food Security Investment Plan (TAFSIP).


Source: allAfrica.com: Tanzania: Kilimo Kwanza Achievements Explained
 
zomba hizi copy & paste hazina maana hapa JF, hiki siyo kijiwe cha kahawa hapa zinatakiwa fact tu Mkuu wangu.

Hizo sio facts? wewe ulipo copy and paste ahadi 69 za Kikwete ulikuwa hujui ulifanyalo? Nikupe facts kama hii ya chini halafu nisikupe source si utaleta ubishi wa bure. Soma:

Thursday, 03 November 2011 22:59
By Ludger Kasumuni
The Citizen Reporter
Dar es Salaam. Tanzanians now have higher life expectancy fixed at 58.2 years at birth than the rest of the citizens of East African Community (EAC), the 2011 Human Development Report (HDR) released by the United Nations Development Programme (UNDP) shows.

Source: Tanzania

Takwimu hazidanganyi.

Naona kompyuta imepona saa hizi au bado upo internet cafe?
 
zomba huu ni mwanzo wa kuijenja JF upya mimi na wewe tunapaswa kuondoa na kukemea religion hatred hapa JF. Historia itatuhukumu au itatulinda mimi na wewe kama tutasimaia katika ukweli.

Nakutakia daku njema , nadhani utapata msg kutoka kwa Bi Roulette, maana hata mimi nmsubili yeye kabla sijalala.

La "udini" linahusu nini tena? umeona kuna hata moja la "udini" katika maandiko yangu kwenye hii nyuzi? nashangaa sana. Akinianzisha yeyote yule kuniongelea dini yangu visivyo sitokaa kimya. Usingizi mwema.
 
quote_icon.png
By Edson

swali la 3. kwa maoni yako zomba ningependa kujua je demokrasia inakua au inadidimizwa nchini? na vipi kuhusu haki za binadamu je serikali ya kikwete inajali haki za binadamu? jibu swali hili kwa kutumia mifano hai

Hapa tulipo na yote haya tunayaongea inaonesha ni vipi demokrasia ilivyo leo. Ni bora kuliko wakati wowote ule. Msikilize Mtikila anasemaje:

Did people live in fear during the Nyerere era?
We experienced a very strange way of living because of the terror campaign with the security officers trained in the communist block. It was terrible.

People did not trust anyone, even in the families. Wives would not trust their husbands and vice versa because it was a very severe terror campaign. People would disappear silently and no one would be allowed to think about them because if you are suspected to be thinking treason, then you also disappear.

We lived under that repressive regime, I mean, all these years until this guy retired after the failure of Ujama, because we did not achieve all these things. We were made to think about things which were not there and believe they are there. To say otherwise was to say treason.

This is the terror campaign which subdued us to the level of livestock, which always live in fear of slaughter anytime.

Source: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/291644-mtikila-mahojiano-kiingereza.html
 
Hatujafikika huko, kuna maswali kumi na tano. Tutafika punguza ghadhab. Hakuna wakati "ufisadi" wa mali za Serikali unashughulikiwa kama wakati huu wakikwete na kwa ushahidi kamili, kuna kesi nyingi za ubadhirifu na rushwa kuliko wakati wowote ule. Takukuru imeboreshwa na kuwa chombo cha taifa zima na si Dar pekee. Mkaguzi wa mahesabu tunaona jinsi ukaguzi wake unavyojadiliwa bungeni na madudu yanavyoibuka. Hii yote ni wakati huu wa Kikwete, haijawahi kuwepo kabla yake. Au nalo hukubali?
zomba hapa nakubaliana nawe manake pia uozo huu Kikwete kaurithi kutoka kwa waliomtangulia. Sasa nataka uonyeshe jinsi ambavyo kesi hii zimekuwa na tija kwa taifa kwa kupunguza ama kutokomeza kabisa nia ya wengine kuendelea kufanya ubadhirifu serikalini. manake sasa hivi inaonekana kana kwamba kesi zipo lakini zinasha kwa watu kujiuzuli na mahakamani unakuta huku ni sawa na ya aliye iba kuku hata kama kaiba mabilioni.
 
Last edited by a moderator:
Naona unachanganya mada, unachangaya kodi na unachanganya kazi za CAG. Hebu tulia kidogo na ulete moja moja tulichambuwe. CAG analeta ripoti na inajadiliwa bungeni na madudu yake, kitu ambacho ilikuwa hakuna kabla ya Kikwete, jamani hamjui kuwa Kikwete ndiye aliyefanya mabadiliko ya sheria na kanuni za CAG na kumpa wigo mpana zaidi na kufikishwa ripoti yake bungeni kwa haraka zaidi.

Soma hapa kidogo ujuwe mambo ya CAG; allAfrica.com: Tanzania: Bankers, Councils Cited in Massive Swindling Scams

Na hapa: Tanzania: Ministers quizzed over CAG report - In2EastAfrica - East African news, Headlines, Business, Tourism, Sports, Health, Entertainment, Education

Labda nikukumbushe kitu CAG anakagua hesabu za serikali zote ambazo zinapatikana kwaa ajili ya kazi za serikali. Hesabu hizi lazima zionyeshe zimetoka wapi revenues and expenditures na ziwe zinaonyesha je zilitumika sahihi?

Katika ripoti yake huko TRA section alionyesha kabisa kwamba fedha ambazo Tra wanakausanya zinatoka kwenye kodi za wafanyakazi na aliagiza tra kufikir juu ya kuweza kukusanya kodi kwa wafanyabiashara na akapropose juu ya misamaha ya kodi ama hukuielewa?

Iko hivi ktk ukusanyaji wa kodi serikali hii imefeli ila sasa yatupasa kuonyesha na kuuthibitishia umma kwamba palipobakia nini kitafanyika manake sasa hivi watu makini na wanahitaj kuona realities na siyo maneno tu.
 
"hadi Juni mwaka 2010 idadi ya shule za sekondari za Serikali ilifikia 3,397 ikilinganishwa na shule 824 zilizokuwepo mwaka 2004."

Au na hayo si mafanikio?
Zomba, nadhani wote tunajua kwamba ongezeko hilo la shule za serikali linasababishwa na project wa ujenzi wa shule za kata, lakini serikali imetangaza mwezi huu kusitisha ujenzi wa shule hizo sababu zimekuwa zikitoa kiwango kidogo sana cha elimu, ikiwa na maana kwamba hatimaye serikali imekubaliana na kilio cha wananchi wengi, au naweza kusema imepata akili za kujua kwamba shule sio madarasa.

Sitaki kuyataja mapungufu ya educational/academic infrastructure katika shule hizo sababu na wewe unayajua na hii ni kwa sababu nakuheshimu. nadhani sasa unaweza kuondoa hoja yako.
 
Kukopi na ku paste kwa data zenye ushahidi kamili ndio haswa inavyotakiwa. Huwezi kuielezea taasisi ya Urais unaoendesha watu millioni zaidi ya 40 bila kuja na majibu yaliyo na ushahidi kamili. Nafurahi kuwa hakuna hata moja lililokuwa challenged na Matola.

Nilibadili strategy baada ya mwenzangu ku declare kuwa kompyuta yake inampa tabu na anatumia kompyuta za internet cafe. Nikaona nisimshushie nondo kali kali kisha weka ngao.....

Tatizo ni kwamba cut paste zingine zilikuwa zinajicontradict kwa mfano, kuna sehemu ulipaste inasema kipindi cha utawala wa mwalimu Tanzania ilibadirika kutoka kwenye nchi iliyokuwa mzalishaji mkubwa wa chakula ikawa the biggest importer of food,

Ghafla tena ukasema utawala wa mwinyi ulifanya mabadiriko makubwa kwenye sera za kiuchumi za mwalimu na kuondoa import restrictions, mpaka sasa bado haijaniingia akilini tuliwezaje kuwa biggest importers of food katika kipindi ambacho tulikuwa tumeweka import restrictions kibao?
 
Nimechelewa kujiunga na mjadala huu. Zomba na wengine mtaniwia radhi kama nitarudia maswali ambayo tayari yameulizwa. Nitajikita zaidi kwenye huduma za jamii ambazo kwa maoni yangu ndizo zinazogusa maisha ya MTANZANIA wa kawaida.

Kwa sasa tuna TANZANIA mbili kama sio tatu kwa masuala huduma za jamii kama ifuatavyo:
ELIMU: Huduma hii imetugawa sana kimatabaka sasa kuliko ilivyokuwa wakati mwingine wowote tangu uhuru;​
AFYA: Huduma hii sasa ndio balaa zaidi. Mgomo wa hivi karibuni wa madaktari wetu umeeleza mengi;​
HAKI: Sijui kama Zomba na wengine mmetembea vijijini mkaziona mahakama zetu za mwanzo zilivyo?​
USAFIRI: Kama unatumia daladala hapa mjini kwenda kazini asubuhi hauhitaji maelezo ya ziada.

​

Labda kama akina Zomba wanaongelea maendeleo ya VITU na sio WATU. Hali ya WATANZANIA kwa ujumla wao ni mbaya sana sasa kuliko wakati mwingine wowote. Tuendelee kufurahia mafanikio ya wachache hasa wanaSIASA na WAFANYABIASHARA matapeli wa nchi hii.
 
Bado upo dunia ya zamani sana ndugu yangu, leo kila kitu kipo wazi na Tanzania tuna tuzo za utawala bora, Ni moja katika nchi yenye uongozi wa kuigwa.

Dunia ya leo "you're either with us or you are against us" hachekewi mtu ambae hafai kuwepo. Kikwete analijuwa hilo na ndio maana unaona yupo na anafanya vizuri sana tena sana ukilinganisha na Rais yeyote wa kabla yake kwenye nyanja zote. Ntaendelea kutoa ushahidi humu kila muda unavyokwenda.

Mh.

Thank you for you sugar coated bullets.

Waliowapeni tuzo ya utawala bora ni Watanzania au ni wale mmnaowaita wawekezaji wenu? Mimi nawaita wabakaji wa uchumi na kikwete analijua hilo. Sababu moja kubwa ni kwamba unawafaidisha wawekezaji kuliko wenye ardhi.

Ni kweli mko na waliowaweka madarakani (Bush and co.) sisi hatuko nanyi ndiyo maana unayoeleza ni sukari kwa nje lakini ni risasi ya moto kwa ndani. Na hii imelengwa sisi ambao hatujui system at work.

Mwisho si vizuri kujitetea na takwimu (data) zisizo na tafsiri (Statistics). Nina maanisha takwimu zako zote hizo zinatafiriwaje na sisi watu wa kawaida nje ya system? Labda jibu kwa sasa hakuna ila tutasubiri fursa yetu ya kura tutapata majibu ya mnavyotutenda na system yenu at work. NI JANGA LA KITAIFA KATIKA HISTORIA YETU NA HUU UTAWALA WA KIKWETE 10 yrs of development will go with the wind.
 
zomba amekunywa maji ya bendera na data anazipata toka kwa baba yake aliyekuwa may be kiongozi au kwenye gahawa hajui chochote sijui linaishi wapi hili mtu maana kama anapitaga mitaani akaona idada ya wamama wauza mihogo na vibeseni na watoto wachanga bila uji na jua linawachoma mpaka mama amalize trey la mihogo huyu bwana asingetetea huu ujinga wake anatuweke matarakimu meeeengi kweli kweli ,pato la mtanzania limekuwa kivipiii zomba PROOV IT BEYOND REASONABLE DOUGHT
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom