Mizengo Pinda: Mnaitaka Tanganyika ipi?.

Mizengo Pinda: Mnaitaka Tanganyika ipi?.

Serikali ya Tanganyika Huru, siyo serikali ya bara! Unaposema bara una maana gani? Dsm, Lindi, Mtwara, TAnga na Pwani,Ukerewe na Mafia ni bahari na visiwa pia,hivyo kusema bara unatumia kigezo gani. Ni Tanganyika huru, kama ilivyo Zanzibar huru.

Ndicho nilichotaka kujua, kwa hiyo siyo swala la jina la Tanganyika, bali ni kuwa na Nchi huru, hivyo tunaweza hiyo nchi tukaipata na kuibatiza jina lolote lile, Je hapo ni sawa?
 
Huyo Mpindwa awe anakatibu kutumia akili japo kidogo.
imamaana yeye anawaona akina nyerere na wengine waliopigania uhuru Ni mafala kwa kuwa kipindi wanazaliwa tayari walikua chino ya mkoloni.
anataka kuwaambia walioenda na waliopo shuleni Ni wajingajinga kwa kua wanatafuta elimu na maarifa ambauo hawana? Ana maamisha yeye Ni hamnazo kwa kitendo cha kusimamia kuleta maendeleo ambayo watanzania hawana na hawajawahi kua mayo?
 
wewe nijibu swali kwanza moja kwa moja kama nilivyokuuliza kwanza kama ukipenda, halafu hayo mengine yatafwatia, napenda kujua tatizo ni Jina Tanganyika au Serikali ya Bara? Yaani manataka Serikali ya Bara au mnataka jina la Tanganyika?

Kwani jina la Tanganyika halipo ?
 
Wewe unaona tatizo lipo wapi ni bara au nchi kavu !

Mimi sijui hasa tatizo ni nini, na ndio maana nauliza, kwa maana nasikia "tunataka Tanganyika yetu", sasa napenda kujua mnataka Nchi ambayo itaitwa (lazima) Tanganyika au mnataka Nchi ambayo inaweza ikapewa jina lolote lile mradi iwe inatimiza hayo matakwa yenu ya kuwa na Nchi?
 
Ofisi ya waziri Mkuu ipo Tanganyika tu kule Visiwani Hana Ofisi kule kuna Makamu wa Rais wawili mmoja anaact Kama waziri Mkuu kimtindo hv lakini kiujumla Pinda Pale Zenji hapagusi ni Kama Magufuri hagusi miladi ya Barabara za Zenji ingawa yeye wakati wa Bunge la Bajeti Dodoma wabunge wa Zenji hukaa kwenye vikao na kuvuta posho kwenye vikao vya Wizara ambazo si za muungano lakini Hakuna Mbunge wa Bara ananusa Bunge Lao la zenji ambalo ni kubwa sana japo Aridhi Yao ni ndogo lakini wao wanawachuna buzz watanganyika kupitia Utitiri wa Viongozi kisha wanafurumusha malalamiko kibao ili kuwasahaulisha haraka

Kuna mazingatio makubwa sana kwa Watanganyika hasa kwenye Comment ya huyu bwana kutoka Znz, ingefaa hata Mh. Rais au Waziri mkuu au Viongozi waandamizi wa CCM wangesoma maelezo ya huyu bwana kutoka Zanzibar, nina uhakika wangekubali na wao kwa nini watu wanataka Tanganyika yao, na serikali tatu kwa ujumla. Siyo kwamba Watanganyika wanaitaka bure tu, ni kutokana na malalamiko ya wenzetu, lakini pia ni umimi wa wenzetu kuvunja katiba kuu ya nchi na kutengeneza kinyemela katiba ndani ya katiba, hivi hili CCM wanaona ni sawa, hivi licha tu ya msimamo wa chama, hivi mwana CCM mmoja mmoja hawalioni. Hivi wanasimamia wapi kutetea serikali 2? Tuwe wakweli jamani.
 
Wanasiasa ushangaza wanapotetea matakwa yao hata kama hayana mashiko. Mh. Pinda aliposema bungeni kwa dhati na ukweli kwamba Zanzibar si nchi alipingwa na kukejeliwa isivyo kifani. Lakini alikuwa kweli katika kauli yake. Mh Rais alipoza mambo baada ya kutoa tafasiri ya kisiasa kuwa Zanzibar si nchi nje lakini ni nchi ndani! Na yote haya ni kwa sababu ya muundo wa Serikali mbili.

Nilitarajia kuwa mh. Pinda sasa angesaidia kwa kutetea kitu ambacho kitaleta mwafaka ili tuwe na nchi moja ndani na nje. Suluhisho jema ni kuwa na Serikali moja na kutoa uhuru wa aina fulani kwa washirika kujitawala. Kwani Tanganyika kudumu kwa miaka mitatu ndani ya uhuru wetu unazuia uwepo wake sasa ati kwa sababu tu watu hawaijui? Mbona tunaona nchi nyingi tu zilizaliwa upya baada ya dola la kisovieti kuanguka. Sisi hatutaki tuanguke ndiyo tuwe na Tanganyika, lakini tuuboreshe muungano wetu tukiwa na Tanganyika na Zanzibar zetu. Acheni siasa za kivyama, angalieni mstakabari wa taifa letu moja nje ya mifumo yenu ya kivyama.

Siasa bhana: Ni nchi ndani ila si nchi nje!!!! Na wenyewe wanaona ni sahihi. Hapa kauli ya mwanzo ya Mh. Pinda ilikuwa sahihi Kisheria, na ile ya pili ya Mh President ilikuwa sahihi KISIASA ili ku Neutralize tu, ila kauli ya PM ni sahihi Kisheria!
 
Nashangaa kuulizwa nataka Tanganyika ipi. Nimuulize Tanzania ipi yenye kaa nchi kaliko huru ndani yake kakinyonya. Je Afrika kusini na Swazland kwanini isiwe na muungano. Ni aibu kuuliza Tanganyika ipi kama hajui anyamaze ataijua ni ipi. Mama yetu aje kutuhudumia mama wakambo hatupendi kama sisi tulikuwa radhi kuondoa uraia wetu hawa watu wameshindwa nini kutuunga mkono na kuwa wamoja. Imefikia kikomo ni kejeli kwa Watanganyika kwa swali hili Pin d afahamu nilazima ama serikali moja ama Tanganyika irudi wanaogopa kipi muungano wa viongozi wa ccm tu nini maana yake. Ni lazima Tanganyika au nchi yetu Tanzania nikupoteza muda kuanza kutunga kitu kilicho kinyume na wenye katiba yao. Warioba mlimchagua afanye nini sasa ni aibu ya kihistoria mtakumbukwa kwa ubaya huu
 
Ndicho nilichotaka kujua, kwa hiyo siyo swala la jina la Tanganyika, bali ni kuwa na Nchi huru, hivyo tunaweza hiyo nchi tukaipata na kuibatiza jina lolote lile, Je hapo ni sawa?

Kwa nini tuanze kufikiria kubadilisha jina ili iweje? Tuipate Tanganyika Huru halafu mengine baadae. By the way kubaki na jina la asili ni bora zaidi. Congo-Zaire-RDC/DRC!
 
Kama leo usiku mh. Waziri mkuu aliangalia taarifa ya habari ITV (23/02/2014) angesikia kiongozi wa AFP Zanzibar, pamoja na mambo mengine aliyoongea amewasisitiza Wazinzibar kama walivyokubaliana wote bila kujali chama kuunga mkono muundo wa Serikali 3 ili Zanzibar ipate aliouita Uhuru Kamili na wapate kile alichokiita KUPUMUA. Kwa hiyo waheshimiwa hawa wa CCM wawe tayari mambo mawili, kukwamisha mchakato mzima kwa kung'ang'ania serikali2 ili column ya Zanzibar wapinge kura ya NO, au wakubali matakwa ya wale wanaopenda Serikali3 ili wengine WAPUMUE, na wengine Wapate TANGANYIKA YAO. Sasa kupanga ni kuchagua, kama hela zote walizotumia Tume ya Mabadiliko ya Katiba, hela zote watakazotumia Bunge Maalumu la Katiba zipotee bure basi wang'ang'anie serikali2 ambapo kule Zanzibar, ukijumlisha na Watanyika by Nature, hatari ya NO VOTE ni kubwa. Hivyo busara na kujishusha kwa mustakabali wa Taifa kunagitajika sana ili hela za Walipakodi zitoe kile kilichojusudiwa.!
Ndiyo maana nikasema kwa maoni yangu ninataka serikali moja kwa sababu sioni njia nyingine itakayoweza kuondoa hizi kero ambazo kila upande wa nchi unalalamikia.

Sioni kama serikali tatu ndiyo zitaondoa kero, ninachoona serikali tatu ni njia ya kutengeneza mazingira kuelekea kuvunjika kwa muungano lakini kwa gharama kubwa hasa kama ukizichunguza kauli za viongozi wa kisiasa wa upande wa Zanzibar.

Haya ndiyo matatizo ya kutokuwepo kura ya maoni kabla ya kuingia kwenye mchakato wa kuandika Rasimu ya Katiba. Kwa sasa kinachoongelewa kwenye mchakato wa Katiba ni Muungano wakati kuna mambo mengi sana ndani ya Rasimu ya Katiba ambayo yanahitaji critical observation and examination kama inavyofanyika kwenye swala la Muungano.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Kwa nini tuanze kufikiria kubadilisha jina ili iweje? Tuipate Tanganyika Huru halafu mengine baadae. By the way kubaki na jina la asili ni bora zaidi. Congo-Zaire-RDC/DRC!

Bado unazunguka na haujajibu Swali, nimekuuliza TATIZO ni jina la Tanganyika au tatizo kutokuwa na Serikali ya hiyo mnayoiita huru?
Haya mambo mawili ndio mnanichanganya nayo, naomba tu kupata jibu la moja kwa moja kama ukipenda, na sio maelezo meeengi!


 
Ndiyo maana nikasema kwa maoni yangu ninataka serikali moja kwa sababu sioni njia nyingine itakayoweza kuondoa hizi kero ambazo kila upande wa nchi unalalamikia.Sioni kama serikali tatu ndiyo zitaondoa kero, ninachoona serikali tatu ni njia ya kutengeneza mazingira kuelekea kuvunjika kwa muungano lakini kwa gharama kubwa hasa kama ukizichunguza kauli za viongozi wa kisiasa wa upande wa Zanzibar.Haya ndiyo matatizo ya kutokuwepo kura ya maoni kabla ya kuingia kwenye mchakato wa kuandika Rasimu ya Katiba. Kwa sasa kinachoongelewa kwenye mchakato wa Katiba ni Muungano wakati kuna mambo mengi sana ndani ya Rasimu ya Katiba ambayo yanahitaji critical observation and examination kama inavyofanyika kwenye swala la Muungano.
Huwa napata tabu sana mtu akisema anaogopa muungano kuvunjika? Kama wananchi hawataki muungano/kuendeelea kuungana kwa nini "walazimishwe" kwa kuweka protactive structure? Serikali moja ama tatu ingalikuwa ni kipimo sahihi cha kuweza kujua kama muungano huu ni wa hiari ama wa kulazimishana. Tusiogope muungano kuvunjika kama hivyo ndivyo wananchi walio wengi wanataka iwe.Lakini suala la serikali moja kwa sasa sio mojawapo ya options kwa sababu serikali ya Zanzibar ni lazima iwepo(kwa mujibu wa ToR).
 
· Wanajamvi mimi nina mtazamo tofauti,naamini kabisa hawa wote wanaodai serikali mbili wako kwenye makundi mawili
· kundi la kwanza ni lile ninaloliona kuwa wanafiki na WABAKAJI WA DEMOKRASIA.hii inatokana na kundi hili kujua lakini kupotosha ukweli na kutozungumzia uchaguzi huru,wa haki na vyama vingi uliofanyika 1963 zanzibar na matokeo kutangazwa na serikali kuundwa ila ikapinduliwa kabla ya kuapishwa ,.badala yake wanahubiri i mapinduzi kumuondoa Sultani(UCHAGUZI ULE ULIKUWA WA NINI) ikumbukwe chama cha CCM kwa sasa ndicho kinatawala Zanzibar na Tanganyika aka Tanzania ukizungumza tofauti na mfumo wa serikali mbili utaitwa mchochezi asiyetakia mema nchi yetu!!!!!!
Kundi la pili ni lile la mashabiki bendera kufuata upepo ambao wakipewa khanga , Tishirt na mlo mmoja huku wakiporwa maliasili kwa njia ya mikataba isiyo na mashikoi hushangilia kushiba kumbe wanaporwa mali zao bila kujua huku wakipambwa na ngonjere kulinda utaifa mshikamano amani na utulivu wakijaribu kuuliza madeni ya kitaifa wanaambiwa wachochezi na hawalitakii Tafaletu mema
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amekiri kuwa Bunge Maalumu la Katiba, limeanza na changamoto, huku akihoji wanaotaka Serikali ya Tanganyika, wanakusudia ipi ya mkoloni au ya baada ya uhuru ya miaka mitatu.

Mbali na hilo, amesisitiza yeye na chama chake cha Mapinduzi wanataka mfumo wa serikali mbili na si tatu kama Rasimu ya Katiba ilivyopendekeza.

Amekiri kuwa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo, utakuwa na misukosuko mingi, lakini utavuka salama.

Pinda aliyasema hayo jana wakati akifungua semina ya viongozi na watendaji wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwenye Makao Makuu ya chama hicho, White House mjini hapa.

Pinda ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, alisema zipo hoja nyingi za msingi katika mchakato huo wa kutunga Katiba, lakini kubwa na litakalochukua muda mwingi ni muundo wa Serikali. Hata hivyo, alisema wazi msimamo wake na ule wa CCM kuhusu pendekezo lao la kuwa na Serikali mbili, kinyume cha Rasimu ya Katiba inayopendekeza Serikali tatu.

“Hata ukiniamsha usingizini usiku wa manane, kwangu mimi bado Serikali mbili ni muundo mahsusi.

“Mwalimu Nyerere hata wakati ule alikaa na Tanganyika kwa kipindi kifupi, mwaka 1961 Tanganyika ikawa huru, 1962 tukawa Jamhuri, 1963 Zanzibar ikapata uhuru (baadaye alisema Uhuru wa bandia), mwaka 1964 ikazaliwa Tanzania.

“Tanganyika ya kikoloni ndiyo iliyokaa muda mrefu, hii nyingine ni kutoka mwaka 1961, 1962 na 1963. Ikazaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Leo hii miaka 50 tuko ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunadai Tanganyika,” alihoji Pinda na kuongeza:

“Tanganyika ipi? Nikadai ile ya mkoloni? Kipi kimo katika Tanganyika ya miaka mitatu? Tanganyika wakati inazaliwa nilikuwa na miaka 13, Tanzania nilikuwa na miaka 16, naujua vizuri Muungano. Kuanzia pale sijui chochote kingine, kama ilivyo wengi wetu humu.

“Au wale waliozaliwa miaka 50 iliyopita, wanaijua vizuri zaidi Tanzania. Tanganyika ipi mnazungumzia? Maana haikuwapo zaidi ya ile ya kikoloni iliyokaa muda mrefu.”

Alisema njia bora ni kukaa chini na kuzungumzia matatizo ya muundo wa Serikali mbili na kuyaboresha kwa nia ya kusonga mbele kuliko kudai Serikali ya Tanganyika. Waziri Mkuu alisema si vyema kuanza sasa kujaribu muundo wa Shirikisho baada ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, huku akitolea mfano wa Shirikisho la Afrika Mashariki (EAC).

“Pale kuna Shirikisho la Afrika Mashariki, lakini angalia mambo yanavyokwenda sasa wakubwa wakikutana. Utasikia wanazungumzia ardhi, mara pasipoti.

“Haiwezekani miaka 50 baada ya Muungano tuanze majaribio ya Shirikisho. Aah, wapi tunataka kwenda. Tanzania Bara na Zanzibar wana historia ya udugu na ushirikiano. Ukaribu, lugha moja na kuoleana,” alisema Pinda.

Huku akirejea kauli mbalimbali za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alisema hata hilo Shirikisho linalopendekezwa litakwama, kwa sababu Rais wake hatakuwa na ardhi, na kama nchi wanachama zitakataa kutoa ardhi, atafanyaje kazi zake.

Alisema tatizo lililopo ni utambulisho wa Zanzibar na suala la umiliki wa ardhi kwa Tanzania Bara wakiwa visiwani, ambayo alisema ni mambo yanayozungumzika.

“Suala hapa ni utambulisho wa Zanzibar ambalo hata hivyo si suala kubwa na tunaweza kulisahihisha. Pia liko suala la ardhi Zanzibar. Lakini wanaotaka ardhi huko, lazima wajiulize je, kweli iko ardhi ya kutosha,” alieleza.

Akizungumzia Bunge Maalumu la Katiba alisema, “Tumeanza mchakato wa kutunga Katiba, lakini tayari kuna changamoto zetu, lakini tumeanza kwa kuchagua Mwenyekiti wa Muda na kutengeneza Kanuni wiki ijayo zitakuwa tayari ili tulifikishe mwisho hili,” alisema na kuongeza:

Bunge Maalumu la Katiba limeanza vikao vyake wiki iliyopita, lakini wiki ijayo linatarajiwa kuanza mijadala baada ya kupitishwa kwa Kanuni na kuchaguliwa kwa Mwenyekiti na hatimaye kuzinduliwa rasmi.

Hata hivyo, tayari kuanza hali ya sintofahamu kwa wabunge kuanzia kudai suala la nyongeza ya posho, hadi katika vikao vyao ya kazi ambako zimeshuhudiwa kauli zinazoashiria kazi nzito mbele na inayopaswa kuwa na udhibiti ili mijadala isitawaliwe na jazba na kutekwa na makundi yaliyowapeleka bungeni humo.

Aliwaomba wajumbe wa semina hiyo ya Jumuiya ya Wazazi kuwaombea wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, watimize majukumu yao kwa maslahi ya Taifa.

Kwa hisani ya Habari leo.
 
Katiba iliyopo ilishavunjwa kabla na ninachkiona tatizo kubwa wala si Muungano,tatizo letu kubwa ni viongozi wetu wa siasa kupenda mno madaraka na kujilimbikizia mali.Wameweka mbele maslahi binafsi kuliko taifa,wamebadili hata malengo ya uongozi na sasa ukitaka kuwa kiongozi basi lazima uwe mwanafamilia if not rafiki.
 
Hizo serikali mbili sidhani kama kwa sasa zitakuwa suluhisho, ccm watake wasitake ama serikali moja au tatu, tanganyika yetu irudi haijarishi ya mkoloni au ya miaka miwili ya uhuru. Ife tanganyika ife zanzabar ibaki tanzania. Ccm wajue wako milion 4 na watanganyika tuko milion 40. Tumefuga kupe kwa miaka 50 sasa basi. Ccm wajue wamekaa juu ya gunia ambayo chini kuna moto. Kwa upofu wao wanajua kama moto utazima. Hicho wanachokifanya hakitakuwa kiu ya wazanzibar maana wazanzibar wanataka zanzibar yao. Na sisi watanganyika tunataka tanganyika yetu.
 
Katiba iliyopo ilishavunjwa kabla na ninachkiona tatizo kubwa wala si Muungano,tatizo letu kubwa ni viongozi wetu wa siasa kupenda mno madaraka na kujilimbikizia mali.Wameweka mbele maslahi binafsi kuliko taifa,wamebadili hata malengo ya uongozi na sasa ukitaka kuwa kiongozi basi lazima uwe mwanafamilia if not rafiki.

Waulize kwanini isiwe serikali moja!!!!!!?????


Kwa nini isiwe serikali moja




Tanganyika yetu tunahitaji sisi kwa miaka 50 tumekuwa radhi kuacha utaifa wetu wao je



Bila serikali moja basi tatu na wachangie gharama wakishindwa go to hell, kwao kila mtaa kuna mbunge hawaridhiki




Tujibu.i ccm kwanini isiwe serilalioja
 
Namuunga mkono moja kwa moja eti mtu ana miaka 25 eti kwa sababu kapata tiketi ya kuingia bungeni kama mjumbe unasikia anasema serikali Tatu wakati hata wakati Tanganyika inapata uhuru hakuwepo,Pinda nakupongeza kwa msimamo wako thabiti
Hivi wewe unaona ni haki Rais wa Muungano kushushwa hadhi huko Zanzibar? Je, kweli Rais wa Muungano ni wa Zanzibar na Tanganyika au ni wa Tanganyika tu. Jaribu kufanya upembuzi wa serikali tatu, na kwa nini isiwe moja tu?????
 
Pinda mwenyewe KAPINDA. Hajui analolisema, anasema kwa sababu anajua watatumia wingi wao kuonesha kuwa wana mawazo sahihi.
Mw. Nyerere angekuwa hai leo angetamani auone muungano wa kweli sio huu fabricated. Muungano wa kweli ni moja jumlisha na moja ije moja. Yaani nchi ya Tanganiyka kuungana na nchi ya Zanziba izae nchi Moja kamili ya Jamhuri ya Muungano yaTanzania.
Huu ndio muungano. Tuwe na Serekali moja tu. Watu walio ridhiana, kukaa pamoja. Mtu awe huru, kuishi Bukoba au Kisiwandui. Afurahi kuitwa Mtanzania wala sio Mtanganyika au Mzanzibari. Tanzania hatuna ukabila, udini, ukanda.
Hatuna haja ya Baraza la Mapinduzi bali ni historia, Hatuna Baraza la Wakilishi bali Bunge la JMT pale Dodoma. Tupange kuhamia Dodoma kwani ndio katikati ya JMT au Manyoni.
Pinda, usipindishe mambo, usiwaogope hao Wazenj, waambie wafute tu kauli zao na kujiweka katika muungano. Watakuvunjia hilo limuungano lako very very soon. Nashauri tu
 
Back
Top Bottom