Mizengo Pinda Waziri mkuu!

Nampa hongera Mh Pinda ni mtu makini na amekuwa pale kwa waziri ofisi ya Waziri Mkuu muda mrefu kidogo naamini atamudu
 
Angalieni posts yangu ya mwisho jana usiku.. na mkiwa na uwezo kimbilieni KLH News.. We set the standard!!
 
Pinda mtandao au si Mtandao? Kama mtandao basi nothing new will come!!!

Pia kama alikuwa kwa Wazir Mkuu inawezekana kweli akawa na uzoefu,lkn wasiwasi wangu isije ikawa ni UZOEFU WA UFISADI.
 
Naona wabunge wanamshangilia sana hapa ukumbini na EL kwa kweli anatia huruma sana sana kwani na yeye yupo ndani na kakaa viti vya nyuma.
 
Usalama wa taifa kwa kuchukua vyeo vikubwa vikubwa! Pongezi nyingi kwa Mheshimiwa Pinda. Tunakutakia kazi njema na mafanikio katika kubadili utendaji wa serikali yetu.

Ila sisi JF kama kawaida tunajipanga upya na kunoa majembe kuendelea kupambana na mafisadi.
 
Binafsi sitarajii makubwa kutoka kwa huyu mzee. I dont know naona kama upole wake umezidi sana kiasi anaweza akawa mtu wa ndio mzee zaidi. Anyway labda kwa kuwa na authority kubwa itamsaidia kuwa active.
 
Kiongozi wa upinzani bungeni anamfagilia Pinda sana kuwa ni mwadilifu na mwenye kusimamia haki na anawataka wabunge wamuunge mkono m.

Anamtaka Pinda Kuhakikisha kuwa ataweka mbele masilahi ya wabunge na kuhakikisha kuwa bunge linatimiza wajibu wake kikamilifu na kuweka mbele masilahi ya kitaifa.

Anamtahadharisha kuwa awe anasimamia haki.

Spika anamwita Lowassa kama mbunge wa Monduli naye anampongeza rais kwa kugusa nyoyo za wabunge.

Anampongeza rais kwa kumchagua mbunge anayejua bunge na anasema amefarijika sana kwani anaingia waziri mkuu anayefanana naye sana ....

Anasema kuwa Pinda ni kada, mzoefu, anaijua nchi vizuri, anajali sana masilahi ya wanyonge, hufanya kazi muda wowote hata usiku, anasema kuwa bunge limempata waziri mkuu mahiri na makini.

Anamalizia kwa kuunga mkono hoja.
 
Jamaa yuko serious ila hua nashindwa kumwelewa ni Simba mwenda pole au ni serious wa serious kweli!!!!!!!????

Watu wa Mwanza uwanja wa Nyamagana ndio umeondoka maana alikua anaupigia debe sana..anyway lets pray for him may be he can make a nice move
 
Hongera sana Mh Mizengo kwa kuteuliwa,.............. it is a challenge to you, and you have to prove that you are capable kwa manufaa ya wananchi

........natumaini na ule mradi wa mvua kutoka Thailand utaufuta kabisa, na zile hadithi za ndege kupaa zitakoma.....tunataka kazi ifanyike kwa maendeleo yetu sote
 
Mama Mongela anampongeza Pinda kwa kusema kuwa alipokuwa waziri Pinda akiwa ikulu na mwalimu Nyerere alikuwa anawahudumia kwa unyenyekevu mkubwa sana , pia anasema ni mtu mwema sana .

Anampongeza Lowassa kuwa ni kiongozi shupavu na aombewe kwani anarudi kuimarisha safu za nyuma ndani ya bunge.

Anamtaka Lowassa kuwa kuna haja ya yeye kushirikiana na wabunge wengine ili kuimarisha bunge husika.
 
Usalama wa taifa kwa kuchukua vyeo vikubwa vikubwa! Pongezi nyingi kwa Mheshimiwa Pinda. Tunakutakia kazi njema na mafanikio katika kubadili utendaji wa serikali yetu.

Ila sisi JF kama kawaida tunajipanga upya na kunoa majembe kuendelea kupambana na mafisadi.

Nakuambia itabidi Mkjj asimuandike tena waziri mkuu maana wana usalama sasa hivi wanamiliki hiyo ofisi rasmi.......lol

Kupambana na Raisi mwanajeshi na waziri mkuu ambaye ni usalama wa taifa itakuwa kama Russia ndogo vile ...... naona friday hii imeanza vyema hapa.
 
Hivi CV ya bwana Pinda ikoje

Name Mizengo Pinda Mizengo Pinda
Surname Pinda
First Names Mizengo Kayanza Peter
Alternate Name
Title
Country of Birth Tanzania
Positions
From To Organisation Position
2006 Prime Minister's Office Minister of State for Regional Administration & Local Government
2005 Mpanda Mashariki Constituency MP for Mpanda Mashariki
Date of Birth 12 Aug 1948
Political Affiliation CCM
eMail
Telephone
Address
Notes EDUCATION
School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
University of Dar es Salaam LLB 1971 1974 GRADUATE
CERTIFICATIONS
Certification Name or Type Certification No. Issued Expires
No items on list
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From Date To Date
Prime Minister’s Office - Regional Admin.& Local Governments. Minister 2006
Prime Minister’s Office - Regional Admin.& Local Governments. Deputy Minister 2000 2005
State House Clerk to the Cabinet 1996 2000
State House Assistant Private Secretary to the President 1982 1992
State House Security Officer 1978 1982
Ministry of Justice State Attorney 1974 1978
[ Retrieved on 6/7/2006 - www.parliament.go.tz ]
 
Back
Top Bottom