Pinda anazungumza na anaanza kwa kusema kuwa yeye ni mtoto wa mkulima na kwenye familia yao yeye ni wa kwanza .
Anasema kuwa anajua hata nyumbani kwake wazazi wake wakisikia amepewa wadhifa mkubwa kiasi hicho watakuwa wamepata taabu sana .
Alifanya kazi na Chenge 1974-76 , kama mwanasheria , na baada ya hapo aliitwa ikulu kufanya kazi chini ya uongozi wa Butiku akiwa katibu wa rais msaidizi, akawa na mwinyi kwa miaka kumi kama katibu wake , na pia alifanya kazi na mkapa .
Anasema kuwa alijifunza kufanya kazi kwa nidhamu ya Ikulu, na pia anakiri kuwa yeye sio mwanasiasa ila ndio anajifunza siasa kwa kuwa karibu na viongozi wa kisiasa haswa ikulu.
Anasema kuwa alijaribu kuingia kwenye siasa ila Mkapa akamwambia ataweza kwenda kufanya kazi ya siasa na haswa ubunge?
Anasema kufanya kazi kama mwanasiasa amefanya kwa kipindi cha miaka saba tuu.
Ila anasema kuwa ukifanya kazi TAMISEMI hata ukiwa nani lazima utakomaa tuu, anawashukuru viongozi waliomsaidia kumkomaza akianza na mkapa ,Ngwilizi na Lowassa na kusema kuwa viongozi hao ndio ambao walimlea.
Anamshukuru sana Lowassa kwani ndani ya kipindi kifupi amemkomaza sana , anasema kuwa Lowassa ni kiongozi mzuri sana kwa maana ya utendaji wa kazi za kila siku.
Anamshukuru Lowassa kwa kumsaidia sana kumjenga kisiasa na kiutendaji, na pia anaomba kura kwa kusema kuwa maelezo aliyotoa ndio.
Anasema kitu kipya ni kuwa ni madaraka tuu ila kwa maana ya Pinda kamam mbunge ,na kama walivyomzoea ataendelea kubakia yuleyule , na atafanya kazi na wabunge na haswa kujenga mahusiano baina yao.
Atajitahidi sana kujenga bunge moja litakalokuwa linasimamia masilahi ya taifa hili, na anatamani sana kufanana na mabunge ya uingereza, marekani na israeli kwani wao kwenye kusimamia masilahi ya taifa huwa wanasimama pamoja hakuna tofauti za vyama ,na hicho ndicho ambachoa anakitamani sana sana kukijenga.