Mjadala: Side Comments: Tathmini ya Utawala wa Rais Kikwete (2005-2012)

Mjadala: Side Comments: Tathmini ya Utawala wa Rais Kikwete (2005-2012)

Break ni masaa mawili?Mwali vipi?Wewe na Zomba mko time zone moja?Ama kila mtu masjid kwa time yake?Ninaamini masaa mawili yamepita.Samahani kwa usunbufu lakini.Kama wewe uko tayari,basi jaribu kuwa pm wapambanaji,tunawasikilizia hapa.
 
Tumepigiwa sim na Matola, anaomba mjadala uendelee kesho. Alijitolea kwa kuchangia katika mjadala huu kupitia internet cafe kwa muda wa masaa sita, ila sasa anaona it's getting too late. Kesho asubuhi nitarudi kuwajulisheni muda kamili wa kuendelea mjadala. In the mean time tuendelee kukusanya comment na masuali ya members wote katika hii thread ya "side comments"
Samahani sikuiona hii,Zomba yeye yuko tayari?
 
Hivi Zomba anaweza kuelezea mafanikio ya Utawala wa Kikwete kwenye kuboresha elimu ya primary na secondary?? ngoja nione.

"hadi Juni mwaka 2010 idadi ya shule za sekondari za Serikali ilifikia 3,397 ikilinganishwa na shule 824 zilizokuwepo mwaka 2004."

Au na hayo si mafanikio?
 
Kwa jinsi Zomba alivyochemka, nahisi anaweza akakaimisha ID kwa Wanalumumba wenzie bila sisi kujua.

Ila wasiwasi unapungua maana nao ni wachemfu tu kama yeye a.k.a "walewale"
 
"hadi Juni mwaka 2010 idadi ya shule za sekondari za Serikali ilifikia 3,397 ikilinganishwa na shule 824 zilizokuwepo mwaka 2004."

Au na hayo si mafanikio?
Zina walimu??
Vitabu je?
Tofauti za fonts ni ishara kua "copy & paste" imefanya kazi.
 
hivi utawala huu wa kikwete kiukweli kabisa umeleta nafuu gani kwa mtanzania zaid tu ya juhudi za watu binafsi? hebu atumbie kwanini tunashuhudia mfumuko wa bei mkubwa kiasi hiki tena kwa bidhaa za ndani kuliko za nje?

Nafuu kubwa iliyopatikana ni kuwa Mtanzania wa leo ana uwezo wa kununua hicho ambacho kimepanda bei. Mfumuko wa bei uliopo sasa usikutie mashaka sana kwani chanzo kinajulikna na njia madhubuti zinawekwa ili kuuzuia kuendelea kukuwa na kuushusha kabisa.

Huwezi kuwa na Taifa linaondelea bila kuwa na mtafaruku na mifumuko ya bei, hususan ukichukulia Tiafa letu ni la walaji kuliko wazalishaji. Njia za kudumu na za kuzuwia hii mifuko ya bei ni kuubadili mfumo mzima kutoka kuwa walaji pekee na kuelekea kwenye uzalishaji.

Serikali imeshachukuwa hatua madhubuti za kupigana na hiyo mifuko ya bei, kwanza kwa kubadili namna mkulima wa Tanzania anavyolima, kutoka kwenye jembe la mkono kwenda kwenye jembe la mashine. Njia nyingine ni kuhamasisha uwekezaji wa mitaji mikubwa kwenye kilimo kwa kuanzisha SAGCOT, naomba isome hii hapa: Southern Agricultural Corridor of Tanzania: home ili twende sambamba.
 
Sioni hata moja alilofanya la maana kuisaidia nchi hii zaidi ya upuuzi mwingi wa kuliangamiza taifa hayo yako mengi naweza kutaja nikajaza kitabu
 
Nafuu kubwa iliyopatikana ni kuwa Mtanzania wa leo aauwezo wa kununua hicho ambacho kimepanda bei. Mfumuko wa bei uliopo sasa usikutie mashaka sana kwani chanzo kinajulikna na njia madhubuti zina wekwa ili kuuzuia.

Huwezi kuwa na Taifa linaondelea bila kuwa mtafaruku na mifumuko ya bei, hususan ukichukulia Tiafa letu ni walaji kuliko wazalishaji. Njia za kudumu na za kuzuwia hii mifuko ya bei ni kuubadili mfumo mzima kutoka kuwa walaji pekee na kuelekea kwenye uzalishaji.

Serikali imeshachukuwa hatua madhubuti za kupigana na hiyo mifuko ya bei, kwanza kwa kubadili namana mkulima wa Tanzania anavyolima, kutoka kwenye jembe la mkono kwenda kwenye jembe la mashine. Njia nyingine ni kuhamasisha uwekezaji wa mitaji mikubwa kwa kuanzish SAGCOT naomba isome hii hapa: Southern Agricultural Corridor of Tanzania: home ili twende sambamba.

Unadhani tatizo la watanzania kua "walaji zaidi kuliko wazalishaji" ni la kitabia au kimfumo wa uongozi?

Yaani ni Watanzania hatutaki kua wazalishaji? Au watendaji na viongozi hawajajenga mazingira ya kua wazalishaji?
 
zomba naona kama labda unaongea ili tu kunijibu lakini si ukweli. hivi ni watanzania wangapi ambao wanauwezo wa kumudu huu mfumuko wa bei? hivi unaongelea watanzania wanaoish masaki na mbezi /kawe chini? hivi unajua sasa hivi kwa mfumuko wa bei wapo watu wanakula mlo mmoja hapa tz? nenda mburahati mtu anakwenda dukani kuminyiwa dawa ya mswaki ya sh20 just try to imagine. nenda uswahilini keko huko mama anasonga ugali watoto wanakula na mguu/kwato ya kuku ya sh 50 tena wanamegeana kinachowalisha ugali ni ile kachumbari inayouzwa nayo, wengine anakula utumbo wa kuku eti ndo watu wana mudu?

jamani kilimo kina tija kwa taifa hili?wanaanzisha SAGCOT ili hali bado kilimo chetu hakiendelezwi? tizama nilisafiri kwenda moshi last month/arusha nilichokutana nacho ni aibu wachagga wamelima ile mbaya ukipita ni mashamba mazuri yametandazwa mahindi na ufuta bahati mbaya mvua zimewakatili maind yana sinyaa watu kuyanusuri wana mwagilia kwa mfereji ile staili ya kusembua nilishangaa sana sana hivi mtu ananyesha kwa mfereji heka 15-8 how??? hivi zaid ya soil erosion kuna nini tena hapo? tena unanyesha maji ya kugombea? eka sh 20000/=kumwagilia usipobahatika kupata imekula kwako.

najiuliza kuna sababu gani ya kuwa na sagcot kabla hata wale wakulima wadogo kama hawa hawajawezeshwa kulima pasi kutegemea mvua? kwanini hizo hela zisingeelekezwa katika kilimo cha umwagiliaji wa matone kwasababu mkoa huu una maji na yanawezekana kabisa kutumiwa kwa kazi hiyo?

zomba nenda nchi jirani hapo kenya angalia maisha yao ndipo urudi uje useme juu ya hali yetu hii. hivi mkulima kama huyu anavuna bei ya kuuzia iko chini kuliko gaarama alizozalishia so to him hana faida sasa wasema serikali inampango madhubuti?
 
Last edited by a moderator:
Unadhani tatizo la watanzania kua "walaji zaidi kuliko wazalishaji" ni la kitabia au kimfumo wa uongozi?

Yaani ni Watanzania hatutaki kua wazalishaji? Au watendaji na viongozi hawajajenga mazingira ya kua wazalishaji?

Kumbuka Tanganyika wakati inapata Uhuru ilikuwa ni nchi ya kwanza katika Afrika kusafirisha bidhaa za kilimo nje, lilipozinduliwa Azimio la Arusha na Nyerere kutuingiza kwenye siasa ya ujamaa "immediately" tukawa waagiazaji hata wa chakula basic kabisa. Kuanzia hapo na kwa miaka yote iliyobaki ya utawala wa Nyerere (Mtikila anasema ni 44 kwani anaamini hata utawala wa Mwinyi na Mkapa ulikuwa ni wa Nyerere) tukawa Taifa maskini duniani, tunategemea kuomba kuomba hata chakula.

Hayo kwa miaka hii ya Kikwete tunaona yanabadilika, tunakusanya kodi kwa wingi, tunaanzisha njia mbadala za uzalishaji, tunaanzisha viwanda vikubwa vingi, tunaanzisha kilimo kikubwa na si cha jembe la mkono. Hilo pekee litutoa katika kuwa tegemezi wa asilimia zaidi ya 60 ya bajeti yetu wakati wa Nyerere, Mwinyi na 50 Kwa Mkapa hadi sasa tuko chini ya asilimia 40. Ni hatua kubwa sana na hivi karibuni, tukianza kuzalisha gas ya kuuza tunategemea kuondoka kabisa kwenye utegemezi wa nje kwa maendeleo yetu na kuwa 100% sufficient. Hizi zote ni katika kazi nzuri sana za Kikwete.

Kumbuka kuwa bajeti ya leo ni kubwa sana ukilinganisha na za wakati wa nyuma.
 
Ok,
Je wafikiri hata hiyo 40% ya utegemezi tuliyonayo ni sahihi kwetu?
Nafikiri tuache sana ku-refer previous leadership kwani comparison yaweza kua "vertically"au "horizontally", what about other countries?

Be realistic, Unaamini resources tulizonazo + geographical boundaries zinatu-favor kua na "competitive advantages" ambazo tumeshindwa kuzitumia.

Nyerere alikua na falsafa ya kuyaacha madini yetu huko chini yalipo mpaka tutakapopata uwezo wetu wenyewe kwa Imani kwamba "hayaozi",

Walifuata wakaja na falsafa kua bora yatolewe na wageni huko chini japo tuambulie kidogo. Leo Makampuni ya kigeni yanagombania "njia/mikanda" na wachimbaji wadogo huko chini na kuishia kupiga raia risasi.

Tuna vivutio vingi sana vya utalii ikiwemo uwindaji ambapo Mawaziri wanaishia kujinufaisha wenyewe, huku wakipumzishwa kupisha wengine pale wanapobainika bila kuchukuliwa hatua.

Unakiri liko tatizo hapa ambalo one of the course ni Kikwete as Chief in charge of ruling Government??
 
"hadi Juni mwaka 2010 idadi ya shule za sekondari za Serikali ilifikia 3,397 ikilinganishwa na shule 824 zilizokuwepo mwaka 2004."

Au na hayo si mafanikio?
Karibu tena,unaweza kutuambia kama kiwango cha elimu nacho kimepanda?uwingi wa shule(nadhani ni za kata)unatakiwa uambatane na data za kukuwa kwa kiwango cha elimu nchini,hapo ndo ita make sense,otherwise,ni sawa na ile issue ya umeme alipozungumzia JK kuwa toka awe rais uzalishaji wa umeme umeongezeka kuliganisha na awamu zilizopita,ila hali inazidi kuwa mbaya na umeme ni wa mgawo,so ongezeko la uzalishaji halikuendana na matumizi ama hitaji,mifano hiyo inalingana.Hii ina maana kuwa kuattribute ongezeko la shule kama sifa,basi matokeo kama ni mabaya ie kiwango cha elimu kimeshuka,lazima pia yawe attributed to the leadership as a total failure in an overall issue of education accordingly...
 
Kumbuka Tanganyika wakati inapata Uhuru ilikuwa ni nchi ya kwanza katika Afrika kusafirisha bidhaa za kilimo nje, lilipozinduliwa Azimio la Arusha na Nyerere kutuingiza kwenye siasa ya ujamaa "immediately" tukawa waagiazaji hata wa chakula basic kabisa. Kuanzia hapo na kwa miaka yote iliyobaki ya utawala wa Nyerere (Mtikila anasema ni 44 kwani anaamini hata utawala wa Mwinyi na Mkapa ulikuwa ni wa Nyerere) tukawa Taifa maskini duniani, tunategemea kuomba kuomba hata chakula.

Hayo kwa miaka hii ya Kikwete tunaona yanabadilika, tunakusanya kodi kwa wingi, tunaanzisha njia mbadala za uzalishaji, tunaanzisha viwanda vikubwa vingi, tunaanzisha kilimo kikubwa na si cha jembe la mkono. Hilo pekee litutoa katika kuwa tegemezi wa asilimia zaidi ya 60 ya bajeti yetu wakati wa Nyerere, Mwinyi na 50 Kwa Mkapa hadi sasa tuko chini ya asilimia 40. Ni hatua kubwa sana na hivi karibuni, tukianza kuzalisha gas ya kuuza tunategemea kuondoka kabisa kwenye utegemezi wa nje kwa maendeleo yetu na kuwa 100% sufficient. Hizi zote ni katika kazi nzuri sana za Kikwete.

Kumbuka kuwa bajeti ya leo ni kubwa sana ukilinganisha na za wakati wa nyuma.
zomba hebu tuwe wakweli hapo kwenye red kwa msaada wa chama chetu ripoti ya CAG ilibainisha nini hapa? hihi wataka kusema kwamba ilikosewa? kodi gani ambayo serikali hii imekusanya? FYI uliza watu wa TRA serikali hii inategemea kodi kutoka kwa wafanyakazi tu na ndio maana kila mwaka kodi pay as you earn inapanda. hii ndio kodi pekee ambayo ni reliable kwa serikali hii. ila wafayanbiashara ndo kabisaa wengi wao ni wakwepa kodi na hta ripoti ya CAG ilisema hili. sasa unataka kusema nini zaid hapo?

njia mbadala gani zaid? kumbuka hata maswala ya kukopeshwa wakulima pembejeo ulianza enzi za Ben huku kafanya kuendeleza tu. trekata zenyewe zilizokusudiwa ndio hizo mchina type ipeleke nchi yenye mawe kama iringa uone kama itasembua. pia ni wakulima wangapi ambao wana wakusudia peasant ama farmers? peasants wetu wanatafuta for subsistance na surplus ni ndogo sana hao wakulima wakubwa wanakopesheka ndo akina METL sui dewj ambao kwanza hawana nia thabiti ya kulima bali kuwa na mashamba ili wakakopeshwe na mabenki hivi wafikiri watu hawayajui haya?
 
Last edited by a moderator:
mm naomba nidiklee kabisa kwamba zomba umechemka best yaani umeangausha chama chetu pendwa bana lol,.yaani kuona kwamba hata ishu ya ufisadi umeshindwa kuisemea ni kazi basi.

Hatujafikika huko, kuna maswali kumi na tano. Tutafika punguza ghadhab. Hakuna wakati "ufisadi" wa mali za Serikali unashughulikiwa kama wakati huu wakikwete na kwa ushahidi kamili, kuna kesi nyingi za ubadhirifu na rushwa kuliko wakati wowote ule. Takukuru imeboreshwa na kuwa chombo cha taifa zima na si Dar pekee. Mkaguzi wa mahesabu tunaona jinsi ukaguzi wake unavyojadiliwa bungeni na madudu yanavyoibuka. Hii yote ni wakati huu wa Kikwete, haijawahi kuwepo kabla yake. Au nalo hukubali?
 
Zomba kaulizwa swali la ufisadi akamtaja mramba kama wengi tulivyotegemea,na hakujali kutuambia kuwa alinyanyuliwa mkono na JK kwenye kampeni za ubunge?hi ni madharau,kasingizia masjid,nampa benefit of doubt kwenye mwezi huu mtukufu,ila namsubiri akishafuturu arudi hapa.Pole sana ndugu Zomba,kweli hiyo signature yako ya "system at work" si ya bure,ndo maana kina Nape huwa wanajifanya vichaa ati!

Wakati ulikuwa hauniruhusu kuendelea, ukitazama nilipojibu mramba niliuliza na huyo nae ni dagaa?

Kwa kifupi hakuna wakati "ufisadi" wa mali za Serikali unashughulikiwa kama wakati huu wa Kikwete na kwa ushahidi kamili, kuna kesi nyingi za ubadhirifu na rushwa kuliko wakati wowote ule. Takukuru imeboreshwa na kuwa chombo cha taifa zima na si Dar pekee. Mkaguzi wa mahesabu tunaona jinsi ukaguzi wake unavyojadiliwa bungeni na madudu yanavyoibuka. Hii yote ni wakati huu wa Kikwete, haijawahi kuwepo kabla yake. Au nalo hukubali?
 
Mkuu ni kweli siyo dagaa,hukunipata vyema,dagaa kivipi na alipigiwa kampeni na mkulu?isitoshe,wale wote waliotajwa kuhusika,kumweka mramba na wale wahindi mahabusu kwa siku kadhaa iyo changa la macho?Style ya JK inajulikana,mbona alimweka Iddi Simba kwenye kamati ya uchunguzi wa EPA eti kukusanya ushahidi na wakati pesa zenyewe zilipotoka yeye alikuwa muhusika mkuu akiact kama mwenyekiti wa ccm wazazi?
 
Nadhani amegundua kwamba ameshtukiwa, maswali mengine ni sawa na kusema kaacha kucut na kupaste matokeo yake kawa dolo kweli kweli nadhani amepaniki. au swaumu imemfanya uwezo wa kufikiria upungue?

Kukopi na ku paste kwa data zenye ushahidi kamili ndio haswa inavyotakiwa. Huwezi kuielezea taasisi ya Urais unaoendesha watu millioni zaidi ya 40 bila kuja na majibu yaliyo na ushahidi kamili. Nafurahi kuwa hakuna hata moja lililokuwa challenged na Matola.

Nilibadili strategy baada ya mwenzangu ku declare kuwa kompyuta yake inampa tabu na anatumia kompyuta za internet cafe. Nikaona nisimshushie nondo kali kali kisha weka ngao. Cha kushangaza ni pale yeye alipokuja na ahadi 69 za Kikwete ambazo zimo humu humu JF au hiyo siyo kopi na paste? mbona hakuna aliyeuliza kuwa hiyo ni copy and paste? wala mimi sina wasiwasi nayo sitegemei kwa dakika 15 angeweza kuyakumbuka yote na kutoa kichwani.

Na nashkuru kuwa kayaleta hayo na nimeahidi kuyajibu yote kwa ushahidi na kule nilianza na mawili na mengine ntaendelea nayo hapa, ntayajibu yote moja baada ya jingine kwa ushahidi wa humuhumu kwenye mitandao (copy and paste).

Copy and Paste sio kosa kabisa kwenye mjadala kama huu na hapa hatushindani memory zetu, tunajibu maswali ya miaka 7 ya Kikwete na maswali mengine yamegusia kabla ya Kikwete ni vyema tukaleta data zinazoeleweka na ni vizuri zaidi yakawa na ushahidi kamili. Takwimu hazikopeshi. Na mimi si Magufuli wa kukumbuka takwimu zote kwa kichwa.
 
Back
Top Bottom