Mizengo Pinda: Mnaitaka Tanganyika ipi?.

Mizengo Pinda: Mnaitaka Tanganyika ipi?.

Kwa maoni yako, hutaki Tanganyika kwa sababu hujawi kuiona, lakini wakati huo huo unapendekeza kuvunja muungano kitendo ambacho kitarejesha Serikali ya Tanganyika moja kwa moja ambayo huitaki! Je si vyema ukawa na Serikali hiyo ndani ya muungano?

Tz Bara kuna watu 43 million na ZNZ kuna watu million 1.5 lakini hao Wachache wamakuwa wajanja wanawapeleka puta wengi kiasi kwamba wengi hawana jinsi inabidi kufuata kile cha wachache wajanja zaidi
 
waliokuwepo wamefanya nini toka walipokabidhiwa nchi??? mpaka imefikia hatua ya kutaka katiba mpya, wakati miongoni mwenu kunaealioenda mbali mpaka walifikia hatua ya kupinga hata hoja ya kuwa na katiba mpya??? muombe Mungu akupe "macho" uone.
Mtoto wa digital hayaoni yaliotendeka mpaka sasa kweli wwe unamatatizo muombe Mungu akufunulie
 
Hawajui walikotoka watajuaje wanako kwenda ndio maana wataka serikali Tatu ,Nne nk .Pinda tuko nyuma yako tuna kuunga mkono

Pinda ndio hajui alikotoka. Kuwa nyuma yake sio ajabu maana mlifundishwa nidhamu ya ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI WA CCM
 
Pinda kauliza swali zuri sana hasa kwa wale wafaidhina Tanganyika ipi unayoifahamu ? ya mkoloni au ya uhuru mjibuni basi
 
Tanganyika ipi unayoijua wewe?

Mamlaka huru ya Tanzania Bara kama ilivyo serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar...

Hii ndio hoja ya watu wote wanaodai Tanganyika na wala sio hoja hiyo anayojaribu kuiibua Mr Pinda...

Alichofanya Mizengo ni kujaribu kuwachanganya Watanzania bara na kauli mbiu hiyo ya kisiasa wakati mjadala wa katiba ni wa kisheria.
 
SASA NAANZA KUPIGA KAMPENI YA KUWA NA SERIKALI MOJA TU. maana mnapotaka kuturudisha ndipo palipopelekea haya yote........!!!!
 
Wanasiasa ushangaza wanapotetea matakwa yao hata kama hayana mashiko. Mh. Pinda aliposema bungeni kwa dhati na ukweli kwamba Zanzibar si nchi alipingwa na kukejeliwa isivyo kifani. Lakini alikuwa kweli katika kauli yake. Mh Rais alipoza mambo baada ya kutoa tafasiri ya kisiasa kuwa Zanzibar si nchi nje lakini ni nchi ndani! Na yote haya ni kwa sababu ya muundo wa Serikali mbili.

Nilitarajia kuwa mh. Pinda sasa angesaidia kwa kutetea kitu ambacho kitaleta mwafaka ili tuwe na nchi moja ndani na nje. Suluhisho jema ni kuwa na Serikali moja na kutoa uhuru wa aina fulani kwa washirika kujitawala. Kwani Tanganyika kudumu kwa miaka mitatu ndani ya uhuru wetu unazuia uwepo wake sasa ati kwa sababu tu watu hawaijui? Mbona tunaona nchi nyingi tu zilizaliwa upya baada ya dola la kisovieti kuanguka. Sisi hatutaki tuanguke ndiyo tuwe na Tanganyika, lakini tuuboreshe muungano wetu tukiwa na Tanganyika na Zanzibar zetu. Acheni siasa za kivyama, angalieni mstakabari wa taifa letu moja nje ya mifumo yenu ya kivyama.
 
Ni UTOTO wa hali ya juu kupinga mfumo wa serikali tatu!

Tunamuomba Pinda atuambie ni kwa nini hakupencdekeza serikali moja?

Sababu zinazomfanya akane kupendekeza serikali moja ndizo hizo hizo zilizotufanya wengi wetu tupendekeze serikali tatu kwenye rasimu ya mabadiliko ya katiba!!

Kwani Zanzibar huru imekaa miaka mingapi kutoka mikononi mwa wakoloni?

Mbona sasa inataka uhuru kamili na imevunja katiba ya jamuhuri kwa kutengeneza mpaka katiba yake ikijipambanua kuwa ni nchi?Walikuwa wapi wakati yakifanyika hayo?

Serikali tatu HAZIEPUKIKI!

Idumu serikali ya watu wa TANGANYIKA!

Wazenji million 1.5 tu wanawapelekesha watu 43 million watakavyo wao wana katiba Yao tayari wana baraza Lao la wakilishi wana wimbo wao wa Taifa wana Bendera Yao yaani Wazenji ni Wajanja kuliko Wabara Mara 1000 kwani wanachofanya sasa ni kuwasanifu kwani hii katiba ya sasa inayoandaliwa wao ni Kama wanaichora tu wanasubiri ikamilike kisha wang'ang'anie katiba Yao utokee Mkanganyiko kisha iandikwe katiba Mbili mpya yaani katiba ya Tanganyika pekee na Katiba ya Muungano
 
Kunashida moja ya watanzania kutotaka kujielimisha na kutafuta ukweli ndiyo maana wengine hubeba jambo hata kama halijui undani wake.

mtuelimshe basi,mnasema serikali mbili na huku hamfafanui uzuri wake,maana yake nini?halafu katiba nzuri inayowafaa wananchi ni ile inayotokana na maoni ya wananchi.kwanini nyinyi ccm inapinga mawazo ya wananchi?hiyo itakuwa ni katiba ya ccm kwa manufaa ya ccm tu.na hilo linaonesha jinsi gani ccm haiwajali wananchi wake.inawaoma kama wapumbavu fulani wasiofaa kuishi katika nchi hii kwahiyo kila jambo hupanga wao kwa manufaa yao.nimekuwa nikisema watanzania wengi kwakuwa ni maskini wakiugua hawanamatumaini ya kuishi kwani hospitali huduma mbovuuu!lakini wao ccm hutibiwa ulaya sasa nikuulize wewe simiyu hiki chama kinawajali wananchi?wanaokichagua nao ni ma mburula kama ulivyo wewe,utasikia eti ccm imenilea,ukimuona anayesema hayo kachooooookaaa!nitaichukia ccm na watu wake daima.
 
Tatizo linakuja pale mnapoanza kulazimishana bila hoja. Na mbaya zaidi huku kulazimishana kunaonekana ni kwa faida ya watu wachache wenye tamaa zao.
 
Ni UTOTO wa hali ya juu kupinga mfumo wa serikali tatu!
Hapana, siyo utoto bali ni kutofautiana kifikra na mtazamo tu.
Tunamuomba Pinda atuambie ni kwa nini hakupencdekeza serikali moja?
Kwa mtazamo wangu uko sahihi na kuboresha zaidi hoja yako ninasema hivi, Kwa nini hatukupewa haki ya kupiga kura ya maoni kwanza kuhusu muungano ambao ndiyo msingi wa katika. Kura ya maoni ("act of popular sovereignty) kuhusu Muungano ndiyo ingeonyesha mwerekeo wa taifa letu katika kipindi cha miaka 50 ijayo.
Sababu zinazomfanya akane kupendekeza serikali moja ndizo hizo hizo zilizotufanya wengi wetu tupendekeze serikali tatu kwenye rasimu ya mabadiliko ya katiba!!
Hakuna aliyekana kuhusu serikali moja bali wanaogopa hata kulitamka hili neno ambalo ndiyo ulikuwa msingi wa sera la CCM kuhusu Muungano. Viongozi wetu wanasumbuliwa na ulafi wa madaraka kwa sababu kuanzisha serikali moja ni kupunguza ulaji wao.
Kwani Zanzibar huru imekaa miaka mingapi kutoka mikononi mwa wakoloni?
Haya ni maneno ya kisiasa ambayo wanasiasa wanaanza kuyatumia kwa manufaa yao. Ukiitimgisha hoja yake utagundua mashimo mengi sana ya kimantiki.
Mbona sasa inataka uhuru kamili na imevunja katiba ya jamuhuri kwa kutengeneza mpaka katiba yake ikijipambanua kuwa ni nchi?Walikuwa wapi wakati yakifanyika hayo?
Hatufahamu kama Wazanzibari wanataka uhuru kamili lakini ukweli ni kwamba, Katiba yao imevunja Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania 1977 wakati huyu huyu Mizengo Pinda akiwa ni Waziri Mkuu.

Hakuna aliyekemea huu uvunjaji wa Katiba ya JMT badala yake anakuja na maneno ambayo hayana msingi kabisa katika mantiki ya hoja ya Muungano.
Serikali tatu HAZIEPUKIKI!
Idumu serikali ya watu wa TANGANYIKA!
Serikali tatu haziwezi kupatikana ndani ya serikali ya CCM. Sera ya CCM ni serikali moja kwa maana kwamba, labda CCM ipoteze uhalali wa kuongoza mchi ndiyo serikali tatu zitapatikana!.
 
Ningemsifu ka ma angeuliza swali hilohilo kwa Zanzibar. Unafiki ni mbaya sana. Anawaogopa?

Tambua ZNZ wana Serikari ni Vigumu kwa Waziri Mkuu kuwasemea kwani Waziri Mkuu Ofisi yake ipo Tanganyika Hana ofisi Zenji . Mpaka hapa tuliposimama matokea ni Zanzibar goli 7-0
 
Ningemsifu ka ma angeuliza swali hilohilo kwa Zanzibar. Unafiki ni mbaya sana. Anawaogopa?

Tambua ZNZ wana Serikari ni Vigumu kwa Waziri Mkuu kuwasemea kwani Waziri Mkuu Ofisi yake ipo Tanganyika Hana ofisi Zenji . Mpaka hapa tuliposimama matokea ni Zanzibar goli 7 na bara goli 0 kwani Wazenji wao wapo mbele sana wanasonga kijanja zaidi
 
There is no logic kwenye maneno ya Mizengo Pinda, yeye kama mwanaCCM alikuwa wapi kuzungumza na Wazanzibar ili kutatua hizo shida? hadi leo anakuja kubwabwaja hapa maneno kama hayo? Hata sisi amabao hatukuishi miaka yake hiyo anayosema hatuutaki huo muungano wa serikali mbili kwa sababu kipindi hizo nchi zinaungana hatukuwepo.
Hili ndilo swali ambalo wanaotaka serikali mbili lazima kwanza walijibu.

Kwa sasa wamepata msukumo gani zaidi wa kuzipatia ufumbuzi kero za Muungano ambazo badala ya kupungua, ndiyo zinaongezeka. Hata huyu Waziri Mkuu wa JMT anayeenda kwa jina la Mizengo Pinda hatambuliwi kiitifaki akiingia Zanzibar.

Lakini wanaCCM bwana wanafikiri wao tu ndiyo wana hatimiliki ya kufikiri na sio wenzao!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Siyo WanaCCM wote wanaotaka serikali mbili kwa hiyo kuweka mwamvuli kwa wanaCCM wote ni kupotosha kihoja.
 
teh....teh...teh....teh......serikali moja inatosha au tuvunje muungano au kipengele hicho kiondolewe kwenye mjadala wa bunge la katiba unaoendelea bungeni sasa na badala yake turudishiwe wananchi tukipigie kura ya maoni na kuamua kati ya serikali moja, mbili, tatu au kuuvunjilia mbali muungano. baada ya kura ya maoni ndiyo kipengele hicho kiingizwe kwenye katiba na kuwekewa utaratibu. maana yake ni kwamba kazi ya bunge la katiba itakuwa ni kuweka utaratibu tu lakini maamuzi tutakuwa tumefanya sisi wananchi.
 
Tatizo linakuja pale mnapoanza kulazimishana bila hoja. Na mbaya zaidi huku kulazimishana kunaonekana ni kwa faida ya watu wachache wenye tamaa zao.

Hoja ipi unaitaka ?Tanganyika haina Katiba yake Binafsi ! Sasa inasakwa Katiba ya Muungano wakati Zanzibar wao tayari wana katiba Yao Binafsi una Uhakika Kama zenji wataifuta katiba Yao Binafsi ?
 
Back
Top Bottom