Anaanza kwa kumshukuru rais kwa kumteua , anaahidi kuwa atajitahidi sana kutimiza majuku yake ili aweze kufikia azima ya rais ya kulijenga taifa hili.
Anarudia tena kumshukuru Lowassa na kusema kuwa uamuzi wake wa kujiuzulu ni jambo la mfano mkubwa kwake , na kila mmoja akifikwa na hali kama hiyo lazima naye awe tayari kujiuzulu.
Anasema kuwa ni kweli amevaa kiatu cha Lowassa ila hana hakika kuwa kama kitamtosha kwani lowassa amefanya makubwa sana kwenye elimu na atajitahidi ili aweze kuenea.
Anamshukuru tena Ngwilizi, na makatibu wakuu wote ambao amefanya nao kazi kwa pamoja tangu kipindi chote.
Anashukuru wabunge kwa kumpa kazi ya kufanya ndani ya bunge, anashukuru ushirikiano ambao amekuwa akiupata kutoka kwa spika ,naibu na wenyeviti wa kamati za bunge.
Anasema kuwa alipoingia bungeni kwa mara ya kwanza aliwakuta wabunge wengi wa muda mrefu ila baada ya kukaa kwa muda mfupi alijiona anafanana nao kwani bunge limejenga uwanja wa kuweza kujenga mahusiano mema kati ya wabunge.
Anasema kuwa kamati teule imefanya kazi yake na pengine kazi hiyo ndio imemfanya yeye kuwa hapo alipo, anasema kuwa kwake kubwa ni kukubali kuwa ktk utendaji wa kazi za serikali lazima kila mmoja ahakikishe kuwa anatimiza wajibu wake kwa jinsi inavyopaswa.
Kila waziri lazima ahakikishe kuwa wataalamu wao wanafanya kazi kwa kina na kwa ukweli.
Anasema kuwa ripoti ilionyesha kuwa anapaswa kuhakikisha kuwa anafanya kazi ya kukomesha maovu yote ndani ya serikali na kuyakomesha .
Anasema kuwa yeye kama kiongozi yupo kwa ajili ya kuitumia ripoti hiyo kama dira ya kumwongoza.
Kwake TAKUKURU,POLISI NA USALAMA kazi yao kubwa ni kuweza kuisaidia serikali ili kuweza kufanya kazi zao kwa kina zaidi.
Anaamini kuwa yapo mabadiliko muhimu ili kuhakikisha kuwa majukumu yao yanafanyiwa kazi ipasavyo ,na anaahidi mabadiliko ili kuweza kuhudumia wananchi inavyotakiwa.
Anawataka mawaziri watakaoteuliwa lazima wawe tayari kufanya kazi za wananchi kwa kadri walivyodhamiria.
Anasema kuwa bunge linakidhi mahitaji ya mfumo wa vyama vingi na kuna kipindi wasipokuwa makini kuna tatizo, anasisistiza kuwa jambo kuwa sio vyama ila ni bunge na hoja itakuwa ni kujenga bunge na sio vyama ili kuweza kujenga nchi .
Anawashukuru wote aliokuwa nao ndani ya bunge kwa muda wake wa vipindi viwili.
Katika kutekeleza ilani ya CCM anasema wote tushirikiane na kufuchua maovu yote ili kuijenga nchi na kazi hiyo sio ya mtu mmoja-maovu yafichuliwe kwenye ngazi za serikali za mitaa na serikali kuu.
Anawashukuru sana vyombo vya habari ktk kutoa habari kwa watanzania na atajitahidi kufanya nao kazi,ila taarifa zao watakazozitoa ziwe za kweli na zenye kukidhi haja ya watanzania.
Anawashukuru sana wazazi wake baba 81 yuko mama 79 na wapo hai,anawashukuru kwa sababu anaamini walijitahidi kumlea vizuri na kwa makuzi ya maisha ya kijijini huenda taifa limempata mtu ambaye linamhitaji.
Angependa kuwa na wazazi wake kwenye siku ya kuapishwa, anamshukuru mkwewe wanawe Janneth, fotunata,Henuiq na anaamini kuwa watamsaidia kwenye maisha yake .
Anawashukuru wabunge kutoka mkoa wa Rukwa na anaamini kuwa hawatamtupa kwenye wakati huu mzito.
Anawashukuru wana Rukwa wote kama mjumbe wa halimashauri kuu ya CCM ,na anawaomba wamsaidie kuifanya kazi yake.
Anawaomba wabunge washikamane,waheshimiane, na ana hakika kuwa wakienda kwa mtazamo huo bunge litaweza kutimiza matarajio ya watanzania.
Anawashukuru viongozi wote wa Tanzania bara na visiwani,na hata wale wa CCM ,pande zote.
Anawashukuru sana viongozi wa upinzani na wabunge wote wa upinzani kwa kazi waliyompa ngumu, na anaamini kuwa kwa jinsi anavyoona ni kuwa a=wataweza kushirikiana kujenga nchi kwa pamoja.
Anawashukuru waliompa kura na waliomnyima.
Anarudia kuwa yeye sio mwanasiasa ila ataendelea kujifunza na hapo wataweza kuleta maisha bora .
Anasema kuwa huenda pakawa na hisia juu ya ripoti ya richmond,anaamini kuwa hakuna hisia za nia mbaya ila ni njia ya kuweza kujenga nchi,anawapongeza wote waliojiuzilu na lowassa na anaamini kuwa hiyo ndio njia ya kujenga taifa na CCM .
anaomba kuambia ukweli juu ya yale yote watu wakiona kuwa hayajengi na yeye yupo tayari kuyaacha mara moja.
Anamalizia kwa kushukuriu