Mjadala: Side Comments: Tathmini ya Utawala wa Rais Kikwete (2005-2012)

Mjadala: Side Comments: Tathmini ya Utawala wa Rais Kikwete (2005-2012)

zomba mimi na Kongosho na Mr Rocky tunapenda kukupongeza sana kwa juhudi zako za kuitetea serikali za hali ya juu. ambazo kwakweli umeweza kutuletea data ambazo zipo na kutuonyesh jinsi ambavyo serikali yetu inapotosha hali halisi. Yaani hela inayoombwa ama inayotafutwa inatafutwa with purpose fulan lkn kumbe haitumiki hivyo kwasababu ingekuwa inatumika hivyo basi data zilizopo zingeonyesha hali halisi tofauti na hivi sasa zilivyokaa kiunadharia. Mipango yao ni mizuri lakin si inayotekelezeka.

however siyo kwamba tunapinga kila kitu hapana vingine umesema viko sahhih lakin vingine ni sahihi kwenye makabrasha lakin siyo ukweli kwenye field. big up brother.
 
Last edited by a moderator:

Ungeonesha kama nilivyoonesha mimi unavyosema havipo sahihi, badala ya kurusha shutuma bila ushahidi.

Isitoshe, mimi hapa nilikuwa siitetei Serikali ila namtetea Kikwete na kuonesha mipango na maboresho aliyoyafanya amabyoo yote yamefanikiwa kwa kiwango kikubwa.

Siitetei Serikali nzima kwa kuwa najuwa bado kuna watu Serikalini ambao sio safi na saa nyingine huhisi wanafanya makusudi kabisa kuupaka matope uongozi wa Kikwete.

Kikwete kama Kikwete kafanya mema mengi sana katika uongozi wake kwa manufaa ya umma. Lakini ukumbuke katika kila msafara wa mamba kenge hakosi.

Hujasikia Mchungaji au Sheikh akazaa mtoto jambazi? na wema wote na mafunzo mema yote lakini hayakosekani hayo. Cha msingi ni kutazama Kikwete kama Kikwete anafanya nini? ni mengi sana mema. Lakini Kikwete atapomteua kiongozi mwengine halafu huyo afanye madudu halafu umlaumu Kikwete? itakuwa humtendei haki Kikwete. Tazama aliyeteuliwa katumwa afanye nini na yeye kafanya nini. Kama katumwa kufanya mabaya na Kikwete basi hapo Kikwete atakuwa haepuki lawama, lakini kama Kikwete kasema nataka ununuliwe mtambo wa kufulia nguo Muhimbili wa kisasa, huyo alietumwa akaenda akaununuwa substandard na akala rushwa ya asilimia 10, hapo utamlaumu Kikwete?
 
JK legacy yake itakuwa ni matuta alojenga kwenye highway zetu, jk ni comic dunia haijawhi kuona.
 
Ungeonesha kama nilivyoonesha mimi unavyosema havipo sahihi, badala ya kurusha shutuma bila ushahidi.

Isitoshe, mimi hapa nilikuwa siitetei Serikali ila namtetea Kikwete na kuonesha mipango na maboresho aliyoyafanya amabyoo yote yamefanikiwa kwa kiwango kikubwa.

Siitetei Serikali nzima kwa kuwa najuwa bado kuna watu Serikalini ambao sio safi na saa nyingine huhisi wanafanya makusudi kabisa kuupaka matope uongozi wa Kikwete.

Kikwete kama Kikwete kafanya mema mengi sana katika uongozi wake kwa manufaa ya umma. Lakini ukumbuke katika kila msafara wa mamba kenge hakosi.

Hujasikia Mchungaji au Sheikh akazaa mtoto jambazi? na wema wote na mafunzo mema yote lakini hayakosekani hayo. Cha msingi ni kutazama Kikwete kama Kikwete anafanya nini? ni mengi sana mema. Lakini Kikwete atapomteua kiongozi mwengine halafu huyo afanye madudu halafu umalumu Kikwete? itakuwa humtendei haki Kikwete. Tazama aliyeteuliwa ktumwa afanye nini na yeye kafanya nini. Kama katumwa kufanya magaya na Kikwete basi hapo Kikwete atakuwa haepuki lawama, lakini kama Kikwete kasema nataka ununuliwe mtambo wa kufulia nguo Muhimbili wa kisasa, huyo alietumwa akaenda akaununuwa substandard na akala rushwa ya asilimia 10, hapo utamlaumu Kikwete?
Hapo umeongea point,
Kweli nimeamini hata milembe kuna wengine wamepelekwa kwa kusingiziwa tu, I mean jamii haikuwaelewa wanataka nini wakizani vichaa.
Llkiani pamoja na kuwa kikwete kachagua waziri aliyeenda kufanya madudu kwa nini kikwete akae kimya mpaka vyombo vya habari na wabunge wapige kelele? unakumbuka ilichukua muda gani kumuondoa ekelege? mpaka wabunge wakataka waziri mkuu ajiuzuru?? hapo nani ana kosa. nazani kosa ni kukaa kimya bila kukemea wazembe.
 
Kwangu mimi serikari kwa kipindi 2005-2015 imefanikiwa zaid katika sehemu ya uhuru wa watu kutoa maoni na kusema madukudu yao ni moja kati ya sehemu walio jitahidi.,
 
kwakweli kikwete anapewa kazi nzito na kuonekana sio mtenda mema kwasababu ya watendaji wake wanamuangusha sanaa
 
halafu watu tumekuwa tukitoa maoni mengi ila maoni yetu hayawi implemented na serikali its like tunajifurahisha kuongea and actions are not there at all.
 
nawasalimu katika jna la MUNGU muumba wa mbingu na nchi!
kwa habari yatathmini ya utawala wa huyu kiongozi wa sasa wa Taifa letu, nimepitia maoni na maswali mengi ya wachangiaji wenzangu nimejifunza mengi, kwa kuzingatia ukweli kwamba; mahitaji ya watanzania katika maisha ya kila siku hasa kwa mambo makuu matatu, malazi...chakula na mavazi, ambayo ni ya msingi sana kiasi haipashwi mtu kuyakosa. pia kwamba, mchango wa serikali yetu katika kuwawezesha raia wake kupata mahitaji hayo ( ikumbukwe huu ni wajibu kwa serikali zote duniani ) unaweza kupimwa kwa hali halisi ya wepesi au ugumu wa maisha katika jamii, hili halihitaji shahada kuliamua kwani hata watoto wa fukara wanaweza kulichabua kwa uhalisi kwa kiwango cha weledi wao na likaeleweka, na kwamba;

`uwiano wa nini kimefanikiwa na nini hakijafanikiwa kwa kiwango tarajiwa kiutawala ni vema ukazingatia uhalisi wa mambo toka katika jamii husika, na hasa kuzingatia tija kwa wananchi na hali ya uendelevu wa yale yaliyotekelezwa na pia ukweli kama namna yalivyotekelezwa hayana madhara / hasara kwa wananchi?

sasa basi; nawashangaa wote ambao wanamacho bali hawaoni, wanamasikio hawasikii, tena wana akili nao hawatafakari na kuona uhalisi, bali kwa akili mbovu wanakandamiza mzani upande mmoja. hawaoni hali mbaya katika mandhari ya miji na vijiji, hawaoni misiba ya albino isiyo kwisha, hawaoni mauaji ya raia wasiomakosa, wala matendo ya upendeleo ya spika bungeni ambayo yanampaka aibu kama kanuni ya dhambi inavyo taka ( mwisho ni aibu halafu mauti), pia hawaoni jirani anpokosa kuhudhuria chooni bila ugonjwa wa kumzuia kufanya hivyo bali kuto kula. hawaoni meeeengi yanayoendelea kwenye jamii wanayoishi,hata viwanda vilivyoporwa na wachache wasio na tija kwa umma bali kwa wachache, tena waliodhurumu mafao ya wafanyakazi katika viwanda baadhi hadi leo wanakufa tu hawayaoni haya, sera na mikataba mibaya itakayo tuumiza hata wakitoka madarakani hamvioni wala kusikia pia heee!

pia hasikii; vilio vya kudai haki vinazidi kula uchao ( madaktari, walimu, wafanyakazi kwa jumla na hata raia wengine) hawasikii wazazi wa albino wakilia msiba wala albino anaye omba ulinzi hawamsikii jamani!, hata kelele za migodini kusiko na haki kwa wazawa hawasikii, yaani hata malalamiko juu ya uporwaji madini katika taifa letu wapi jamani!, hasikiki hata mama anayeporwa mtoto ndani ya vyombo vya sheria tena hadharani huku tukisikia wengine daah! MUNGU wasaidie!

sasa wanaamua kutotafakari haya yote kwa kuwianisha na hayo mazuri yasiyo na mashiko, wanayabebea bango kana kwamba yapo pekee katika jamii isiyo na hayo matatizo hapo juu. ILA NAFASI WANAYO WABADILIKE ILI WENZAO WANAPOCHUKUA HATAMU KUONGOZANCHI ANGALAU WAONEKANO WANAMAWAZO YALIYOPONDEKA NA MOYO UNAOTUBU KWA UBAYA HUU.

KWA HAKIKA; mapumba ni mengi kuliko mchele katika utawala huu wa kikatili unaojificha kwenye kauli zisizotosha kuwaficha kama serikali sikivu na kiongozi anaye jali. haya hayaondoi ukweli un aokua kila siku na ndio utakao wamaliza.
MUNGU Ni mwaminifu Tanzania itabadilika na kufika inakotakiwa si muda mrefu. ameni.
 
Nadhani hajui dira ya hii nchi
aliingia madarakani akiwa hajui anaenda kufanya nini kwa watanzania
 
Back
Top Bottom